Wednesday, February 10, 2016

Fahamu Kuwa Kila Kitu Huanza Na Wewe.

Habari za wakati huu ndugu mpendwa msomaji wa makala za mtandao huu. Ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaednelea vizuri katika
kuhakikisha kuwa unapambana na hatimaye kujiletea mafanikio makubwa maishani mwako. Nami nasema pambana mpaka utakapo hakikisha kuwa yale uliyokuwa unayataka umeyafanikisha kwa kiwango ambacho ulikikusudia na kama bado we endelea kupambana. Baada ya kimya cha muda mfupi kutokana na majulumu kuingiliana kwa kiasi kikubwa naomba tuendelee katika kuelimishana kwetu kama kawaida yetu.

Kama kichwa cha makala hii kinavyosomeka kuwa kila kitu huanza na sisi basi natumaini umesha anza kufikiri kitu juu ya kichwa hiki. Kabla sijaingia ndani zaidi na kuanza kudadafua nayo taka kuyasema naomba uache kwa muda mfupi kusoma makala hii na utamke kauli hii mara kumi sema hivi ”kila kitu huanza na mimi”. Naam kila kitu huanza na wewe. Hakikisha unatamka kauli hii mara kumi ndipo uendelee na kusoma makala hii.

Tumekuwa ni watu wenye kulalama sana juu ya matatizo au hali zetu utasikia tukijisemea kuwa sina amani siku hizi , sina raha kabisa mimi jamani, mimi masikini, mimi sina hela, mimi sina akili n.k. kiujumla kuna rundo la kauli ambazo huwa tunazitumia mara kwa mara na si vyema mimi kuziorodhoshe zote bali nimekupatia mifano ya kauli hizo ili upate kutambua kauli zingine zenye kufanana na hizo. Sasa ni vyema utambue kuwa kwa kila linalokutokea au hali uliyokuwa nayo ni wewe ndiye mwanzilishi.

Unakosa furaha maishani na kwa kiasi kikubwa unaanza kulaumu kuwa sina raha, tukikuuliza nani anakufanya usiwe na furaha utaanza kutaja watu au vitu vingine. Sasa leo nakuambia na naomba unielewe kuwa hakuna mtu anayeweza kukukosesha raha maishani mwako. Kuna kauli kama mbili ambazo nilishawahi kuzisikia alafu nikazitathimini na kugundua kuwa kweli kila kitu huanza na sisi. Kauli ya kwanza ni ile yenye kusema “ukweli hauwezi kuwa ukweli mpaka pale ambapo utaukubali au tutaukubali kuwa ukweli” na kauli ya pili ni ile yenye kusema kuwa “hakuna mtu anayeweza kukusumbua hata kidogo kama wewe hujamruhusu akusumbue” hivyo basi kama unakosa furaha basi ni wewe mwenyewe ndiye uliyeruhusu hali hii ya kukosa furaha na sio wengine au vingine.

Hamasa huanza na wewe na wala sio wengine, ni kweli kuwa katika dunia ya leo kuna wahamasishaji wengi sana tena sana ambao ukiwasikiliza kweli wanahamasisha sana, kwa hapa Tanzania nikichukulia mfano wapo watu kama kina Erick shigongo, james mwangamba, Paulo mashauri n.k. wote hawa wanahamasisha lakini hamasa zao haziwezi kufanya kitu kama wewe hujazikubali hivyo basi hamasa huanza na wewe na sio wengine. Wengine hutoa hamasa na unapozikubali wewe ndipo hujidhihirisha sasa kuwa hamasa kwako.

Umasikini huanza na wewe, hili ni kweli kabisa maana kuna watu wanasingizia sijui mimi nimezaliwa katika familia masikini oo sijui sina bahati na porojo nyingi sana mfululizo lakini zote hizo hazikusaidi bali ndio zinazidi kukuangamiza na kukufanya uwe masikini zaidi na zaidi. Sasa kama unasingizia nani aliyeleta hivyo visingizio kama sio wewe. Hivyo basi umasikini umeanza na wewe maana badala ya kuwaza utafanyaje ili uepukane na umasikini wako wewe umeanza kulaumu sasa lawama zimekufanya uzidi kuwa masikini na sasa unataka utoke huko lakini umesahau kuwa wewe ndiye uliyejipeleka huko.
Leo hii kwa kuwa umegundua kuwa kila hali na kila jambo hapa duniani linalokukabili huanza labda kutokana na ama uzembe wako katika eneo lako Fulani la kimaisha, kujisahau, kuto kujua au uvivu sasa ni wakati wa kuamuka na kutaka kutenda zaidi na zaidi.  Uovu, uzuri, furaha, huzuni, woga, mafanikio, hamasa n.k vyote huanza na wewe hivyo basi kwa kuwa umeelewa haya basi chukua hatua mathubuti sasa na ujinasue katika mtego wa kutaka kuwasingizia watu wengine na hatimaye ukajikuta unadidimia zaidi na zaidi na mafanikio hatimaye yakakupika kushoto.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.

Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0654612410 au kwa barua pepe:- Bmaganga22@gmail.com.

2 comments: