Monday, December 21, 2015

Hakuna Uhusiano Wa Moja Kwa Moja Kati Ya Vitu Hivi Viwili.


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vyema katika harakati zako za kuhakikisha unayatekeleza yale ambayo umekwisha jiweke na ukizingatia kuwa mwaka ndio huo uko ukingoni.
Leo nataka kukushirikisha juu ya jambo hili nalo ni kukosekana kwa uhusiano wa moja kwa moja kati ya elimu ya darasani na mafanikio, hii ni kutokana na sababu kuwa kuna watu ambao wamekuwa wakiamini kuwa ili wafanikiwe ni lazima wae na elimu ya darasani. Yaani kwao wao ni kuwa ili mtu aweze kufanikiwa ni lazima awe amesoma sana na angalau awe na elimu ya degree au masters hapo ndipo atafanikiwa.Jambo hili limeshamili sana miongoni mwa jamii nyingi sana hapa kwetu Tanzania ndio maana leo hii msisitizo kwa wazazi kwa watoto wao ni kuwa soma sana mwanangu ili uje kuwa na maisha mazuri na yenye mafanikio. Kwa wazazi wengi hapa nchini kwetu ni kuwa mafanikio hutokana na kusoma na kuwa na degree au masters. Yaani msisitizo wao mkubwa ni katika elimu ya darasani ambayo itakufanya uajilliwe na katika ajira, ajira hutolewa kutokana na elimu ya mtu, yaani mwenye elimu ya juu ndiye hupewa ajira yenye mshara mkubwa na kwa kuwa tunaamini kuwa mshara mkubwa ndio hukufanya uwe na pesa na kwa kuwa wengi wetu hupima mafanikio kwawingi wa pesa basi huwa tunaamini katika ajira na ajira huja kutokana na elimu yako ndio maana wazazi wamekuwa wakitusisitiza juu ya elimu ya darasani.
Lakini ndugu msomaji wa makala hii nataka ujiulize kama kweli unaamini kuwa mafanikio hutokana na elimu ya darasani je ni wangapi ambao pamoja na masters zao na degree zao lakini bado ni masikini?, hawana mafanikio yoyote yaani ila wanaringia elimu zao za darasani?. Jibu nadhani ni wengi, sasa kama ni wengi huo uhusiano unatoka wapi wa kukufanya wewe uamini kuwa mafanikio ya kweli hutokana na elimu ya darasani pekee?. kama elimu ya darasani ndio kigezo cha mafanikio ya watu je nani angekataa kusoma mpaka kupata hizo degree na masters?, maana hakuna asiyependa mafanikio.
Na jiulize tena ni wangapi ambao pamoja na kutokuwa na elimu ya darasani lakini wanamafanikio makubwa sana na nimatajiri wakubwa duniani?. Mfano ni tajiri Bill gate ambaye aliachana na habari za shule na kuamua kujifundisha mwenyewe na kisha kugundua program ya Microsoft katika computer. Matajiri wangapi au wafanyabiashara wangapi unaowajua hapo mtaani hawana elimu ya darasani lakini ndio matajiri wakubwa.
Utamaduni wa kuwasisitiza watoto au ndugu zetu kusoma sana ili kupata maksi nzuri darasani na baadae kupata ufaulu wa juu kisha wapate kulipwa kutokana na elimu zao ni utamaduni wa zana za kale za mawe sio utamaduni muhimu katika ulimwengu wa sasa wa taarifa. Ulimwengu wa sasa hausemi kuwa mwenye elimu ndiye atakaye fanikiwa bali unasema kuwa mwenye taarifa sahihi ndiye atakaye fanikiwa.  Yaani utofauti wa taarifa ya kitu fulani kati yako na mtu mwingine ndio utaamua nani afanikiwe. Utaratibu wa kasome mwanangu ili uje kuwa na maisha mazuri kutokana na ajira yako ni utaratibu ambao umepitwa na wakati sasa. Na kwa mujibu wa mwandishi mashuhuru wa marekani bwana Robert Kiyosaki huu ni utaratibu mbovu yeye anasema kuwa kitakachomfanya mtu afanikiwe ni elimu juu ya pesa na elimu hii haifundishwi shuleni badala yake mtu anatakiwa ajifunze kutoka kwa wazazi wake. Mwandishi huyu anasisitiza katika umuhimu wa elimu juu ya fedha maana haifundishwi darasani na ndio maana hata wenye degree na masters zao wanakuwa masikini na waliokosa mafanikio.
Sisemi kuwa elimu ya darasani sio elimu ya msingi, ni elimu ya msingi sana tena sana kwa ulimwengu wa leo ambao umejaa ushindani sana ambapo ni muhimu kwa mtu kupata angalau degree hata moja, nachopinga ni kuwa elimu hii isitumiwe kama tiketi ya kufanikiwa yaani kwana kwamba mwenye elimu ya darasani ndiye mwenye uhalali wa kufanikiwa hili ndilo nilipingalo maana kuna watu ambao wana elimu na wanamafanikio na wakati huo huo kuna wale wenye elimu hiyo na hawana mafanikio, na kwa upande wa pili wa shilingi kuna wasio na elimu na wanamafanikio na hapo hapo kuna watu ambao hawana elimu na hawajafanikiwa.
Kinachohitajika katika mafanikio ni namna ya kujifunza kupitia watu waliofananikiwa na kutumia mafanikio yao kama somo na sio kitu kingine. Elimu ya darasani ni kichocheo tu ambacho peke yake hakiwezi kufanya kazi. Hivyo usikae kisa huna elimu ya darasani na ukasema huwezi kufanikiwa. Pia jifunze kuhusu elimu ya pesa maana ndio muhimu sana kwa ulimwengu wa sasa.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.

0754612413/0652612410.

No comments:

Post a Comment