Habari za
wakati huu ndugu msomaji wa makala za mtandao huu, ni matumaini yangu kuwa hu
mzima na unaendelea vizuri. Mimi pia naendelea vizuri katika harakati za
kupambana kimaisha. Leo nakuletea mambo kumi ambayo kwangu nimeyaita sumu
ambazo zinatukumba vijana wengi sana kwa sasa.
1. Kupenda starehe
kuliko kazi,hili ni tatizo ambalo limekuwa likitukumba wengi sana kwa sasa.
Leo hii kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wengi sana ambao wanataka wao
wastarehe tu siku zote ambapo mambo haya hayawezekani. Yaani huwezi kuishi kwa
starehe siku zote, na kingine tulichosahau vijana ni kuwa starehe huja baada ya
kazi lakini sisi kazi hatutaki kufanya ila tunachotaka ni starehe tu. Kwanzia leo
acha hii tabia ya kupenda starehe kuliko kazi.
2. Kupenda kupewa
kuliko kutoa, unapokuwa unataka kupewa jiulize wewe umetoa nini. Maisha ni
kitu ambacho kina kanuni zake bhana, maisha sio kitu cha kukurupuka tu bali ni
kitu ambacho kinahitaji kujipanga sana. Hivyo kama unapenda kupewa kumbuka na
wewe kutoa. Usiwe mtu wa kutaka tu kupewa wakati wewe hutaki kutoa. Kuna mambo
mengi ndani ya kutoa hivyo anza leo kutoa na kupokea kutakuja baadae.
3. Kufikiri siku
zote wazazi watakuwepo,huu ni mkondo wa mawazo ambao ni mbovu kuishi ni
kama wazazi watakuwepo siku zote ni kujidanganya sana. Jijengee uwezo wa kujitegemea
mwenyewe sio kuwategemea wazazi kila siku.
4. Kudhani kuna
njia za mkato, wengi sana tumekuwa tukijidanganya kuwa maishani kuna njia
za mkato jambo ambalo ni kujidanganya sana, maishani hakuna njia ya mkato hivyo
acha kujidanganya kwanzia sasa.
5. Tamaa ya mambo
tusiyoyaweza au tusiyo na uwezo nao kwa wakati husika, vijana tumekuwa na
taama za mambo ambayo hayana msingi wala umuhimu mkubwa sana maishani mwetu. Jifunze
leo kufanya mambo ya maana. Pia jifunze kuepuka tamaa ya mambo usiyoyaweza.
6. Kuto kuwa na
makundi sahihi, vijana wengi sana tumekuwa hatuna makundi sahihi, yaani
makundi tuliyonayo sio ya kutujenga bali ni ya kurudisha nyuma zaidi na zaidi. Leo
hii utakuta kijana anataka kuwa labda mtu fulani lakini makundi aliyonayo
hayawezi kumfanya akafanikiwa. Nacho maanisha hapa ni marafiki ambao
hatuendani.
7. Kuamini kuwa, kuwa
na masters PhD au degree ndo kuwa na pesa, kuna wengi ambao tunaamini kuwa
maishani kuwa na elimu za juu ndio kufanikiwa. Yaani ndio kuwa na pesa na
mengineyo. Lakini maishani ukweli ni kuwa unauwezo wa kufanikiwa hata kama
haukusoma kabisa. Hivyo basi futa hiyo imani yako.
8. Kuamini kuwa
kujifunza au kusoma kunaishia vyuoni basi, vijana wengi sana tumekuwa
tukiamini kuwa pindi tumalizapo elimu zetu za darasani basi ndio mwisho wa
kujifunza. Huku ni kujidangaya na ndio maana tumekuwa hatufanikiwi. Hivyo kuanzia
leo achana na habari hizi bali wewe endelea kujifunza hata baada ya kumaliza
elimu yako ya darasani.
9. Kudhani kuwa na
simu Kali ndio ufahari na utajiri, kila mtu leo hii anapigania kuwa na simu
kali sijui iphone ngapi, sijui tecno gani n.k. huu ni ufahari kwa wale ambao
hawajisomi lakini sio kwako wewe unayeyataka mafanikio. Kuwa na simu ya gharama
ambayo haikusaidii kitu haina maana yoyote katika maisha yako.
10. Ujuaji hata kwa
tusiyoyajua, tabia ya kujikuta unajua kila kitu inaponza maana hata kwa
yale ambayo hujui wewe unajidai unajua, sasa hii wakati mwingine inakunyima
fursa ya kujifunza maana wewe unahisi kuwa unajua kila kitu utajifunzaje sasa. Hivyo
achana na tabia hii ambayo haifai.
Hizi ni
sumu ambazo nimekuwekea kazi ni kwako kuendelea nazo au kuachana nazo, kila
kheri.
Mwandishi:
Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.
KWEL MKUU KWAA ASILIMIA 70 VIJANA TULIOWENGI VINATUKUMBA
ReplyDelete