Habari za leo ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya
maarifa ni matumaini yangu kua hu mzima na waendelea vizuri katika kuyasaka
mafanikio. Kama ilivyokawaida ya mtandao huu, ambao umejidhatiti katika
kuhakikisha kuwa unakupatia maarifa ambayo ukiyatumia vyema yatakuwa kama
chachu na kirainisho katika safari yako ya mafanikio. Leo natakaa ujifunze
jambo hili nndugu msomaji nalo ni kujifunza kupitia vitu hivi viwili. Je vitu
hivyo ni vipi?, endelea….
Leo nataka ujifunze kupitia vitu viwili kama nilivyokutambulisha
hapo awali lakini najua vitu hivyo bado ni fumbo kwako. Basi vitu hivyo ni hivi
hapa:-
1.
Vikwazo, najua wengi wetu tunaamini
kuwa vikwazo vipo kwa ajili ya kutuzamisha au kutukwamisha na kutudidimiza
kabisa na kutufanya tusipige hatua yoyote ile katika maisha. Hii ni imani ya
watu wengi juu ya vikwazo. Sasa leo
nataka uvunje hii imani kabisa maana haina msingi wowote kwa wale ambao
wanataka mafanikio,lakini kama hautaki kufanikiwa endelea kushikiria imani hiyo
hivyo hivyo ilivyo.
Nimesema uachane na imani kuwa vikwazo vipo
ili vikukwamishe na badala yake tumia vikwazo kama somo ambalo ukilielewa basi
itakuwa chachu ya mafanikio yako. Vikwazo huja kwa malengo fulani haviji tu. Vikwazo
vinaweza kuja kwa sura kama hizi:-
(a)
Vikwazo huja
ili kutukomaza, kumbuka kuwa safari ya mafanikio sio safari nyoofu siku
zote na wala sio safari rahisi, hivyo basi uwepo wa vikwazo upo ili kutukomaza
vyema. Kabla hujapata mafanikio vikwazo vipo ili kukufanya ukabiliane navyo na
ukishaweza kufanya hivyo hata pale utakapofanikiwa basi hata vikija vikwazo wewe
utakuwa na uzowefu navyo na hivyo hauto shindwa kupambana navyo. Yaani vikwazo ni kama mafunzo ya awali kwa
askari ambaye hajawa askari bado.
(b)
Vikwazo huja
kupima imani zetu, muda mwingine vikwazo huja kama kipimo cha imani zetu
yaani kupitia vikwazo imani zetu hupimwa. Tambua kuwa kuna uhusiano wa moja kwa
moja kati ya mafanikio na imani ya mtu yaani anaeamini kuwa atafanikiwa mara
nyingi huwa anafanikiwa na asiye amini kuwa atafanikiwa nae huwa hivyo. Hivyo basi
vikwazo huja kupima imani zetu. Kumbuka mfano wa ayubu katika biblia
ambaye aliwekewa vikwazo mbalimbali ili tu kupimwa imani yake.
(c)
Vikwazo huwa
kipimo cha uvumilivu, mafanikio huusisha watu ambao ni wavumilivu watu
ambao wanaweza kukisubiria kile wanachokitaka hata kwa miaka saba mpaka kumi
hata kama hakiji. Na wala hayahusishi watu ambao wanakata tama kirahisi rahisi.
Hivyo basi vikwazo huja ili kutaka kupima uvumilivu wako.
2.
Makosa, hakuna asiyekosea katika kutaka kujifunza kitu hapa duniani, ni
vyema ujenge tabia ya kujifunza kupitia makosa yako na wala sio vinginevyo. Unapofanya
makosa usianze kujilaumu kuwa kwanini imekuwa hivi au kwanini nimefanya hivi
nina tatizo gani. Bali jifunze kupitia makosa unayoyafanya maana ni jambo la
kawaida kukosea. Pengine makosa huweza kuwa na malengo haya yafuatayo:-
(a)
Kukurekebisha,
makosa huja ili yakurekebishe na hii hutokea haswa pale ambapo unajiona au
kujikuta kuwa umekamilika. Mfano unaweza kuwa unajifunza ukajiona umeshafuzu
masomo husika, kwa kuwa hakukuwa kosa ambalo ulilifanya hapo awali hivyo kosa
linapojitokeza linakuwa limekuja kukurekebisha ili ujue kuwa bado kuna mengi
inabidi ufanye.
(b)
Kukuongezea
ujuzi, makosa huja ili kukupatia ujuzi mpya hasa kwa yale mambo ambayo
ulikuwa huwezi kuyafanya katika hali ya kujaribu hiki na kile alafu ukawa
unakosea hapo ndipo hujikuta umepata ujuzi fulani.
(c)
Kukufanya
uende na wakati, hii hutokea kwa wale ambao hufanya mambo kwa mazoea, pindi
wafanyapo makosa kutokana na kuwa wamefanya vitu kinyume na wakati ndipo huwa
wanashituka kuwa wapo nyuma ya wakati. Nini kimewafanya washituke basi, hakika
ni makosa waliyoyafanya.
Kimsingi mtu anaetaka kufanikiwa huwa anatumi vikwazo na makosa kama
darasa na wala sio kama nuksi au mkosi. Hivyo basi jifunze nawe kufanya hivyo
maana naamini unatamani kufanikiwa na utafanikiwa tu.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
Simu: 0754612413 au
0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com.
No comments:
Post a Comment