Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona
ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea kupambana kwa
hali na mali ili tu uweze kufanikisha yale ambayo umekuwa ukiyahangaikia mara
kwa mara. Vizuri endelea kupambana naama hakuna kitu cha bure hapa duniani,
maana hata miujiza huja kwa wale ambao huwa wanakuwa wakiitafuta miujiza hiyo.
Sio waliokaa tu wakisubiri miujiza hivyo nakusihii endelea kupambana ndugu msomaji
wa mtandao huu.
Ukiwa bado unaendelea
kupambana katika harakati zako basi jifunze
kufurahia mateso,matatizo na vipingamizi mbalimbali uvipatavyo kwa sasa.
Kwanini nasema jifunze kuyafurahia mateso, matatizo na vipingamizi vya sasa?.
Sababu ninazo kupa hapa basi zinaweza kuwa muhimu kwako kuweza kukufanya
uyafurahie mateso, matatizo na vipingamizi kadha wa kadha.
1.
Vinakufunza,ni
kweli kuwa watu tulishawahi kupita, tunapitia na pengine tunaweza kuja kupitia
katika mateso, matatizo na vipingamizi vya aina mbalimbali. Kama ulishawahi
kupita katika mateso, vipingamizi au matatizo fulani basi utakubaliana nami
kuwa vitu hivi huwa vinafunza. Jiulize swali hili huwa unajisikiaje pindi
unapokuwa unapitia katika matatizo?, au pindi unapopitia vipingamizi fulani?,
kama huwa unachukulia vitu hivi kwa hasira alafu unaanza kulalamika basi tambua
kuwa una mtazamo hasi, na hivyo inabidi ubadili mtazamo huu na ujenge mtazamo
wa kuyaangalia mateso, matatizo na vipingamizi vyako kwa hasira kisha acha
kulaumu na baadae jiulize umejifunza nini kutokana na mambo hayo?. Huwa
unajifunza nini pindi unapopingwa na wenzio je? unajawa na hasira na kuishia
kulaumu au huwa unapatwa na hasira na unajifunza kuwa unapaswa kubadilika
pengine unapingwa kutokana na kutokuwa bora katika jambo fulani, hivyo jifunze
kutokana na kupingwa na ukajiboreshe zaidi na zaidi. Mateso unayoyaona leo
yageuze kuwa kama somo. Matatizo pia yawe somo mfano unapokuwa na tatizo la
pesa unajisikiaje?, unakubali hali au unajifunza na kulitatua tatizo hilo.
2.
Vinakuimalisha,
matatizo, vipingamizi na matatizo, muda mwingine huwa kama viimalisho vyetu.
Mfano matatizo yako yapo ili kukufanya uwe bora zaidi na zaidi. Mfano unapopata
pingamizi kutoka sehemu mbalimbali kama vile unapopingwa kutokana na kigezo cha
ukosefu wa elimu katika sehemu fulani ni muda wa kwenda kujiimalisha sasa ili
uwe bora zaidi na usije ukapigwa tena na tena. Mateso muda mwingine
usiyachukulie kama yapo kwa ajili ya kukutesa bali yapo kwa ajili ya
kukuimalisha zaidi katika Nyanja mbalimbali za maisha.
3.
Vinakuamsha
katika usingizi mzito, mateso, vipingamizi na matatizo yapo
ili kukuamsha katika usingizi mzito
ambao umelala. Mfano halisi ni kuwa sisi binadamu huwa tunakumbwa na hali ya
kujisahau pindi tunapojikuta kuwa tumefanikiwa kwa kiasi fulani na hapo ndipo
wakati mwingine vipingamizi huja kwa ajili ya kutuamsha kutoka katika usingizi
mzito ambao huwa tunakuwa tumelala pengine ni kutokana na baadhi ya mafanikio
ambayo tunakuwa tumelala kwa muda. Binadamu huwa tunakuwa na hali ya kujisahau
sana pindi tunapokuwa tumeona kuwa hali kwetu ni nzuri na hapo huwa tunajisahau
sasa kwa wakati huu ndio huwa ni muhimu sana tena sana kuweza kuamshwa kutoka
katika usingizi huu tulio lala. Matatizo mengi huja kwetu ili kutuamsha kutoka
katika usingizi mzito tuliokuwa tumelala na hivyo kuweza kutuamsha. Mfano kama
mfanyabiashara ukiwa umezoea kupeleka biadhaa zako mahali Fulani kwa wateja
wako, kutokana na kufanya biashara kwa mazoea maana unafanya tu hutaki
kuboresha bidhaa zako siku bidhaa yako ikipingwa na wateja wako, utakuwa
umeamshwa sana. Pengine unateswa kwa kuwa umelala sasa inatakiwa uamke ili
usiendelee kuteseka kama ukiendelea kulala maana yake utaendelea kuteseka.
Hivyo
basi furahia mateso, matatizo na vipingamizi kwa maana ndani yake vimebeba mafunzo
zaidi na zaidi.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua
pepe: Bmaganga22@gmail.com
No comments:
Post a Comment