Wednesday, February 3, 2016

Njia Tano Za Kukuwezesha Kuwa Na Hali Ya Kuendelea Kutenda.

Mara nyingi sana tumekuwa watu wenye kukosa hali ya kuendelea kutaka kufanya mambo ambayo tumekuwa tukitaka kuyafanya. Ukosefu wa hali hii ndiyo ambayo
hutupelekea sisi kuweza kukata tama ndio maana tumekuwa mabingwa wa kukata tamaa. Sasa ili  kuthibiti hali hii nimeona ni bora nikuletee njia tano rahisi ambazo zinaweza kukufanya wewe uwe na hali ya kutaka kuendelea kutenda mambo yako. Zifuatazo ni njia hizo tano:-


1.    Fikira chanya, kuwa na fikira chanya wakati wote, hapa ni kuwa inatakiwa uziondoe fikira hasi zote katika ubongo wako ili uwe na fikira chanya. Fikira chanya ni muhimu sana kuliko unavyoweza kudhani maana fikira chanya zitakufanya ufute zile fikira za kukata tamaa, kushindwa, hofu, woga n.k. fikira chanya ni muhimu sana kama kweli unataka kufanikiwa maana mtu mwenye fikira chanya huona fursa hata pale ambapo wengine hawazioni.

2.    Jua ni nini unataka maishani, ni muhimu ujue nini unataka maishani. Usihishi kwa kuwa inabidi uishi badala yake tafuta kisha utambue ni nini haswa unakitaka maishani. Kujua unachokitaka maishani kutakupa hamasa kubwa sana kuliko unavyodhani. Nadhani wewe binafsi unajua hali unayokuwa nayo pindi unapokuwa unajua kitu na pale ambapo unakuwa haujui kitu. Kujua kitu kunakuwa ni kama kumekupa ramani hivyo basi utakuwa na hali ya kutaka kutenda mambo.


3.    Ifahamu kwanini yako, hapa nina maanisha kuwa lazima ujue kwanini unafanya jambo fulani, mfano unapotaka kuwa mwalimu lazima ujiulize kwanini unataka kuwa mwalimu, unapotaka kuwa daktari lazima ujiulize kwanini unataka kuwa daktari, mwanasheria lazima ujue kwanini unataka kuwa mwanasheria n.k. Majibu ya maswali haya na mengine mengi yatakupa hamasa ya kuendelea kufanya kwa kuwa tayari ushajua kwanini unafanya jambo hilo tofauti na pale ambapo utakuwa unafanya kisa tu unatakiwa ufanye. Hii ni hatari sana katika nyakati za sasa ambapo mtu anafanya kitu bila kujua kwanini anafanya hicho kitu. Hivyo basi ifahamu kwanini yako.

4.    Tengeneza mpango wa mambo yako, ni muhimu ukayaendesha maisha yako kwa mipango mathubuti. Usiishi bila mipango hii ni hatari sana maishani mwako. Pangilia mambo yako hii itakusaidia katika kufanya mambo yako maana utakuwa unajua wapi uanze wapi umalizie, pia itakupa uelewa wa ni shughuli ipi uipe kipao mbele sana kuliko nyingine na shughuli ipi ni muhimu itimizwe mapema kuliko nyingine. Usihishi bila mpango ndugu mpendwa msomaji wa makala hii. Kuishi bila mpango ni sawa na kuishi kama mfugo ambao hauna mpango wowote bali unasubiri kufunguliwa bandani au zizini ukale huko kisha urudishwe na kufungiwa tena bandani ama zizini humo, hii ni hatari kwa binadamu wa kisasa. Weka weka mipango ya maisha yako.


5.    Chukua hatua ndogo ndogo, waswahili wanasema polepole ndio mwendo hii ni sahihi sana na ndio maana nasema chukua hatua ndogo ndogo maana ukichukua hatua kubwa kubwa kwa wakati mmoja hii inaweza kukuletea shida huko mbeleni. Hatua ndogo ndogo hizi zinatoka katika mipango yako, ndio maana hapo juu nimekusisitiza kuwa weka mipango ya maisha yako kisha baada ya hapo anza kuchukua hatua ndogo ndogo yaani hapa ni sawa na kusema anza kufanyia kazi mpango mmoja mmoja na sio yote kwa pamoja hii ndio maana yangu ya msingi nayo taka kuimaanisha hapa. Chukua hatua ndogo ndogo.

Hizi ni hatua muhimu ambazo ukizifuata utakuwa umejiepusha katika mtego wa ile hali ya kutaka kukata tamaa. Hivyo basi fuata njia hizi ambazo ni rahisi na hazi hitaji nguvu nyingi wala muda mwingi sana. TWENDE SOTE 
Ni mimi rafiki yako Baraka Maganga,. Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0652612410. Au kwa barua pepe ambayo ni Bmaganga22@gmail.comNo comments:

Post a Comment