Thursday, February 4, 2016

Sababu Za Kwanini Unapaswa Kuwa Mwaminifu.

Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa, ni matuimaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea
vizuri katika kupambana na harakati za hapa na pale ili tu kutaka kujiletea mafanikio makubwa zaidi. Vizuri endelea na hali hiyo wala usiache kufanya hivyo, kwa kuwa lengo la mtandao huu ni kukupa elimu juu ya mambo mbalimbali ya kukufanya uweze kufanikiwa basi tuingie katika mada ya leo ambayo ni kuhusu uaminifu.



Uaminifu ni kitu muhimu sana kwa mtu yoyote yule ambaye anataka kupiga hatua zaidi katika maisha yake husika. Uaminifu ni ile hali ya kuwa  na uwezo wa kutimiza ahadi ambazo unakuwa umejiwekea mwenyewe. Hii ikiwa na maana kuwa kama ulijiwekea ahadi fulani au uliweka ahadi fulani na mtu au juu ya mtu au kitu fulani katika maisha yako na ukaweza kukitekeleza pasipo kuvunja makubaliano sahihi ambayo yaliwekwa au uliweka hapo tunasema umekuwa mwaminifu. Sasa hapa ntaligawa swala la uaminifu katika sehemu kuu mbili ambazo ni uaminifu juu yako mwenyewe na uaminifu juu  yako na wengine.

Uaminifu juu yako wewe mwenyewe ni ile hali ya kuwa na uweze wa kutekeleza ahadi ulizojiwekea wewe mwenyewe pasipo kutaka au kuruhusu ile hali ya kutaka kusitisha sitisha ahadi zile ambazo uliziweka mwenyewe. Tumekuwa watu wenye kuvunja ahadi ambazo tumekuwa tukijiwekea binafsi katika maisha yetu na hii inamaanisha kuwa tumekuwa ni watu ambao sio waaminifu sisi kama sisi na hili limekuwa tatizo kubwa miongoni mwetu. Jiulize ni mara ngapi umekuwa ukitimiza zile ahadi ambazo umekuwa ukijiwekea wewe binafsi? Jibu la swali hili litakuwa ni kipimo cha uaminifu wako  wewe kama wewe.

Uaminifu baina yako wewe na watu wengine, hapa ndipo penye shida. Maana uaminifu baina yetu na watu wengine imekuwa ni tatizo sana. Yaani leo hii ni watu wachache sana kati ya wengi wenye uwezo wa kutunza ahadi kati yao na watu wengine. Marafiki wengi siku hizi wanagombana na urafiki wao unavunjika kutokana na ukosefu wa uaminifu baina yao. Ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu ya kukosa uaminifu miongoni mwa wana ndoa husika.  Mahusiano mengi leo hii haya dumu kutokana na uaminifu kukosekana.

Baada ya kusema hayo hapo juu ni muhimu sasa nikakuhasa ndugu mpendwa msomaji wa makala hii kuwa  jitahidi sana kuwa mwaminifu juu yako wewe mwenyewe na juu ya wenzio. Na uaminifu wa kwanza ni ule wa kuwa mwaminifu juu yako yaani wewe kama wewe uwe mwaminifu sasa. Uaminifu utakupanulia uwezo wa kuweza kuaminika na kwa kiasi na kila mtu. Kuna watu leo hii hawa haminiwi hata na ndugu zao, majirani zao, marafiki zao kiasi kwamba hata wakipata shida leo hii hawawezi kupewa msaada wowote kwa kuwa watu hawa hawaaminiki.

Kuna watu leo hii hawakopesheki na taasisi za kifedha kama vile mabenki na taasisi zingine, achilia mbali taasisi tu hata wale watu wao wa karibu hawawezi kuwakopesha watu hawa hii ni kwa sababu tu sio waaminifu watu hawa katika maisha yao. Sasa watu hawa wakati mwingine ndio huanza kuwatupia watu wengine lawama, kumbe ni wao ndio wamekosa uminifu na matokeo yake wamejikuta katika shida hizo.

Mimi nikusihi kuwa kwanzia sasa anza kuwa mwaminifu, jenga uaminifu kwako wewe mwenyewe na baadae kwa watu wengine. Ukiwa mwaminifu juu yako mwenyewe na wengine pia watakuamini pia.

Ni mimi rafiki yako Baraka Maganga,. Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0652612410. Au kwa barua pepe ambayo ni Bmaganga22@gmail.com


No comments:

Post a Comment