Saturday, March 26, 2016

Tabia Moja Muhimu Kwako Wewe Unaetaka Kufanikiwa.

Habari za wakati huu ndugu msomaji wa makala za mtandao huu ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vyema mimi pia naendelea vyema katika mapambano. Turudi katika mada yetu ya leo ambapo nataka kukushirikisha juu ya jambo muhimu ambalo unatakiwa kuwa nalo kama kweli unataka kufanikiwa. Jambo lenyewe ni kuhusu Kuendelea kujifunza. Kama kweli unataka kufanikiwa hakikisha unajijengea tabia hii kuanzia sasa.

Image result for continue learning


Ipo nguvu kubwa sana katika kujifunza  kama kweli unataka kuwa mwenye mafanikio basi hakikisha kuwa unajifunza kila siku. Yaani usikae bila kujifunza katika kila jambo ambalo unalifanya. Uwe mkulima, uwe daktari, uwe mwanafunzi, uwe hakimu uwe nani wewe endelea kujifunza tu. Nakuambia hivyo kwa kuwa takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 40% ya watu wengi duniani huacha kujifunza pindi tu wanapomaliza elimu zao yaa iwe sekondari au chuo, huo ndio huwa mwisho wa kujifunza kwao. Sasa kwa wewe unayetaka kufanikiwa hakikisha kuwa haufanyi makosa katika kujifunza.

Labda unajiuliza kuwa ni vipi sasa unaweza kujifunza, pengine unawaza kuwa  nirudi shule tena au la?, hapana, hapa nakupatia  namna nne ambazo unaweza kuzitumia katika kujifunza tena kwa gharama ndogo kuliko unavyofikiria sasa. Njia hizi ni zifuatazo:-

1.    Kupitia kusafiri, unaweza kujifunza kupitia kusafiri, hii ni kutokana na sababu kuwa wanadamu tunatofautiana kiutamaduni kwa kiasi kikubwa sana, hivyo katika kusafiri kutoka sehemu moja kwenda kwingine kunaweza kukusaidia wewe kubadili  maisha yako kwa kuwa utaweza kujifunza  namna watu wanavyoishi na wanavyofanya vitu tofauti tofauti, hivyo hii inaweza kukusaidia wewe katika kujifunza na hivyo kubadili maisha yako. Unaweza kujifunza namna mpya ya kuendesha shughuli Fulani kutokana na safari uliyosafiri, hii ni kutokana na sababu kuwa umebadilisha mazingira ulikuwapo awali.

2.    Kusoma vitabu, unaweza kutafuta kitabu cha mada ambayo unaitaka vitabu vipo vingi sana swala ni kwako wewe kuamua ni kitabu gani na kinachohusu nini unachotaka kusoma. Kuna vitabu vya kusoma online, kuna vya kununua ambapo kampuni kama vile amazoni zinauza vitabu vya kila namna, pia waweza kuingia google na ukasearch kitabu unachotaka kuhusiana na mada unayotaka na hivyo basi ukapata kujifunza mengi zaidi na zaidi.

   Kusoma magazeti, nakuona unasema magazeti dah, mbona yamejaa habari hasi, habari za kusikitisha, habari za majonzi na simanzi na mengine mengi. Ni kweli kwa hayo unayoyasema lakini sio kweli kuwa magazeti yamejaa mada hasi tu bali hata mada chanya zipo. Kwenye magazeti  kuna makala juu ya mambo kama vile, afya, kilimo n.k. hivyo jambo la kufanya ni kuwa katika gazeti wewe nunua gazeti na fuata taarifa chanya tu. Yaani fata kile ambacho unahisi kimekufanya ununue gazeti, kama umenunua gazetiu kwa ajiri ya kusoma makala za kilimo basi zitafute mahali zilipo kisha soma na achana na mengine.

4.    Kusoma katika blog mbalimbali, hii pia ni njia moja wapo na mabayo inakuwa kwa kasi sana ambayo wewe unayetaka kufanikiwa unaweza kuitumia kwa kiasi kikubwa sana. Leo hii kuna blog nyingi sana ambazo zinatoa mafunzo ya namna mbalimbali, sasa kazi ni kwako wewe kuamua blog gani inakufaa kutokana na mada zake. Blog ni nyingi mno na zinatoa elimu tofauti tofauti hivyo basi hakikisha kuwa unatafuta blog ya kukuwezesha wewe kupata elimu unayota.

Maisha yanabadilika badilika kila siku na pia utaratibu wa uzalishaji, usafirishaji na hata mawasiliano unabadilika kila wakati hivyo ni  bora uwe katika hali ya kujifunza ili tu uwe katika nafasi nzuri ya kujifunza na  hivyo kukabiliana na mabadiliko haya.

Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.
                    :-barua pepe -Bmaganga22@gmail.com.

KARIBU KATIKA DARASA HURU.
Je? unataka kujifunza na kuwa bora zaidi?,Je? unataka usihangamie kwa kukosa maarifa?,Je? unataka kujua namna ya kutatua matatizo na changamoto mbalimbali zinazokukabili?,Je? unakumbana na hali ya kukata tama mara kwa mara?,Je? unashindwa kujiwekea malengo n.k.Kama jibu ndio basi karibu katika darasa huru. Namna ya kujiunga na darasa huru tuma kiasi cha pesa cha shilingi 5000/= kwa namba 0754612413 kwa mpesa (jina. Baraka magama) au 0652612410 kwa tigo pesa. (jina: Baraka maganga). Kiasi hiki ni kwa mwezi mmoja ambapo ukiisha utatakiwa kuchangia tena kiasi hicho hicho. Kisha, tuma namba yako ya simu kwenda namba moja kati ya hizo huku ukiwa umeambatanisha na jina lako kamili kama linavyojitokeza katika m-pesa au tigo pesa. Kumbuka kufanya hivyo huku ukiwa na uhakika kuwa pesa yako imepokelewa na hapo utaunganishwa kwenye kundi la whatsapp ambalo litakuwa na jina la DARASA HURU.
N.B, huduma hii itatolewa kwa njia ya whatsapp, hivyo hakikisha simu yako ina uwezo wa whatsapp ndipo ujiunge ili kuepuka usumbufu.Masomo yataanza tarehe 1/4/2016. Saa tatu kamili usiku.
Barikiwa.
Karibu sana.


No comments:

Post a Comment