Saturday, December 5, 2015

Ijue Silaha Muhimu Ya Kutumia Kupambana Katika Safari Yako Ya Mafanikio

.
Habari za siku ya leo mpenzi msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya. Pia matumaini kuwa unaendelea kupambana vikali katika kuhakiukisha kuwa unatimiza yale uliyopanga kuyatekeleza mwaka huu maana mwaka ndio huo uko ukingoni, basi na kusihi endelea kupambana kwa moyo mmoja na wala usikate tama.


 Najua kila mtu anafahamu kuwa mwanajeshi hawezi kuingia uwanja wa vita pasipo kuwa na silaha za kivita au silaha ya kutumia katika vita hiyo. Usishangae kusikia habari ya mwanajeshi maana unaweza kudhani kuwa nimeanza kuongelea habari za vita Fulani lakini mimi sizungumziii vita vya namna ambayo wewe umeanza kuhisi. Vita nayo zungumzia mimi ni vita ya kuyasaka mafanikio, na mwanajeshi anayehitaji silaha au kuwa na silaha ni wewe, ndio ni wewe wala sio mwingine. Wewe ndiye mwanajeshi ambaye ndiye unapambana katika kuhakikisha unapata ushindi katika vita kali ya mafanikio.
Lakini tofauti ya mapambano ya vita vya mafanikio na ile vita nyingine ni kuwa  vita ile nyingine kama ile ya kwanza ya dunia au ya pili, inakuwa na silaha nzito ambazo huwa na lengo la kuwateketeza kabisa maadui. Silaha hizo huwa kama vile bunduki, mabomu, vifaru n.k. unaweza kujiuliza na kuanza kushangaa kuwa inamaana nami nahitaji silaha hizo?, mbona nchi hairuhusu watu wa kawaida kumiliki ovyo hizo silaha?, mbona sina uwezo wa kununua hata moja? N.k. ila nakusihi tulia ndugu msomaji maana safari ya mafanikio haiitaji silaha hizo.
Ingawa silaha hii ya kutumia kupambana katika uwanja wa vita vya mafanikio ina lengo sawa na zile za vita ingine ambayo ni kuwateketeza maadui. Unaweza kujiuliza kuwa sasa maadui hao ni wapi?, mbona siwafahamu?, mbona sijui hata wanakojifisha?,  ntawezaje kupambana nao sasa?. Ndugu msomaji maadui wako  katika vita ni hawa hapa ambao ni, uvivu, hofu(woga), kukata tama, kukosa malengo, kulalamika na kuhairisha mambo. Hapo nadhani ushawajua maadui wa kupambana nao sasa katika hiyo vita yako. Swali lingine ni wanaishi wapi, vizuri lakini jibu ni rahisi maana ulipo wewe nao wapo, kwa maana hii ni kuwa mbona unaishi nao kila siku.
Kwa kuwa ushawajua maadui ni kina nani na ni wapi wanapatikana basi sasa ni wakati wa kuchukua silaha, silaha yenyewe ni uvumilivu. Inawezekana kuna silaha nyingi sana ambazo unazifikiria katika vita yako lakini leo mimi nataka uchukue hii hapa moja na ukapambane vikali katika vita yako hiyo maana naamini kati ya silaha nyingi ambazo zipo hii ni silaha moja muhimu sana. mwanajeshi aendapo katika vita huwa kwanza na imani ya kushinda, baada ya hapo huitaji kuwa wavumilivu wasio wepesi wa kukata tama. Maana kuna mambo mengi sana ambayo atapambana nayo, ikiwa ni pamoja na kukabiliana na kundi kubwa la maadui, pili kushuudia wenzake wakijeruhiwa na kuumia vibaya na pengine kushuhudia maiti nyingi. Lakini pamoja na yote haya mwanajeshi hutakiwa kuvumilia ili aweze kushinda maana anajua akishindwa kuna mawili kifo au kuwa mateka na kufanywa mtumwa katika maisha yake yote.
Hivyo ndivyo ilivyo na kwako katika safari yako ya mafanikio unahitaji kuwa mvumilivu maana utakutana na maadui au kundi kubwa la maadui kama ilivyo kwa mwanajeshi katika vita yoyote ile. Maadui hao ni kama watakao kuvunja moyo, watakao kukatisha tama, uvivu, kuridhika, woga au hofu na kutegemea wengine. Kumbuka tumesema kuwa mwanajeshi hupambana vilivyo katika vita hata kama akikutana na maadui wa aina gani hii ni kwasababu anajua kuwa akishindwa kuna mawili aidha kuwa mateka au kifo. Sasa kwako wewe katika safari ya mafanikio ni kwamba huta kufa ila utabaki kuwa masikini mkubwa, tena masikini wa kutupwa. Hivyo basi katika vita hii hakikisha unapambana kushinda ili usiwe masikini wa kutupwa.
Ndugu msomaji swala la uvumilivu limesisitizwa hata katika maandiko matakatifu (biblia). Ambapo swala la uvumilivu limeonekana katika kitabu cha AYUBU, soma sura ya kwanza na kuendelea utaona jinsi gani ayubu alivumilia mikiki mimiki yote pamoja na kuwa, kuna wakati mkewe alimsihi na kumsisitza amkufuru mungu lakini ayubu alikataa. Soma kitabu cha ayubu ili upate mengi.
Nimekupa silaha moja lakini hii ni silaha kubwa na muhimu ambayo ukiwa nayo maadui kwako watakuwa kama watoto maana utawashinda kila mara na hata wakirudi  wakiwa wamejipanga vipi wewe utashinda tu.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.

0754612413/0652612410.

1 comment:

  1. Jiamin,sali pia shirikisha mawazo yako kwa marafiki wazuri

    ReplyDelete