Thursday, December 17, 2015

Zifahamu Sumu Nne (4) Za Mafanikio Yako.


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vizuri katika harakati zako za kutekeleza majukumu yako na hatimaye kuzifikia ndoto zako.
Wengi tumekuwa tukiimba wimbo mafanikio mara kwa mara, lakini jiulize ni wangapi waimbao wimbo huu wanafanikiwa? Nadhani jibu ni wachache kati ya wengia ambao wanaimba wimbo huu wa mafanikio ambao wanafanikiwa kweli. Sababu za kutokufanikiwa zinaweza kuwa nyingi sana miongoni mwetu. Hapa nina kuletea sumu nne za mafanikio, yaani vitu vinne ambavyo vinaweza kuhatarisha mafanikio iwe umeyapata tayari, au ndio unaelekea kuyapata.
1 .lawama, hii ni sumu nambari moja ya mafanikio, ukijiona wewe ni mtu wa kulaumu mara kwa mara jua kuwa huwezi kufanuikiwa au kwa lugha rahisi ni kuwa jua kuwa mafanikio yatakukimbia. Ukiwa wewe ni mtu wa kuilaumu serikali, wazazi, waalimu, wanafunzi wenzako, mpenzi wako au mkeo/mumeo, tambua kuwa hutoweza kufanikiwa. Lawama hukuondoa katika mafanikio au katika mstari wa kuyapata mafanikio kwa kuwa  lawama inakufanya uyakimbie majukumu. Yaani tabia ya mtu anayelaumu ni kuwa huwa anawalaumu watu hata kwa yale ambayo yanamhusu yeye moja kwa moja. Mfano mwanafunzi hajasoma vizuri kwa ajili ya mtihani wake wa mwisho lakini akilini mwake anawazo la kufaulu, inapotokea amefeli huanza kuwalaumu waalimu kuwa hawakufundisha ipasavyo.
2.  visingizio, huyu ni pacha wa lawama, kwanini nimesema hivyo ni kwa kuwa lawama na visingizio vinaendana kimatendo na kitabia. Yaani wakati mwingine huwa ni vigumu sana kutofautisha mtu mwenye kulaumu na mtu mwenye visingizio. Wakati yule wa kulaumu anawalaumu watu basi yule wa visingizio huwasingizia watu. Yaani mfano katika mfano wetu hapo juu wa mwanafunzi aliyefeli kuwalaumu waalimu, basi hapa atawasingizia waalimu kuwa hawakufundisha vizuri ndio maana akafeli wakati sio. Watu wengi wamekuwa wakiwasingizia watu wengi sana juu ya kutokufanikiwa kwao wapo wanaowasingizia wazazi, waalimu, madaktari, serikali n.k. lakini ukiwachunguza watu hawa utagundua kuwa kadri wanavyosingizia ndivyo wanavyojiweka mbali na mafanikio. Hivyo basi achana na habari za kusingizia singizia. Kama ulikuwa hujui basi faha,u kuwa visingizio pia hutuondelea uwezo wa kufikiri na kutufanya tushindwe hata kutatua matatizo madogo na badala yake tusingizie tu watu wengine. Hivyo acha kabisa tabia hii.
3. hofu, sumu nyingine ya mafanikio ni hofu, mara nyingi watu wamekuwa na mipango na mawazo makubwa sana ambayo yanaweza kuwafanya wakafanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini punde tu watakapo kujalibu kutekeleza mipango yao na malengo yao, hofu huja na kupeperusha mipango na malengo yao na huo ndio huwa mwisho wao. Anza kwa kupinga hofu mara moja kama kweli unataka kufanikiwa. Utakapoweza kujikwamua katika mtego huu wa hofu basi mafanikio yatakuwa halali yako. Hofu itakukosesha mambo mengi kama ukiiruhusu ikutawale, na njia moja wapo ya kukabiliana na hofu ni kufanya kile ambacho unakiuogopa zaidi kuliko vingine.
4.Kuhairisha mambo,jiulize leo hii ni mara ngapi umekuwa ukitaka kujihusiha na jambo fulani, tena la msingi na ambalo lina tija kwako, lakini ghafla ukatishwa tu kidogo au ukaingiwa na hofu kidogo na matokeo yake unaacha kulifanya jambo hilo husika. Leo hii watu wengi wamekuwa wakibaki pale pale walipo kwa kuwa wametawaliwa na tabia ya kuhairisha mambo. Kama kweli unataka kufanikiwa hakikisha unaipinga vikali tabia hii kwani kuhairisha mambo ni hatari sana kwa maendeleo yako. Wapo watu wengi ambao wamekuwa wakiona ufahari kuhairisha mambo yao ya msingi, na wasijue kuwa wanajiua wenyewe alafu baadae huanza kuwalaumu na kuwasingizia watu wengine kumbe sababu ni kuwa watu hawa wametawaliwa na roho ya kuhairisha mambo. Ndio maana siku hizi kuna msemo maarufu huko mtaani kuwa “watu wengi wanakufa na ndoto zao, hivyo ndoto nyingi zipo makaburini”, ni kwasababu ya tabia ya kuhairisha mambo.
Kwa ujumla sumu hizi nne za mafanikio, zinaweza kutokana na sisi wenyewe au kutokana na wale wanatuzunguka. Hilo lisikupe shida bali jambo la msingi ni kuwa wewe pingana nazo kwa kuwa umeshazifahamu vizuri na madhara yake pia umeyafahamu.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.

0754612413/0652612410.

No comments:

Post a Comment