Kila mtu ana ndoto zake maishani hilo ni swala ambalo
naliamini maishani kuwa wewe una ndoto, yule anandoto zake na mimi ninazo za
kwangu ambazo kwa kiasi kikubwa sana zinatofautiana sana tena sana. Kwa kuwa
ndoto zetu zinatofautia hili ni jambo jema maana hili ndilo hupelekea hata sisi
kutofautiana kimaisha na kimatendo. Hivyo sio jambo baya kuwa na tofauti ya
ndoto kati yangu mimi na wewe na yule.
Leo nataka nikushirikishe mambo matatu ambayo yanaweza
kukufanya ushindwe kutimiza ndoto zako mambo hayo ni kama yafuhatayo.
Hofu, ile hali ya kuwa na
wasiwasi mwingi juu ya lile unalotaka kulifanya inaweza kuwa adui mkubwa sana
wa ndoto zako. Najua kuwa unazifahamu aina nyingi sana za hofu, lakini mimi
nataka kugusia hofu ya aina moja tu ambayo ni hofu ya kuto kujulikana. Mara ngapi
umekuwa kila unapotaka kufanya jambo fulani unasikia ndani yako kuna sauti
inakuhamaasisha kuwa nani anakujua wewe hapa mjini nani?, ukisikia sauti hiyo
usijidanganye kusema ni malaika wa mungu anakusihi uache, hapana jua hiyo ni
hofu. Ni kweli hakuna anayekujua lakini hilo halikuzui wewe kuweza kutekeleza
jambo fulani. Kweli hawakujui kwa sababu hujajitambulisha kwao wewe ni nani. Sasa
pengine kupitia lile unalotaka kulifanya
ndilo linaloweza kukufanya ufanikiwe kwa kiasi kikubwa na hatimaye ukawa
umejitambulisha kuwa wewe ni nani na ukawa usha fahamikia tayari. Sasa kabiliana
na hii hofu tenda lile unaloliona ni sahihi na utajulikana tu. Hakuna aliyezaliwa
akiwa anajulikana.
2. Kutaka kuanza na makubwa,umekuwa
ni mtu wa kutaka kusubiri eti mpaka uwe na kitu kikubwa ndio uweze kutenda
jambo fulani. Ndugu msomaji waswahili walisema “haba na haba hujaza kibaba”. Anza
na kidogo wala hata usiogope kuanza na kitu kidogo maana kidogo huzaa kikubwa
sasa wewe unaposubiri eti upate kikubwa ndipo utende huko ni kujidanganya na
kujipotezea muda na kuendelea kudumaza ndoto yako maana hakuna namna ambayo
unaweza kupata kitu kikubwa bila kupitia
kitu kidogo hivyo basi njia ya uhakika ya kukufanya wewe uweze kufanikisha
ndoto zako ni kuanza na kidogo siku zote. Hata kama ni biashara unataka kuwa na
biashara kubwa sana wewe anza na mtaji hata wa milioni mbili hata kama ndoto
yako ni kuwa na biashara ya milioni ishirini na hiyo milioni mbili baada ya
muda itajizalisha na kufikia hizo milioni ishirini unazozitaka. Hivyo nakusii
usiue ndoto yako kwa kutaka eti kuanza na kikubwa maishani bali wewe anza tu
pale unapohisi upo tayari na unachakuanzia hata kama ni kidogo.
3. Kuto kuwa na maono sahihi,
kama unataka kufanikiwa lazima uwe na maono. Maaono ni ile hali ambayo unaweza
kuwa unajionea mambo ya mbele kifikira zaidi. Mfano unajionaje wewe baada ya
miaka mitano toka leo. Kila mtu ana namna ambayo anajiona atakavyokuwa baaada
ya miaka mitano mwingine anaweza kujiona kuwa anakuwa mtu maarufu sana, anakuwa
mfanyakazi bora, mjasiriamali mkubwa n.k. hayo ndio maono. Sasa ikitokea huna
uwezo wa kuona ndani ya miaka mitano utakuaje basi hii ni njia moja wapo ya
kuweza kuua ndoto zako. Maono huwa kama tasirwa/picha mabayo unayaona maisha
yako kifikira zaidi. Na maono sio malengo hivyo usijichanganye niliposema labda
unajiona kuwa mfanyakazi bora baada ya miaka mitano ukajua ni malengo hapana
malengo na maono vinatofautiana. Ingawa maono yanategemea malengo yako na
malengo yako yanategemea maono yako. Hivyo basi hakikisha una maono sahihi
yaani unauwezo wa kujiona ndani ya miaka mitano utakuaje au utakuwa wapi
kimaisha.
Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.
:-barua pepe -Bmaganga22@gmail.com.
No comments:
Post a Comment