Habari ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa,
ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri katika kuhakikisha kuwa
unashughulikia ipasavyo yale unayo yahangaikia ili tu kujiletea mafanikio
ambayo ndio kila mtu anayoyahangaikia. Nami nikusihi kwa moyo mmoja kuwa
endelea kupambana mpaka uyatimize yale unayoyaamini kama mafanikio kwako.
Pambana pambana bila kuchoka na mafanikio utayaona tu.
Wakati unaendelea kupambana katika kuhakikisha kuwa
unafanikiwa ni vyema ukatambua kuwa yafuatayo ni mambo ya msingi ambayo
yatakufanya ufanikiwe zaidi na zaidi. Mambo hayo ni yafuatayo:-
Wazo, wazo ni kitu muhimu
sana katika maisha ya binadamu lakini cha ajabu ni kuwa watu hawaelewi na
badala yake wamekuwa wakihangaika na vitu vingine na kujikuta wakipoteza muda
bure bila mafanikio na hatimaye huanza kuhangaika huku na kule na kutafuta
tatizo la kutofanikiwa kwao kumbe tatizo ni kuwa mawazo yao ndio yenye
matatizo. Kuna msemo maarufu miongoni mwa watu waliofanikiwa kuwa wazo ni
pesa/fedha. Hivyo basi hata katika biashara wazo ndio mtaji muhimu kwa maana
hiyo ni kuwa wazo ndilo huleta pesa sio pesa kuleta wazo. Na sio kila wazo
huleta pesa bali lile wazo sahihi juu ya pesa ndilo liletalo pesa. Wataalamu
wanasema tunakuwa kadri ya fikira zetu. Hivyo kama kweli unataka kufanikiwa jenga
mawazo chanya akilini mwako juu ya maisha yako na utafanikiwa tu.
2. Malengo,hili
ni jambo la msingi sana maishani mwako. Zunguka kote duniani tafuta mtu yoyote
aliyefanikiwa maishani na ambaye unaamini kuwa anamafanikio unayoyataka muulize
siri ya mafanikio yake jambo la msingi atakalokuambia ni kuwa weka malengo.
Malengo ni kama dira katika meli, meli haiwezi kwenda bila dira, ndivyo ilivyo
kwa binadamu binadamu asiye na malengo juu ya maisha yake hana tofauti na mfugo
ambao upo upo tu. Hivyo basi weka malengo kama kweli unataka kufanikiwa
maishani.
3. kujituma,
hakika hakuna mtu awezae kufanikiwa pasipo kujituma katika shughuli zile zenye
kumletea maendeleo. Kujituma ni jambo la msingi sana maishani jitume katika
shughulli zako, zifanye kwa kujitoa kisawasawa, hakikisha unafanya shughuli
kiuhakika usifanye tu bora umefanya bali fanya kama mtu anayejielewa kuwa
anafanya kitu chenye tija kwake na hapo ndipo utauona umuhimu wa kujituma. Na
hatimae mafanikio utayaona.
4. Uwajibikaji,
kama hutaki kuwajibika katika shughuli zako jua kuwa mafanikio kwako yatapita
kushoto. Hili naomba nikuambie dhahiri hata kama ikitokea leo umeanzisha
kampuni ukaajili wafanyakazi usikae ukabweteka kuwa si kunawafanyakazi
watafanya tu, usikae nyumbani kuangalia tamthiliya eti kisa umewaajili watu
wanakufanyia kazi. Jiunge nawe kuwa sehemu ya wafanyakazi na utayaona mafanikio
kwa kuwa wewe ndiye mwenye wazo la kuanzisha kampuni husika wala sio
wafanyakazi hivyo ukiwaachia wafanyakazi pekee hii inamaanisha kuwa umejitoa na
wazo lako pia umetoka nalo hivyo basi ni rahisi sana kwako kushindwa
kufanikiwa. Uwajibikaji umekuwa tatizo kubwa sana miongonui mwa watanzania
wengi ndio maana leo hii utawakuta watu wakiilaumu serikali hata kwa yale
ambayo ilibidi wayafanye wao wenyewe.
5. Kujiamini,
maishani lazima ujiamini, amini kuwa unaweza kufanya mambo makubwa na kuwa na
mafanikio makubwa sana maishani japo watu wengi wanaweza kuwa wanakukatisha
tama kwa kusema kuwa hauwezi lolote. Hakuna aliyezaliwa anajua kila kitu au
anajua bali kila mmoja wetu hujifunza kupitia watu fulani, hivyo basi kama
waliweza kujifunza basi hata wewe unaweza kujifunza pia. Jambo la msingi ni
kujituma, kuweka nia na kuwa na imani kuwa unaweza.
6. Shirikiana na watu sahihi,
sio lazima ushirikiane na kila mwanajamii maana jamii ina watu tofauti tofauti
na kila mtu huwa anachagua lile kundi analoliona kuwa lina tija kwake na sio
kila mtu. Leo hii inabidi uchague ni nani haswa wa kushirikiana nae na ni
kwanini kama unataka kufanikiwa shirikiana na watu wenye mtazamo chanya. Tambua
kuwa kila watu hukaa katika makundi yanayofana nao hivyo usije ukajichanganya
ukaka katika kundi lisilo kufaa maana utaumia na laweza kuwa kikwazo cha
kufanikiwa kwako.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua
pepe: Bmaganga22@gmail.com
No comments:
Post a Comment