Katika maisha tumekuwa tukifanya mambo kadha wa kadha
ambayo wakati tukifanya mambo haya huwa tunakuwa na uhakika kuwa mambo hayo ni
yenye kutulendea mafanikio makubwa maishani. Lakini kuna wakati huwa tukijikuta
tumeshindwa kufanya jambo fulani huwa tunafanya tafakari ya hali ya juu kwa
ajili ya kutaka kutambua sababu haswa iliyofanya tusiweze kufanikiwa. Baada ya kugundua sababu hapa ndipo matatizo
huanza na mara nyingi tatizo hili ndilo limekuwa likitufanya tusifanikiwe siku
zote.
Unaweza ukashindwa kutekeleza jambo fulani, na baada ya
kufanya tathimini ya nini kimekufanya usifanikiwe ukagundua pengine ni kwa
sababu uliswhindwa kutumia muda vizuri yaani kuna vitu ambavyo ulivifanya na
hatimaye vikawa chanzo cha kukupotezea muda kwa kiasi kikubwa sana na hatimaye
ukajikuta umeshindwa kulitekeleza hilo
jambo. Swala la kuwa umeshindwa kutekeleza jambo ulilolipanga kutokana na
kufanya mambo ambayo ni kinyume na uliyotakiwa kufanya ili kulitekeleza jambo fulani,
umekuja kuligundua baada ya kufanya tathimini ya kina ya nini kimekufanya
usifanikishe jambo husikia. Sasa hapa suluhu ya yote haya ni kuyaacha yaende
yale mambo yote yanayokupotezea muda lakini hapa ndipo huwa tunafanya makosa
makubwa sana maana huwa hatukubali kuyaacha yaende badala yake tunayashikilia
tu na hatimaye tunajikuta tumeshindwa zaidi na zaidi. Hivyo basi makala hii
inasema unashindwa kwa sababu umeshindwa kuyaacha yaende, hiki ndicho kitu
kimoja kinachokufanya usifanikiwe.
Ni vyema ukatambua kuwa maishani usiwe kinganganizi wa
mambo yasiyo ya msingi wala maana yoyote kwako badala yake fanya jambo moja tu
kwa yale ambayo unahisi kuwa yanakupotezea muda wako kwa kiasi kikubwa au
hayana maana maishani mwako basi yaache yaende tu hakuna namna nyingine bali ni
kuyaacha yaende tu. Usiwe mtu wa kuhaha huku na huku kuyakumbatia mambo ambayo
kimsingi hayana maana. Tumekuwa ni watu wa kushikilia mambo ambayo hayana tija
kwetu na mbaya zaidi ni kuwa huwa tunakuwa tunafahamu kabisa kuwa jambo fulani halina
tija wala maana kwangu lakini huwa tunaendelea kukomaa nayo tu au zaidi na
zaidi yaani tunakomaa nayo tu. Sasa jambo hili ndilo linatufanya tuzidi
kushindwa kila mara maishani.
Nyani ni kiumbe ambaye kwa wakati mwingine huonekana ni
mjanja sana na ni msumbufu kwa wanadamu, hili kwa wale ambao wanafanya shughuli
za kilimo katika maeneo ambayo nyani ni wengi watakuwa wananielewa kirahisi
sana, lakini nyani huyu huyu ambaye huonekana mjanja huwa anaponzwa na tabia
moja tu nayo ni ile ya kuto kuacha yaende. Kule nchini Brazili wanaowinda nyani
hutumia njia rahisi sana ya kumtega nyani, wao huchukua mtego ambao huwa na
uwazi sehemu moja ambapo nyani anaweza kupitisha mkono wake, kisha katika lile
tundu huwa wanatumbukiza ndizi na kisha kuweka ule mtego pahali fulani. Sasa nyani
akija huwa anataka kuchukua ile ndizi, lakini kwa jinsi ambavyo mtego ule
ulivyo ni kuwa nyani akishaingiza mkono wake hawezi kutoka akiwa ameshikilia
ndizi, nyani hulitambua hilo kuwa hawezi kutoa mkono akiwa na ndizi hivyo aidha
aiachie ndizi ili asikamatwe au la. Lakini cha ajabu ni kuwa nyani huyu
huendelea kung’ang’ania ndizi husika mpaka wenye mtego hufikia na kuweza
kumkamata. Hivyo kinachomponza nyani siku zote ni ile tabia ya kuto acha
yaende.
Sasa tabia hii ya nyani ndio hata binadamu tumekuwa nayo
mtu utakuta anayafahamu fika madhara ya utumiaji wa pombe kupita kiasi lakini
anaendelea, madhara ya uvivu lakini anaendelea, madhara ya kutokuweka malengo
lakini anaendelea tu kufanya mambo ambayo yanamfanya asiweke malengo n.k.
Tambua kuwa uwezo wa kushindwa au kushindwa upo mikononi
mwako chagua leo kushinda na utashinda tu na chagua leo kutokushinda na
hutoshinda kamwe vilevile.
Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.
:-barua pepe
-Bmaganga22@gmail.com
No comments:
Post a Comment