Wednesday, January 20, 2016

Lazima Kitu Hiki Kiendelee Kuwepo Duniani, Na Ni Muhimu Kiwepo.

.Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea kupambana kwa hali na mali ili tu uweze kufanikisha yale ambayo umekuwa ukiyahangaikia mara kwa mara. Vizuri endelea kupambana naama hakuna kitu cha bure hapa duniani, maana hata miujiza huja kwa wale ambao huwa wanakuwa wakiitafuta miujiza hiyo. Sio waliokaa tu wakisubiri miujiza hivyo nakusihii endelea kupambana ndugu msomaji wa mtandao huu.Ikiwa unapambana katika kuhakikisha unasonga mbele na wala sio kurudi nyuma basi ni vyema ukaelewa kuwa kitu hiki kimoja kisikutishe sana maana ni lazima kiendelee kuwepo hapa duniani, yaani usikihofie kitu hiki kwa maana ni cha muhimu sana tena sana. Kitu chenyewe ni tofauti zilizopo baina yetu sisi wanadamu. Ni wazi na ukweli usio pingika kuwa binadamu tunatofautiana sana tena sana na kwa kiasi kikubwa, kama ulikuwa hujui kuwa binadamu tunatofautiana basi anza kuelewa kwanzia sasa kuwa binadamu tunatofautiana na tofauti hizi zipo baina yetu na zinajionesha wazi wazi miongoni mwetu. Ngoja nikuwekeee mifano kadhaa ili uwezo kuelewa ni namna gani binadamu tunatofautiana tena kwa makundi tofauti tofauti.
Mfano katika maisha ya kawaida utofauti wetu unaweza kujionesha kutokana na  shughuli au kazi zetu, ndio maana katika maisha tuna madaktari, tuna manesi, tuna waalimu, tuna wafanyabiashara, tuna madereva, tuna wasio waajiriwa, tuna wawekezaji pamoja na wajasiliamali n.k. bado katika makundi hayo hayo  yanatofauti pia mfano katika kundi la madaktari tuna madaktari bingwa wa macho na wale bingwa kwa magonjwa ya watoto, katika waalimu tuna waalimu wakuu na waalimu wasio na cheo au kitengo chochote, katika kundi la madereva tuna madereva wa mabasi ya mikoani, daladala na madereva wa malori. Huu ni ufafanuzi kidogo ambao unaonesha  jinsi gani binadamu tunatofautiana sana tena sana.
Sasa utofauti huu usikutishe maaana haupo ili ukutishe bali upo ili kukupa changamoto na fursa wewe ili upate kuelewa ni wapi ambapo panakufaa haswa. Utofauti huu upo ili kukufanya wewe ufanye uchaguzi sahihi ni kundi gani linakufaa haswa na ni wapi unapataka. Hivyo basi badala ya kutishika na utofauti huu wewe chukulia utofauti huu kama fursa ya wapi panakufaa. Usitishike wala kuogopa unapoona mtu fulani kawa mfanyabiashara maarufu, fulani kawa daktari bingwa, kawa mchezaji bora, kawa mwamasheria n.k bali chukulia kama fursa ya wewe kuchagua ni wapi haswa panapokufaa na upange ni jinsi gani haswa utaweza kufika pale.
Pia ni muhimu ukatambua kuwa utofauti huu wa kimaisha unaweza kukusaidia wewe kufanya mambo fulani fulani, mfano utofauti unaweza kupelekea yafuatayo kwako:-
1)    Utofauti huu ndio hutukumbusha ya kuwa tunapaswa kuwajibika, kupitia tofauti zilizopo au zinazojitokeza kati yetu ndizo huwa kichocheo cha sisi kupambana ili kuhakikisha kuwa tunasonga mbele au kupata molari ya kujikwamua katika hali ambazo tunazo. Hebu chukulia mfano ni hali gani huwa unakuwa nayo pindi unapokutana na rafiki yako ambaye mnaendana kwa baadhi ya vitu kama vile umri, elimu, historia ya kimalezi na zaidi mlisoma na kucheza pamoja lakini  baada ya kuacha nae kwa muda anarudi akiwa na mafanikio makubwa sana kuliko wewe, tayari mmeshatofautiana japo mlikua na kusoma pamoja, sasa baada ya kuyaona mafanikio ya huyo rafiki yako, ni nini unachopata kwa mara ya kwanza?. Nadhani ni hisia za kuwajibika ili uweze kuwa kama rafiki yako.

2)    Hutufanya tuzichukie hali fulani, kupitia utofauti tulionao basi hutufanya tuzichukie baadhi ya hali zetu. Mfano pindi unapowaona wenzio wakifanikiwa ili hali wewe unabaki kuwa masikini wa kutupwa basi hapa ndipo huwa unapata hasira na kuanza kuuchukia umasikini lakini kiuhakika ni kuwa usingeweza kupata hasira ya kuichukia hali hii ya umasikini. Lakini sababu ya kukufanya uanze kuuchukia umasikini ni baada tu ya kuona tofauti iliyopo kati yako na wengine.


3)    Hutufanya tujifunze zaidi,tofauti zilizopo baina yetu na wengine wakati mwingine huwa kama somo kwetu maana tofauti hizi hutufanya tuanze kujihoji sana ni kwanini wengine wako hivi na sisi tuko hivi. Mfano leo hii unapata wazo gani unapowaona watu waliofanikiwa mbele yako, sina shaka kuwa itakuwa uwa unapata hamu ya kujifunza zaidi kutoka kwa watu hao.

Ni muhimu tofauti ziendelee kuwepo miongoni mwetu ili tuweze kuchagua ni wapi panatufaa, ili tuweze kubadilishana huduma maana  wote tukiwa wafanyabiashara nani atakuwa mnunuzi tena isitoshe wote tukiwa tunauza bidhaa sawa, ingekuwaje kama wote tungekuwa madereva na kila mtu, angelikuwa na gari lake, bila shaka kusingekuwepo abiri kwa sababu hizo na nyingine nyingi ni dhahiri kuwa tofauti ni lazima ziendelee kuwepo miongoni mwetu.


Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com


No comments:

Post a Comment