Thursday, January 12, 2017

Fahamu Kuwa Hata Wewe Ni Dereva Mzuri Tu.


Image result for driver clipartNajua unaweza kuwa umeshangazwa kidogo na kichwa cha makala yetu ya leo, lakini usiogope wala kushangaa sana na kuaanza tayari kusema haiwezekani bwana mimi sio dereva. Punguza presha ndugun msomaji na uwe mpole maana taratibu utanielewa. Nasema wewe ni dereva ndio wewe unaesoma makala hii kwa sasa wewe ni dereva, acha kubisha uliza dereva wa nini?.
Kabla sijakujibu nataka nitoe maana ya dereva kwa uelewa wangu, dereva ni mwongozaji wa chombo Fulani inaweza kuwa gari, meli, ndege lakini mwongozaji huyu ambae anajulikana kama dereva huwa ni Yule anaeongoza magari tu hivyo ndivyo ilivyozoeleka lakini ukweli ni kuwa dereva ni mwongozaji wa chombo cha moto. Kazi kubwa ya mwongozaji huyu ni kukifanya chombo kisiende mlama na hatimae kikaleta madhara. Mfano dereva wa gari huwa na kazi ya kuliongoza gari ili kama kabeba abiria wafike salama na kama kabeba mizigo pia ifike salama. Nadhani umenielewa.
Nataka nikujibu sasa swali lako kuwa kwanini  nimekuita dereva na ni dereva wa nini. Wewe ni dereva mzuri na ni dereva mzuri wa maisha yako. Hapo naona tumeanza kuelewana kwanini nasema wewe ni dereva mzuri wa maisha yako, ni kwa kuwa hakuna anaekujua zaidi ya wewe unavyojijua. Achana na ile misemo kuwa namfahamu Yule bwana au bibi fika, hiyo ni misemo ya watu ambao wakati mwingine hawana maana yoyote wewe ndiye unaejifahamu, yaani unajijua uko vipi, ubora na udhaifu wako unaujua wewe na sio kaka, dada, mama, baba, mke au mume. Nakuambia leo sasa kuwa mke wako hawezi kukujua kuliko wewe unavyojijua, na wewe mke mumeo hawezi kukujua kuliko unavyojijua wewe. Ndio maana nakuambia wewe ni dereva mzuri sana wa maisha yako.

Sababu iliyonisukuma kuweza kuandika makala hii ni kutokana na upotoshaji mkubwa sana uliopo miongoni mwa watu haswa sisi vijana maana mimi ni mtu ambae nimekuwa nikiandika sana kuhusu vijana, kuwa tumekuwa na tabia moja ya kuhisi kuwa kuna mtu tunamsubiri aje atuongozee maisha yetu. Yaani sisi tunataka kuwa abiria wa maisha yetu. Yaani tunataka kila kitu tufanyiwe, kila kitu tuletewe kama vile hatujiwezi sasa jambo hili huwa ni hatari sana. Kumbuka dereva ni mwendeshaji wa chombo cha moto hivyo kama ni gari tutasema ni dereva wa gari. Sasa nikisema wewe ni dereva hata kama unaesoma hii makala ni dereva wa gari, bodaboda, na vingine jua udereva wa kwanza ni wa kuendesha maisha yako. Watu wengi wamekuwa sio madereva wa maisha yao na hapa utawakuta aidha wanaendesha maisha ya wenzao au wanakuwa abiria wa maisha yao. Yani wanasubiri kuendeshwa.


 Nachokutaka leo jenga misingi ya maisha yako, yasimamie maisha yako mwenyewe maana hakuna mtu mwenye kuweza kuyasimamia maisha yako wakati nae anayo ya kwake. Nataka uwe na utawala wa maisha yako na sio maisha yako yatawaliwe na mtu fulani au watu fulani, kumbuka nishakuonya toka mwanzao kuwa baba, mama, shangazi, mjomba sijui mume hawezi kuwa dereva wa maisha yako. Chukua hatua mwanzoni mwa mwaka huu uanze kujipanga na kusimamia na kuendesha maisha yako. Huo ndio udereva nao uzungumzia hapa. Usijidanganye hata siku kutaka kuwa abiria wa maisha yako kwani kwa kufanya hivyo huwezi kufanikiwa hata siku moja.
Kila kheri katika kuuanza udereva wako.


 Rafiki Yako
Baraka Maganga

0754612413

No comments:

Post a Comment