Friday, December 4, 2015

Vitu vine (4) Muhimu Katika Safari Yako Ya Kuelekea Mafanikio.


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendeleza mapambano ya kuzisaka fursa na kuzitumia na kwa zile ambapo zimekwisha patikana unahakikisha hazikuponyoki kizembe nami nasema kazana kwani mapambano yanaendelea hakuna kuchoka mpaka tutimize malengo yetu.
Leo nataka kukushirkisha mambo manne muhimu ambayo unahitaji kuwa nayo ili kuweza kufanikisha safari yako ya mafanikio. Kama ilivyo katika safari za kawaida ambazo tumekuwa tukisafiri mara kwa mara aidha kwa usafiri wa magari, ndege au meli. Huwa kuna kuwa na vitu ambavyo ndio kama mahitaji ya safari zetu, yaani bila vitu hivyo safari zetu zinaweza kuwa za kusuasua na zenye kukosa mwelekeo. Chukulia mfano leo hii unataka kwenda sehemu alafu huna tiketi ya kukuwezesha kufika huko, nina uhakika safari yako itakuwa ya kusuasua na unaweza usisafiri sidhani kama leo hii unaweza kusafiri kwa basi au ndege pasipo kuwa na nauli. Mambo haya yafuatayo ni muhimu sana katika safari yako ya mafaniko yaani ni kama tiketi katika safari yako. Endelea……..
1. Njozi, ili ufanikiwe unahitaji kuwa na njozi tena si njozi bora njozi bali njozi kubwa njozi itakayokunyima usingizi wakati mwingine . njozi kwa lugha nyingine huitwa ndoto(dream). Njozi ni namna au kadiri unavyoyaona maisha yako na yatakavyokuwa baada ya kipindi Fulani cha maisha mfano,unayaonaje maisha yako baada ya miaka miwili,mitano, kumi au ishirini ijayo mbele. Unajiona kuwa utakuwa unamiliki nini haswa je unaliona gari la ndoto yako ukiwa ndani yake, nyumba, shamba ama viwanja?. Uwezo huo ndio hujulikana kama ndoto na ni muhimu sana katika maisha yako kama kweli unataka kufanikiwa.
2. Elimu, elimu ni kitu cha muhimu sana tena sana, iwe ile ya darasani au ile ya kujiendeleza baada ya ile ya darasani kwa wakati huu ambapo kuna ushindani mkubwa sana katika soko ni bora ukawa na hata degree moja. Elimu ya darasani ni muhimu kwa kuwa itakufungua na kukupa mwanga wa maisha, lakini pia katika dunia ya sasa elimu ya darasani pekee haitoshi kukufanya wewe mwenye mafanikio. Bali elimu hii nyingine ya tofauti na ile ya darasani ina umuhimu mkubwa sana katika ndunia ya sasa ambayo imejaa changamoto nyingi. Kuna semina mbalimbali ambazo zimekuwa zikiendeshwa kuhusu mambo mbalimbali kama vile ujasiriamali na biashara, kuna vitabu mbalimbali vya uhamasishaji,ujasiriamali, uwekezaji, biashara n.k.vile vile kuna  video ambazo unaweza kuzipata youtube ama kununua dvd. yote haya ni katika kuhakikisha unapata elimu ya kile unachokitaka.
3. Afya, hiki ni kitu cha muhimu pengine kuliko vyote kati ya vile ambavyo ntavitaja hapa. Hii nikwa kuwa afya inahusisha uzima wa mwili ambapo uzima wa mwili utakufanya ufanye kazi zako kwa ufanisi mkubwa sana sidhani kama ipo siku ambayo utaweza kufanya shughuli zako kwa kiwango kile ambacho huwa unafanya siku zote ikiwa unaumwa. Hivyo kwa kutambua umuhimu wa afya ya mwili wako basi hakikisha unafuata kanuni za kiafya kama vile kuhakikisha unafanya mazoezi, punguza kula vitu vyenye mafuta mengi, chumvi, sukari n.k. tunza afya ya mwili wako.
4. Muda, hapa ndio penye tatizo maana tumekuwa wapoteza muda wakubwa yaani ni watu ambao hatujui ni namna gani tutautumia muda wetu vizuri na kutufanya tuuone muda huo unatutosha sana lakini cha ajabu sasa matumizi mabovu ya muda yametufanya tuwe mabingwa wa kulalamika kuwa muda haututoshi, lakini wewe unaelalamika kumbuka kuwa mungu hana upendeleo katika jambo lolote lile maana kila mtu tajiri kwa masikini,kipofu kwa kiwete, mvuvi kwa mlinzi wote wanamasaa sawa ambayo ni ishirini na nne (24), sasa katika,masaa haya haya wapo wanaozitimiza ndoto zao na wanaoendelea kulalamika hivyo basi jambo la msingi kwako ni kupangilia mambo yako kwa muda uliopewa na sio kulalamika kuwa muda haukutoshi.
Hayo ni mambo muhimu manne ambayo ukiyafuatilia vyema utapata mafanikio makubwa kuliko unavyodhani.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.
Bmaganga22@gmail.com.
0754612413/0652612410.


1 comment: