Saturday, March 26, 2016

Tabia Moja Muhimu Kwako Wewe Unaetaka Kufanikiwa.

Habari za wakati huu ndugu msomaji wa makala za mtandao huu ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vyema mimi pia naendelea vyema katika mapambano. Turudi katika mada yetu ya leo ambapo nataka kukushirikisha juu ya jambo muhimu ambalo unatakiwa kuwa nalo kama kweli unataka kufanikiwa. Jambo lenyewe ni kuhusu Kuendelea kujifunza. Kama kweli unataka kufanikiwa hakikisha unajijengea tabia hii kuanzia sasa.





Image result for continue learning


Ipo nguvu kubwa sana katika kujifunza  kama kweli unataka kuwa mwenye mafanikio basi hakikisha kuwa unajifunza kila siku. Yaani usikae bila kujifunza katika kila jambo ambalo unalifanya. Uwe mkulima, uwe daktari, uwe mwanafunzi, uwe hakimu uwe nani wewe endelea kujifunza tu. Nakuambia hivyo kwa kuwa takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 40% ya watu wengi duniani huacha kujifunza pindi tu wanapomaliza elimu zao yaa iwe sekondari au chuo, huo ndio huwa mwisho wa kujifunza kwao. Sasa kwa wewe unayetaka kufanikiwa hakikisha kuwa haufanyi makosa katika kujifunza.

Labda unajiuliza kuwa ni vipi sasa unaweza kujifunza, pengine unawaza kuwa  nirudi shule tena au la?, hapana, hapa nakupatia  namna nne ambazo unaweza kuzitumia katika kujifunza tena kwa gharama ndogo kuliko unavyofikiria sasa. Njia hizi ni zifuatazo:-

1.    Kupitia kusafiri, unaweza kujifunza kupitia kusafiri, hii ni kutokana na sababu kuwa wanadamu tunatofautiana kiutamaduni kwa kiasi kikubwa sana, hivyo katika kusafiri kutoka sehemu moja kwenda kwingine kunaweza kukusaidia wewe kubadili  maisha yako kwa kuwa utaweza kujifunza  namna watu wanavyoishi na wanavyofanya vitu tofauti tofauti, hivyo hii inaweza kukusaidia wewe katika kujifunza na hivyo kubadili maisha yako. Unaweza kujifunza namna mpya ya kuendesha shughuli Fulani kutokana na safari uliyosafiri, hii ni kutokana na sababu kuwa umebadilisha mazingira ulikuwapo awali.

2.    Kusoma vitabu, unaweza kutafuta kitabu cha mada ambayo unaitaka vitabu vipo vingi sana swala ni kwako wewe kuamua ni kitabu gani na kinachohusu nini unachotaka kusoma. Kuna vitabu vya kusoma online, kuna vya kununua ambapo kampuni kama vile amazoni zinauza vitabu vya kila namna, pia waweza kuingia google na ukasearch kitabu unachotaka kuhusiana na mada unayotaka na hivyo basi ukapata kujifunza mengi zaidi na zaidi.

   Kusoma magazeti, nakuona unasema magazeti dah, mbona yamejaa habari hasi, habari za kusikitisha, habari za majonzi na simanzi na mengine mengi. Ni kweli kwa hayo unayoyasema lakini sio kweli kuwa magazeti yamejaa mada hasi tu bali hata mada chanya zipo. Kwenye magazeti  kuna makala juu ya mambo kama vile, afya, kilimo n.k. hivyo jambo la kufanya ni kuwa katika gazeti wewe nunua gazeti na fuata taarifa chanya tu. Yaani fata kile ambacho unahisi kimekufanya ununue gazeti, kama umenunua gazetiu kwa ajiri ya kusoma makala za kilimo basi zitafute mahali zilipo kisha soma na achana na mengine.

4.    Kusoma katika blog mbalimbali, hii pia ni njia moja wapo na mabayo inakuwa kwa kasi sana ambayo wewe unayetaka kufanikiwa unaweza kuitumia kwa kiasi kikubwa sana. Leo hii kuna blog nyingi sana ambazo zinatoa mafunzo ya namna mbalimbali, sasa kazi ni kwako wewe kuamua blog gani inakufaa kutokana na mada zake. Blog ni nyingi mno na zinatoa elimu tofauti tofauti hivyo basi hakikisha kuwa unatafuta blog ya kukuwezesha wewe kupata elimu unayota.

Maisha yanabadilika badilika kila siku na pia utaratibu wa uzalishaji, usafirishaji na hata mawasiliano unabadilika kila wakati hivyo ni  bora uwe katika hali ya kujifunza ili tu uwe katika nafasi nzuri ya kujifunza na  hivyo kukabiliana na mabadiliko haya.

Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.
                    :-barua pepe -Bmaganga22@gmail.com.

KARIBU KATIKA DARASA HURU.
Je? unataka kujifunza na kuwa bora zaidi?,Je? unataka usihangamie kwa kukosa maarifa?,Je? unataka kujua namna ya kutatua matatizo na changamoto mbalimbali zinazokukabili?,Je? unakumbana na hali ya kukata tama mara kwa mara?,Je? unashindwa kujiwekea malengo n.k.Kama jibu ndio basi karibu katika darasa huru. Namna ya kujiunga na darasa huru tuma kiasi cha pesa cha shilingi 5000/= kwa namba 0754612413 kwa mpesa (jina. Baraka magama) au 0652612410 kwa tigo pesa. (jina: Baraka maganga). Kiasi hiki ni kwa mwezi mmoja ambapo ukiisha utatakiwa kuchangia tena kiasi hicho hicho. Kisha, tuma namba yako ya simu kwenda namba moja kati ya hizo huku ukiwa umeambatanisha na jina lako kamili kama linavyojitokeza katika m-pesa au tigo pesa. Kumbuka kufanya hivyo huku ukiwa na uhakika kuwa pesa yako imepokelewa na hapo utaunganishwa kwenye kundi la whatsapp ambalo litakuwa na jina la DARASA HURU.
N.B, huduma hii itatolewa kwa njia ya whatsapp, hivyo hakikisha simu yako ina uwezo wa whatsapp ndipo ujiunge ili kuepuka usumbufu.Masomo yataanza tarehe 1/4/2016. Saa tatu kamili usiku.
Barikiwa.
Karibu sana.


Thursday, March 24, 2016

Unashindwa Kwa Sababu Kitu Hiki Kimoja Kimekushinda Kufanya.


Katika maisha tumekuwa tukifanya mambo kadha wa kadha ambayo wakati tukifanya mambo haya huwa tunakuwa na uhakika kuwa mambo hayo ni yenye kutulendea mafanikio makubwa maishani. Lakini kuna wakati huwa tukijikuta tumeshindwa kufanya jambo fulani huwa tunafanya tafakari ya hali ya juu kwa ajili ya kutaka kutambua sababu haswa iliyofanya tusiweze kufanikiwa.  Baada ya kugundua sababu hapa ndipo matatizo huanza na mara nyingi tatizo hili ndilo limekuwa likitufanya tusifanikiwe siku zote.


Unaweza ukashindwa kutekeleza jambo fulani, na baada ya kufanya tathimini ya nini kimekufanya usifanikiwe ukagundua pengine ni kwa sababu uliswhindwa kutumia muda vizuri yaani kuna vitu ambavyo ulivifanya na hatimaye vikawa chanzo cha kukupotezea muda kwa kiasi kikubwa sana na hatimaye ukajikuta umeshindwa  kulitekeleza hilo jambo. Swala la kuwa umeshindwa kutekeleza jambo ulilolipanga kutokana na kufanya mambo ambayo ni kinyume na uliyotakiwa kufanya ili kulitekeleza jambo fulani, umekuja kuligundua baada ya kufanya tathimini ya kina ya nini kimekufanya usifanikishe jambo husikia. Sasa hapa suluhu ya yote haya ni kuyaacha yaende yale mambo yote yanayokupotezea muda lakini hapa ndipo huwa tunafanya makosa makubwa sana maana huwa hatukubali kuyaacha yaende badala yake tunayashikilia tu na hatimaye tunajikuta tumeshindwa zaidi na zaidi. Hivyo basi makala hii inasema unashindwa kwa sababu umeshindwa kuyaacha yaende, hiki ndicho kitu kimoja kinachokufanya usifanikiwe.

Ni vyema ukatambua kuwa maishani usiwe kinganganizi wa mambo yasiyo ya msingi wala maana yoyote kwako badala yake fanya jambo moja tu kwa yale ambayo unahisi kuwa yanakupotezea muda wako kwa kiasi kikubwa au hayana maana maishani mwako basi yaache yaende tu hakuna namna nyingine bali ni kuyaacha yaende tu. Usiwe mtu wa kuhaha huku na huku kuyakumbatia mambo ambayo kimsingi hayana maana. Tumekuwa ni watu wa kushikilia mambo ambayo hayana tija kwetu na mbaya zaidi ni kuwa huwa tunakuwa tunafahamu kabisa kuwa jambo fulani halina tija wala maana kwangu lakini huwa tunaendelea kukomaa nayo tu au zaidi na zaidi yaani tunakomaa nayo tu. Sasa jambo hili ndilo linatufanya tuzidi kushindwa kila mara maishani.

Nyani ni kiumbe ambaye kwa wakati mwingine huonekana ni mjanja sana na ni msumbufu kwa wanadamu, hili kwa wale ambao wanafanya shughuli za kilimo katika maeneo ambayo nyani ni wengi watakuwa wananielewa kirahisi sana, lakini nyani huyu huyu ambaye huonekana mjanja huwa anaponzwa na tabia moja tu nayo ni ile ya kuto kuacha yaende. Kule nchini Brazili wanaowinda nyani hutumia njia rahisi sana ya kumtega nyani, wao huchukua mtego ambao huwa na uwazi sehemu moja ambapo nyani anaweza kupitisha mkono wake, kisha katika lile tundu huwa wanatumbukiza ndizi na kisha kuweka ule mtego pahali fulani. Sasa nyani akija huwa anataka kuchukua ile ndizi, lakini kwa jinsi ambavyo mtego ule ulivyo ni kuwa nyani akishaingiza mkono wake hawezi kutoka akiwa ameshikilia ndizi, nyani hulitambua hilo kuwa hawezi kutoa mkono akiwa na ndizi hivyo aidha aiachie ndizi ili asikamatwe au la. Lakini cha ajabu ni kuwa nyani huyu huendelea kung’ang’ania ndizi husika mpaka wenye mtego hufikia na kuweza kumkamata. Hivyo kinachomponza nyani siku zote ni ile tabia ya kuto acha yaende.
Sasa tabia hii ya nyani ndio hata binadamu tumekuwa nayo mtu utakuta anayafahamu fika madhara ya utumiaji wa pombe kupita kiasi lakini anaendelea, madhara ya uvivu lakini anaendelea, madhara ya kutokuweka malengo lakini anaendelea tu kufanya mambo ambayo yanamfanya asiweke malengo n.k.

Tambua kuwa uwezo wa kushindwa au kushindwa upo mikononi mwako chagua leo kushinda na utashinda tu na chagua leo kutokushinda na hutoshinda kamwe vilevile.

Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.

                    :-barua pepe -Bmaganga22@gmail.com

Wednesday, March 23, 2016

Hii Ndio Siri Ya Kushinda Maishani.


Ni wengi sana tumekuwa tukitaka kushinda maishani yaani kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Ni kweli kila mpambanaji huwa anataka kushinda katika kila pambano analoshiriki na ndio maana kiuhalisia kila binadamu anapenda kufanikiwa na ndio maana kichwa cha makala nimeamua kukiita siri ya kushinda maishani nikiwa nataka kulenga siri ya kufanikiwa maishani.
Tumekuwa ni watu wenye kutaka kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kila mtu anapenda apate mafanikio makubwa, mimi nataka mafanikio, wewe unataka mafanikio na yule anataka mafanikio. Lakini kwanini tumekuwa tukijikuta kila mara tuko pale pale tulipokuwa jana yaani hatuendi mbele hata hatua moja kimaisha. Kila mara tumekuwa watu wa kushindwa hata kama tukijitahidi kupanga mipango muhimu na mizuri lakini wapi huwa tunajikuta tumeshindwa tena na tena.


Je unakumbwa na tatizo hili la kushindwa mara kwa mara pamoja na kwamba umejiwekea malengo, umepanga mikakati ya kutekeleza malengo yako na mengine mengi? Kama jibu ndio karibu nikupe njia rahisi ya kuweza kuepukana na hiyo hali.

Siri ya kushinda ni vitendo. Hii ndio siri kubwa na ambayo ninata uifahamu kwanzia leo kuwa siri ya kushinda ni vitendo. Kwanini nimesema hivyo, nimesema hivyo ni kwa kuwa takwimu zinaonyesha kuwa watu wengi sana wamekuwa au tumekuwa ni mabingwa wa kupanga mipango mizuri, kuweka mikakati kabambe, kuweka malengo mazuri sana ambayo ukiyasoma kwa kiasi kikubwa ni yanavutia sana tena sana, kiasi kwamba kila ukiyasoma yanakuvutia na unayafurahia lakini wakati unafanya hivyo unasahau kitu kimoja kwamba mipango tunayoiweka sio kwa ajili ya kuiweka kwenye makaratasi au kwenye karatasi tu bali tunatakiwa kuifanyia kazi yaani tuweke katika vitendo.

Kila kitu huanza kwa mpango, malengo na mikakati ambayo mara nyingi sana huwa inakuwa imeandikwa kwenye karatasi, wengi tunaweza kufanya hili jambo lakini jambo ambalo linatushinda ni kuhamisha yale yaliyomo katika makaratasi au karatasi na kuyapeleka katika vitendo, hili ndio jambo ambalo linatushinda kwa kiasi kikubwa sana na ndio maana tunashindwa kushinda (kufanikiwa).

Kama sio mtu wa kuchukua hatua ya kutenda kamwe sahau kuhusu kushinda maana huto weza kushinda kamwe maishani, kushinda huja kutokana na kuamua kuweka ile mipango tuliyojiwekea katika vindeo hivyo basi siri ya kushinda ni vitendo. Unatakiwa kutenda na uendelee kutenda bila kuchoka, kuhairisha wala kukata tamaa maana katika matendo ndimo huwa tunapata ushindi.

Mara nyingi tumekuwa tunashindwa kuchukua hatua ya kutenda kutokana na sababu mbalimbali kama vile:-

1.    Kuhisi uvivu pale tunapotaka kutenda, kama unakabiliwa na hii hali basi jua kabisa hiyo hali sio nzuri kwako na inaweza kukuzuia wewe kutenda jambo. Hivyo tambua kuwa hakuna matunda mazuri katika uvivu, yaani uvivu hauzai matunda mazuri hata siku bali huzaa matunda mabovu hivyo uogope uvivu.

2.    Uoga, wakati mwingine pale unapotaka kuchukua hatua ya kutenda unakabiriwa na hali ya kuogopa kuwa watanichukuliaje au ntaonekanaje hali hii inaweza kukufanya usichukue hatua yoyote na hivyo kujikuta umeshindwa kutenda na hatimaye unabaki pale pale.

3.    Hofu, wakati mwingine huwa unakumbwa na hofu pale unapotaka kutenda jambo fulani. Hofu ya kushindwa, hofu ya kuto kujulikana ni mifano wa hofu ambazo zinaweza kukuzuia wewe kuto tenda jambo fulani. Kabiliana na hofu hizi mara moja.

Hakika siri ya mafanikio/ kushinda ni vitendo, kuweka malengo sio mafanikio ila kuyaweka malengo yako katika matendo ndiko huleta mafanikio, kupanga mikakati, na mipango pia hakuleti mafanikio ila kutenda. Hiyo ndio siri niliyopanga kukushirikisha leo hii, natumaini utakwenda kushinda sasa.

Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.
                    :-barua pepe -Bmaganga22@gmail.com.



Mambo Matatu Yanayoweza Kukufanya Usitimize Ndoto Yako.


Kila mtu ana ndoto zake maishani hilo ni swala ambalo naliamini maishani kuwa wewe una ndoto, yule anandoto zake na mimi ninazo za kwangu ambazo kwa kiasi kikubwa sana zinatofautiana sana tena sana. Kwa kuwa ndoto zetu zinatofautia hili ni jambo jema maana hili ndilo hupelekea hata sisi kutofautiana kimaisha na kimatendo. Hivyo sio jambo baya kuwa na tofauti ya ndoto kati yangu mimi na wewe na yule.

Leo nataka nikushirikishe mambo matatu ambayo yanaweza kukufanya ushindwe kutimiza ndoto zako mambo hayo ni kama yafuhatayo.


  Hofu, ile hali ya kuwa na wasiwasi mwingi juu ya lile unalotaka kulifanya inaweza kuwa adui mkubwa sana wa ndoto zako. Najua kuwa unazifahamu aina nyingi sana za hofu, lakini mimi nataka kugusia hofu ya aina moja tu ambayo ni hofu ya kuto kujulikana. Mara ngapi umekuwa kila unapotaka kufanya jambo fulani unasikia ndani yako kuna sauti inakuhamaasisha kuwa nani anakujua wewe hapa mjini nani?, ukisikia sauti hiyo usijidanganye kusema ni malaika wa mungu anakusihi uache, hapana jua hiyo ni hofu. Ni kweli hakuna anayekujua lakini hilo halikuzui wewe kuweza kutekeleza jambo fulani. Kweli hawakujui kwa sababu hujajitambulisha kwao wewe ni nani. Sasa  pengine kupitia lile unalotaka kulifanya ndilo linaloweza kukufanya ufanikiwe kwa kiasi kikubwa na hatimaye ukawa umejitambulisha kuwa wewe ni nani na ukawa usha fahamikia tayari. Sasa kabiliana na hii hofu tenda lile unaloliona ni sahihi na utajulikana tu. Hakuna aliyezaliwa akiwa anajulikana.

2.    Kutaka kuanza na makubwa,umekuwa ni mtu wa kutaka kusubiri eti mpaka uwe na kitu kikubwa ndio uweze kutenda jambo fulani. Ndugu msomaji waswahili walisema “haba na haba hujaza kibaba”. Anza na kidogo wala hata usiogope kuanza na kitu kidogo maana kidogo huzaa kikubwa sasa wewe unaposubiri eti upate kikubwa ndipo utende huko ni kujidanganya na kujipotezea muda na kuendelea kudumaza ndoto yako maana hakuna namna ambayo unaweza kupata kitu kikubwa  bila kupitia kitu kidogo hivyo basi njia ya uhakika ya kukufanya wewe uweze kufanikisha ndoto zako ni kuanza na kidogo siku zote. Hata kama ni biashara unataka kuwa na biashara kubwa sana wewe anza na mtaji hata wa milioni mbili hata kama ndoto yako ni kuwa na biashara ya milioni ishirini na hiyo milioni mbili baada ya muda itajizalisha na kufikia hizo milioni ishirini unazozitaka. Hivyo nakusii usiue ndoto yako kwa kutaka eti kuanza na kikubwa maishani bali wewe anza tu pale unapohisi upo tayari na unachakuanzia hata kama ni kidogo.


3.    Kuto kuwa na maono sahihi, kama unataka kufanikiwa lazima uwe na maono. Maaono ni ile hali ambayo unaweza kuwa unajionea mambo ya mbele kifikira zaidi. Mfano unajionaje wewe baada ya miaka mitano toka leo. Kila mtu ana namna ambayo anajiona atakavyokuwa baaada ya miaka mitano mwingine anaweza kujiona kuwa anakuwa mtu maarufu sana, anakuwa mfanyakazi bora, mjasiriamali mkubwa n.k. hayo ndio maono. Sasa ikitokea huna uwezo wa kuona ndani ya miaka mitano utakuaje basi hii ni njia moja wapo ya kuweza kuua ndoto zako. Maono huwa kama tasirwa/picha mabayo unayaona maisha yako kifikira zaidi. Na maono sio malengo hivyo usijichanganye niliposema labda unajiona kuwa mfanyakazi bora baada ya miaka mitano ukajua ni malengo hapana malengo na maono vinatofautiana. Ingawa maono yanategemea malengo yako na malengo yako yanategemea maono yako. Hivyo basi hakikisha una maono sahihi yaani unauwezo wa kujiona ndani ya miaka mitano utakuaje au utakuwa wapi kimaisha.

Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.
                    :-barua pepe -Bmaganga22@gmail.com.



Monday, March 21, 2016

Jambo Hili Halitakusaidia Lolote Maishani.

Habari za wakati huu ndugu mpendwa msomaji wa  makala za mtandao huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unandelea vizuri katika kupambana zaidi na zaidi ili tu kuhakikisha kuwa unajiletea mafanikio ambayo umeyakusudia maishani. Nami nasema vizuri na endelea kupambana zaidi na zaidi bila kuchoka kwani mafanikio ndio kila kitu ambacho mtu anakitaka maishani hivyo ni haki yako wewe kupambana ili kuhakikisha unayapata mafanikio.



Ni wengi sana ambao tumekuwa tukipigana kwa hali na mali katika kuhakikisha kuwa tunajiletea mafanikio, hili ni jambo ambalo huwa tunalifanya wengi wetu na tumekuwa tukilifanya kwa muda mrefu. Ni vizuri sana  kufanya hivyo binafsi huwa nafarijika sana napowakuta vijana wenzangu wanazungumzia mafanikio na wanapambana ili kujiletea mafanikio kama unafanya hivyo naomba pokea pongezi zangu. Hongera hongera sana.

Leo nataka kuzungumzia swala moja ambalo linaweza kukufanya usifanikiwe na ndio maana kichwa cha makala hii kinasema jambo hili halitakusaidia lolote. Jambo lenyewe ni kuwa na mtazamo hasi juu ya watu waliofanikiwa. Nimeamua kulizungumzia hili kwa kuwa kumekuwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa na mtazamo mbovu juu ya watu waliofanikiwa mfano wanawachukia watu waliofanikiwa, wanawaona kama ni watu wachoyo, wabinafsi, walaghai, wanyanyasaji na wenye tamaa za pesa kuliko watu wengine.
Pengine unasababu zako za kukufanya uwachukulie watu wenye mafanikio kwa namna ambayo unawachukulia hivi sasa, lakini naomba nikuambia haya kuwa kwanza pole sana kwa kuwatazama watu waliofanikiwa katika mtazamo hasi, pili naomba nikuambie kuwa siujali ukubwa wala udogo wa sababu inayokufanya wewe kuwachukia watu waliofanikiwa ila nachotaka kukuambia ni kuwa unachofanya sio sahihi. Sio sahihi kwa sababu haupaswi kufanya hivyo badala yake unatakiwa kuwachukulia watu walio fanikiwa kama darasa na waalimu wako.

Hakika kama unataka kufanikiwa hakikisha kuwa unajenga uhusiano mzuri na walio fanikiwa na kubwa jenga mtazamo chanya juu yao. Waone kuwa ni kama watu ambao ndio nyenzo muhimu ambazo unaweza kuzitumia na ukafanikisha mambo yako kwa kiasi kikubwa. Ukiwachukia watu wenye mafanikio ni dhahiri kuwa hata mafanikio nayo utayachukia, japo unaweza kujifariji kuwa mi nawachukia tu wenye mafanikio ila mafanikio nayapenda huko ni kujidanganya kwa hali ya juu yaani unahisi upo sahihi kwa mwonekano wa nje lakini ndani yake umejiharibia kila kitu.

Wachukulie watu wenye mafanikio kama darasa kwako, wachukulie kama watu ambao unaweza kuwa tumia kama daraja la kuweza kukuvusha wewe toka hapo ulipo na kukupeleka kule unako kutaka. Ukiwa na mtazamo chanya juu ya watu wenye mafanikio  hii itakusaidia wewe kuweza kuwafuata na kuweza kujifunza mambo mengi kutoka kwao tena kwa kiasi kikubwa.


Jambo la msingi ambalo unatakiwa ulijue kuanzia sasa na ulifahamu kwa asilimia zote ni kuwa mafanikio huja kwa kujifunza kutoka kwa walio fanikiwa sasa kama unawachukia watu wenye mafanikio hii inamaanisha nini, hii inamaanisha kuwa hutoweza kujifunza kutoka kwao, na kama ukishindwa kujifunza kutoka kwao maana yake utajifunza kutoka kwa walioshindwa na kama ukijufunza kutoka kwa walioshindwa basi na wewe utashindwa tu.

Hakuna sababu ya kuwachukia waliofanikiwa bali jambo ambalo wewe unatakiwa kufanya ni kuwapenda na kutaka kujifunza zaidi kutoka kwao, hii ndio njia ambayo inaweza kukufanya wewe kuwa mwenye mafanikio makubwa kama wao.

Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Waweza wasiliana nami kwa nambari za simu
0754-61-24-13 au 0652-61-24-10.
Au kwa barua pepe
Bmaganga22@gmail.com