Habari ya wakati huu ndugu msomaji wa
makala za mtandao huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vyema
katika kupambana ili kuboresha maisha yako. Karibu tujifunze kwa pamoja mambo
matano ya kutusaidia katika kukuza biashara zetu.
Ubora wa huduma yako, hapa tunahusisha
kiwango cha utoaji wa huduma yako kama ni katika mgahawa mfano tunazingatia
vitu kama vile usafi wa mahali husika na mwonekano kwa ujumla,ikiwa ni pamoja
na mpangilio wa vitu. Kama ni duka jambo la kuzingatia ni mpangilio wa bidhaa
zako zimekaaje kaaje, kama ni baa je mwonekano ukoje na mpangilio wa viti na
namna ya kukaa ukoje, vile vile swala la usalama lazima lizingatiwe hapo.
Maswala kama vile ukalimu kwa wateja, mwonekano wa wahudumu au wafanyakazi kama
utakuwa nao ni muhimu sana na yote haya yanakuwa katika kipengele cha ubora wa
huduma yako. Hivyo hakikisha unazingatia swala hili.
2.
Ubora wa bidhaa zako, hapa tunaangalia
licha ya kuwa na huduma nzuri je? Kile unachouza au kutoa kama huduma kwa
wateja wako kina ubora gani kwa wateja wako?. Ni muhimu sana kuuza bidhaa zenye
ubora kama unataka kuwa mfanyabiashara mkubwa na mwenye kuheshimika na kupendwa
na watu. Epuka uuzaji wa bidhaa feki au zilizokwisha muda wake maana hili
halitakusaidia daima bali siku ikigundulika ndio kutakuwa kufirisika kwako kwa
moja kwa moja na kumbuka muda mwingine unaweza kusababisha madhara makubwa kwa
watumiaji, mfano kwa wale wauzaji wa bidhaa ambazo ni chakula au zinatumika
moja kwa moja kwa binadamu kama chakula au madawa zaweza kusababisha madhara au
hata kifo/vifo hivyo kwa wewe muuzaji zaweza kukusababishia hata kifungo cha
kudumu jera.
3.
Matumizi ya lugha, je ni lugha gani
unatumia kwa wateja wako?, nakusihi jifunze lugha ya biashara usiwe mtu wa
kuongea na wateja kwa kuwafokea au ni kama unawalazimisha badala yake ongea na
mteja ni kama unamnyenyekea vile au kumbembeleza. Kuwa na lugha ya maelewano na
wateja hii itakusaidia kwa kiasi kikubwa sana. Jifunze kumsikiliza mteja hata
pale unapohisi kakukosea au kakudharau wewe jifanye ni kama huelewi hivi swala
tu usipoteze wateja kwa jambo dogo ambalo ungeweza kulizuia kwa kukaa kimya tu.
4.
Ogopa kukosa chenji, wafanyabiashara
wengi sana sasa wamekuwa na mtindo ambao binafsi nauita ni utaratibu mbovu
sana, nao ni ule wa chenji utaijia baadae au muda mwingine anakuambia chenji
sina. Naomba niseme hii tabia inakera sana unakuta mtu ni dereva bodaboda
kakubeba saa sita za usiku au saa kumi na moja alfajiri unamlipa labda
unampatia shilingi elfu kumi anakuambia hana chenji, ukimwambia tunafanyaje
unasikia niachie ila yeye ukimwambia sikulipi utasikia aa mafuta gharama sijui
hesabu ya bosi maneno mengi sana. Ngoja nikuambie kitu wakati mwingine jifunze
kutafuta chenji kabla hujafungua au kuanza biashara yako kama uko karibu na
benki nenda hata benki ukatafute chenji hii itakusaidia maana wateja hawapendi mfanyabiashara
mbabaishaji. Pia hii itakusaidia katika ushindani maana ambae atakosa chenji
siku hiyo kama mteja akikukariri hawezi rudi tena siku nyingine.Wewe mwenye
duka acha maswala ya kusema chenji baadae sijui kesho kama mtu anamatumizi
mengine?
5.
Usikopeshe ili kuonekana mwema, hii
itakusaidia kulinda mtaji wako maana kuna mtu au watu unaweza kuwakopesha
bidhaa za pesa nyingi kiasi kwamba inafika wakati sasa hauwezi hata kuongeza
bidhaa katika biashara yako hii inakuwa hatari, badala yake kuwa na mipaka ya
kukopesha na ili kukusaidia kopesha faida tu ambayo hata ikichelewa kurudi
mtaji utakuwepo wa kununua bidhaa za kiwango kile kile. Hii itakusaidia kulinda
mtaji wako. Hivyo kamwe usikopeshe ili kuonekana mwema machoni pa watu au ili
uonekane mfanyabiashara mwema wakati inakuumiza maana biashara yako hapo
haiwezi kuendelea.
Nakutakia kila la kheri
katika kuboresha biashara yako au kuanzisha biashara yako.
Kama bado hujajipatie
kitabu cha safari ya kuelekea mafanikio basi
hakikisha hukikosi. Namna ya kukipata tuma meseji yenye neno kitabu kwenda
namba 0754612413 kwa njia ya telegram, au whatsapp(hakikisha whatsapp unayotumia ni new version inayosupport
kutuma na kupokea document kama pdf n.k kama sio ingia play store ili kuiupdate)
au pia kwa njia ya email ambayo ni Bmaganga22@gmail.com.
Rafiki yako,
Baraka Maganga
Mawasiliano: 0754612413 au 0652612410. Au barua
pepe-Bmaganga22@gmail.com.
No comments:
Post a Comment