Thursday, December 31, 2015

Hii Ni Silaha Mojawapo Ya Watu Waliofanikiwa.


Habari za leo mpendwa msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vizuri katika kuhakikisha kuwa unaupokea mwaka mpya vizuri ikizingatiwa kuwa tumebakiza masaa sasa kuukamilisha mwaka 2015 na kuingia mwaka mpya wa 2016. Basi katika kumaliza mwaka nataka umalize na wazo hili ili ukalitumie vizuri mnamo mwaka wa 2016 na kuendelea.
Je unazijua silaha muhimu za watu waliofanikiwa?, pengine unazijua baadhi kama vile kujiamini, kujituma, kujiwekea malengo, uwajibikaji, kushirikiana na timu sahihi n.k. hizo ni baadhi kati ya silaha nyingi ambazo waweza kuwa unazijua, lakini leo nakupatia silaha moja muhimu sana ya watu waliofanikiwa na kwa kuwa nawe unataka kufanikiwa ichukue na uitumie silaha hii ipasavyo.Matumizi sahihi ya muda, hii ndio silaha muhimu ya watu waliofanikiwa na kama nawe kweli unataka kufanikiwa hakikisha unaichukua silaha hii na kuitumia katika safari yako. Watu waliofanikiwa wanajua kutumia muda ipasavyo, wanajua kuwa kwa kila siku tuna masaa ishirini na nne (24) na katika hayo masaa kuna muda wa uzalishaji na muda usio zalishi (uzalishaji). Kwa kutambua hilo uhakikisha kuwa hawapotezi muda ovyo.
Watu waliofanikiwa wanatumia muda wao mwingi sana katika shughuli zao na sio katika starehe wala kupumzika, au kuangalia televisheni. Hii ni kwa kuwa wanatambua kuwa kuna muda wa uzalishaji na muda usio zalishi na kwa kuwa wanalitambua hilo basi wao hutumia muda vizuri katika shughuli zao yaani kama ana biashara basi muda mwingi sana atautumia katika biashara yake na sio kukaa kijiweni kupiga stori. Na kama ni mwekezaji basi muda wake mwingi atautumia katika shughuli zake za kiuwekezaji.
Watu waliofanikiwa wanatumia muda wao vizuri kwa kuwa wanajua kuwa muda ni mali ya kipekee ambayo ukiipoteza huwezi kuitafuta na kuipata tena yaani wao wanafalsafa ya kuwa muda ni kitu cha kipekee kisichoweza kurudishwa. Kama kweli unataka kufanikiwa naomba ujenge picha hii akilini mwako ili ukusaidie kuutumia muda wako vizuri. Ufananishe muda wako sawa na mafuta katika gari, mafuta katika gari ni kitu cha muhimu sana maana bila mafuta gari haliwezi kwenda popote, lakini mafuta haya huwa hayana kuongezeka bali ni kupungua tu na hatimaye kuisha ambapo ukitaka gari liendelee kwenda inabidi ukatafute mengine (kununua), uweke ndipo gari liendeleee na safari zake. Ndivyo ulivyo muda kama ambavyo hakuna nyongeza ya mafuta katika tenki la gari basi hata muda ni hivyo hivyo yaani tuna masaa ishirini na nne kwa siku moja basi hakuna pungufu wala nyongeza ya hapo. Hivyo basi inabidi ujifunze kufanya shughuli zako ipasavyo kulingana na muda  husika uliopewa.
Muda ni kitu ambacho kimekuwa kikidharauliwa na watanzania wengi sana tena sana na kwangu mimi matumizi mabovu ya muda ni sababu moja wapo ya watu wengi kutofanikiwa maishani. Watanzania wengi sana tumekuwa na tatizo ya kutojua kutumia muda na ndio maana hatuuthamini. Hauwezi kukithamini kitu bila kujua umuhimu wake, leo nataka utambue kuwa muda ni kitu muhimu sana tena sana na kwanzia sasa anza kuuthamini muda maana muda unaweza kuwa kigezo cha kutofautisha mafanikio na kushindwa.
Dunia imebadilika na itaendelea kubadilika na kubadilika, maendeleo ya sayansi na teknolojia yameleta vitu vingi sana vya kukuibia muda usipokuwa makini utajikuta kila siku ukiwauzia watu wengine muda bila wewe kunufaika na chochote bali kuwanufaisha wengine, zinduka wewe ukiyekatika usingizi mzito, acha kupoteza muda wako ovyo kwani muda ni rasilimali muhimu kwako ambayo ni ya bure kabisa kwako.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com.


Wednesday, December 30, 2015

Jifunze Kupitia Vitu Hivi Viwili.


Habari za leo ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kua hu mzima na waendelea vizuri katika kuyasaka mafanikio. Kama ilivyokawaida ya mtandao huu, ambao umejidhatiti katika kuhakikisha kuwa unakupatia maarifa ambayo ukiyatumia vyema yatakuwa kama chachu na kirainisho katika safari yako ya mafanikio. Leo natakaa ujifunze jambo hili nndugu msomaji nalo ni kujifunza kupitia vitu hivi viwili. Je vitu hivyo ni vipi?, endelea….
Leo nataka ujifunze kupitia vitu viwili kama nilivyokutambulisha hapo awali lakini najua vitu hivyo bado ni fumbo kwako. Basi vitu hivyo ni hivi hapa:-


1.       Vikwazo, najua wengi wetu tunaamini kuwa vikwazo vipo kwa ajili ya kutuzamisha au kutukwamisha na kutudidimiza kabisa na kutufanya tusipige hatua yoyote ile katika maisha. Hii ni imani ya watu wengi juu ya vikwazo.  Sasa leo nataka uvunje hii imani kabisa maana haina msingi wowote kwa wale ambao wanataka mafanikio,lakini kama hautaki kufanikiwa endelea kushikiria imani hiyo hivyo hivyo ilivyo.
Nimesema uachane na imani kuwa vikwazo vipo ili vikukwamishe na badala yake tumia vikwazo kama somo ambalo ukilielewa basi itakuwa chachu ya mafanikio yako. Vikwazo huja kwa malengo fulani haviji tu. Vikwazo vinaweza kuja kwa sura kama hizi:-
(a)    Vikwazo huja ili kutukomaza, kumbuka kuwa safari ya mafanikio sio safari nyoofu siku zote na wala sio safari rahisi, hivyo basi uwepo wa vikwazo upo ili kutukomaza vyema. Kabla hujapata mafanikio vikwazo vipo ili kukufanya ukabiliane navyo na ukishaweza kufanya hivyo hata pale utakapofanikiwa basi hata vikija vikwazo wewe utakuwa na uzowefu navyo na hivyo hauto shindwa kupambana navyo.  Yaani vikwazo ni kama mafunzo ya awali kwa askari ambaye hajawa askari bado.
(b)   Vikwazo huja kupima imani zetu, muda mwingine vikwazo huja kama kipimo cha imani zetu yaani kupitia vikwazo imani zetu hupimwa. Tambua kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya mafanikio na imani ya mtu yaani anaeamini kuwa atafanikiwa mara nyingi huwa anafanikiwa na asiye amini kuwa atafanikiwa nae huwa hivyo. Hivyo basi vikwazo huja kupima imani zetu. Kumbuka mfano wa ayubu katika biblia ambaye aliwekewa vikwazo mbalimbali ili tu kupimwa imani yake.
(c)    Vikwazo huwa kipimo cha uvumilivu, mafanikio huusisha watu ambao ni wavumilivu watu ambao wanaweza kukisubiria kile wanachokitaka hata kwa miaka saba mpaka kumi hata kama hakiji. Na wala hayahusishi watu ambao wanakata tama kirahisi rahisi. Hivyo basi vikwazo huja ili kutaka kupima uvumilivu wako.
2.       Makosa, hakuna asiyekosea  katika kutaka kujifunza kitu hapa duniani, ni vyema ujenge tabia ya kujifunza kupitia makosa yako na wala sio vinginevyo. Unapofanya makosa usianze kujilaumu kuwa kwanini imekuwa hivi au kwanini nimefanya hivi nina tatizo gani. Bali jifunze kupitia makosa unayoyafanya maana ni jambo la kawaida kukosea. Pengine makosa huweza kuwa na malengo haya yafuatayo:-
(a)    Kukurekebisha, makosa huja ili yakurekebishe na hii hutokea haswa pale ambapo unajiona au kujikuta kuwa umekamilika. Mfano unaweza kuwa unajifunza ukajiona umeshafuzu masomo husika, kwa kuwa hakukuwa kosa ambalo ulilifanya hapo awali hivyo kosa linapojitokeza linakuwa limekuja kukurekebisha ili ujue kuwa bado kuna mengi inabidi ufanye.
(b)   Kukuongezea ujuzi, makosa huja ili kukupatia ujuzi mpya hasa kwa yale mambo ambayo ulikuwa huwezi kuyafanya katika hali ya kujaribu hiki na kile alafu ukawa unakosea hapo ndipo hujikuta umepata ujuzi fulani.
(c)    Kukufanya uende na wakati, hii hutokea kwa wale ambao hufanya mambo kwa mazoea, pindi wafanyapo makosa kutokana na kuwa wamefanya vitu kinyume na wakati ndipo huwa wanashituka kuwa wapo nyuma ya wakati. Nini kimewafanya washituke basi, hakika ni makosa waliyoyafanya.
Kimsingi mtu anaetaka kufanikiwa huwa anatumi vikwazo na makosa kama darasa na wala sio kama nuksi au mkosi. Hivyo basi jifunze nawe kufanya hivyo maana naamini unatamani kufanikiwa na utafanikiwa tu.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com. 

Tuesday, December 29, 2015

Acha Kuangalia Matawi Pekee Kama Kweli Unataka Kufanikiwa.


Habari za siku ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa, ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vizuri kuhakikisha unayatekeleza yale uliyojiwekea na ikizingatiwa kuwa mwaka ndio huo unakwenda mwishoni. Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vyema kwa kuwa mungu kakujalia afya njema na uzima. Tuendelee kuelimishana juu ya mambo mbalimbali ambayo yatatufanya tuweze kuyafikia mafanikio. Leo tena tumekutana hapa katika hali ya kuendelea kupeana maarifa mapya na leo nataka uelewe juu ya jambo hili moja ambalo nalo ni kuachana na tabia ya kuangalia matawi pekee kama kweli unataka kufanikiwa.

Najua kila mtu anaifahamu miti na kama kila mtu anaifahamu miti sina haja ya kueleza zaidi kuwa mti una nini na nini. Kimsingi mti unaweza kuwa na sehemu nyingi sana lakini mimi ntauangalia mti katika sehemu mbili ambazo ni mizizi na matawi. Mizizi ni sehemu ya chini kabisa ya mti ambayo hukua kuelekea chini, na matawi ni sehemu ya juu ya mti ambayo hutawanyika katika pande mbalimbali za dunia na wakati mwingine hutupatia kivuli kizuri.
Matawi ni nini basi maishani au katika mafanikio haswa?, au kuangalia matawi ni nini haswa?. Napo sema acha kuangalia matawi pekee kama kweli unataka kufanikiwa namaanisha kuwa acha ile tabia ya kuamini kuwa maisha yamejaa raha tu, na kama ni katika biashara acha ile hali ya kuangalia faida tu bila kuangalia hasara. Au kwa kifupi usitegemee raha tu maishani, na katika biashara nyingi sana watu wamekuwa wakiangalia faida peeke bila kujali hasara. Hapa ndipo naposema acha kuangalia matawi pekee.
Nitajikita zaidi katika biashara,biashara nyingi sana zimekuwa zikianzishwa nyingi nyingi mno lakini kati ya hizo ni biashara chache zimekuwa zikifanikiwa sababu kubwa nayo iona ni ile tabia ya kutegemea faida tu wakati wote. Takwimu zinaonesha kuwa kati ya biashara kumi ambazo huanzishwa basi ni biashara tatu au mbili ndizo hudumu zingine zote saba au nane hufa baada ya muda mfupi. Biashara nyingi zinazoazishwa hazidumu kwa sababu wafanyabiashara wengi wanaoanzisha biashara hizo wanauelewa mdogo juu ya biashara husika ndio maana wao hulenga tu katika faida na sio hasara, wao huwa hawaelewi kuwa kuna kitu hasara katika biashara ndio maana hata inapotoke hasara ndogo tu hawawezi kumudu na matokeo yake biashara zao hupeperushwa na upepo na kuwaacha watupu na huo ndio huwa mwisho wao.
Uimara wa matawi hutokana na uimara wa mizizi yake yaani kama mti ni dhaifu katika mizizi yake basi hata matawi yake yatakuwa dhaifu na kinyume chake.  Leo hii mtu anapokuuliza juu ya biashara fulani yeye hukuuliza swali moja tu vipi biashara hii inalipa? Akiambiwa ndio inalipa yeye hukurupuka mara moja na kujiiingiza katika biashara bila hata kufanya uchunguzi wa kina swala yeye amejua kwa kuchukua bidhaa, gharama ya usafirishaji na bei ya kuuzia basi anajiingiza katika biashara  husika bila hata kujali taarifa zingine.
Biashara nzuri inamtegemea sana mfanyabiashara yaani ujuzi na uwajibikaji wa mtu husika katika biashara husika ndivyo viikuzavyo biashara kinyume cha hapo biashara haiwezi kukua yaani ikiwa mfanyabiashara anaujuzi mdogo basi hata biashara yake itakuwa ya kawaida. Biashara za siku hizi sio zile zenye kufanya kwa mazoea au kuiga zinahitaji muda mwingi kujifunza ili kuzielewa vizuri sio kuingia kichwa kichwa maana ukiingia kichwa kichwa kesho tu utakuwa nje kwa kuwa hujajipanga.
Mfanyabiashara bora na mzuri ni yule mwenye uwezo, ujuzi, na elimu juu ya biashara husika sio elimu ya darasani   bali elimu ya juu ya biashara husika. Mfanya biashara mzuri ni yule anayejua kama kuna faida basi kuna hasara hivyo huanza kuandaa mikakati ya atafanyaje pindi swala la hasara litakapo tokea na sio Yule anaewaza faida tu muda wote huyu ni yule anayeangalia matawi tu bila kujali mizizi na huyu hatodumu muda mrefu katika biashara bali atafirisika mapema.
Jifunze kuangalia mizizi kabla ya matawi japo matawi ndio huonekana kiurahisi. Yaani jifunze kutafuta chanzo cha tatizo fulani kabla ya kuanza kulaumu au kupiga makelele ovyo na kuanza kulaumu. Jifunze kuchunguza jambo kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho wake sio unachunguza katikati na mwisho kama kweli unataka kufanikiwa.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.

0754612413/0652612410.

Monday, December 28, 2015

Jiulize Swali Hili Kwa Kila Unalolifanya.


Habari za siku ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa, ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vizuri kuhakikisha unayatekeleza yale uliyojiwekea na ikizingatiwa kuwa mwaka ndio huo unakwenda mwishoni. Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vyema kwa kuwa mungu kakujalia afya njema na uzima. Tuendelee kuelimishana juu ya mambo mbalimbali ambayo yatatufanya tuweze kuyafikia mafanikio. Leo nataka  kukushirikisha jambo moja ambalo ni umuhimu wa kujiuliza swali kwanini kwa kila unalolifanya.


Ndugu msomaji kumbuka siku zote kuwa ubongo wa mwanadamu hukaa katika hali ya kufanya kazi pale unaposukumwa kutafuta majibu ya maswali unayojiuliza kinyume na hapo akili hudumaa na kufanya ubaki kuwa vile vile, hii ni sababu namba moja ya mimi kukuambia kuwa jifunze kujiuliza kwanini kwa kila jambo unalolifanya. Sababu ya pili ni kwa kuwa utapata majibu ya yale uliyokuwa huyajui. Pengine kuna kitu unakifanya au kuna hali uliyonayo lakini hujajua haswa kwanini unayo hiyo hali husika, ndio maana nakusihi jiulie swali hili.
Kuna watu ni wavivu sana tena sana, yaani wao hawapendi kufanya shughuli yoyote zaidi hutaka wao waletewe kila kitu. Daima watu hawa huwa ni mabingwa wa kutazama runinga, kupenda kwenda sehemu za starehe. Kama wewe ni mmoja wapo wa watu wa namna hiyo ulishawahi kujiuliza kwa nini wewe uko hivyo?, ukijiuliza kwanini unaweza kupata majibu kuwa pengine ni mazingira au ni katika hali ya kutaka kuiga vitu ili kuonekana ni mwenye kwenda na wakati. Majibu utakayo yapata yatakusaidia kubadili hali husika kama utakuwa hauipendi hali hiyo.
Wewe ulie mlevi, ulishawahi kujiuliza kwanini umechagua na kuyafata maisha ya kunywa pombe na kulewa kila siku?, kwanini unafanya hivyo ili hali unajua madhara yaletwayo na ulevi wa kupindukia?, je ulishawaza itakuwaje ukiacha pombe?, kwanini unang`ang`ania pombe? , kwanini hutaki kuacha?. Ukijiuliza maswali juu ya tabia yako hii na kama kweli huipendi unaweza kujinasua katika mtego huu.
Wewe ulie mnene na hauufurahii unene wako je ulishawahi kujiulia kwanini unanenepa nenea ovyo? Pengine unene wako unatokana na kula sana vyakula vyenye mafuta alafu hutaki kufanya mazoezi ili kuyapunguza mafuta hayo. Kwanini unaendelea kula vyakula vinavyokufanya unenepe ovyo wakati unajua?  Na kwanini hutaki kuacha?
Mifano hapo juu mitatu nimeiweka kama baadhi ya tabia tu ambazo wengi tunazo na hatujui pengine ni kwanini tunapenda kuwa hivyo. Nimeweka mifano ya matendo au tabia mbaya haimaanishi kuwa kwa zile tabia nzuri haupaswi kujiuliza swali la kwanini bali nazo unapaswa kujiuliza lakini nimeweka tabia hizo kwasababu inawezekana ndizo zinazotusumbua sana wengi wetu na kutufanya tusiweze kusonga mbele hivyo basi kwa kujiulia swali kwanini tunaweza kupata majibu ambayo yatatusaidia kufanya  uamuzi wa ni namna gani tunaweza kuziacha tabia hizo mbaya.
Kwa ile nzuri tunapaswa kuwa na majibu pia ya kwanini tunafanya hivyo kwa sababu kuna muda tabia au matendo yetu mazuri yanaweza kuwafurahisha watu hivyo wakaja kutuomba ushauri lakini  hii ikiwa ni katika hali ya kutaka kujifunza kutoka kwetu wanaweza kutuuliza swali la kwanini tunafanya hivyo. Mfano unapenda sana kujisomea vitabu mbalimbali unaweza kuulizwa kwanini unafanya hivyo?, swali hili litakuwa jepesi ikiwa ulishatangulia kujijibu mwenyewe kwamba kwanini unafanya kitu husika. Lakini kama hukuwahi kufanya hivyo itakusumbua sana.
Naamini kuwa kila jambo lina sababu yake ya kufanyika hivyo kwa kila unalolifanya tafuta sababu ya wewe kufanya hivyo haijalishi jambo hilo ni zuri au ni baya jambo la msingi kwako ni kujiuliza tu kwanini unafanya hivyo ili kuiamusha akili yako ambapo kwa lile jambo zuri itaamuka na kulifanya zaidi na zaidi na hivyo utapiga hatua kubwa sana katika hilo.
Ewe ulie mwalimu, dereva, daktari, kondakita, mjasiriamali, mchungaji, nesi, padre, sheikh, msanii, mwinjilisti, mlokole, mpagani, mchawi, mfanyabiashara, muongo, mzinzi, mlevi, mwamasishaji, mwandishi, mcheza soko, mwajiliwa n.k. ulishawahi kujiuliza kwanini unafanya au umechagua hilo unalolifanya sasa?.
Ni mimi rafiki yako
Baraka maganga.

0754612413/0652612410.

Monday, December 21, 2015

Hakuna Uhusiano Wa Moja Kwa Moja Kati Ya Vitu Hivi Viwili.


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vyema katika harakati zako za kuhakikisha unayatekeleza yale ambayo umekwisha jiweke na ukizingatia kuwa mwaka ndio huo uko ukingoni.
Leo nataka kukushirikisha juu ya jambo hili nalo ni kukosekana kwa uhusiano wa moja kwa moja kati ya elimu ya darasani na mafanikio, hii ni kutokana na sababu kuwa kuna watu ambao wamekuwa wakiamini kuwa ili wafanikiwe ni lazima wae na elimu ya darasani. Yaani kwao wao ni kuwa ili mtu aweze kufanikiwa ni lazima awe amesoma sana na angalau awe na elimu ya degree au masters hapo ndipo atafanikiwa.Jambo hili limeshamili sana miongoni mwa jamii nyingi sana hapa kwetu Tanzania ndio maana leo hii msisitizo kwa wazazi kwa watoto wao ni kuwa soma sana mwanangu ili uje kuwa na maisha mazuri na yenye mafanikio. Kwa wazazi wengi hapa nchini kwetu ni kuwa mafanikio hutokana na kusoma na kuwa na degree au masters. Yaani msisitizo wao mkubwa ni katika elimu ya darasani ambayo itakufanya uajilliwe na katika ajira, ajira hutolewa kutokana na elimu ya mtu, yaani mwenye elimu ya juu ndiye hupewa ajira yenye mshara mkubwa na kwa kuwa tunaamini kuwa mshara mkubwa ndio hukufanya uwe na pesa na kwa kuwa wengi wetu hupima mafanikio kwawingi wa pesa basi huwa tunaamini katika ajira na ajira huja kutokana na elimu yako ndio maana wazazi wamekuwa wakitusisitiza juu ya elimu ya darasani.
Lakini ndugu msomaji wa makala hii nataka ujiulize kama kweli unaamini kuwa mafanikio hutokana na elimu ya darasani je ni wangapi ambao pamoja na masters zao na degree zao lakini bado ni masikini?, hawana mafanikio yoyote yaani ila wanaringia elimu zao za darasani?. Jibu nadhani ni wengi, sasa kama ni wengi huo uhusiano unatoka wapi wa kukufanya wewe uamini kuwa mafanikio ya kweli hutokana na elimu ya darasani pekee?. kama elimu ya darasani ndio kigezo cha mafanikio ya watu je nani angekataa kusoma mpaka kupata hizo degree na masters?, maana hakuna asiyependa mafanikio.
Na jiulize tena ni wangapi ambao pamoja na kutokuwa na elimu ya darasani lakini wanamafanikio makubwa sana na nimatajiri wakubwa duniani?. Mfano ni tajiri Bill gate ambaye aliachana na habari za shule na kuamua kujifundisha mwenyewe na kisha kugundua program ya Microsoft katika computer. Matajiri wangapi au wafanyabiashara wangapi unaowajua hapo mtaani hawana elimu ya darasani lakini ndio matajiri wakubwa.
Utamaduni wa kuwasisitiza watoto au ndugu zetu kusoma sana ili kupata maksi nzuri darasani na baadae kupata ufaulu wa juu kisha wapate kulipwa kutokana na elimu zao ni utamaduni wa zana za kale za mawe sio utamaduni muhimu katika ulimwengu wa sasa wa taarifa. Ulimwengu wa sasa hausemi kuwa mwenye elimu ndiye atakaye fanikiwa bali unasema kuwa mwenye taarifa sahihi ndiye atakaye fanikiwa.  Yaani utofauti wa taarifa ya kitu fulani kati yako na mtu mwingine ndio utaamua nani afanikiwe. Utaratibu wa kasome mwanangu ili uje kuwa na maisha mazuri kutokana na ajira yako ni utaratibu ambao umepitwa na wakati sasa. Na kwa mujibu wa mwandishi mashuhuru wa marekani bwana Robert Kiyosaki huu ni utaratibu mbovu yeye anasema kuwa kitakachomfanya mtu afanikiwe ni elimu juu ya pesa na elimu hii haifundishwi shuleni badala yake mtu anatakiwa ajifunze kutoka kwa wazazi wake. Mwandishi huyu anasisitiza katika umuhimu wa elimu juu ya fedha maana haifundishwi darasani na ndio maana hata wenye degree na masters zao wanakuwa masikini na waliokosa mafanikio.
Sisemi kuwa elimu ya darasani sio elimu ya msingi, ni elimu ya msingi sana tena sana kwa ulimwengu wa leo ambao umejaa ushindani sana ambapo ni muhimu kwa mtu kupata angalau degree hata moja, nachopinga ni kuwa elimu hii isitumiwe kama tiketi ya kufanikiwa yaani kwana kwamba mwenye elimu ya darasani ndiye mwenye uhalali wa kufanikiwa hili ndilo nilipingalo maana kuna watu ambao wana elimu na wanamafanikio na wakati huo huo kuna wale wenye elimu hiyo na hawana mafanikio, na kwa upande wa pili wa shilingi kuna wasio na elimu na wanamafanikio na hapo hapo kuna watu ambao hawana elimu na hawajafanikiwa.
Kinachohitajika katika mafanikio ni namna ya kujifunza kupitia watu waliofananikiwa na kutumia mafanikio yao kama somo na sio kitu kingine. Elimu ya darasani ni kichocheo tu ambacho peke yake hakiwezi kufanya kazi. Hivyo usikae kisa huna elimu ya darasani na ukasema huwezi kufanikiwa. Pia jifunze kuhusu elimu ya pesa maana ndio muhimu sana kwa ulimwengu wa sasa.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.

0754612413/0652612410.

Friday, December 18, 2015

Kitu Hiki Kimoja Kinakufanya Usifanikiwe Maishani.


Habari ya leo na wakati huu ndugu msomaji wa mtandao Huu wa kona ya maarifa, ni matumaini yangu Kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vizuri katika kutekeleza majukumu yako ya kila Siku.
Leo nataka kukushirikisha jambo muhimu ambalo wengi wetu tumekuwa tukilifanya, lakini limekuwa likitulete madhara makubwa sana jambo lenyewe ni  Kukata tamaa. Tumekuwa tukijijengea tabia hii Mara kwa Mara na wengine tumefikia kiasi cha kuhararisha tabia hii na kuifanya kama sifa fulani yaani kuna watu wanaona Kuwa ni fahari kwao wao kukata Tamaa, na wana haki ya kufanya hivyo.
Nataka ujiulize maswali haya muhimu (1) je unauhakika hapo ulipofika ndio mwisho wa uwezo wako mpaka unakata tamaa? (2) je wewe pekee ndiye wa kwanza kupitia mikasa hiyo? (3) je umefanya juhudi gani kutatua tatizo hilo? (4) je umewaona wataalamu na je wataalamu hao ndio wa mwisho duniani?. Maswali yanaweza kuwa mengi sana lakini hayo ni baadhi tu ya maswali mengi ambayo inabidi ujiulize. Kuna watu ambao binafsi huwa wananisikitisha sana watu Hawa ni wa aina mbili ambao nambari Moja ni wale ambao hufanya Mara moja na kukata Tamaa bila kujaribu Mara ya pili. Na watu wa aina ya pili ni wale ambao wanakata tamaa bila hata kujaribu. Yaani Hawa ni wale mabingwa wa kutumia historia za watu walioshindwa tu bila kujua kuwa katika yale ambayo wengine wameshindwa kuna wengine wamefanikiwa katika hayo hayo. Hawa ni wale ambao wamejaa mtizamo hasi na kawaida yao ni kutazama upande mmoja wa shilingi. Yaani wao huwa wanaangalia mabaya tu, kwa sababu mawazoni mwao wanawaza ubaya tu.
Pengine nikujuze sababu kadhaa ambazo zinaweza kukufanya ukawa na tabia hii ya kukata tamaa. Sababu hizo ni pamoja na;-
1. Kuamini kuwa maishani kuna njia ya mkato ya kuelekea mafanikio, wapo watu ambao wamejaza bongo Zao na fikira kuwa maishani kuna njia ya mkato ya kuelekea mafanikio. Sasa watu kama hawa pindi waanzishapo safari ya kuelekea mafanikio ndipo hukumbuka kuwa yale mawazo yao yalikuwa ya uongo tu maana kwa hakika maishani hakuna njia ya mkato, na hapo ndipo huwa wanakata tamaa kabisa maishani.
2. Kukosa uvumilivu, kuna watu amabao sio wavumilivu kabisa, hawa ni wale wenye kupenda mafanikio ya haraka haraka hivyo wanapokuja kugundua kuwa mafanikio hayahitaji haraka kiasi hicho hukata tamaa mapema.
3. Mtu asiyetambua neno hasara, kuna watu ambao Hawatambui kama kuna kitu hasara hasa katika biashara wao huamini na kujua Kuwa biashara ina faida tu sasa watu kama hawa wapatapo hasara huwa ni wepesi sana wa kukata tamaa maana hawakukijua hicho kitu wala kujiandaa nacho hapo kabla.
4. Kukosa malengo, kuna watu ambao hawana utamaduni wa kujiwekea malengo binafsi, hivyo wao huishi kwa kutangatanga yaani wao huamia shughuli moja kwenda nyingine maana hawana malengo na ndio maana hukata tamaa. Ukiwa na utamaduni wa kujiwekea malengo na kuyasimamia ili kuyatekeleza kamwe huwezi kukata tamaa.
5. Kutumia historia za watu vibaya, Watu wanaokata tamaa ni wale wenye kuzitumia historia za watu kimakosa. Siamini kama kweli historia za watu zipo ili zitutishe bali naamini kuwa historia za watu zipo ili zitufunze. Hata katika historia ya mtu aliyefanikiwa kuna anaeweza kujifunza vitu toka kwake na akakata Tamaa. Hivyo basi usiruhusu historia ya mtu mwingine iamue maisha yako na kukufanya ukate tamaa.
Ukitawaliwa na tabia ya kukata tamaa sahau kuhusu mafanikio ukiwa mtu wa kukata tamaa kamwe huwezi fanikiwa hata ufanyaje maana mafanikio huitaji uvumilivu na kuto kata tamaa mapema.
Rafiki yako,
Baraka Maganga.
Bmaganga22@gmail.com.
0754612413/0652612410.


Thursday, December 17, 2015

Zifahamu Sumu Nne (4) Za Mafanikio Yako.


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vizuri katika harakati zako za kutekeleza majukumu yako na hatimaye kuzifikia ndoto zako.
Wengi tumekuwa tukiimba wimbo mafanikio mara kwa mara, lakini jiulize ni wangapi waimbao wimbo huu wanafanikiwa? Nadhani jibu ni wachache kati ya wengia ambao wanaimba wimbo huu wa mafanikio ambao wanafanikiwa kweli. Sababu za kutokufanikiwa zinaweza kuwa nyingi sana miongoni mwetu. Hapa nina kuletea sumu nne za mafanikio, yaani vitu vinne ambavyo vinaweza kuhatarisha mafanikio iwe umeyapata tayari, au ndio unaelekea kuyapata.
1 .lawama, hii ni sumu nambari moja ya mafanikio, ukijiona wewe ni mtu wa kulaumu mara kwa mara jua kuwa huwezi kufanuikiwa au kwa lugha rahisi ni kuwa jua kuwa mafanikio yatakukimbia. Ukiwa wewe ni mtu wa kuilaumu serikali, wazazi, waalimu, wanafunzi wenzako, mpenzi wako au mkeo/mumeo, tambua kuwa hutoweza kufanikiwa. Lawama hukuondoa katika mafanikio au katika mstari wa kuyapata mafanikio kwa kuwa  lawama inakufanya uyakimbie majukumu. Yaani tabia ya mtu anayelaumu ni kuwa huwa anawalaumu watu hata kwa yale ambayo yanamhusu yeye moja kwa moja. Mfano mwanafunzi hajasoma vizuri kwa ajili ya mtihani wake wa mwisho lakini akilini mwake anawazo la kufaulu, inapotokea amefeli huanza kuwalaumu waalimu kuwa hawakufundisha ipasavyo.
2.  visingizio, huyu ni pacha wa lawama, kwanini nimesema hivyo ni kwa kuwa lawama na visingizio vinaendana kimatendo na kitabia. Yaani wakati mwingine huwa ni vigumu sana kutofautisha mtu mwenye kulaumu na mtu mwenye visingizio. Wakati yule wa kulaumu anawalaumu watu basi yule wa visingizio huwasingizia watu. Yaani mfano katika mfano wetu hapo juu wa mwanafunzi aliyefeli kuwalaumu waalimu, basi hapa atawasingizia waalimu kuwa hawakufundisha vizuri ndio maana akafeli wakati sio. Watu wengi wamekuwa wakiwasingizia watu wengi sana juu ya kutokufanikiwa kwao wapo wanaowasingizia wazazi, waalimu, madaktari, serikali n.k. lakini ukiwachunguza watu hawa utagundua kuwa kadri wanavyosingizia ndivyo wanavyojiweka mbali na mafanikio. Hivyo basi achana na habari za kusingizia singizia. Kama ulikuwa hujui basi faha,u kuwa visingizio pia hutuondelea uwezo wa kufikiri na kutufanya tushindwe hata kutatua matatizo madogo na badala yake tusingizie tu watu wengine. Hivyo acha kabisa tabia hii.
3. hofu, sumu nyingine ya mafanikio ni hofu, mara nyingi watu wamekuwa na mipango na mawazo makubwa sana ambayo yanaweza kuwafanya wakafanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini punde tu watakapo kujalibu kutekeleza mipango yao na malengo yao, hofu huja na kupeperusha mipango na malengo yao na huo ndio huwa mwisho wao. Anza kwa kupinga hofu mara moja kama kweli unataka kufanikiwa. Utakapoweza kujikwamua katika mtego huu wa hofu basi mafanikio yatakuwa halali yako. Hofu itakukosesha mambo mengi kama ukiiruhusu ikutawale, na njia moja wapo ya kukabiliana na hofu ni kufanya kile ambacho unakiuogopa zaidi kuliko vingine.
4.Kuhairisha mambo,jiulize leo hii ni mara ngapi umekuwa ukitaka kujihusiha na jambo fulani, tena la msingi na ambalo lina tija kwako, lakini ghafla ukatishwa tu kidogo au ukaingiwa na hofu kidogo na matokeo yake unaacha kulifanya jambo hilo husika. Leo hii watu wengi wamekuwa wakibaki pale pale walipo kwa kuwa wametawaliwa na tabia ya kuhairisha mambo. Kama kweli unataka kufanikiwa hakikisha unaipinga vikali tabia hii kwani kuhairisha mambo ni hatari sana kwa maendeleo yako. Wapo watu wengi ambao wamekuwa wakiona ufahari kuhairisha mambo yao ya msingi, na wasijue kuwa wanajiua wenyewe alafu baadae huanza kuwalaumu na kuwasingizia watu wengine kumbe sababu ni kuwa watu hawa wametawaliwa na roho ya kuhairisha mambo. Ndio maana siku hizi kuna msemo maarufu huko mtaani kuwa “watu wengi wanakufa na ndoto zao, hivyo ndoto nyingi zipo makaburini”, ni kwasababu ya tabia ya kuhairisha mambo.
Kwa ujumla sumu hizi nne za mafanikio, zinaweza kutokana na sisi wenyewe au kutokana na wale wanatuzunguka. Hilo lisikupe shida bali jambo la msingi ni kuwa wewe pingana nazo kwa kuwa umeshazifahamu vizuri na madhara yake pia umeyafahamu.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.

0754612413/0652612410.

Monday, December 14, 2015

Anza Na Kitu Hiki Kimoja Kama Kweli Unataka Kufanikiwa.


Habari ya siku ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vizuri na majukumu ya hapa na pale, yote haya  ni katika kuhakikisha kuwa unapata kuyatimiza yale ambayo umekwisha kuyaweka kama malengo yako na  mwisho wa siku unapata mafanikio ambayo umekuwa ukiyatafuta kwa nguvu. Baada ya kuwa kimya kwa siku mbili tatu hivi kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wangu, naomba tureje na kuweza kuendelea kupeana maarifa ya hapa na pale.
Katika makala ya leo nataka kukushirikisha juu ya jambo moja,Jambo lenyewe ni umuhimu wa kuanza kuheshimu vitu vidogovidogo. Nimeamua kuandika juu ya jambo hili ili kuweza kukunasua  katika mtego huu ambao unawaangamiza watu wengi. Ndugu msomaji wa mtandao huu nataka nikusihi kwamba kwanzia leo jenga tabia hii muhimu ambayo ni ya kuheshimu vitu vidogovidogo.

Nataka ujenge tabia hii kwa kuwa itakufanya ufanikiwe zaidi. Kwanini jambo hili litakuifanya ufanikiwe ni kwa sababu vitu vidogo ndivyo huwa vinavijenga vitu vikubwa. Chukulia mfano wa nyumba, nyumba haiwi nyumba bila msingi sasa kwa hesabu za kawaida ukichukulia kigezo cha ukubwa kimsingi,msingi wa nyumba ni mkubwa kuliko nyumba, lakini ukweli ni kwamba nyumba haiwi nyumba bila msingi. Hivyo ili ujenge nyumba lazima uanze na msingi bila msingi hakuna nyumba hivyo basi kwa kutumia mfano huu wa nyumba jenga tabia ya kuvithamini vitu vidogovidogo.

Leo hii kuonesha ni jinsi gani watu hawathamini vitu vidogo utamsikia mtu akikuambia siwezi kufanya biashara fulani kwa sababu nina pesa chache ambayo haiwezi kunifanya nianzishe biashara hiyo husika, leo hii watu wamekuwa wakisubiri kupata milioni kadhaa ndio waanzishe biashara zao hizo wanazo zifikiria, lakini cha ajabu ni kuwa wamekuwa wakisubiri kwa miaka kadhaa na wasipate hizo milioni za kuanzisha biashara zao husika. Kumbuka kuwa huwezi kufika kumi bila kuanza na moja. Hivyo kama unataka kufika kumi lazima upitie moja, mbili, tatu na kuendelea ndipo utafika kumi. Hivyo hata kama unataka kufanya biashar ya mamilioni anza hata na maelfu yatakuwa na baadae itafika hiyo milioni hakuna namna nyingine. Usiendelee kusubiri kupata milioni wakati hauthamini pesa ndogo ambayo itakufanya ufike kwenye mamilioni.
Kudharau vitu vidogovidogo kumewaponza watu wengi sana na kuwafanya wabaki pale pale na wasipige hatua yoyote ile ya kimaendeleo. Leo hii watu hawawezi kujiwekea akiba ya pesa,kwa kuwa hawathamini pesa ndogondogo. Leo hii mtu huona shilingi mia moja ni kama pesa ya kuchezea tu maana ni ndogo na hawezi kuifanyia chochote. Kama unatabia hii acha mara moja maana itakugharimu sio muda. Kuna msemo wa Kiswahili usemao “mazoea hujenga tabia”. Hivyo basi kama huwezi kuthamini pesa ndogo kama shilingi mia uwapo na wazo la elfu kumi,vivyo hivyo huto weza kuja kuithamini shilingi elfu kumi ukiwa na wazo la milioni, hii ni kwa sababu usha jijengea tabia ya kuto kuthamini vitu vidogo huko nyuma.
Wapo watu ambao wamevithamini vitu vidogo na matokeo yake wakapata mafanikio makubwa, kuna mifano ya watu ambao waliamua kuanzisha biashara zao wakiwa na mitaji midogo sana ambayo hata wakikuambia leo hii utawaona kama waongo wenye lengo la kukudanganya tu, lakini ukweli ni kuwa watu hawa walielewa umuhimu wa kuvithamini vitu vidogo ndio maana wakaamua kuanzisha biashara zao japo kuwa walikuwa na mitaji midogo na matokeo yake ni kuwa walifanikiwa sana maishani mwao, hivyo jifunze kupitia watu hao ambao wamefanikiwa.
Kama kweli unataka kufanikiwa basi jenga tabia ya kuvithamini vitu vidogo maana hivyo ndivyo huleta mafananikio makubwa kumbuka mfano wa punje moja ya mhindi ambayo hufukiwa ardhini na baadae huzaa punje nyingi ambazo hutumika kama chakula cha kuwasaidia watu.
Ni mimi rafiki yako
Baraka Maganga.

0754612413/0652612410.

Monday, December 7, 2015

Lini Basi Itakuwa Zamu Yako?


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na mwenye kiu ya kuendeleza harakati za kuyasaka mafanikio. Nami nakusihi endelea na hali hiyo wala usikate tamaa, maana yote yanawezekana tu swala ni imani na juhudi tu ndio zitatufanya tuweze kuyatekeleza yale tuliyojiwekea  kama malengo kwetu.
Ni wasaa mwingine tena ambapotumekutana tena ilikuweza kupeana maarifa mapya ambayo yatatufanya tuwe bora na hatimaye kuweza kuyafanikisha yale tuliyojiwekea. Leo kuna swali moja ambalo nataka ujiulize ndugu msomaji wa makala hii, swali lenyewe ni kuwa ni lini haswa itakuwa zamu yako?. Nataka ufanye hivyo kwa kuwa naamini kuwa akili ya binadamu huanza kufanya kazi pale inapochochewa kufikiri juu ya jambo fulani tofauti na pale inapokuwa imekaa tu bila kuchochewa kufanya jambo lolote.Umekuwa ukiona wenzio wakifanikiwa katika biashara zao, miradi yao, kazi zao, elimu zao n.k. nachotaka kumaanisha hapa ni kuwa katika kila ngazi ambayo upo wewe sio wa kwanza yaani kuna watu ambao wamekutangulia katika kufanya jambo fulani. Kama wewe ni mfanyabiashara kuna wafanyabiashara maarufu na wakubwa zaidi yako, mchezaji, mwanafunzi, mfanyakazi n.k. wapo walio juu yako sasa tunaelewa kuwa mtu anapokuwa amefanya mambo makubwa naya msingi huwa anakuwa anasifika, anapewa heshima kubwa, anachukuliwa kama mfano wa kuigwa n.k. najua vitu hivyo huwa unakutana navyo katika maisha yako. Sasa ulishawahi kujiuliza kuwa ni lini nawe itakuwa zamu yako kusifika au kusifiwa kwa jambo fulani,au kutumiwa kama mfano wa kuigwa?.
Kila mtu maishani huwa kunakuwa mtu mwenye mafanikio ambaye yeye huvutiwa nae mfano mchezaji chipukizi wa Tanzania anaweza kuvutiwa na kiwango cha Mbwana Samtta na akatamanikuwa kama yeye sasa jambo la msingi la kujiuliza ni kuwa ni lini unataka kuwa kama huyo Mbwana Samatta. Pengine unatamani kuwa mfanyabiashara mkubwa na mwekezaji mkubwa na mashuhuri kama Reginald Mengi, lakini hujui ni lini na nivipi utakuwa kama yeye, sasa jambo unalotakiwa kujiuliza nikuwa ni lini utakuwa kama mengi?. Pengine unatamani kuwa mchekeshaji maarufu kama Masanja Mkandamizaji wa orijino komedi, unachotakiwa kufanya ni kujiuliza tu ni lini haswa unataka kuwa hivyo?
Nimeshakwisha kutangulia kusema hapo awali kuwa akili ya binadamu hufanya kazi pale inapoulizwa maswali kama vile kivipi?, kwanini?, wapi?, saa ngapi? Na memgine mengi kulikopale inapokuwa imeachiwa tu na kukaa tu huru, bila kufanya kazi yoyote. Kwa kuwa akili ya binadamu hufanya kazi au huwa katika hali ya kufanya kazi pale inapokuwa inaulizwa maswali mbalimbali kuliko pale ambapo haiulizwi maswli hivyo basi jijengee mazoea ya kujiuliza maswali mbalimbali kila wakatiili tu kuhakikisha unapata majibu ambayo yatakuwa msaada mkubwa kwako na kukupa uvumbuzi wa majibu ya changamoto zako.
Pili nataka ujiulize swali la ni lini haswa itakuwa zamu yako ili majibu ya maswali yako uyatumie katika kupanga malengo yako. Watu wengi wamekuwa hawapangi malengo yao kwa kuwa wamekuwa hawajiulizi maswali mbalimbali ukijiuliza swali mfano ni lini unataka kuwa mfanyabiashara maarufu na ukajijibu kuwa  mwezi mei 2017, hili litakuwa tayari kama lengo lako ambapo utaifanya akili yako ifanye kazi ili kuhakikisha jambo hili linakuwa ukweli kwako na hatimaye kulitekeleza.
Ni muhimu kujiuliza maswali mbalimbali juu ya ni lini unataka kupata kitu Fulani na ni lini utakuwa mtu Fulani. Jingine kujiuliza swali ni lini haswa itakuwa zamu yako, kujulikana, kusifiwa na kutumika kamamfano wa kuigwa?, kutaiamusha akili yako na kuifanya ifanye kazi ya kukupatia majibu.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka maganga,

0754612413/0654612410

Saturday, December 5, 2015

Hiki Ni Kitu Muhimu Sana Kuliko Unavyodhani.

Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu. Ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vizuri na shughuli zako.Leo tena nakupa kitu kipya na kitu hicho ni umuhimu wa hatua moja. Je ulishawahi kufikiria umuhimu wa hatua moja? Basi endelea kusoma makala hii ili uweze kuufahamu umuhimu wa hatua moja.
Chukulia mfano ulikuwa unatembea kuelekea mahali usipo kujua katika kutembea huko ukafika sehemu ambapo kuna korongo kubwa sana ambapo ukitumbukia huko hakuna kupona na katika safari yako ilikuwa imebaki hatua moja tu ambayo ungeimalizia tu basi ulikuwa unatumbukia kwenye korongo hilo hivyo basi unamua kutokupiga ile hatua ya mwisho na hapo unakuwa umeokoa maisha yako.
Mfano mwingine, chukulia upo katika mashindano fulani ya mbio ambapo mshindi anapewa zawadi ya gari na nyumba. Ukaingia katika mashindano hayo huku ukiwa na uhakika na shauku ya kushinda hivyo ukaanza mbio hizo kwa kasi sana ukawaacha wapinzani mbali sana,lakini ghafla kabla ya kufika kwenye mstari wa mwisho ambapo ni hatua moja tu ili kufika mwisho ukaanguka vibaya sana na ikawa ngumu sana kwa wewe kuinuka, lakini kumbuka ni hatua moja tu ndio ilikuwa imebakia basi kwa kutambua hilo unajikakamua pamoja na maumivu yako unainuka na kumaliza mbio wa kwanza na hivyo kutangazwa mshindi na kujishindia zawadi. Jiulize ingekuwaje kama usinge jikakamua na kumalizia ile hatua moja.
Nimekuwekea mifano miwili ambapo mfano wa kwanza unaonesha umuhimu wa kupunguza hatua ili kuokoa maisha yetu. Inawezekana umekuwa ukifanya mambo mengi sana, sasa chagua jambo moja kati ya mambo mengi unayofanya na ulishikilie hilo mpaka ulikamilishe. Pia mfano huo unatuonesha na kutufunza kuwa ni muhimu tuyachunguze maisha yetu ili tuweze kubaini vikwazo vya ndoto zetu na tuvitoe.
Mfano wa pili unatuonesha kuwa tunaweza kukutana na vikwazo mbalimbali maishani ambavyo vinaweza kusababisha tusiyafikirie malengo yetu na hivyo kushindwa kabisa kuyatekeleza malengo yetu. Vikwazo hivyo ni kama kushindwa, kukata tamaa, hasara katika biashara, uvivu n.k. hivyo basi mfano huu unatuonesha kuwa pamoja na vikwazo vyote sisi tusonge mbele tu tusirudi nyuma kamwe.
Hatua moja ni muhimu iwe kwa kuiongeza au kuipunguza, hivyo jifunze wapi pa kuongeza hatua na ni wapi pa kupunguza. Maana hatua moja kati ya nyingi ndio huamua maisha yetu.
Ni Mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.
Bmaganga22@gmail.com.
0754612413/0652612410.

posted from Bloggeroid

Ijue Silaha Muhimu Ya Kutumia Kupambana Katika Safari Yako Ya Mafanikio

.
Habari za siku ya leo mpenzi msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya. Pia matumaini kuwa unaendelea kupambana vikali katika kuhakiukisha kuwa unatimiza yale uliyopanga kuyatekeleza mwaka huu maana mwaka ndio huo uko ukingoni, basi na kusihi endelea kupambana kwa moyo mmoja na wala usikate tama.


 Najua kila mtu anafahamu kuwa mwanajeshi hawezi kuingia uwanja wa vita pasipo kuwa na silaha za kivita au silaha ya kutumia katika vita hiyo. Usishangae kusikia habari ya mwanajeshi maana unaweza kudhani kuwa nimeanza kuongelea habari za vita Fulani lakini mimi sizungumziii vita vya namna ambayo wewe umeanza kuhisi. Vita nayo zungumzia mimi ni vita ya kuyasaka mafanikio, na mwanajeshi anayehitaji silaha au kuwa na silaha ni wewe, ndio ni wewe wala sio mwingine. Wewe ndiye mwanajeshi ambaye ndiye unapambana katika kuhakikisha unapata ushindi katika vita kali ya mafanikio.
Lakini tofauti ya mapambano ya vita vya mafanikio na ile vita nyingine ni kuwa  vita ile nyingine kama ile ya kwanza ya dunia au ya pili, inakuwa na silaha nzito ambazo huwa na lengo la kuwateketeza kabisa maadui. Silaha hizo huwa kama vile bunduki, mabomu, vifaru n.k. unaweza kujiuliza na kuanza kushangaa kuwa inamaana nami nahitaji silaha hizo?, mbona nchi hairuhusu watu wa kawaida kumiliki ovyo hizo silaha?, mbona sina uwezo wa kununua hata moja? N.k. ila nakusihi tulia ndugu msomaji maana safari ya mafanikio haiitaji silaha hizo.
Ingawa silaha hii ya kutumia kupambana katika uwanja wa vita vya mafanikio ina lengo sawa na zile za vita ingine ambayo ni kuwateketeza maadui. Unaweza kujiuliza kuwa sasa maadui hao ni wapi?, mbona siwafahamu?, mbona sijui hata wanakojifisha?,  ntawezaje kupambana nao sasa?. Ndugu msomaji maadui wako  katika vita ni hawa hapa ambao ni, uvivu, hofu(woga), kukata tama, kukosa malengo, kulalamika na kuhairisha mambo. Hapo nadhani ushawajua maadui wa kupambana nao sasa katika hiyo vita yako. Swali lingine ni wanaishi wapi, vizuri lakini jibu ni rahisi maana ulipo wewe nao wapo, kwa maana hii ni kuwa mbona unaishi nao kila siku.
Kwa kuwa ushawajua maadui ni kina nani na ni wapi wanapatikana basi sasa ni wakati wa kuchukua silaha, silaha yenyewe ni uvumilivu. Inawezekana kuna silaha nyingi sana ambazo unazifikiria katika vita yako lakini leo mimi nataka uchukue hii hapa moja na ukapambane vikali katika vita yako hiyo maana naamini kati ya silaha nyingi ambazo zipo hii ni silaha moja muhimu sana. mwanajeshi aendapo katika vita huwa kwanza na imani ya kushinda, baada ya hapo huitaji kuwa wavumilivu wasio wepesi wa kukata tama. Maana kuna mambo mengi sana ambayo atapambana nayo, ikiwa ni pamoja na kukabiliana na kundi kubwa la maadui, pili kushuudia wenzake wakijeruhiwa na kuumia vibaya na pengine kushuhudia maiti nyingi. Lakini pamoja na yote haya mwanajeshi hutakiwa kuvumilia ili aweze kushinda maana anajua akishindwa kuna mawili kifo au kuwa mateka na kufanywa mtumwa katika maisha yake yote.
Hivyo ndivyo ilivyo na kwako katika safari yako ya mafanikio unahitaji kuwa mvumilivu maana utakutana na maadui au kundi kubwa la maadui kama ilivyo kwa mwanajeshi katika vita yoyote ile. Maadui hao ni kama watakao kuvunja moyo, watakao kukatisha tama, uvivu, kuridhika, woga au hofu na kutegemea wengine. Kumbuka tumesema kuwa mwanajeshi hupambana vilivyo katika vita hata kama akikutana na maadui wa aina gani hii ni kwasababu anajua kuwa akishindwa kuna mawili aidha kuwa mateka au kifo. Sasa kwako wewe katika safari ya mafanikio ni kwamba huta kufa ila utabaki kuwa masikini mkubwa, tena masikini wa kutupwa. Hivyo basi katika vita hii hakikisha unapambana kushinda ili usiwe masikini wa kutupwa.
Ndugu msomaji swala la uvumilivu limesisitizwa hata katika maandiko matakatifu (biblia). Ambapo swala la uvumilivu limeonekana katika kitabu cha AYUBU, soma sura ya kwanza na kuendelea utaona jinsi gani ayubu alivumilia mikiki mimiki yote pamoja na kuwa, kuna wakati mkewe alimsihi na kumsisitza amkufuru mungu lakini ayubu alikataa. Soma kitabu cha ayubu ili upate mengi.
Nimekupa silaha moja lakini hii ni silaha kubwa na muhimu ambayo ukiwa nayo maadui kwako watakuwa kama watoto maana utawashinda kila mara na hata wakirudi  wakiwa wamejipanga vipi wewe utashinda tu.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.

0754612413/0652612410.

Friday, December 4, 2015

Vitu vine (4) Muhimu Katika Safari Yako Ya Kuelekea Mafanikio.


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendeleza mapambano ya kuzisaka fursa na kuzitumia na kwa zile ambapo zimekwisha patikana unahakikisha hazikuponyoki kizembe nami nasema kazana kwani mapambano yanaendelea hakuna kuchoka mpaka tutimize malengo yetu.
Leo nataka kukushirkisha mambo manne muhimu ambayo unahitaji kuwa nayo ili kuweza kufanikisha safari yako ya mafanikio. Kama ilivyo katika safari za kawaida ambazo tumekuwa tukisafiri mara kwa mara aidha kwa usafiri wa magari, ndege au meli. Huwa kuna kuwa na vitu ambavyo ndio kama mahitaji ya safari zetu, yaani bila vitu hivyo safari zetu zinaweza kuwa za kusuasua na zenye kukosa mwelekeo. Chukulia mfano leo hii unataka kwenda sehemu alafu huna tiketi ya kukuwezesha kufika huko, nina uhakika safari yako itakuwa ya kusuasua na unaweza usisafiri sidhani kama leo hii unaweza kusafiri kwa basi au ndege pasipo kuwa na nauli. Mambo haya yafuatayo ni muhimu sana katika safari yako ya mafaniko yaani ni kama tiketi katika safari yako. Endelea……..
1. Njozi, ili ufanikiwe unahitaji kuwa na njozi tena si njozi bora njozi bali njozi kubwa njozi itakayokunyima usingizi wakati mwingine . njozi kwa lugha nyingine huitwa ndoto(dream). Njozi ni namna au kadiri unavyoyaona maisha yako na yatakavyokuwa baada ya kipindi Fulani cha maisha mfano,unayaonaje maisha yako baada ya miaka miwili,mitano, kumi au ishirini ijayo mbele. Unajiona kuwa utakuwa unamiliki nini haswa je unaliona gari la ndoto yako ukiwa ndani yake, nyumba, shamba ama viwanja?. Uwezo huo ndio hujulikana kama ndoto na ni muhimu sana katika maisha yako kama kweli unataka kufanikiwa.
2. Elimu, elimu ni kitu cha muhimu sana tena sana, iwe ile ya darasani au ile ya kujiendeleza baada ya ile ya darasani kwa wakati huu ambapo kuna ushindani mkubwa sana katika soko ni bora ukawa na hata degree moja. Elimu ya darasani ni muhimu kwa kuwa itakufungua na kukupa mwanga wa maisha, lakini pia katika dunia ya sasa elimu ya darasani pekee haitoshi kukufanya wewe mwenye mafanikio. Bali elimu hii nyingine ya tofauti na ile ya darasani ina umuhimu mkubwa sana katika ndunia ya sasa ambayo imejaa changamoto nyingi. Kuna semina mbalimbali ambazo zimekuwa zikiendeshwa kuhusu mambo mbalimbali kama vile ujasiriamali na biashara, kuna vitabu mbalimbali vya uhamasishaji,ujasiriamali, uwekezaji, biashara n.k.vile vile kuna  video ambazo unaweza kuzipata youtube ama kununua dvd. yote haya ni katika kuhakikisha unapata elimu ya kile unachokitaka.
3. Afya, hiki ni kitu cha muhimu pengine kuliko vyote kati ya vile ambavyo ntavitaja hapa. Hii nikwa kuwa afya inahusisha uzima wa mwili ambapo uzima wa mwili utakufanya ufanye kazi zako kwa ufanisi mkubwa sana sidhani kama ipo siku ambayo utaweza kufanya shughuli zako kwa kiwango kile ambacho huwa unafanya siku zote ikiwa unaumwa. Hivyo kwa kutambua umuhimu wa afya ya mwili wako basi hakikisha unafuata kanuni za kiafya kama vile kuhakikisha unafanya mazoezi, punguza kula vitu vyenye mafuta mengi, chumvi, sukari n.k. tunza afya ya mwili wako.
4. Muda, hapa ndio penye tatizo maana tumekuwa wapoteza muda wakubwa yaani ni watu ambao hatujui ni namna gani tutautumia muda wetu vizuri na kutufanya tuuone muda huo unatutosha sana lakini cha ajabu sasa matumizi mabovu ya muda yametufanya tuwe mabingwa wa kulalamika kuwa muda haututoshi, lakini wewe unaelalamika kumbuka kuwa mungu hana upendeleo katika jambo lolote lile maana kila mtu tajiri kwa masikini,kipofu kwa kiwete, mvuvi kwa mlinzi wote wanamasaa sawa ambayo ni ishirini na nne (24), sasa katika,masaa haya haya wapo wanaozitimiza ndoto zao na wanaoendelea kulalamika hivyo basi jambo la msingi kwako ni kupangilia mambo yako kwa muda uliopewa na sio kulalamika kuwa muda haukutoshi.
Hayo ni mambo muhimu manne ambayo ukiyafuatilia vyema utapata mafanikio makubwa kuliko unavyodhani.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.
Bmaganga22@gmail.com.
0754612413/0652612410.


Thursday, December 3, 2015

Hili Ndilo Kosa Ambalo Wengi Hulifanya.


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa, ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vizuri katika mapambano yako na kuhakikisha mwisho wa siku unafika kule ulikokuwa unahitaji kufika. Nami nasema usikatetama wala kurudi nyuma kwani mapambano yanaendelea.
Binadamu tumekuwa watu wa kufanya makosa mbalimbali, ambapo mengine huwa tunayatenda ama kwa kujua au kuto kujua. Yote kwa yote ni katika mfumo wa maisha kwa kuwa kuna usemi wa kiingereza usemao “we learn through mistakes and those who never commit mistakes they never learn” ukiwa na maana kuwa tunajifunza kupitia makosa na yule asiyefanya makosa hajifunzi. Nianzie hapa kauli imesema tunajifunza kupitia makosa hii haina maana kuwa ufanye kosa  makusudi alafu useme najifunza. Kauli hii haswa ipo kwa lengo la kutuhamasisha kuwa tuwe watu wa kujaribi tena tusiwe watu wa kuogopa kujaribu kisa tunahofia kushindwa au kufanya makosa maana tunajifunza kupitia makosa.
Ulishawahi kuambiwa kuwa fanya kitu fulani kisha ukatoa jibu kuwa siwezi bila hata kuthubutu kujaribu?, mara ngapi umekuwa ukiwasihi ndugu, jamaa, marafiki na watu wengine wa karibu nawe kuwa wafanye jambo fulani wakakujibu pale pale pasipo hata kufanya tathimini ya kile unachowaambia wakatoa jibu la kuwa hawawezi. Kauli ya siwezi imekuwa kauli maarufu na naiona ikishika kasi sana miongoni mwa watanzania. Na hili ndio kosa ambalo wengi tumekuwa tukilifanya ama kwa kujua au kuto kujua. Kama ulikuwa hujui hili ni kosa leo nakuambia hili ni kosa tena kosa  kubwa sana ambalo unalifanya. Unaweza kujiuliza kivipi si nasema ukweli kuwa siwezi kwa mambo ambayo naamini siwezi au mbona hili kwangu mimi najua haliwezekani ndio maana nimesema siwezi n.k. baada ya hapo ukaongeza na swali kuwa kivipi sasa nasema unafanya kosa?
Uchunguzi unaonesha kuwa miongoni mwa watu wengi wanaosema hawawezi ni wale wenye kukosa hali ya uthubutu yaaani ni wale ambao wao huogopa kufanya jambo fulani kisa tu wamejijengea imani kuwa hawawezi . Mafanikio huja kwa kuziona fursa na kuzitumia sasa kwa kuwa hauna  ule moyo wa uthubutu kila fursa inayokuja wewe unasema huwezi na matokeo yake unaendelea kubaki pale pale bila kufanya lolote zaidi unaendelea kujididimiza kwa kauli yako mbovu ya siwezi. Ki vipi unawezaje kusema hauwezi ikiwa haujajalibu jambo husika? Umewezaje kujua kuwa hauwezi kwa kukaa tu kuliangalia jambo bila kujihusisha nalo kisha ukasema aaa! Jambo hilo siwezi. Nimesema kuwa watu wanaopenda kutumia kauli ya siwezi ni wale wenye kukosa ile hali ya uthubutu yaani wao kwa namna yoyote ile huwa hawataki kujaribu mambo, wao hukaa tu na kusema hawawezi.
Naamini wewe unayesoma makala hizi na kunufaika nazo umeweza kufanya hivyo kwasababu ulithubutubu kujifunza kusoma na pengine kuandika, ndio maana leo hii unauwezo wa kusoma makala hii na nyingine nyingi. Sasa kama ulithubutu kujifunza kusoma na ukaweza na faida zake umeziona na unaendelea kuziona, sasa  kwanini leo hii linapokuja suala la fursa fulani unagoma kuifuata kwa madai kwamba hauwezi. Nani kakuambia huwezi?, Nani kakuaminisha kuwa hauwezi?, Unawezaje kusema hauwezi ikiwa haujajaribu jambo husika?,. Ukijiuliza maswali haya na jibu likawa sijui. Yaani hauna majibu ya ni nani alikuambia huwezi, uliamini vipi hauwezi ikiwa hujajaribu basi jua fika unajidanganya na kujipotezea muda wako.
Jambo la msingi ambalo inabidi ulifahamu ni kuwa akili ya mwanadamu hufanya kazi vizuri pale inapowekwa katika hali ya kufikiri juu ya changamoto zinazokukabili. Akili yako huamka na kuchemka kufanya jambo pindi unapojiuliza maswali kama kivipi ntafanya jambo hili, vile vile akili yako hulala pale ambapo hauifanyi ikafikiri juu ya changamoto zinazokukabili na ndio maana umekuwa bingwa wakauli za siwezi.
 Acha mara moja kutumia kauli ya siwezi hata kwa mambo ambayo hujajaribu, na hata kama ulijaribu ukashindwa wafuate wale waliofanikiwa katika jambo husika ili uwaombe ushauri pengine hautumii njia sahihi katika jambo husika ndio maana unashindwa.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.

0754612413/0652612410.

Wednesday, December 2, 2015

Hii Sio Sababu Sahihi Ya Kutokufanikiwa Kwako.


Habari ya wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa mtandao ambao umejidhatiti katika kuhakikisaha unakupatia maarifa mapya, maarifa ambayo yatakufanya uwe bora na kuweza kuyafikia mafanikio makubwa sana maishani. Tumekutana tena katika kutaka kuelimishana juu ya mambo mbalimbali ambatana name ili ujue leo nimekuletea nini………
Ukizunguka mitaani ukawauliza vijana wengi wanaoshinda vijiweni wakipiga soga badala ya kufanya kazi kuwa kwanini wanafanya hivyo watakuambia hatuna kazi ya kufanya, ukiendelea  kuwauliza kuwa ,mbona kuna biashara nyingi, nanyi hamtaki kuzifanya? utasikia eeh! bwana eeh! hatuna mitaji. Hii ndio imekuwa kauli kubwa sana miongoni mwetu vijana,na hili ndilo lililonisukuma kuandaa makala hii pengine ulishawahi kukutana na kauli kama hii ya tatizo ni mtaji miongoni mwa vijana wengi au pengine nawe ni mojawapo ya watu wanaoitumia na kuiendekeza kauli hii ya tatizo ni mtaji.
Watanzania tumekuwa bendera fuata upepo, usinielewe vibaya  kwa kusema au kutumia kauli hii lakini haina budi kusema maana lazima tuwekane wazi maana ongezeko la kauli kuwa tatizo mtaji ni dhahiri kuwa ni jinsi gani vijana tumekosa fikira za kimapinduzi na badala yake tumekuwa vibendera fuata upepo ambapo ukisikia mwenzio kasema kuwa hajaanzisha jambo Fulani kwa sababu hana mtaji basi nawe unachukulia hivyo hivyo na kujivika sababu hiyo na kuifanya kuwa kama ngao kubwa ya kushindwa kwako katika biashara.
Kwanza jambo ambalo ni baya sana ambalo tumekuwan nalo na kwa kiasi kikubwa tumekuwa nalo ni kuamini kuwa pesa ndio mtaji muhimu katika biashara zetu, jambo hili ni imani potofu sana pamoja na kuwa tumeamini kuwa pesa ndio mtaji wa kwanza ambayo tayari ni imani potofu tuliyo nayo bado tumeendelea kujenga imani potofu juu ya imani potofu ambayo ni kuwa pamoja na kuamini kuwa pesa ndio mtaji nambari moja kwetu bado tumekuwa tukiamini kuwa ili kuanzisha biashara, ufugaji au shughuli za uwekezaji ama kilimo lazima tuwe na mitaji mikubwa yaani pesa nyingi. Leo hii sio ajabu kumkuta  kijana akitaka kuanzisha biashara fulani utakuta anapiga hesabu za mamilioni kama mtaji wakati anaweza kuanzisha biashara husika kwa mtaji hata wa laki moja.
Tabia ya kufikiria pesa nyingi katika uanzishaji wa biashara, kilimo au uwekezaji ndio kimekuwa chanzo kikubwa cha kuanza kwa kauli ya tatizo mtaji. Tumesahau kuwa hatua moja ndio huanzisha safari na ni hatua hiyo hiyo ndiyo umaliza safari ya umbali mrefu. Sio lazima uanze na pesa nyingi sana katika biashara yako au pesa nyingi katika uwekezaji wako. Nina mfano hai wa ndugu yangu ambaye alianza uwekezaji kwa mtaji wa shilingi 25,000, lakini leo hii anamiliki ekari za kutosha za mashamba ya miti ikiwa ni pamoja na usafiri wake binafsi( gari ya kutembelea). Yaani hapa ni rahisi sana kuuelezea mfano huu ni kuwa shilingi elfu 25 ndio iliyo zaa mamilioni. Kwahiyo ndio maana tunasema hatua moja ni muhimu kuliko hatua nyingi ulizotembea au utakazotembea. Kama mtu huyu angeogopa kutumia shilingi elfu 25 leo hii angebaki kulalamika kama wewe kuwa tatizo mtaji na wala leo nisingalimtumia kama mfano katika makala hii.
Ni kweli pesa kwa kiasi kikubwa ndio kila kitu katikashughuli za kilimo, biashara, uwekezaji na maeneo mengine ya kibiashara na kiuzalishaji lakini pesa pekee haitoshi. Je kama pesa pekee haitoshi nini basi kinatakiwa kitangulie kabla ya pesa?.
Kabla ya mtaji wa pesa kuanza mtaji nambari moja ni fikira au wazo/mawazo. Yaani huu ndio mtaji nambari moja ambao kila mtu anao leo hii huwezi kusema eti mtu fulani huwa hafikirii, yaani huo ni upotoshaji maana hakuna mtu ambaye huwa hafikirii. Kila mtu aliumbwa na uwezo huu wa kufikiri, na uwezo wa kufikiri unatofautiana toka kwa mtu hadi mtu na kinachofanya utofautiane ni namna ambayo kila mtu hutumia fikira zake katika kupambana na chagamoto zinazomkabili. Wale ambao hawataki kumiza bongo zao juu ya ni jinsi gani watakabiliana na changamoto za kimaisha ndio hukimbilia kusema pesa ndio mtaji na pamoja na kutambua kuwa pesa ni mtaji bado hao hao hurudi na kusema mtaji ambao ni pesa ni tatizo. Kila kitu huanza kama wazo kisha wazo hilo ndio hugeuzwa na kufanywa au kuleta pesa.  Kuna historia ya dada mmoja ambayo niliisoma katika kitabu fulani yeye alieleza kuwa hakuwa na pesa ya kuanzisha biashara aliyokuwa akiifikiria lakini alikuwa na wazo ambalo ndio mtaji wake, hivyo akashirikisha watu na baadae akapata pesa kwa ajili ya kuanzisha biashara yake hiyo. Mfano huu unatuonesha kuwa tatizo sio mtaji ambao unatufanya tushindwe kuanzisha biashara au shughuli za kilimo, au za uwekezaji bali mawazo yetu mabovu ndio hupelekea hali hiyo. Hivyo kwa kuwa wazo ndio mtaji mkubwa na mtaji huu ukiwa mbovu basi hatutaweza kufanya chochote zaidi ya kulaumu kuwa tatizo ni mtaji.
Usikae na kupiga piga makelele kijiweni kuwa tatizo ni mtaji bali kaa tulia na ufikiri utajikwamua vipi katika changamoto zinazokukabili na kumbuka matatizo hayatatuliwi kwa kukaa kijiweni na kupiga soga badala yake muda unaoutumia kupiga soga utumie katika kusoma vitabu au kufuatilia hadithi za watu waliofanikiwa wa ndani na nje ya nchi.
Ni mimi rafiki yako
Baraka Maganga

0754612413/0652612410.

Tuesday, December 1, 2015

Wafahamu Maadui Watano (5) Wa Mafanikio Yako.


Habari ya siku ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa. Ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya huku ukiwa mwenye hamasa na uliyejithatiti katika kuhakikisha kuwa unasonga mbele katika kuyatekeleza yale ambayo umekwisha kujiwekea kama malengo yako.
Leo tena tumekutana katika kuendelea kupeana mbinu na maarifa ambayo yatatufanya tuweze kuyafikia malengo yetu. Mara nyingi tumekuwa tukishindwa kutekeleza mipango yetu na pindi inapojitokeza hali hii huwa ni wepesi sana wa kuanza kutafuta sababu za kutokufanikiwa kwetu. Jambo baya ambalo tumekuwa tukilifanya ni kuangalia sababu za nje na kusahau sababu za ndani ambazo zimekuwa zikitupelekea kushindwa. Si ajabu kumkuta mtu kashindwa kwa ajili ya uvivu, uzembe, ukosefu wa hamasa kwake lakini anawageukia watu wengine na kuanza kuwashutumu kwa kushindwa kwake. Mara nyingi tabia hii ndio inayotufanya tusifanikiwe maana tunashindwa kugundua chanzo cha matatizo yetu ili tujirekebishe.  Hapa nakuletea maadui watano wa mafanikio yako kama ifuatavyo:-
1) Kuiga watu, kuna watu wanapenda sana kuwaiga wenzao. Kuiga au kumwiga mtu ni ile hali ya kuchukua au kufanya jambo kwa namna ambayo mtu mwingine anaifanya aidha kwa ruhusa(ridhaa) yake au kwa kuiba.Najua wapo watakao ona kuwa nikama nawadaganya hivi naposema kuiga ni adui wa mafaniko yao. Nasema kuiga ni adui wa mafanikio kwa kuzingatia msingi mmoja tu wa uigaji au aina moja ya uigaji ambayo ni ule uigaji wa kuiba. Huu ndio umekuwa ukifanywa na watu wengi yaani ukiona mtu fulani anafanya jambo fulani basi nawe unaanza kulifanya. Mfano umemwona mtu fulani anafanya biashara fulani basi nawe unaanza kuifanya biashara hiyo pengine kichwani mwako umemwiga biashara hiyo ili tu uweze kumwaribia yeye. Nitoe sababu iliyonifanya niseme kuiga ni adui wa mafanikio yako, kuiga kutakuwa adui wa mafanikio yako kwa sababu uigaji unaoufanya unakupunguzia wewe ubunifu na kukufanya usiwe mbunifu bali mtu ambaye anasubiri kutafuniwa alafu yeye ameze kiulaini. Chunguza leo hii, biashara, kazi za maofisini zinasuasua kwa kuwa zimejaa waigaji ambao ubunifu wamekosa kabisa. Chakufanya sasa kama umeyapenda mafanikio ya mtu kajifunze kutoka kwake mwombe akuelekeze hapo utapata vitu Vingi tofauti na pale ambapo wewe unataka uwe unamvizia tu nakufanya mambo yako kama yeye.
2) Kukosa uvumilivu,kabla hujafanikiwa utakumbana na changamoto kadha wa kadha. Safari ya mafanikio imejaa mabonde, mito, milima na vikwazo vya namna mbalimbali atakaye weza kupambana na vikwazo hivi ndiye atakaye yafikia mafanikio. Mafanikio yanahitaji mipango ya muda mrefu je? Upo tayari kuandaa mpango wa miaka kumi mpaka ishirini na kuhakikisha kuwa unakaa nao kwa miaka yote hiyo. Hapa sizungumzii uvumilivu wa muda mchache nazungumzia uvumilivu wa muda mrefu. Uvumilivu ni jambo gumu sana miongoni mwetu, wachache sana ambao wanaweza kuvumilia ndio maana leo hii wengi wamekuwa wakijidanganya kuwa mafanikio yana njia ya mkato jambo ambalo ni gumu sana tena sana. Katika mafanikio hakuna njia ya mkato bali uvumilivu unatakiwa sana tena sana ili kuweza kuyafikia mafanikio husika.
3) Kuambatana na makundi mabovu, makundi kila mtu anayo lakini wangapi tunauhakika kuwa makundi yetu sio mabovu. Kama unataka kujua kundi lako ni bovu au la angalia nini unapata kutoka katika kundi hilo. Je kundi linakusaidia wewe katika kutimiza ndoto yako au malengo yako. Kama jibu ni hapana kwa swali hilo basi jua kuwa kundi hilo ni bovu na halikufai lakini kama jibu ni ndio basi kundi hilo ni bora kwako na endelea nalo. Naposema kundi namaanisha watu ambao umekuwa ukishirikiana nao katika mambo yenu mbalimbali. Watu hawa waweza kuwa marafiki, ndugu au wanajamii wenzako wengine tu.
4) Kukosa mipango, maisha sio kuishi tu bali maisha ni kuishi kwa mipango, usiishi tu kwa kuwa kila ukiamka unaliona jua likichomoza basi unaridhika tu na hali hiyo pia ukiona giza limeanza kutanda unaona ni wakati wa kulala sasa. Hayo sio maisha, maisha ni pale utakapo jihoji na kupata majibu kuwa pale jua litakapo chomoza utafanya nini maana kila tulionapo jua ndipo tunajua kuwa ni siku nyingine sasa weka mipango kuwa kwa kila uitwao leo utafanya nini. Usiishi tu kwasababu kuishi kupo bali ishi kwa sababu unataka kuishi.
5) kukosa midhamu, nidhamu ni ule uwezo au Hali ya kuweza kupanga mambo yako na kuweza kuyasimamia pasipo kushindwa kuyasimamia. Yaani kama ulipanga kufanya jambo fulani alafu ukashindwa kwa sababu zako za uongo na kweli jua dhahiri hauna nidhamu. Mafanikio yanahitaji nidhamu katika kuyatekeleza Yale ambayo umekwisha kujiwekea usiweke tu mipango alafu ukashindwa kuitekeleza. Pindi utakapoweka mipango alafu ukashondwa kuitekeleza huo ni ukosefu wa nidhamu. Ukosefu wa nidhamu utakurudisha nyuma sana katika kuyaelekea mafanikio. Na wengi wetu hatufanikiwi kwa kuwa tumekosa nidhamu yaani hatuwezi kuisimamia mipango yetu ipasavyo.
Mafanikio hayana njia ya mkato na usipende kutafuta sababu za nje za kutokufanikiwa kwako bali chunguza sana mambo yako ya ndani ambayo ndio kikwazo cha mafanikio.
Ni Mimi rafiki yako.
Baraka Maganga.
Bmaganga22@gmail.com
0754612413/0652612410.