Friday, January 29, 2016

Lazima Uwe Tayari Kufanya Jambo Hili Katika Safari Yako Ya Kuelekea Mafanikio.


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumani yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri katika kupambana ili kuhakikisha kuwa

Thursday, January 28, 2016

Fahamu Leo Kuwa Maneno Yana Nguvu Sana Katika Maisha Yako.

Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumani yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri katika kupambana ili kuhakikisha kuwa unapata kile unachokitafuta katika maisha. Kwa kuwa lengo la mtandao huu ni kuhakikisha kuwa unapata vitu vya kukusukuma mbele zaidi katika kuelekea safari yako hiyo ya mafanikio, basi nasema pambana endelea kupambana bila kuchoka hata pale unapohisi umechoka jilazimishe maana kuridhika baaada ya hatua chache huleta anguko.

Najua umekuwa ukupambana sana katika kuhakikisha kuwa unafanikisha mambo yako lakini kuna wakati ukikaa na kupiga tathimini unajikuta ukitamani kukata tamaa hii ni baada ya kuona au kupata matokeo ya tathimini yako  na hapo ndipo wengi huwa tunapatwa na hofu ya kuacha na mara nyingi sana huwa tunaanza kuona ni kama hatupigi hatua hivyo basi tunatamani kuachana na harakati zetu ambazo tumekuwa tukizianzisha na kuamini kuwa zitakuwa na msaada kwetu. Unatamani kuacha nakuona unasoma hii makala na huku unasema dah yaani sioni matokeo yoyote, niliambiwa hivi na vile, nilisoma hivi na vile lakini sioni matokeo yake, naacha bwana.








Kabla hujafikiria kufanya kitu hicho unachotaka kufanya nataka ujichunguze sehemu hii moja, yachunguze maneno yako. Kabla hujafikiria kufanya uamuzi wa kuacha kufanya jambo fulani kwa kuwa tu hujapata matokeo mazuri yachunguze maneno yako,  narudia tena yachunguze maneno yako. Unajua binadamu tuna namna mbili za kuongea, nakuona unashangaa kusikia namna mbili za kuongea, namaanisha kuwa tunakule kuongea kwa kawaida ambapo tunaongea na wenzetu huku kumezoeleka na ni maarufu lakini aina ya pili ni ile ya kujiongelesha wenyewe, yaani  kuna muda huwa unajikuta uwapo mwenyewe kuna maneno unayojiongelea mwenyewe sasa maneno haya ndio nayo taka uyachunguze.
Jiulize mwenyewe hapo ulipo je kauli unazojisemesha mwenyewe ni hasi au chanya, nakuona unasita kutoa jibu kwa kuwa unajua ni hasi. Wengi tumekuwa hatujui nguvu iliyopo katika maneno yetu ambayo tumekuwa tukijisemesha mara kwa mara na ndio maana tumekuwa tukihangaika kuchunguza mchawi wa maisha yetu kumbe sisi wenyewe ndio tunao jiloga. Unajiloga kwa maneno yako mwenyewe alafu unajikuta unalalama eti nalogwa na ndugu zangu hawataki nifanikiwe kabisa. Dah wewe, nani asiyetaka ufanikiwe wewe au wao?, jibu unalo mwenyewe mpaka hapo.

Pengine unajiuliza sasa mbona mimi sielewi ni kauli gani sasa, sawa mimi nipo kukuletea hizo kauli, mara ngapi umekuwa ukijisemea kuwa wewe unamikosi, nuksi au gundu. Ndio umekuwa ukijiambia ukisema unamikosi, gundu au nuksi maana yake huwezi kufanikiwa sasa kwanini unataka kufanikiwa ikiwa kila siku unajisemesha mwenyewe kuwa hauwezi kufanikiwa. Huoni kuwa unafanya kazi ya kuchanganya maji machafu kwenye maji masafi alafu unategemea maji masafi yaendelee kuwa masafi. Eti unataka kuacha kufanya mambo ya kukusogeza mbele kisa unamikosi, na ukiamini na kujisemesha kuwa unamikosi kweli utakuwa nayo tena mingi haswa. Acha kujisemesha na kujitazama kama mtu mwenye mikosi, gundu, na nuksi. Acha mara tu baada ya kusoma makala hii.

Mara ngapi umekuwa ukisalimiwa asubuhi unaambiwa habari ya asubuhi ndugu unajibu aa bora kumekucha, au dah bora ya jana, hivi unajua maana ya hayo maneno unayoyasema. Unayasema maneno hayo alafu akilini mwako unawaza kuwa biashara yako itakwenda sawa. Nani kakudanganya wewe acha kujidanganya, ukisema bora kumekucha maana yake haukutaka kukuche sasa unaendeleaje na shughuli kama hautamani kukuche?, ukisema dah bora ya jana maana yake siku ya leo ni ya ovyo sasa unategemea vipi kudharisha katika siku mbovu?, anza siku yako na kauli nzuri na mafanikio utayaona
.
Nakuona kila ikifika ijumaa unajifanya mzungu eti “thanks God it is Friday” ukimaanisha asante mungu kwa kuwa leo ni ijumaa. Unajua tafsiri yake hapo tafsiri yake ni kuwa siku zote zilikuwa mbaya kwako ndio maana unafurahia kuiona ijumaa. Sasa kwanini utake kufanikiwa jumatatu wakati kwako ni mbaya? Au alhamisi wakati ilikuwa mbayas?
Kuwa makini na kauli unazojinenea mwenyewe maana mnamo maneno mna nguvu sana, maneno huumba hilo waswahili waliliona na sio kuumba tu, maneno yanaamua maisha yetu ya sasa na baadae.hivyo basi kuwa makini sana tena sana juu ya maneno yako kama kweli unataka kufanikiwa. TWENDE SOTE.


Ni mimi Baraka Maganga, rafiki na mwalimu wako.  Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0652612410. Au kwa barua pepe ambayo ni Bmaganga22@gmail.com.  

Wednesday, January 27, 2016

Hivi Ndivyo Mambo Yatakavyokuwa Baada Ya Wewe Kufanya Kitu Hiki Kimoja.


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea kupambana kwa hali na mali ili tu uweze kufanikisha yale ambayo umekuwa ukiyahangaikia mara kwa mara. Vizuri endelea kupambana naama hakuna kitu cha bure hapa duniani, maana hata miujiza huja kwa wale ambao huwa wanakuwa wakiitafuta miujiza hiyo. Sio waliokaa tu wakisubiri miujiza hivyo nakusihii endelea kupambana ndugu msomaji wa mtandao huu.






Mafanikio yanahitaji ahadi ndugu mpendwa msomaji wa makala hii. Hili ni jambo ambalo ningependa uweze kulifahamu kuanzia sasa,kuwa mafanikio yanahitaji ahadi. Yaani baada ya kujiwekewa malengo unapaswa sasa kuweka ahadi juu ya utekelezaji wa malengo yako. Pengine umekuwa ukijiwekea ahadi bila kujua ahadi ni kama pale unaposema kuwa nataka kupunguza uzito likiwa kama lengo lako sasa pale unaposema lazima kila siku nifanye mazoezi kwa muda wa nusu saa, tayari hapo unakuwa umejiwekea ahadi katika maisha yako. Au unasema nataka kuamka kila siku saa kumi na moja alfajiri ili niweze kufanya shughuli zangu za ndani kabla ya kwenda katika mihangaiko yangu, kuamka saa kumi na moja ni ahadi tayari uliyokwisha jiwekea katika maisha yako.

Tumekuwa watu wa kujiwekea ahadi nyingi nyingi tena ahadi zingine zinakuwa kubwa na zenye kututisha kiasi kwamba tunaweza kufikiri kuwa hatutoweza kutimiza ahadi hizo. Kimsingi ahadi na malengo ni vitu ambavyo vinaenda sambamba na vinaweza kukupatia shida katika kuvitofautisha lakini tofauti ni kuwa malengo yanaanza alafu ndio ahadi hufata. Sasa kwa kuwa ahadi ni hatua moja wapo katika kuyaelekea mafanikio basi ni vyema ukatambua kuwa yafuatayo ni mambo ambayo yatakukumba baada ya kuwa umejiwekea ahadi zako wewe mwenyewe:-

1.    Vikwazo vitaibuka, baada ya kuwa umeshajiwekea ahadi zako vikwazo vitaibuka sana tena vingi kuliko unavyodhani. Vitaibuka vikwazo vya aina mbili ambavyo ni vikwazo vya nje na vya ndani. Vikwazo vya nje ni vile ambavyo vitatokana na wale watu wanaokuzunguka kama vile marafiki, ndugu au hata wazazi, ambao wanaweza kukuzuia wewe katika kuweza kutekeleza ahadi yako, zinaweza zikawa kauli zao juu ya ahadi yako au hata kukucheka na kukupinga zaidi na zaidi. Vikwazo vya ndani ni vile ambavyo unajiwekea mwenyewe kama vile uvivu, kukosa umakini, kupuuzia ahadi yako n.k. hivyo vikwazo vyote hivi visikutishe katika kuweza kuishikiria ahadi yako na hatimaye kuweza kuitekeleza ipasavyo.

2.    Utafanya makosa, katika kuelekea kutekeleza ahadi yako utafanya makosa kadha wa kadha, makosa haya yapo ili tu kukufunza. Kama unataka kufanikiwa ni lazima uwe na mtazamo tofauti juu ya makosa unayoyafanya. Kama kweli unataka kusonga mbele katika safari yako ya mafanikio sasa ni wakati wa kubadili mtazamo wako katika makosa unayoyafanya. Amini kuwa makosa yapo tu ili kuweza kukufunza na sio kingine. Hivyo basi usirudi nyuma katika kuitekeleza ahadi yako uliyojiwekea, makosa yasikutishe bali jifunze jifunze kutokana na makosa.


3.    Utavunjwa moyo, hili nalo litakukumba kwa kiasi kikubwa na hasa kitakacho kuvunja moyo ni pale utakapo kuja kujikuta umefanya makosa mengi na pale utakapo ona kuwa unakumbwa na vikwazo vingi sana. Mambo haya yote yanaweza kukuvunja moyo  kwa kiasi kikubwa sana, lakini kwa wewe unae yasaka mafanikio kamwe usivunjike moyo bali wewe endelea kuishikiria ahadi yako.

Tambua kuwa haya yote ni majaribu ambayo dunia itakuwekea ili kukupima ni jinsi gani uko makini juu ya ahadi yako. Mara nyingi watu wengi hutamani kuachana na ahadi zako, lakini wewe unaye yasaka mafanikio hutakiwi, hutakiwi kukata tamaa kamwe. Kama alivyosema bwana winstone Churchill “never never never give up” au kama alivyosema bwana james .J. Gorbelt “you become a champion by fighting one more round, when things are tough you fight one more round”. Yaani unakuwa mshindi baada ya kupambana hatua moja zaidi na zaidi hata kama mambo yakiwa magumu pambana hatua moja zaidi.
Twende sote.

Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com


Tuesday, January 26, 2016

Ni Muda Wa Kuachana Nazo Sasa

.
Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea kupambana kwa hali na mali ili tu uweze kufanikisha yale ambayo umekuwa ukiyahangaikia mara kwa mara. Vizuri endelea kupambana naama hakuna kitu cha bure hapa duniani, maana hata miujiza huja kwa wale ambao huwa wanakuwa wakiitafuta miujiza hiyo. Sio waliokaa tu wakisubiri miujiza hivyo nakusihii endelea kupambana ndugu msomaji wa mtandao huu.






Je unakumbwa na wasiwasi wa kufanikiwa kutokana na historia yako ya nyuma zile kauli wanazokuambia wanaokuzunguka zinakurudisha nyuma katika hali ya kutaka kusonga mbele katika kuhakikisha kuwa unafanikiwa katika maisha yako. Je? unajua ni kwa nini kauli ulizopandikizwa kutoka utotoni  zinaendelea kukurudisha nyuma katika safari yako ya kuyaelekea mafanikio, ni kwasababu umeziamini na kuzifanya kuwa ukweli wako. Sasa jiambie mwenyewe kuwa ni wakati wa kuachana nazo sasa.

Zile imani ulizojijengea zamani ya kuwa hutofanikiwa na kuwa tajiri kwa kuwa wazazi wako ni masikini, imani ya kuwa huto fanikiwa kwa kuwa wazazi wako ni masikini, ni muda wa kuachana nazo maana hazina msingi wowote na wala hazikujengi wala kukusaidia chochote bali zinakudidimiza zaidi na zaidi badala yake wewe pambana kweli kweli hata kama unatokea katika familia masikini, na mafanikio utayaona tu, maana wapo waliokuwa kama wewe na waliotokea chini kama wewe na wakafanikiwa hivyo hilo lisikupe shide sana bali achana na hiyo imani.

Uliambiwa kuwa wewe ni mjinga na hauwezi chochote na mwalimu wako, ni wakati wa kuachana na kauli hii ambayo ulikuwa umeiamini kwa kuwa ilitoka kwa mwalimu wako na kupitia kigezo cha sifa ya ualimu basi ukaamini kuwa hauto fanikiwa fanya kama Thomas Edison ambaye pamoja na kukataliwa na walimu watatu tofauti kuwa hafai kuwa mwanafunzi wa kujifunza chochote lakini alijifunza na kuwa mwanasayansi mkubwa duniani na mpaka leo anaheshimika kama mwanasayansi mashuhuri duniani. Hii ni kutokana na sababu kuwa yeye aliachana na kauli za waalimu wake, hivyo basi hata wewe unaweza kufanya hivyo na ukafanikiwa pia, hivyo achana na kauli mbovu alizokuambia mwalimu wako.

Walikuita mbumbumbu mtaani kwenu, mtaani kwenu wewe ndio ulionekana kuwa mtoto mbumbumbu kuliko wote na ukafutwa kabisa kwenye watoto ambao wanaweza kuleta mabadiliko yoyote au kuleta mafanikio yoyote ambayo yataisaidia jamii yako na wewe ukaamini kuwa kweli hauwezi kutokana na maneno yao. Ni muda sasa wa kuachana na kauli hizo ambazo hazina msingi wowote bali ni za ukatishaji taama.

Lazima utambue kuwa  tunakuwa kadri tunavyofikiri, hata bibilia imeliandika hilo kuwa kadri ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo huwa. Hii inamaana kuwa wewe mwenye ndiye mwamuzi wa maisha yako yaani ni kadiri unavyojiona wewe mwenyewe ndivyo huwa unakuwa. Na biblia haijasema kadri wamwonavyo watu ndivyo mtu huwa, hilo ni jambo ambalo halijaandikwa wala kusemwa. Hivyo basi kama wamesema hauwezi kufanikiwa ni wao na sio wewe, wewe usizifuate kauli zao ambazo hazina msingi wowote bali wewe endelea kushikilia ukweli ambao unauona nafsini mwako na katika kuushikilia ukweli huu uwe ni ukweli ule ambao ni  chanya achana na kauli hasi kabisa maana hazikufikishi popote.

Kumbuka nimesema ni muda wa kuachana nazo zile kauli zote ambazo ni hasi, ni muda wa kuachana nazo maana hazina msaada kwako ila zina kudumaza na kukudidimiza zaidi na zaidi. Na kubwa zaidi juu ya kauli chanya ni kuwa haziwezi kukuletea mafanikio yoyote.

Twende sote.

Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com



Monday, January 25, 2016

Wajibika Ipasavyo Kama Kweli Unataka Kufanikiwa.


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea kupambana kwa hali na mali ili tu uweze kufanikisha yale ambayo umekuwa ukiyahangaikia mara kwa mara. Vizuri endelea kupambana naama hakuna kitu cha bure hapa duniani, maana hata miujiza huja kwa wale ambao huwa wanakuwa wakiitafuta miujiza hiyo. Sio waliokaa tu wakisubiri miujiza hivyo nakusihii endelea kupambana ndugu msomaji wa mtandao huu.







Naamini umekuwa ukipambana sana katika kuhakikisha kuwa unafanikiwa katika yale ambayo unayahangaikia nami na kusihi uendelee kupambana maana katika mahangaiko ndiko mafanikio hutokea. Lakini lazima ujue kuwa lazima kitu hiki ukifanye kama unataka kufanuiki. Kitu hiki ni kitu muhimu sana katika maisha yetu na mafaniko kwa ujumla lakini jambo la kushangaza ni kuwa tumekuwa hatulitili maanani sana na ndio maana wengi wetu tumekuwa tukijikuta hatusongi mbele wala nini ila tunabaki pale pale au kurudi nyuma kabisa kimaisha.

Huwa unapata picha gani pindi unapoona mfanyakazi fulani katika kampuni fulani kafukuzwa kazi. Au kasimamishwa kazi kwa muda. Unapata picha gani pindi unapomwona mfanyabiashara fulani kashindwa kibiashara yaani biashara yake imekufa. Unapata wazo gani unapomwona mtu anailaumu serikali yake kwa kushindwa kwake wakati yeye ndiye aliyepaswa kufanya jambo husika. Hakika yote hayo hutokea kutokana na kukosekana kwa kitu hiki kimoja nacho ni uwajibikaji.

Maishani bila kuwajibika tambua kuwa hauto kwenda kokote kule bali utaishia pale pale. Dunia ya sasa imejaa ushindani wa hali ya juu ambao unaongezeka siku hadi siku na atakae weza kusitaimili ushindani huu ni yule tu mwenye kuweza kuwajibika ipasavyo. Kama wewe ni mfanyabiashara na unawajibika bora liende tambua kuwa hauto kwenda popote bali utaishia kufulia tu. Mfanyakazi pia ambae hutaki kuwajibika tambua kuwa utaishia tu kufukuzwa kazi yako hiyo na hatimae kuukaribia umasikini nao utakukaribisha vizuri sana kuliko unavyodhani.

Leo hii takwimu zinaonyesha kuwa kati ya biashara mia moja zinazo anzishwa leo baada ya miaka kumi ni biashara chini ya ishirini ndizo huwa zimekuwa. Hii ni kutokana na uwajibikaji mbovu wa wafanyabiashara husika. Wafanyabiashara hawa wamekuwa hawahangaiki katika kutafuta taarifa sahihi kabla ya kuzianzisha biashara zao na vile vile wamekuwa wagumu wa kuendelea na utafiti baada ya kuanzisha biashara zao, hivyo hata yakitokea mabadiliko wao hawashituki wala nini. Bali huendelea kufanya biashara zao kwa mazoea na matokeo yao hujikuta wamefulia maana hujikuta hawapati wateja. Hii ni kutokana na uvivu ulio letwa na kuto taka kuwajibika kwao na ndio maana wanajikuta wameanguka.

Ukiwa mfanyakazi unajisikiaje pale unapoambiwa tunakuwajibisha kutokana na utendaji wako mbovu angalia leo hii ni watu wangapi wamesimamishwa kazi toka uongozi wa awamu ya tano uingie madarakani na wote sababu zimekuwa zikionekana ni uwajibikaji mbovu na mengine, lakini kubwa ni uwajibikaji mbovu ambao huwapelekea wafanye mambo kiholera holera na matokeo yake ni kuja kuwajibishwa.

Kama unataka kufanikiwa hakikisha unayavaa majukumu yako usisubiri mazingira yaje ya kushitaki na kukuwajibisha vikali. Au usisubiri kufulia kukuwajibishe, ukiwa mfanyabiashara usisubiri anguko la biashara likuwajibishe, mfanyakazi usisubiri kuwajibishwa na bosi wako bali vaa majukumu yako mwenyewe na mafanikio utayaona tu. Ikiwa unasubiri kuwajibishwa basi sahau kuhusu mafanikio na usilizungumzie tena neno hilo.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com