Monday, February 1, 2016

Usitishike Na Watakao Kupinga Kwa Kigezo Hiki.

Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumani yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri katika kupambana
ili kuhakikisha kuwa unapata kile unachokitafuta katika maisha. Kwa kuwa lengo la mtandao huu ni kuhakikisha kuwa unapata vitu vya kukusukuma mbele zaidi katika kuelekea safari yako hiyo ya mafanikio, basi nasema pambana endelea kupambana bila kuchoka hata pale unapohisi umechoka jilazimishe maana kuridhika baaada ya hatua chache huleta anguko.




Mara nyingi sana watu wamekuwa na utamaduni wa kuwapinga watu kwa kutumia vigezo kadha wa kadha na watu hawa ndio wale wajulikanao kama wakatisha tama. Sasa wanaweza kutumia vigezo vingi lakini hapa mimi leo nakupatia kigezo kimoja ambacho ni kabila. Yaani wapo watu watakao kupinga kwa kutumia kabila lao.

wapo watakao kupinga kwa kigezo cha kabila. Yaani watu hawa huwa wanatumia kabila lako kama dhana au kigezo cha kukukwamisha katika safari yako ya kuelekea mafanikio. Kila kabila kwa hapa kwetu limekuwa likipewa sifa zake, ambazo hutumika kama kitambulisho cha kabila hilo wakati mwingine. Ndio maana tunamakabila ambayo yanafahamika kama makabila ya wafugaji, wafanyabiashara, wakulima n.k.  Kuna wakati sifa hizi huwa na ukweli ndani yake na kuna wakati huwa zinakuwa hazina ukweli ndani yake. Lakini kwa mtazamo wangu mimi ni kuwa sifa hizi zitakuwa ukweli pindi utakapo ziamini na kuzikubali kuwa ni za kweli. Itafika wakati utapingwa kwa kigezo hiki cha kabila lako, mfano kwa hapa kwetu Tanzania inaaminika kuwa wafanyabiashara maarufu ni wachanga na waha kutoka kigoma. Kwa kiasi kikubwa hapa kwetu makabila haya ni maarufu sana kwa shughuli hizi ikiwa ni pamoja na ndugu zangu wakinga.

Hivyo kutokana na mtazamo na imani juu ya makabila haya sio ajabu kuwa leo hii wewe ukitaka kuanzisha biashara anaweza kutokea mtu akakupinga vikali kwa kigezo kuwa kwa jinsi ulivyo wewe na kabila lako hilo huwezi kuwa mfanyabiashara maana wewe sio mkinga, mchaga, au mha.

Utapingwa kutokana na kabila lako kwa kuwa hizo ni imani ambazo watu wamejiwekea juu ya makabila mbalimbali lakini jiulize swali je hapa Tanzania mfano kama biashara wanaweza wachaga, waha, na wakinga pekee?, je makabila mengine ni kweli hawafanyi biashara?,tafuta, chunguza na mwishoni uone kama utapata kubaini kama hapa Tanzania hakuna wafanyabiashara wakubwa na maarufu ambao wanatoka katika kabila lako. Kama hakuna basi anza wewe ili uvunje mwiko, na kama wapo basi nawe unaweza kuwa miongoni mwao.

Ni kweli kila kabila huwa na shughuli yake ya kiasili ambayo muda mwingine huwa kitambulisho kwao. Mfano leo hii wamasai na wasukuma hutambulika kama jamii za wafugaji lakini sio sababu ya wewe kupingwa kwamba huwezi kuwa mfugaji kisa wewe sio mmasai wala msukuma. Pia ikumbukwe kuwa dunia inabadilika leo hii sio wamasai wote wanafuga jamii hii, leo hii wamekuwa walinzi na wasusi maarufu sana mjini sasa sijui tuwapinge maana wao asili yao ni kuchunga ng`ombe?.
Kumbuka kuwa kadili ujionavyo nafsini mwako ndivyo unavyokua kumbuka hilo siku zote. Hivyo basi kama unajiona huwezi kufanikiwa kutokana na kabila lako na itakuwa hivyo. TWENDE SOTE  
Ni mimi  rafiki yako Baraka Maganga,. Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0652612410. Au kwa barua pepe ambayo ni Bmaganga22@gmail.com


No comments:

Post a Comment