Tuesday, February 2, 2016

Sababu Tisa (9) Zinazofanya Watu Wengi Kushindwa Maishani.

Mara nyingi sana tumekuwa ni watu wa kujaribu hili na lile katika ile hali ya kutaka pengine kujikwamua kutoka katika hali ngumu za kimaisha tulizokuwa nazo,
na wakati mwingine huwa tunakuwa tunataka kusonga mbele zaidi ya pale tulipo lakini matokeo yake hujikuta tuko pale pale au ndio hujikuta tukiwa tunaanza kurudi nyuma na matokeo yake kujikuta tunadidimia zaidi na zaidi. Hii hupelekea tukashindwa au tukafeli kimaisha. Sababu mbalimbali zinaweza kutufanya tuwe hivyo au kujikuta katika hali hiyo, zifuatazo ni sababu tisa za kwanini watu wengi huwa wanashindwa maishani.






   Kukosa mipango, tafiti zinaonyesha kuwa watu wengi hushindwa maishani kwa kuwa hawajiwekei mipango au hawana mipango. Binadamu ni tofauti na mnyama kama vile mbuzi au kondoo ambaye hufunguliwa na kuongozwa mpaka malishoni, hula na baadae kurudishwa na kufungiwa bandani, ukiyaangalia maisha ya mbuzi mbuzi hana mpango wowote ule juu ya maisha yake. Lakini mambo ni tofauti kwa binadamu. Sisi binadamu ndio wenye uwezo wa kupanga sasa kama haupangi yaani hauna mpangilio wa maisha wala mipango yoyote maishani basi wewe utakuwa sawa na mbuzi tu jambo ambalo ni hatari. Ni vyema kwanzia sasa ukayapangilia maisha yako.

2.    Maandalizi mabovu, tumekuwa na tatizo kubwa sana katika kipengele cha maandalizi. Kukosekana kwa maandalizi katika maisha yetu kumetufanya tushindwe maana tumekuwa watu wa kukurupuka tu na kuanza kufanya mambo pasipo maandalizi ya kizana, rasilimali na akili. Ndio maana biashara nyingi sana leo hii huanzishwa lakini baada ya muda hufa. Mahusiano mengi sana huanzishwa tena kwa bwembwe lakini hufa baada ya muda mfupi tu vile vile  ndoa nyingi hazidumu kwasababu ya ukosefu wa maandalizi. Hivyo fanya maandalizi ya kutosha kabla hujaamua kufanyakitu fulani.


3.    Kushindwa mara moja kunawaondoa katika vita, watu wengi hawana tabia ya kujaribu kwa mara nyingine zaidi na zaidi hii ni baada ya kuwa wameshindwa kwa mara ya kwanza wao huamini kuwa wanapofanya jambo lazima walifanikishe hawatambui kuwa kuna kushindwa maishani. Sasa hii tabia ya kuto taka kujaribu ndio huleta ile tabia ya kushindwa kujaribu kwa mara nyingine. Na ndio maana nasema kushindwa mara moja kunawaondoa katika vita.

4.    Kuwaza mabaya kwa kila jambo, kuna watu huwa wanawaza mabaya kwa kila kitu, yaani leo hii unaweza kuwa unazungumza na mtu ukamshirikisha labda fursa ya kibiashara lakini yeye akakujibu vipi nikipata hasara. Ukiona unaongea na mtu wa namna hii jua kuwa akilini mwake anawaza mabaya kwa kila jambo. Na kama wewe una hii tabia acha mara moja.


5.    Visingizo, hii ndio tabia ambayo wengi tunaona kama sifa fulani kumbe ni ugonjwa mkubwa sana tena sana na inabidi uiache  mara moja. Utakuta mtu kafanya kitu kashindwa anaanza kusingizia watu walio mpa ushauri, serikali mara mungu hakunishika mkono n.k. acha visingizio kwanzia leo.

6.    Woga, hili ni tatizo jingine ambalo linatufanya tushindwe maishani. Watu wengi sana tumekuwa waoga wa kufanya maamuzi, waoga wa kujaribu na waoga pia wa kushindwa. Ndio maana tumekuwa hata pale tunapopewa mbinu za kubadilisha maisha yetu hatutumii kwa kuwa tunaogopa kushindwa na tunajikuta tunashindwa kweli.
7.    Kuwa sehemu zisizo sahihi, lazima ujitambue na ujielewe maishani jua nini unaweza nini hauwezi. Kuwa sehemu mbaya hususa ni katika shughuli zetu ambapo watu wengine hujikuta wapo katika kazi zisizo wahusu au zisizo endana na karama yako hivyo basi ni vyema ukajitambua na uwe na uelewa kuwa lazima uwe sehemu sahihi.

8.    Kuto tilia maanani shughuli zetu au hatuko makini, ukosefu wa umakini juu ya maisha ndio hupelekea sisi tuweze kushindwa maishani. Hatuko makini ndio maana hatuwezi hata kujiwekea malengo, hatuna mipango juu ya maisha yetu, hii yote inaonyesha ni jinsi gani hatupo makini au hatutilii maanani maisha yetu.


9.    Kukata taama, ugonjwa mkubwa wa watanzania wengi sasa ni kukata tama na unatutesa sana kwa kuwa tumekuwa wepesi sana wa kukata tama tofauti na ambavyo maisha yanatakiwa yawe. Hivyo basi usikate tamaa hata kama utapitia mabaya gani.
Kwa kuwa umezijua sababu hizi tisa kama sababu ambazo zinaweza kupelekea wewe kushindwa zigeuze sasa na kinyume chake ndio kitakuwa mambo tisa ambayo yatakufanya ufanikiwe. Mfano badala ya kuwa usikate tama, sema natakiwa nisikate tama.TWENDE SOTE 
Ni mimi rafiki yako Baraka Maganga,. Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0652612410. Au kwa barua pepe ambayo ni Bmaganga22@gmail.com


No comments:

Post a Comment