Friday, January 29, 2016
Lazima Uwe Tayari Kufanya Jambo Hili Katika Safari Yako Ya Kuelekea Mafanikio.
Thursday, January 28, 2016
Fahamu Leo Kuwa Maneno Yana Nguvu Sana Katika Maisha Yako.
Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona
ya maarifa ni matumani yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri katika
kupambana ili kuhakikisha kuwa unapata kile unachokitafuta katika maisha. Kwa
kuwa lengo la mtandao huu ni kuhakikisha kuwa unapata vitu vya kukusukuma mbele
zaidi katika kuelekea safari yako hiyo ya mafanikio, basi nasema pambana
endelea kupambana bila kuchoka hata pale unapohisi umechoka jilazimishe maana
kuridhika baaada ya hatua chache huleta anguko.
Najua umekuwa ukupambana sana katika kuhakikisha kuwa
unafanikisha mambo yako lakini kuna wakati ukikaa na kupiga tathimini unajikuta
ukitamani kukata tamaa hii ni baada ya kuona au kupata matokeo ya tathimini
yako na hapo ndipo wengi huwa tunapatwa
na hofu ya kuacha na mara nyingi sana huwa tunaanza kuona ni kama hatupigi
hatua hivyo basi tunatamani kuachana na harakati zetu ambazo tumekuwa
tukizianzisha na kuamini kuwa zitakuwa na msaada kwetu. Unatamani kuacha
nakuona unasoma hii makala na huku unasema dah yaani sioni matokeo yoyote,
niliambiwa hivi na vile, nilisoma hivi na vile lakini sioni matokeo yake,
naacha bwana.
Kabla hujafikiria kufanya kitu hicho unachotaka kufanya
nataka ujichunguze sehemu hii moja, yachunguze maneno yako. Kabla hujafikiria
kufanya uamuzi wa kuacha kufanya jambo fulani kwa kuwa tu hujapata matokeo
mazuri yachunguze maneno yako, narudia
tena yachunguze maneno yako. Unajua binadamu tuna namna mbili za kuongea,
nakuona unashangaa kusikia namna mbili za kuongea, namaanisha kuwa tunakule
kuongea kwa kawaida ambapo tunaongea na wenzetu huku kumezoeleka na ni maarufu
lakini aina ya pili ni ile ya kujiongelesha wenyewe, yaani kuna muda huwa unajikuta uwapo mwenyewe kuna
maneno unayojiongelea mwenyewe sasa maneno haya ndio nayo taka uyachunguze.
Jiulize mwenyewe hapo ulipo je kauli unazojisemesha
mwenyewe ni hasi au chanya, nakuona unasita kutoa jibu kwa kuwa unajua ni hasi.
Wengi tumekuwa hatujui nguvu iliyopo katika maneno yetu ambayo tumekuwa tukijisemesha
mara kwa mara na ndio maana tumekuwa tukihangaika kuchunguza mchawi wa maisha
yetu kumbe sisi wenyewe ndio tunao jiloga. Unajiloga kwa maneno yako mwenyewe
alafu unajikuta unalalama eti nalogwa na ndugu zangu hawataki nifanikiwe
kabisa. Dah wewe, nani asiyetaka ufanikiwe wewe au wao?, jibu unalo mwenyewe
mpaka hapo.
Pengine unajiuliza sasa mbona mimi sielewi ni kauli gani
sasa, sawa mimi nipo kukuletea hizo kauli, mara ngapi umekuwa ukijisemea kuwa
wewe unamikosi, nuksi au gundu. Ndio umekuwa ukijiambia ukisema unamikosi,
gundu au nuksi maana yake huwezi kufanikiwa sasa kwanini unataka kufanikiwa
ikiwa kila siku unajisemesha mwenyewe kuwa hauwezi kufanikiwa. Huoni kuwa
unafanya kazi ya kuchanganya maji machafu kwenye maji masafi alafu unategemea
maji masafi yaendelee kuwa masafi. Eti unataka kuacha kufanya mambo ya
kukusogeza mbele kisa unamikosi, na ukiamini na kujisemesha kuwa unamikosi
kweli utakuwa nayo tena mingi haswa. Acha kujisemesha na kujitazama kama mtu
mwenye mikosi, gundu, na nuksi. Acha mara tu baada ya kusoma makala hii.
Mara ngapi umekuwa ukisalimiwa asubuhi unaambiwa habari
ya asubuhi ndugu unajibu aa bora kumekucha, au dah bora ya jana, hivi unajua
maana ya hayo maneno unayoyasema. Unayasema maneno hayo alafu akilini mwako
unawaza kuwa biashara yako itakwenda sawa. Nani kakudanganya wewe acha
kujidanganya, ukisema bora kumekucha maana yake haukutaka kukuche sasa
unaendeleaje na shughuli kama hautamani kukuche?, ukisema dah bora ya jana
maana yake siku ya leo ni ya ovyo sasa unategemea vipi kudharisha katika siku
mbovu?, anza siku yako na kauli nzuri na mafanikio utayaona
.
Nakuona kila ikifika ijumaa unajifanya mzungu eti “thanks
God it is Friday” ukimaanisha asante mungu kwa kuwa leo ni ijumaa. Unajua
tafsiri yake hapo tafsiri yake ni kuwa siku zote zilikuwa mbaya kwako ndio
maana unafurahia kuiona ijumaa. Sasa kwanini utake kufanikiwa jumatatu wakati
kwako ni mbaya? Au alhamisi wakati ilikuwa mbayas?
Kuwa makini na kauli unazojinenea mwenyewe maana mnamo
maneno mna nguvu sana, maneno huumba hilo waswahili waliliona na sio kuumba tu,
maneno yanaamua maisha yetu ya sasa na baadae.hivyo basi kuwa makini sana tena
sana juu ya maneno yako kama kweli unataka kufanikiwa. TWENDE SOTE.
Ni mimi Baraka
Maganga, rafiki na mwalimu wako.
Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0652612410. Au kwa barua
pepe ambayo ni Bmaganga22@gmail.com.
Wednesday, January 27, 2016
Hivi Ndivyo Mambo Yatakavyokuwa Baada Ya Wewe Kufanya Kitu Hiki Kimoja.
Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona
ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea kupambana kwa
hali na mali ili tu uweze kufanikisha yale ambayo umekuwa ukiyahangaikia mara
kwa mara. Vizuri endelea kupambana naama hakuna kitu cha bure hapa duniani,
maana hata miujiza huja kwa wale ambao huwa wanakuwa wakiitafuta miujiza hiyo.
Sio waliokaa tu wakisubiri miujiza hivyo nakusihii endelea kupambana ndugu
msomaji wa mtandao huu.
Mafanikio yanahitaji ahadi
ndugu mpendwa msomaji wa makala hii. Hili ni jambo ambalo ningependa uweze
kulifahamu kuanzia sasa,kuwa mafanikio yanahitaji ahadi. Yaani baada ya
kujiwekewa malengo unapaswa sasa kuweka ahadi juu ya utekelezaji wa malengo
yako. Pengine umekuwa ukijiwekea ahadi bila kujua ahadi ni kama pale unaposema
kuwa nataka kupunguza uzito likiwa kama lengo lako sasa pale unaposema lazima
kila siku nifanye mazoezi kwa muda wa nusu saa, tayari hapo unakuwa umejiwekea
ahadi katika maisha yako. Au unasema nataka kuamka kila siku saa kumi na moja
alfajiri ili niweze kufanya shughuli zangu za ndani kabla ya kwenda katika
mihangaiko yangu, kuamka saa kumi na moja ni ahadi tayari uliyokwisha jiwekea
katika maisha yako.
Tumekuwa watu wa kujiwekea ahadi nyingi nyingi tena ahadi
zingine zinakuwa kubwa na zenye kututisha kiasi kwamba tunaweza kufikiri kuwa
hatutoweza kutimiza ahadi hizo. Kimsingi ahadi na malengo ni vitu ambavyo
vinaenda sambamba na vinaweza kukupatia shida katika kuvitofautisha lakini
tofauti ni kuwa malengo yanaanza alafu ndio ahadi hufata. Sasa kwa kuwa ahadi ni hatua
moja wapo katika kuyaelekea mafanikio basi ni vyema ukatambua kuwa yafuatayo ni
mambo ambayo yatakukumba baada ya kuwa umejiwekea ahadi zako wewe mwenyewe:-
1. Vikwazo vitaibuka,
baada ya kuwa umeshajiwekea ahadi zako vikwazo vitaibuka sana tena vingi kuliko
unavyodhani. Vitaibuka vikwazo vya aina mbili ambavyo ni vikwazo vya nje na vya
ndani. Vikwazo vya nje ni vile ambavyo vitatokana na wale watu wanaokuzunguka
kama vile marafiki, ndugu au hata wazazi, ambao wanaweza kukuzuia wewe katika
kuweza kutekeleza ahadi yako, zinaweza zikawa kauli zao juu ya ahadi yako au
hata kukucheka na kukupinga zaidi na zaidi. Vikwazo vya ndani ni vile ambavyo unajiwekea
mwenyewe kama vile uvivu, kukosa umakini, kupuuzia ahadi yako n.k. hivyo
vikwazo vyote hivi visikutishe katika kuweza kuishikiria ahadi yako na hatimaye
kuweza kuitekeleza ipasavyo.
2. Utafanya makosa,
katika kuelekea kutekeleza ahadi yako utafanya makosa kadha wa kadha, makosa
haya yapo ili tu kukufunza. Kama unataka kufanikiwa ni lazima uwe na mtazamo
tofauti juu ya makosa unayoyafanya. Kama kweli unataka kusonga mbele katika
safari yako ya mafanikio sasa ni wakati wa kubadili mtazamo wako katika makosa
unayoyafanya. Amini kuwa makosa yapo tu ili kuweza kukufunza na sio kingine.
Hivyo basi usirudi nyuma katika kuitekeleza ahadi yako uliyojiwekea, makosa
yasikutishe bali jifunze jifunze kutokana na makosa.
3. Utavunjwa moyo,
hili nalo litakukumba kwa kiasi kikubwa na hasa kitakacho kuvunja moyo ni pale
utakapo kuja kujikuta umefanya makosa mengi na pale utakapo ona kuwa unakumbwa
na vikwazo vingi sana. Mambo haya yote yanaweza kukuvunja moyo kwa kiasi kikubwa sana, lakini kwa wewe unae
yasaka mafanikio kamwe usivunjike moyo bali wewe endelea kuishikiria ahadi
yako.
Tambua kuwa haya yote ni majaribu ambayo
dunia itakuwekea ili kukupima ni jinsi gani uko makini juu ya ahadi yako. Mara
nyingi watu wengi hutamani kuachana na ahadi zako, lakini wewe unaye yasaka
mafanikio hutakiwi, hutakiwi kukata tamaa kamwe. Kama alivyosema bwana winstone
Churchill “never never never give up” au kama alivyosema bwana james .J.
Gorbelt “you become a champion by fighting one more round, when things are
tough you fight one more round”. Yaani unakuwa mshindi baada ya kupambana hatua
moja zaidi na zaidi hata kama mambo yakiwa magumu pambana hatua moja zaidi.
Twende sote.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua
pepe: Bmaganga22@gmail.com
Tuesday, January 26, 2016
Ni Muda Wa Kuachana Nazo Sasa
.
Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona
ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea kupambana kwa
hali na mali ili tu uweze kufanikisha yale ambayo umekuwa ukiyahangaikia mara
kwa mara. Vizuri endelea kupambana naama hakuna kitu cha bure hapa duniani,
maana hata miujiza huja kwa wale ambao huwa wanakuwa wakiitafuta miujiza hiyo.
Sio waliokaa tu wakisubiri miujiza hivyo nakusihii endelea kupambana ndugu
msomaji wa mtandao huu.
Je unakumbwa na wasiwasi wa kufanikiwa kutokana na
historia yako ya nyuma zile kauli wanazokuambia wanaokuzunguka zinakurudisha
nyuma katika hali ya kutaka kusonga mbele katika kuhakikisha kuwa unafanikiwa
katika maisha yako. Je? unajua ni kwa nini kauli ulizopandikizwa kutoka
utotoni zinaendelea kukurudisha nyuma
katika safari yako ya kuyaelekea mafanikio, ni kwasababu umeziamini na
kuzifanya kuwa ukweli wako. Sasa jiambie mwenyewe kuwa ni wakati wa kuachana nazo sasa.
Zile imani ulizojijengea zamani ya kuwa hutofanikiwa na
kuwa tajiri kwa kuwa wazazi wako ni masikini, imani ya kuwa huto fanikiwa kwa
kuwa wazazi wako ni masikini, ni muda wa kuachana nazo maana hazina msingi
wowote na wala hazikujengi wala kukusaidia chochote bali zinakudidimiza zaidi
na zaidi badala yake wewe pambana kweli kweli hata kama unatokea katika familia
masikini, na mafanikio utayaona tu, maana wapo waliokuwa kama wewe na
waliotokea chini kama wewe na wakafanikiwa hivyo hilo lisikupe shide sana bali
achana na hiyo imani.
Uliambiwa kuwa wewe ni mjinga na hauwezi chochote na
mwalimu wako, ni wakati wa kuachana na kauli hii ambayo ulikuwa umeiamini kwa
kuwa ilitoka kwa mwalimu wako na kupitia kigezo cha sifa ya ualimu basi
ukaamini kuwa hauto fanikiwa fanya kama Thomas
Edison ambaye pamoja na kukataliwa na walimu watatu tofauti kuwa hafai kuwa
mwanafunzi wa kujifunza chochote lakini alijifunza na kuwa mwanasayansi mkubwa
duniani na mpaka leo anaheshimika kama mwanasayansi mashuhuri duniani. Hii ni
kutokana na sababu kuwa yeye aliachana na kauli za waalimu wake, hivyo basi
hata wewe unaweza kufanya hivyo na ukafanikiwa pia, hivyo achana na kauli mbovu
alizokuambia mwalimu wako.
Walikuita mbumbumbu mtaani kwenu, mtaani kwenu wewe ndio
ulionekana kuwa mtoto mbumbumbu kuliko wote na ukafutwa kabisa kwenye watoto
ambao wanaweza kuleta mabadiliko yoyote au kuleta mafanikio yoyote ambayo
yataisaidia jamii yako na wewe ukaamini kuwa kweli hauwezi kutokana na maneno
yao. Ni muda sasa wa kuachana na kauli hizo ambazo hazina msingi wowote bali ni
za ukatishaji taama.
Lazima utambue kuwa
tunakuwa kadri tunavyofikiri, hata bibilia imeliandika hilo kuwa kadri
ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo huwa. Hii inamaana kuwa wewe mwenye ndiye
mwamuzi wa maisha yako yaani ni kadiri unavyojiona wewe mwenyewe ndivyo huwa unakuwa.
Na biblia haijasema kadri wamwonavyo watu ndivyo mtu huwa, hilo ni jambo ambalo
halijaandikwa wala kusemwa. Hivyo basi kama wamesema hauwezi kufanikiwa ni wao
na sio wewe, wewe usizifuate kauli zao ambazo hazina msingi wowote bali wewe
endelea kushikilia ukweli ambao unauona nafsini mwako na katika kuushikilia
ukweli huu uwe ni ukweli ule ambao ni chanya achana na kauli hasi kabisa maana
hazikufikishi popote.
Kumbuka nimesema ni muda wa kuachana nazo zile kauli zote
ambazo ni hasi, ni muda wa kuachana nazo maana hazina msaada kwako ila zina
kudumaza na kukudidimiza zaidi na zaidi. Na kubwa zaidi juu ya kauli chanya ni
kuwa haziwezi kukuletea mafanikio yoyote.
Twende
sote.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua
pepe: Bmaganga22@gmail.com
Monday, January 25, 2016
Wajibika Ipasavyo Kama Kweli Unataka Kufanikiwa.
Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona
ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea kupambana kwa
hali na mali ili tu uweze kufanikisha yale ambayo umekuwa ukiyahangaikia mara
kwa mara. Vizuri endelea kupambana naama hakuna kitu cha bure hapa duniani,
maana hata miujiza huja kwa wale ambao huwa wanakuwa wakiitafuta miujiza hiyo.
Sio waliokaa tu wakisubiri miujiza hivyo nakusihii endelea kupambana ndugu msomaji
wa mtandao huu.
Naamini umekuwa ukipambana sana katika kuhakikisha kuwa
unafanikiwa katika yale ambayo unayahangaikia nami na kusihi uendelee kupambana
maana katika mahangaiko ndiko mafanikio hutokea. Lakini lazima ujue kuwa lazima
kitu hiki ukifanye kama unataka kufanuiki. Kitu hiki ni kitu muhimu sana katika
maisha yetu na mafaniko kwa ujumla lakini jambo la kushangaza ni kuwa tumekuwa
hatulitili maanani sana na ndio maana wengi wetu tumekuwa tukijikuta hatusongi
mbele wala nini ila tunabaki pale pale au kurudi nyuma kabisa kimaisha.
Huwa unapata picha gani pindi unapoona mfanyakazi fulani katika
kampuni fulani kafukuzwa kazi. Au kasimamishwa kazi kwa muda. Unapata picha
gani pindi unapomwona mfanyabiashara fulani kashindwa kibiashara yaani biashara
yake imekufa. Unapata wazo gani unapomwona mtu anailaumu serikali yake kwa
kushindwa kwake wakati yeye ndiye aliyepaswa kufanya jambo husika. Hakika yote
hayo hutokea kutokana na kukosekana kwa kitu hiki kimoja nacho ni uwajibikaji.
Maishani bila kuwajibika tambua kuwa hauto kwenda kokote
kule bali utaishia pale pale. Dunia ya sasa imejaa ushindani wa hali ya juu
ambao unaongezeka siku hadi siku na atakae weza kusitaimili ushindani huu ni yule
tu mwenye kuweza kuwajibika ipasavyo. Kama wewe ni mfanyabiashara na
unawajibika bora liende tambua kuwa hauto kwenda popote bali utaishia kufulia
tu. Mfanyakazi pia ambae hutaki kuwajibika tambua kuwa utaishia tu kufukuzwa
kazi yako hiyo na hatimae kuukaribia umasikini nao utakukaribisha vizuri sana
kuliko unavyodhani.
Leo hii takwimu zinaonyesha kuwa kati ya biashara mia
moja zinazo anzishwa leo baada ya miaka kumi ni biashara chini ya ishirini
ndizo huwa zimekuwa. Hii ni kutokana na uwajibikaji mbovu wa wafanyabiashara
husika. Wafanyabiashara hawa wamekuwa hawahangaiki katika kutafuta taarifa
sahihi kabla ya kuzianzisha biashara zao na vile vile wamekuwa wagumu wa kuendelea
na utafiti baada ya kuanzisha biashara zao, hivyo hata yakitokea mabadiliko wao
hawashituki wala nini. Bali huendelea kufanya biashara zao kwa mazoea na
matokeo yao hujikuta wamefulia maana hujikuta hawapati wateja. Hii ni kutokana
na uvivu ulio letwa na kuto taka kuwajibika kwao na ndio maana wanajikuta
wameanguka.
Ukiwa mfanyakazi unajisikiaje pale unapoambiwa
tunakuwajibisha kutokana na utendaji wako mbovu angalia leo hii ni watu wangapi
wamesimamishwa kazi toka uongozi wa awamu ya tano uingie madarakani na wote
sababu zimekuwa zikionekana ni uwajibikaji mbovu na mengine, lakini kubwa ni
uwajibikaji mbovu ambao huwapelekea wafanye mambo kiholera holera na matokeo
yake ni kuja kuwajibishwa.
Kama unataka kufanikiwa hakikisha unayavaa majukumu yako
usisubiri mazingira yaje ya kushitaki na kukuwajibisha vikali. Au usisubiri
kufulia kukuwajibishe, ukiwa mfanyabiashara usisubiri anguko la biashara
likuwajibishe, mfanyakazi usisubiri kuwajibishwa na bosi wako bali vaa majukumu
yako mwenyewe na mafanikio utayaona tu. Ikiwa unasubiri kuwajibishwa basi sahau
kuhusu mafanikio na usilizungumzie tena neno hilo.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua
pepe: Bmaganga22@gmail.com
Subscribe to:
Posts (Atom)