
Wakati ukiwa unapambana nataka nikusisitize na
nikuelekeze juu ya jambo moja nalo ni jambo ambalo limekuwa likitukumba na
kutusumbua sana tulio wengi hapa duniani. Jambo lenyewe ni kuwa na hamasa ya
muda mfupi, tumekuwa tukikumbwa na hali hii ya kuwa na hamasa ya muda mfupi.
Yaani ni watu ambao tumekuwa tukihamasika kwa muda mchache alafu baadae tunajikuta
tumerudi kule kule tulikotoka mwanzo yaani ile hamasa haipo tena. Pengine jambo
hili limekuwa likitufanya tushindwe kufanikiwa kwa muda mrefu na laweza kuwa
likisababishwa na mambo kadha wa kadha.
Ni mara ngapi umekuwa ukitamani sana kufanya jambo fulani
baada ya kutoka katika semina fulani, baada ya kusoma kitabu fulani au baada ya
kusikiliza historia ya mtu fulani mwenye mafanikio, au pengine ni mara ngapi
umekuwa ukipata hamasa baada ya kusikiliza mahubiri au mafunzo ya dini lakini
baada ya muda mfupi unakuta hamasa ile imetoweka kama unakumbwa na tatizo hilo
basi karibu nikupe njia nne za kukufanya ubaki na hamasa muda wote.
1. Jifunze kitu kipya kila siku,
njia ya kwanza ya kukufanya ubaki na hamsa kila siku, kila wakati na kila
dakika ni kwa wewe kuhakikisha kuwa kila siku unajifunza kitu kipya. Hakikisha
toka unaanza siku mpaka umeimaliza umejifunza kitu fulani, iwe katika biashara,
mapishi, kilimo, ufugaji n.k swala wewe hakikisha umejifunza kitu ambacho
mwisho wa siku kitakufanya uweze kutimiza ndoto zako.
2. Fanyia kazi yale unayojifunza,
njia ya pili ya kukufanya ubaki kuwa na hamasa ni kuhakikisha kuwa unayafanyia
kazi yale unayojifunza maana yale mambo kwa namna moja au nyingine ndiyo
yaletayo hamsa kwako hivyo basi hakikisha unayafanyia kazi. Wengi wetu tumekuwa
tukikabiliwa na hali ya kuwa na hamasa ya muda mfupi kwa sababu hatutaki
kuyafanyia kazi yale ambayo tumejifunza. Hakikisha unafanyia kazi yale
uliyojifunza achana na habari za nitaanza kesho.
3. Epuka visingizio,
visingizio ni njia ambayo watu wengi sana huwa tunaitumia kama sababu za
kutufanya tusiweze kufanikisha jambo fulani. Naomba nikionye kuwa epuka
visingizio maana havina msaada wowote kwako. Kama unataka kubaki na hamasa muda
wote epuka zile kauli za sijui nina umri mkubwa au mdogo, nitafanya kesho,
sijasoma, mimi ni mtoto wa kijijini/town n.k. hakikisha unaviepuka kwa kiasi
kikubwa ili ubakie na hamasa yako.
4. Kuwa
mvumilivu, usiwe mtu wa kutaka mambo yafanyike hapo hapo na yatokee hapo hapo,
bali jua kuwa utokeaji wa mambo huwa unatofautiana kwa kiasi kikubwa sana.
Yaani kuna mambo yanahitaji muda mrefu ili yaweze kutokea na kuna mambo
yanhitaji muda mfupi ili yaweze kutokea. Sasa msisistizo wangu upo katika yale
mambo ambayo yanahitaji muda ili kutokea maana haya ndio huondoa hamasa, hivyo
basi kwa yale mambo ambayo yanahitaji muda ili kutokea hakikisha unakuwa
mvumilivu. Hiindio njia pekee itakayokufanya ubakie na hamasa katika mambo ya
aina hiyo.
Rafiki yako
Baraka Maganga
Mawasiliano: 0754612413/0652612410.
JE? Unataka kujifunza Zaidi na Zaidi ili
kuwa bora katika maisha yako? Basi hakikisha haukosi kitabu cha SAFARI YA KUELEKEA MAFANIKIO. Hiki
ni kitabu ambacho kinapatikana bure kabisa yaani bila gharama yoyote ile. JINSI
YA KUKIPATA, tuma ujumbe wenye neno kitabu katika whatsapp katika moja ya
namba hizo hapo juu. Au tuma ujumbe katika TELEGRAM
kwenda namba 0754612413. Au tuma
barua pepe(email) yenye jina kitabu
kwenda email niliyoionyesha hapo juu, kisha utatumiwa kitabu bure kabisa.
No comments:
Post a Comment