Wednesday, March 23, 2016

Hii Ndio Siri Ya Kushinda Maishani.


Ni wengi sana tumekuwa tukitaka kushinda maishani yaani kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Ni kweli kila mpambanaji huwa anataka kushinda katika kila pambano analoshiriki na ndio maana kiuhalisia kila binadamu anapenda kufanikiwa na ndio maana kichwa cha makala nimeamua kukiita siri ya kushinda maishani nikiwa nataka kulenga siri ya kufanikiwa maishani.
Tumekuwa ni watu wenye kutaka kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kila mtu anapenda apate mafanikio makubwa, mimi nataka mafanikio, wewe unataka mafanikio na yule anataka mafanikio. Lakini kwanini tumekuwa tukijikuta kila mara tuko pale pale tulipokuwa jana yaani hatuendi mbele hata hatua moja kimaisha. Kila mara tumekuwa watu wa kushindwa hata kama tukijitahidi kupanga mipango muhimu na mizuri lakini wapi huwa tunajikuta tumeshindwa tena na tena.


Je unakumbwa na tatizo hili la kushindwa mara kwa mara pamoja na kwamba umejiwekea malengo, umepanga mikakati ya kutekeleza malengo yako na mengine mengi? Kama jibu ndio karibu nikupe njia rahisi ya kuweza kuepukana na hiyo hali.

Siri ya kushinda ni vitendo. Hii ndio siri kubwa na ambayo ninata uifahamu kwanzia leo kuwa siri ya kushinda ni vitendo. Kwanini nimesema hivyo, nimesema hivyo ni kwa kuwa takwimu zinaonyesha kuwa watu wengi sana wamekuwa au tumekuwa ni mabingwa wa kupanga mipango mizuri, kuweka mikakati kabambe, kuweka malengo mazuri sana ambayo ukiyasoma kwa kiasi kikubwa ni yanavutia sana tena sana, kiasi kwamba kila ukiyasoma yanakuvutia na unayafurahia lakini wakati unafanya hivyo unasahau kitu kimoja kwamba mipango tunayoiweka sio kwa ajili ya kuiweka kwenye makaratasi au kwenye karatasi tu bali tunatakiwa kuifanyia kazi yaani tuweke katika vitendo.

Kila kitu huanza kwa mpango, malengo na mikakati ambayo mara nyingi sana huwa inakuwa imeandikwa kwenye karatasi, wengi tunaweza kufanya hili jambo lakini jambo ambalo linatushinda ni kuhamisha yale yaliyomo katika makaratasi au karatasi na kuyapeleka katika vitendo, hili ndio jambo ambalo linatushinda kwa kiasi kikubwa sana na ndio maana tunashindwa kushinda (kufanikiwa).

Kama sio mtu wa kuchukua hatua ya kutenda kamwe sahau kuhusu kushinda maana huto weza kushinda kamwe maishani, kushinda huja kutokana na kuamua kuweka ile mipango tuliyojiwekea katika vindeo hivyo basi siri ya kushinda ni vitendo. Unatakiwa kutenda na uendelee kutenda bila kuchoka, kuhairisha wala kukata tamaa maana katika matendo ndimo huwa tunapata ushindi.

Mara nyingi tumekuwa tunashindwa kuchukua hatua ya kutenda kutokana na sababu mbalimbali kama vile:-

1.    Kuhisi uvivu pale tunapotaka kutenda, kama unakabiliwa na hii hali basi jua kabisa hiyo hali sio nzuri kwako na inaweza kukuzuia wewe kutenda jambo. Hivyo tambua kuwa hakuna matunda mazuri katika uvivu, yaani uvivu hauzai matunda mazuri hata siku bali huzaa matunda mabovu hivyo uogope uvivu.

2.    Uoga, wakati mwingine pale unapotaka kuchukua hatua ya kutenda unakabiriwa na hali ya kuogopa kuwa watanichukuliaje au ntaonekanaje hali hii inaweza kukufanya usichukue hatua yoyote na hivyo kujikuta umeshindwa kutenda na hatimaye unabaki pale pale.

3.    Hofu, wakati mwingine huwa unakumbwa na hofu pale unapotaka kutenda jambo fulani. Hofu ya kushindwa, hofu ya kuto kujulikana ni mifano wa hofu ambazo zinaweza kukuzuia wewe kuto tenda jambo fulani. Kabiliana na hofu hizi mara moja.

Hakika siri ya mafanikio/ kushinda ni vitendo, kuweka malengo sio mafanikio ila kuyaweka malengo yako katika matendo ndiko huleta mafanikio, kupanga mikakati, na mipango pia hakuleti mafanikio ila kutenda. Hiyo ndio siri niliyopanga kukushirikisha leo hii, natumaini utakwenda kushinda sasa.

Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.
                    :-barua pepe -Bmaganga22@gmail.com.No comments:

Post a Comment