Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona
ya maarifa ni matumani yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri katika
kupambana ili kuhakikisha kuwa unapata kile unachokitafuta katika maisha. Kwa
kuwa lengo la mtandao huu ni kuhakikisha kuwa unapata vitu vya kukusukuma mbele
zaidi katika kuelekea safari yako hiyo ya mafanikio, basi nasema pambana
endelea kupambana bila kuchoka hata pale unapohisi umechoka jilazimishe maana
kuridhika baaada ya hatua chache huleta anguko.
Najua umekuwa ukupambana sana katika kuhakikisha kuwa
unafanikisha mambo yako lakini kuna wakati ukikaa na kupiga tathimini unajikuta
ukitamani kukata tamaa hii ni baada ya kuona au kupata matokeo ya tathimini
yako na hapo ndipo wengi huwa tunapatwa
na hofu ya kuacha na mara nyingi sana huwa tunaanza kuona ni kama hatupigi
hatua hivyo basi tunatamani kuachana na harakati zetu ambazo tumekuwa
tukizianzisha na kuamini kuwa zitakuwa na msaada kwetu. Unatamani kuacha
nakuona unasoma hii makala na huku unasema dah yaani sioni matokeo yoyote,
niliambiwa hivi na vile, nilisoma hivi na vile lakini sioni matokeo yake,
naacha bwana.
Kabla hujafikiria kufanya kitu hicho unachotaka kufanya
nataka ujichunguze sehemu hii moja, yachunguze maneno yako. Kabla hujafikiria
kufanya uamuzi wa kuacha kufanya jambo fulani kwa kuwa tu hujapata matokeo
mazuri yachunguze maneno yako, narudia
tena yachunguze maneno yako. Unajua binadamu tuna namna mbili za kuongea,
nakuona unashangaa kusikia namna mbili za kuongea, namaanisha kuwa tunakule
kuongea kwa kawaida ambapo tunaongea na wenzetu huku kumezoeleka na ni maarufu
lakini aina ya pili ni ile ya kujiongelesha wenyewe, yaani kuna muda huwa unajikuta uwapo mwenyewe kuna
maneno unayojiongelea mwenyewe sasa maneno haya ndio nayo taka uyachunguze.
Jiulize mwenyewe hapo ulipo je kauli unazojisemesha
mwenyewe ni hasi au chanya, nakuona unasita kutoa jibu kwa kuwa unajua ni hasi.
Wengi tumekuwa hatujui nguvu iliyopo katika maneno yetu ambayo tumekuwa tukijisemesha
mara kwa mara na ndio maana tumekuwa tukihangaika kuchunguza mchawi wa maisha
yetu kumbe sisi wenyewe ndio tunao jiloga. Unajiloga kwa maneno yako mwenyewe
alafu unajikuta unalalama eti nalogwa na ndugu zangu hawataki nifanikiwe
kabisa. Dah wewe, nani asiyetaka ufanikiwe wewe au wao?, jibu unalo mwenyewe
mpaka hapo.
Pengine unajiuliza sasa mbona mimi sielewi ni kauli gani
sasa, sawa mimi nipo kukuletea hizo kauli, mara ngapi umekuwa ukijisemea kuwa
wewe unamikosi, nuksi au gundu. Ndio umekuwa ukijiambia ukisema unamikosi,
gundu au nuksi maana yake huwezi kufanikiwa sasa kwanini unataka kufanikiwa
ikiwa kila siku unajisemesha mwenyewe kuwa hauwezi kufanikiwa. Huoni kuwa
unafanya kazi ya kuchanganya maji machafu kwenye maji masafi alafu unategemea
maji masafi yaendelee kuwa masafi. Eti unataka kuacha kufanya mambo ya
kukusogeza mbele kisa unamikosi, na ukiamini na kujisemesha kuwa unamikosi
kweli utakuwa nayo tena mingi haswa. Acha kujisemesha na kujitazama kama mtu
mwenye mikosi, gundu, na nuksi. Acha mara tu baada ya kusoma makala hii.
Mara ngapi umekuwa ukisalimiwa asubuhi unaambiwa habari
ya asubuhi ndugu unajibu aa bora kumekucha, au dah bora ya jana, hivi unajua
maana ya hayo maneno unayoyasema. Unayasema maneno hayo alafu akilini mwako
unawaza kuwa biashara yako itakwenda sawa. Nani kakudanganya wewe acha
kujidanganya, ukisema bora kumekucha maana yake haukutaka kukuche sasa
unaendeleaje na shughuli kama hautamani kukuche?, ukisema dah bora ya jana
maana yake siku ya leo ni ya ovyo sasa unategemea vipi kudharisha katika siku
mbovu?, anza siku yako na kauli nzuri na mafanikio utayaona
.
Nakuona kila ikifika ijumaa unajifanya mzungu eti “thanks
God it is Friday” ukimaanisha asante mungu kwa kuwa leo ni ijumaa. Unajua
tafsiri yake hapo tafsiri yake ni kuwa siku zote zilikuwa mbaya kwako ndio
maana unafurahia kuiona ijumaa. Sasa kwanini utake kufanikiwa jumatatu wakati
kwako ni mbaya? Au alhamisi wakati ilikuwa mbayas?
Kuwa makini na kauli unazojinenea mwenyewe maana mnamo
maneno mna nguvu sana, maneno huumba hilo waswahili waliliona na sio kuumba tu,
maneno yanaamua maisha yetu ya sasa na baadae.hivyo basi kuwa makini sana tena
sana juu ya maneno yako kama kweli unataka kufanikiwa. TWENDE SOTE.
Ni mimi Baraka
Maganga, rafiki na mwalimu wako.
Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0652612410. Au kwa barua
pepe ambayo ni Bmaganga22@gmail.com.
No comments:
Post a Comment