Monday, December 7, 2015

Lini Basi Itakuwa Zamu Yako?


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na mwenye kiu ya kuendeleza harakati za kuyasaka mafanikio. Nami nakusihi endelea na hali hiyo wala usikate tamaa, maana yote yanawezekana tu swala ni imani na juhudi tu ndio zitatufanya tuweze kuyatekeleza yale tuliyojiwekea  kama malengo kwetu.
Ni wasaa mwingine tena ambapotumekutana tena ilikuweza kupeana maarifa mapya ambayo yatatufanya tuwe bora na hatimaye kuweza kuyafanikisha yale tuliyojiwekea. Leo kuna swali moja ambalo nataka ujiulize ndugu msomaji wa makala hii, swali lenyewe ni kuwa ni lini haswa itakuwa zamu yako?. Nataka ufanye hivyo kwa kuwa naamini kuwa akili ya binadamu huanza kufanya kazi pale inapochochewa kufikiri juu ya jambo fulani tofauti na pale inapokuwa imekaa tu bila kuchochewa kufanya jambo lolote.Umekuwa ukiona wenzio wakifanikiwa katika biashara zao, miradi yao, kazi zao, elimu zao n.k. nachotaka kumaanisha hapa ni kuwa katika kila ngazi ambayo upo wewe sio wa kwanza yaani kuna watu ambao wamekutangulia katika kufanya jambo fulani. Kama wewe ni mfanyabiashara kuna wafanyabiashara maarufu na wakubwa zaidi yako, mchezaji, mwanafunzi, mfanyakazi n.k. wapo walio juu yako sasa tunaelewa kuwa mtu anapokuwa amefanya mambo makubwa naya msingi huwa anakuwa anasifika, anapewa heshima kubwa, anachukuliwa kama mfano wa kuigwa n.k. najua vitu hivyo huwa unakutana navyo katika maisha yako. Sasa ulishawahi kujiuliza kuwa ni lini nawe itakuwa zamu yako kusifika au kusifiwa kwa jambo fulani,au kutumiwa kama mfano wa kuigwa?.
Kila mtu maishani huwa kunakuwa mtu mwenye mafanikio ambaye yeye huvutiwa nae mfano mchezaji chipukizi wa Tanzania anaweza kuvutiwa na kiwango cha Mbwana Samtta na akatamanikuwa kama yeye sasa jambo la msingi la kujiuliza ni kuwa ni lini unataka kuwa kama huyo Mbwana Samatta. Pengine unatamani kuwa mfanyabiashara mkubwa na mwekezaji mkubwa na mashuhuri kama Reginald Mengi, lakini hujui ni lini na nivipi utakuwa kama yeye, sasa jambo unalotakiwa kujiuliza nikuwa ni lini utakuwa kama mengi?. Pengine unatamani kuwa mchekeshaji maarufu kama Masanja Mkandamizaji wa orijino komedi, unachotakiwa kufanya ni kujiuliza tu ni lini haswa unataka kuwa hivyo?
Nimeshakwisha kutangulia kusema hapo awali kuwa akili ya binadamu hufanya kazi pale inapoulizwa maswali kama vile kivipi?, kwanini?, wapi?, saa ngapi? Na memgine mengi kulikopale inapokuwa imeachiwa tu na kukaa tu huru, bila kufanya kazi yoyote. Kwa kuwa akili ya binadamu hufanya kazi au huwa katika hali ya kufanya kazi pale inapokuwa inaulizwa maswali mbalimbali kuliko pale ambapo haiulizwi maswli hivyo basi jijengee mazoea ya kujiuliza maswali mbalimbali kila wakatiili tu kuhakikisha unapata majibu ambayo yatakuwa msaada mkubwa kwako na kukupa uvumbuzi wa majibu ya changamoto zako.
Pili nataka ujiulize swali la ni lini haswa itakuwa zamu yako ili majibu ya maswali yako uyatumie katika kupanga malengo yako. Watu wengi wamekuwa hawapangi malengo yao kwa kuwa wamekuwa hawajiulizi maswali mbalimbali ukijiuliza swali mfano ni lini unataka kuwa mfanyabiashara maarufu na ukajijibu kuwa  mwezi mei 2017, hili litakuwa tayari kama lengo lako ambapo utaifanya akili yako ifanye kazi ili kuhakikisha jambo hili linakuwa ukweli kwako na hatimaye kulitekeleza.
Ni muhimu kujiuliza maswali mbalimbali juu ya ni lini unataka kupata kitu Fulani na ni lini utakuwa mtu Fulani. Jingine kujiuliza swali ni lini haswa itakuwa zamu yako, kujulikana, kusifiwa na kutumika kamamfano wa kuigwa?, kutaiamusha akili yako na kuifanya ifanye kazi ya kukupatia majibu.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka maganga,

0754612413/0654612410

No comments:

Post a Comment