Monday, January 25, 2016

Wajibika Ipasavyo Kama Kweli Unataka Kufanikiwa.


Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea kupambana kwa hali na mali ili tu uweze kufanikisha yale ambayo umekuwa ukiyahangaikia mara kwa mara. Vizuri endelea kupambana naama hakuna kitu cha bure hapa duniani, maana hata miujiza huja kwa wale ambao huwa wanakuwa wakiitafuta miujiza hiyo. Sio waliokaa tu wakisubiri miujiza hivyo nakusihii endelea kupambana ndugu msomaji wa mtandao huu.Naamini umekuwa ukipambana sana katika kuhakikisha kuwa unafanikiwa katika yale ambayo unayahangaikia nami na kusihi uendelee kupambana maana katika mahangaiko ndiko mafanikio hutokea. Lakini lazima ujue kuwa lazima kitu hiki ukifanye kama unataka kufanuiki. Kitu hiki ni kitu muhimu sana katika maisha yetu na mafaniko kwa ujumla lakini jambo la kushangaza ni kuwa tumekuwa hatulitili maanani sana na ndio maana wengi wetu tumekuwa tukijikuta hatusongi mbele wala nini ila tunabaki pale pale au kurudi nyuma kabisa kimaisha.

Huwa unapata picha gani pindi unapoona mfanyakazi fulani katika kampuni fulani kafukuzwa kazi. Au kasimamishwa kazi kwa muda. Unapata picha gani pindi unapomwona mfanyabiashara fulani kashindwa kibiashara yaani biashara yake imekufa. Unapata wazo gani unapomwona mtu anailaumu serikali yake kwa kushindwa kwake wakati yeye ndiye aliyepaswa kufanya jambo husika. Hakika yote hayo hutokea kutokana na kukosekana kwa kitu hiki kimoja nacho ni uwajibikaji.

Maishani bila kuwajibika tambua kuwa hauto kwenda kokote kule bali utaishia pale pale. Dunia ya sasa imejaa ushindani wa hali ya juu ambao unaongezeka siku hadi siku na atakae weza kusitaimili ushindani huu ni yule tu mwenye kuweza kuwajibika ipasavyo. Kama wewe ni mfanyabiashara na unawajibika bora liende tambua kuwa hauto kwenda popote bali utaishia kufulia tu. Mfanyakazi pia ambae hutaki kuwajibika tambua kuwa utaishia tu kufukuzwa kazi yako hiyo na hatimae kuukaribia umasikini nao utakukaribisha vizuri sana kuliko unavyodhani.

Leo hii takwimu zinaonyesha kuwa kati ya biashara mia moja zinazo anzishwa leo baada ya miaka kumi ni biashara chini ya ishirini ndizo huwa zimekuwa. Hii ni kutokana na uwajibikaji mbovu wa wafanyabiashara husika. Wafanyabiashara hawa wamekuwa hawahangaiki katika kutafuta taarifa sahihi kabla ya kuzianzisha biashara zao na vile vile wamekuwa wagumu wa kuendelea na utafiti baada ya kuanzisha biashara zao, hivyo hata yakitokea mabadiliko wao hawashituki wala nini. Bali huendelea kufanya biashara zao kwa mazoea na matokeo yao hujikuta wamefulia maana hujikuta hawapati wateja. Hii ni kutokana na uvivu ulio letwa na kuto taka kuwajibika kwao na ndio maana wanajikuta wameanguka.

Ukiwa mfanyakazi unajisikiaje pale unapoambiwa tunakuwajibisha kutokana na utendaji wako mbovu angalia leo hii ni watu wangapi wamesimamishwa kazi toka uongozi wa awamu ya tano uingie madarakani na wote sababu zimekuwa zikionekana ni uwajibikaji mbovu na mengine, lakini kubwa ni uwajibikaji mbovu ambao huwapelekea wafanye mambo kiholera holera na matokeo yake ni kuja kuwajibishwa.

Kama unataka kufanikiwa hakikisha unayavaa majukumu yako usisubiri mazingira yaje ya kushitaki na kukuwajibisha vikali. Au usisubiri kufulia kukuwajibishe, ukiwa mfanyabiashara usisubiri anguko la biashara likuwajibishe, mfanyakazi usisubiri kuwajibishwa na bosi wako bali vaa majukumu yako mwenyewe na mafanikio utayaona tu. Ikiwa unasubiri kuwajibishwa basi sahau kuhusu mafanikio na usilizungumzie tena neno hilo.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com
No comments:

Post a Comment