Monday, April 4, 2016

Usikubali Kutawaliwa Na Vitu Hivi Viwili.

Usikubali Kutawaliwa Na Vitu Hivi Viwili.
Habari za wakati huu ndugu mpendwa msomaji wa makala za mtandao huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri katika kupambana na hatimaye kuhakikisha kuwa unajiletea mafanikio binafsi. Nami nakusihi endelea kupambana mpaka kieleweke.
Wakati unaendelea kupambana ili kujiletea mafanikio basi ni vyema ukatambua kuwa vitu hivi viwili ni hatari sana kwako endapo utaviruhusu vikutawale maishani. Maandiko ya biblia yanatueleza kuwa “kuweni na kiasi”. Maneno haya yana maana kubwa sana na ninaomba uyashike wewe ambae unataka kufanikiwa. Hapa nakwenda kukushirikisha vitu viwili ambavyo kamwe usiruhusu vikutawale maishani mwako.

Tamaa ya pesa, ndugu msomaji wa makala hii ni vyema ukatambua kuwa pesa ni kitu muhimu sana tena sana kwa ajili ya maisha yetu ya kila siku. Natambua kuwa pesa ni kitu muhimu kwa kuwa ndio inayotupatia mahitaji yetu muhimu kama vile chakula, maradhi, nguo na huduma za kiafya. Natambua kuwa bila pesa huwezi kupata hivi vitu. Lakini naomba nikuonye sasa kuwa tamaa ya pesa aikufanyi wewe kuwa na pesa, na kubwa zaidi tamaa ya pesa inaweza kukupelekea wewe kutaka kupata pesa kwa njia zisizo halali. Na hili ndilo jambo ambalo limekuwa likitukumba wengi wetu kwa sasa. Kwamba kutokana na tamaa ya pesa tunajikuta tunaanza kufanya mambo hata ambayo ni kinyume na maadili na miiko ya jamii kisa tu tupate pesa.

Ni vizuri kutamani kuwa na pesa lakini mimi naomba wewe mwanamafanikio penda pesa usitamani pesa maana tamaa ni mbaya. Ndio maana nakuambia kuwa na kiasi. Hata kama unatamani kuwa na pesa basi hiyo tamaa yako iwe na kiasi, isiwe tamaa iliyopitiliza ambayo itakufanya wewe sasa kutaka kuwa mwizi, jambazi, kahaba au hata shoga. Ongezeko la vitendo visivyokubalika na jamii kama vile ushoga,ukahaba, ujambazi na wizi ni kiutokana na tamaa za pesa ambazo watu tumekuwa nazo. Nasisitiza kuwa na kiasi.

2.    Kutaka kulipwa zaidi ya unavyositahiri, hili ni jambo ambalo watu tumeanza kukumbwa nalo nami nakusihi wewe unayetaka kufanikiwa hakikisha kuwa hautawaliwi na jambo hili la kutaka kulipwa zaidi ya unavyositahiri. Hapa nacho maanisha kama unatoa huduma fulani usitake eti kwamba wewe ulipwe zaidi kuliko ubora wa huduma yako. Kama unauza bidhaa fulani basi hakikisha kuwa ule ubora wa hiyo bidhaa unaendana na pesa unayoitaka.

Unafikiri nini chanzo cha matukio ya utapeli na udanganyifu ni kutokana na sababu kuwa watu wanataka kulipwa zaidi ya wanavyostahiri, hiki ndio chanzo. Sasa nakuonya wewe unaetaka kufanikiwa kuwa jambo hili wewe halikufai waache wafanya wengine ila sio wewe. Na nakuonya kwasababu waswahili wanasema “njia ya muongo ni fupi” hivyo kama ukifanikiwa kwa njia hii tambua kuwa njia hii haitakupa mafanikio ya milele.

Kingine nachokusisitiza kuwa usipende kulipwa zaidi tofauti na huduma unayostahili ni kwa sababu dunia inabadilika na ushindani ni mkubwa sana leo hii, hivyo kama unataka kushindana na wenzio na ubaki katika ushindani huo hakikisha kuwa unatoa kitu bora na kitu hicho kiendane na thamani unayotaka. Mfano utakaposema bidhaa fulani labda tuseme unauza nguo fulani elfu hamsini kweli ionekana ni ya elfu hamsini sio nguo ya elfu kumi na tano wewe unataka uiuze elfu hamsini. Huko ndio kulipwa zaidi nako kuzungumzia.
Kila kheri katika kuyasaka mafanikio. Na usisahau kutembelea blog hii ili kuweza kujifunza zaidi na zaidi.
Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.No comments:

Post a Comment