Friday, January 29, 2016

Lazima Uwe Tayari Kufanya Jambo Hili Katika Safari Yako Ya Kuelekea Mafanikio.


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumani yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri katika kupambana ili kuhakikisha kuwa
unapata kile unachokitafuta katika maisha. Kwa kuwa lengo la mtandao huu ni kuhakikisha kuwa unapata vitu vya kukusukuma mbele zaidi katika kuelekea safari yako hiyo ya mafanikio, basi nasema pambana endelea kupambana bila kuchoka hata pale unapohisi umechoka jilazimishe maana kuridhika baaada ya hatua chache huleta anguko.
Mafanikio yanahusu kulipia gharama je upo tayari kulipia gharama hizo?. Ndio mafanikio yanahusu kulipia gharama, mbona unashituka ndugu msomaji, nakuona ukiwa umeanza kutahamaki baada ya kusikia kuwa mafanikio yanahusu gharama. Hii ni kwa kuwa umeanza kuhusianisha gharama na pesa hivyo umeanza kuhisi ni kama unahitaji kujiandaa kwa kiwango fulani cha pesa kisha ukilipie hicho kiasi husika ndipo utakuwa umejikatia tiketi ya kufanikiwa. Kama umewaza hivyo pole sana ndugu msomaji maana gharama nayo maanisha sio pesa bali ni kitu kingine ndugu mpendwa msomaji wangu.

Awali ya yote ningependa kufafanua kwa kusema tunaposema gharama namaanisha kuwa hivi ni vitu ambavyo unatakiwa uvifanye kama kweli unataka kufanikiwa au kuwa mwenye mafanikio. Chukulia mfano kama unataka kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ni lazima ulipe nauli hauwezi kusafiri pasipo nauli kwa hiyo kitendo cha wewe kulipa nauli na kuweza kupata huduma ya kusafiri hii inamaanisha kuwa umekubali kulipia gharama za safari yako.

Unapokuwa unataka kununua kitu fulani hulazimishwi wala kushikiriwa bali unapotaka kununua kitu kwanza ni kile kitu ndicho kinachokuvutia na kwa kuwa umevutiwa nacho basi unatakiwa ukubali gharama yake ndipo uweze kukinunua kitu hicho. Kama haujakubali gharama yake maana yake huta nunua na utakuwa umegoma kulipia gharama yake. Na kubwa zaidi ni kuwa kitu hicho utakuwa umekikosa kwa muda huo mpaka pale utakapo kuwa tayari kulipia gharama yake na kama huta taka hii inamaanisha kuwa maishani mwako hutakuwa na hicho kitu.

Tukirudi katika safari ya kuelekea mafanikio hapa ni rahisi sana gharama za safari ya mafanikio lazima uweze kuzilipia na hapo ndipo utakapo yapata mafanikio. Kama ukishindwa kulipia gharama hizo hiyo inamaanisha kuwa hauto weza kufanikiwa. Gharama za mafanikio ni kama vile uvumilivu, kuweka malengo, kuwa na timu sahihi ya kushirikiana nayo, kuto kukata tamaa, kuwa jasiri, kuwa na hamasa ya kupambanan.k. hizi zote ni gharama ambazo inabidi uzilipe na hapo ndipo mafanikio utakapoyaona. Kama ukishindwa kufanya mambo hayo hutoweza kufanikiwa na mafanikio utakuwa unayasikia kwa wenzio.
Wengi wetu sana tumekuwa tukitaka kufanikiwa lakini hatupo tayari kulipia gharama mfano hatutaki kuwa wavumilivu, yaani mtu anataka leo aanzishe mradi kesho uwe umemlipa amekuwa na pesa nyingi na kuwa maarufu au awe ameshatambulika kama mtu tajiri miongoni mwa watu matajiri kumbe hilo ni jambo ambalo haliwezi kutokea kwa muda mchache kama unavyodhani. Wengi wetu tumekuwa hatupo tayari kulipa gharama hii ya uaminifu ndio maana tunaamini kuwa maishani kuna njia ya mkato jambo ambalo ni hakuna kabisa.

Mara ngapi umekuwa ukitaka kufanikiwa lakini unajikatisha tamaa mwenyewe kuwa dah kitu fulani mimi siwezi sio fani yangu?, ukijisemea hivyo hii inamaanisha kuwa haupo tayari kulipia gharama ya kuto kata tamaa maishani. Mara ngapi umekuwa ukishindwa kujiwekea malengo ili hali unajua kuwa lazima ujiwekee malengo kama kweli unataka kufanikiwa maishani?, lipia gharama ya kujiwekea mafanikio kama kweli unataka kufanikiwa.
Kimsingi mpaka hapo utakuwa umeshanielewa kuwa gharama za mafanikio hazihusu kulipia pesa kama gharama za safari bali gharama zake ni kufuata kile kitu ambacho ukikifanya hakika utafanikiwa tu. Hicho ndicho nacho maanisha naposema lipia gharama kama kweli unataka kufanikiwa.


Ni mimi  rafiki yako Baraka Maganga,. Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0652612410. Au kwa barua pepe ambayo ni Bmaganga22@gmail.com

No comments:

Post a Comment