.
Habari za siku ya leo mpenzi msomaji wa mtandao huu wa
kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya. Pia matumaini kuwa
unaendelea kupambana vikali katika kuhakiukisha kuwa unatimiza yale uliyopanga
kuyatekeleza mwaka huu maana mwaka ndio huo uko ukingoni, basi na kusihi
endelea kupambana kwa moyo mmoja na wala usikate tama.
Najua kila mtu
anafahamu kuwa mwanajeshi hawezi kuingia uwanja wa vita pasipo kuwa na silaha
za kivita au silaha ya kutumia katika vita hiyo. Usishangae kusikia habari ya
mwanajeshi maana unaweza kudhani kuwa nimeanza kuongelea habari za vita Fulani
lakini mimi sizungumziii vita vya namna ambayo wewe umeanza kuhisi. Vita nayo
zungumzia mimi ni vita ya kuyasaka mafanikio, na mwanajeshi anayehitaji silaha
au kuwa na silaha ni wewe, ndio ni wewe wala sio mwingine. Wewe ndiye
mwanajeshi ambaye ndiye unapambana katika kuhakikisha unapata ushindi katika
vita kali ya mafanikio.
Lakini tofauti ya mapambano ya vita vya mafanikio na ile
vita nyingine ni kuwa vita ile nyingine
kama ile ya kwanza ya dunia au ya pili, inakuwa na silaha nzito ambazo huwa na
lengo la kuwateketeza kabisa maadui. Silaha hizo huwa kama vile bunduki,
mabomu, vifaru n.k. unaweza kujiuliza na kuanza kushangaa kuwa inamaana nami
nahitaji silaha hizo?, mbona nchi hairuhusu watu wa kawaida kumiliki ovyo hizo
silaha?, mbona sina uwezo wa kununua hata moja? N.k. ila nakusihi tulia ndugu
msomaji maana safari ya mafanikio haiitaji silaha hizo.
Ingawa silaha hii ya kutumia kupambana katika uwanja wa
vita vya mafanikio ina lengo sawa na zile za vita ingine ambayo ni kuwateketeza
maadui. Unaweza kujiuliza kuwa sasa maadui hao ni wapi?, mbona siwafahamu?,
mbona sijui hata wanakojifisha?,
ntawezaje kupambana nao sasa?. Ndugu msomaji maadui wako katika vita ni hawa hapa ambao ni,
uvivu, hofu(woga), kukata tama, kukosa malengo, kulalamika na kuhairisha mambo.
Hapo nadhani ushawajua maadui wa kupambana nao sasa katika hiyo vita yako.
Swali lingine ni wanaishi wapi, vizuri lakini jibu ni rahisi maana ulipo wewe
nao wapo, kwa maana hii ni kuwa mbona unaishi nao kila siku.
Kwa kuwa ushawajua maadui ni kina nani na ni wapi
wanapatikana basi sasa ni wakati wa kuchukua silaha, silaha yenyewe ni uvumilivu. Inawezekana kuna silaha nyingi
sana ambazo unazifikiria katika vita yako lakini leo mimi nataka uchukue hii
hapa moja na ukapambane vikali katika vita yako hiyo maana naamini kati ya
silaha nyingi ambazo zipo hii ni silaha moja muhimu sana. mwanajeshi aendapo
katika vita huwa kwanza na imani ya kushinda, baada ya hapo huitaji kuwa
wavumilivu wasio wepesi wa kukata tama. Maana kuna mambo mengi sana ambayo atapambana
nayo, ikiwa ni pamoja na kukabiliana na kundi kubwa la maadui, pili kushuudia
wenzake wakijeruhiwa na kuumia vibaya na pengine kushuhudia maiti nyingi.
Lakini pamoja na yote haya mwanajeshi hutakiwa kuvumilia ili aweze kushinda
maana anajua akishindwa kuna mawili kifo au kuwa mateka na kufanywa mtumwa
katika maisha yake yote.
Hivyo ndivyo ilivyo na kwako katika safari yako ya
mafanikio unahitaji kuwa mvumilivu maana utakutana na maadui au kundi kubwa la
maadui kama ilivyo kwa mwanajeshi katika vita yoyote ile. Maadui hao ni kama
watakao kuvunja moyo, watakao kukatisha tama, uvivu, kuridhika, woga au hofu na
kutegemea wengine. Kumbuka tumesema kuwa mwanajeshi hupambana vilivyo katika
vita hata kama akikutana na maadui wa aina gani hii ni kwasababu anajua kuwa
akishindwa kuna mawili aidha kuwa mateka au kifo. Sasa kwako wewe katika safari
ya mafanikio ni kwamba huta kufa ila utabaki kuwa masikini mkubwa, tena
masikini wa kutupwa. Hivyo basi katika vita hii hakikisha unapambana kushinda
ili usiwe masikini wa kutupwa.
Ndugu msomaji swala la uvumilivu limesisitizwa hata
katika maandiko matakatifu (biblia). Ambapo swala la uvumilivu limeonekana
katika kitabu cha AYUBU, soma sura
ya kwanza na kuendelea utaona jinsi gani ayubu alivumilia mikiki mimiki yote
pamoja na kuwa, kuna wakati mkewe alimsihi na kumsisitza amkufuru mungu lakini
ayubu alikataa. Soma kitabu cha ayubu ili upate mengi.
Nimekupa silaha moja lakini hii ni silaha kubwa na muhimu
ambayo ukiwa nayo maadui kwako watakuwa kama watoto maana utawashinda kila mara
na hata wakirudi wakiwa wamejipanga vipi
wewe utashinda tu.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.
0754612413/0652612410.
Jiamin,sali pia shirikisha mawazo yako kwa marafiki wazuri
ReplyDelete