Wednesday, April 13, 2016

Zama Zimebadilika Sasa

.
Dunia inabadilika sasa, dunia inabadilika kila siku, kila saa kila dakika, kila sekunde, kila mwaka dunia inabadilika. Je wewe unabaadilika kulingana na dunia au unaendelea kuwa vile vile. Yaani wewe unabaki kuwa vile vile kila siku, kila wiki, kila mwaka na kila mara au unabadilika kulingana na wakati? Ni muhimu ukajijibu maswali haya bila kigugumizi hata siku.
Kichwa cha makala yetu kinasema zama zimebadilika. Ndio zama zimebadilika sana tena sana ndio maana jambo lililokuwa linafanywa jana leo linaweza kuja kufanywa kwa njia nyingine tofauti na ile ya jana swala hapa nalo taka kulenga ni katika mabadiliko ya kiutendaji. Zamani ilikuwa ni kuwa kila mtu anakula kutokana na nguvu zake, yaani matumizi ya nguvu ndio yalikuwa yanakufanya uishi. Hivyo basi katika zama hizo mwenye nguvu ndiye aliyeweza kudumu na yule dhaifu au asiye na nguvu alikuwa hana nafasi ya kuishi au aliishi kwa shida sana.

Lakini naomba nioneshe masikitiko makubwa sana juu ya hili maana katika wakati wa sasa jambo hili ni haliwezekani kwa sasa, maana mfumo huu wa maisha umekuwa unafanya kazi kwa wanyama tu ambapo mnyama mwenye nguvu mfano simba ndiye mwenye uhakika wa kuishi zaidi kuliko wanyama wasio na nguvu mfano swala ambao mara nyingi hujikuta wakiwindwa na kuliwa na simba hawa. Ndio maana nakuambia kuwa zama zimebadilika.

Zama zikoje sasa? Kwa zama za sasa au zama za leo hii, nguvu sio kitu bali akili ndio kila kitu, kwa kifupi ni kwamba matumizi ya akili yamekuja kufanyiwa mabadiliko na matumizi ya akili hivyo basi matumizi ya nguvu nyingi pasipo na akili ni sawa na kazi bure. Dunia ya sasa inachangamoto na ushindani mkubwa sana ambapo ni lazima uingie katika mapambano hayo ili uweze kufanikiwa lakini silaha ya kupambana kwa sasa sio nguvu tena bali ni matumizi ya akili. Napo zungumzia akili narejelea matumizi ya fikira chanya na ubunifu katika utatuzi wa changamoto ambazo zinatukabili siku hadi siku.

Leo hii kutokana na ongezeko la ushindani wa biashara huwezi kusema utatumia nguvu katika kufanya biashara, nguvu ya mwili haina maana katika ushindani wa biashara bali nguvu ya akili ndiyo yenye tija katika biashara ya leo hii. Yaani ili uweze kushinda na kufanya biashara yako ikuwe kwa kiwango kikubwa sana basi inatakiwa utumie akili na sio nguvu ya mwili.

Zamani ilikuwa ili mkulima aweze kufanikiwa lazima atumie nguvu nyingi sana katika kulima ashinde shambani huko kila siku kuanzia asubuhi hadi jioni lakini sio sasa, naposema matumizi ya akili ni pamoja na kukubaliana na mabadiliko kisha ukachukua hatua mfano katika kilimo anza kutumia mbegu za kisasa, lima kwa wakati, fata ushauri wa kitaalamu n.k hayo ndio matumizi ya akili nayo yarejelea hapa.

Kumbuka kuwa dunia inabadilika kila dakika, kila siku, leo hii hata bondia anaetegemea nguvu zake tu au uwingi wa misuli yake ambayo imetapakaa mwili mzima pasipo kutumia akili ujue kila siku wewe bondia utakuwa unapigwa tu. Ni bora ukavitumia vyote lakini nakushauri kuwa matumizi ya nguvu ndio yazidi kuliko matumizi ya nguvu. Kwanini ni muhimu kufanya hivyo, ni muhimu kufanya hivyo kwa kuwa nguvu zikizidi akili maana yake ni kuwa wewe utakuwa unaendeshwa na matakwa ya mwili, lakini akili zikizidi nguvu ya mwili hii inamaanisha kuwa utaweza kuuzuia mwili wako kwa namna fulani na hapo ndipo mafanikio huanza kujitokeza kwa kiwango kikubwa.

Nikutakie kila kheri katika safari yako ya kuboresha maisha yako ya kila siku.


                                          Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.

KARIBU KATIKA DARASA HURU.
Je? unataka kujifunza na kuwa bora zaidi?,Je? unataka usihangamie kwa kukosa maarifa?,Je? unataka kujua namna ya kutatua matatizo na changamoto mbalimbali zinazokukabili?,Je? unakumbana na hali ya kukata tama mara kwa mara?,Je? unashindwa kujiwekea malengo n.k.Kama jibu ndio basi karibu katika darasa huru. Namna ya kujiunga na darasa huru tuma kiasi cha pesa cha shilingi 5000/= kwa namba 0754612413 kwa mpesa (jina. Baraka magama) au 0652612410 kwa tigo pesa. (jina: Baraka maganga). Kisha, tuma namba yako ya simu kwenda namba moja kati ya hizo huku ukiwa umeambatanisha na jina lako kamili kama linavyojitokeza katika m-pesa au tigo pesa. Kumbuka kufanya hivyo huku ukiwa na uhakika kuwa pesa yako imepokelewa na hapo utaunganishwa kwenye kundi la whatsapp ambalo litakuwa na jina la DARASA HURU.
N.B, huduma hii itatolewa kwa njia ya whatsapp, hivyo hakikisha simu yako ina uwezo wa whatsapp ndipo ujiunge ili kuepuka usumbufu.
Barikiwa.

No comments:

Post a Comment