Friday, December 18, 2015

Kitu Hiki Kimoja Kinakufanya Usifanikiwe Maishani.


Habari ya leo na wakati huu ndugu msomaji wa mtandao Huu wa kona ya maarifa, ni matumaini yangu Kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vizuri katika kutekeleza majukumu yako ya kila Siku.
Leo nataka kukushirikisha jambo muhimu ambalo wengi wetu tumekuwa tukilifanya, lakini limekuwa likitulete madhara makubwa sana jambo lenyewe ni  Kukata tamaa. Tumekuwa tukijijengea tabia hii Mara kwa Mara na wengine tumefikia kiasi cha kuhararisha tabia hii na kuifanya kama sifa fulani yaani kuna watu wanaona Kuwa ni fahari kwao wao kukata Tamaa, na wana haki ya kufanya hivyo.
Nataka ujiulize maswali haya muhimu (1) je unauhakika hapo ulipofika ndio mwisho wa uwezo wako mpaka unakata tamaa? (2) je wewe pekee ndiye wa kwanza kupitia mikasa hiyo? (3) je umefanya juhudi gani kutatua tatizo hilo? (4) je umewaona wataalamu na je wataalamu hao ndio wa mwisho duniani?. Maswali yanaweza kuwa mengi sana lakini hayo ni baadhi tu ya maswali mengi ambayo inabidi ujiulize.



 Kuna watu ambao binafsi huwa wananisikitisha sana watu Hawa ni wa aina mbili ambao nambari Moja ni wale ambao hufanya Mara moja na kukata Tamaa bila kujaribu Mara ya pili. Na watu wa aina ya pili ni wale ambao wanakata tamaa bila hata kujaribu. Yaani Hawa ni wale mabingwa wa kutumia historia za watu walioshindwa tu bila kujua kuwa katika yale ambayo wengine wameshindwa kuna wengine wamefanikiwa katika hayo hayo. Hawa ni wale ambao wamejaa mtizamo hasi na kawaida yao ni kutazama upande mmoja wa shilingi. Yaani wao huwa wanaangalia mabaya tu, kwa sababu mawazoni mwao wanawaza ubaya tu.
Pengine nikujuze sababu kadhaa ambazo zinaweza kukufanya ukawa na tabia hii ya kukata tamaa. Sababu hizo ni pamoja na;-
1. Kuamini kuwa maishani kuna njia ya mkato ya kuelekea mafanikio, wapo watu ambao wamejaza bongo Zao na fikira kuwa maishani kuna njia ya mkato ya kuelekea mafanikio. Sasa watu kama hawa pindi waanzishapo safari ya kuelekea mafanikio ndipo hukumbuka kuwa yale mawazo yao yalikuwa ya uongo tu maana kwa hakika maishani hakuna njia ya mkato, na hapo ndipo huwa wanakata tamaa kabisa maishani.
2. Kukosa uvumilivu, kuna watu amabao sio wavumilivu kabisa, hawa ni wale wenye kupenda mafanikio ya haraka haraka hivyo wanapokuja kugundua kuwa mafanikio hayahitaji haraka kiasi hicho hukata tamaa mapema.
3. Mtu asiyetambua neno hasara, kuna watu ambao Hawatambui kama kuna kitu hasara hasa katika biashara wao huamini na kujua Kuwa biashara ina faida tu sasa watu kama hawa wapatapo hasara huwa ni wepesi sana wa kukata tamaa maana hawakukijua hicho kitu wala kujiandaa nacho hapo kabla.
4. Kukosa malengo, kuna watu ambao hawana utamaduni wa kujiwekea malengo binafsi, hivyo wao huishi kwa kutangatanga yaani wao huamia shughuli moja kwenda nyingine maana hawana malengo na ndio maana hukata tamaa. Ukiwa na utamaduni wa kujiwekea malengo na kuyasimamia ili kuyatekeleza kamwe huwezi kukata tamaa.
5. Kutumia historia za watu vibaya, Watu wanaokata tamaa ni wale wenye kuzitumia historia za watu kimakosa. Siamini kama kweli historia za watu zipo ili zitutishe bali naamini kuwa historia za watu zipo ili zitufunze. Hata katika historia ya mtu aliyefanikiwa kuna anaeweza kujifunza vitu toka kwake na akakata Tamaa. Hivyo basi usiruhusu historia ya mtu mwingine iamue maisha yako na kukufanya ukate tamaa.
Ukitawaliwa na tabia ya kukata tamaa sahau kuhusu mafanikio ukiwa mtu wa kukata tamaa kamwe huwezi fanikiwa hata ufanyaje maana mafanikio huitaji uvumilivu na kuto kata tamaa mapema.
Rafiki yako,
Baraka Maganga.
Bmaganga22@gmail.com.
0754612413/0652612410.


No comments:

Post a Comment