Tuesday, April 12, 2016

Tusihishie Kushabikia Tu.

Leo hii tanzania kimeibuka kitu ambacho kimeibuliwa na serikali ya awamu ya tano. Ambacho kinatufanya wengi wetu tuwe mashabiki sana wa hiki kitu. Wengi wetu leo hii tumekuwa tukishabikia sana sera ya mheshimiwa raisi ya kutumbua majibu, kweli wengi sana tunashangiulia lakini leo nataka kukusisitiza na kukuonya kuwa usiishie kuwa shabiki tu wa hii sera ya kutumbua majipu.
Sera hii ilianzishwa na mheshimiwa raisi kwa lengo moja tu la kuwawajibisha wasiotaka kuwajibika wenyewe kwa ihali yao. Sasa kama wewe unaishabikia sera hii ni muhimu utambue kuwa neno kutumbua jibu ni kwa wale wasiotaka kuwajibika na sio vinginevyo na pindi unaposhabikia kuwa fulani kawajibishwa anza kujiuliza kuwa wewe unawajibika kwa kiasi gani?. Dhana hii imekuja kuonekana kuwa ni mwiba mkali sana kwa viongozi na watumishi wa serikali lakini hapa mimi sipo kuongeana na viongozi naongea na wanamafanikio na wanaotaka mafanikio.

Kwako wewe mwanamafanikio hutakiwi kushabikia tu dhana hii pasipo kuelewa maana yake, mimi nishakupa maana yake kuwa mtu yoyote asiyetaka kutekeleza wajibu wake ni jipu. Sasa kwa kuangalia hilo wewe unahisi hapa tanzania tuna majipu mangapi?. Kwa watumishi na viongozi wa serikali akiwa jipu anatumbuliwa maana yake anakosa kazi, je mambo yakoje kwako wewe unayetaka mafanikio?, kwako wewe unayetaka mafanikio kama ukiwa jipu hii inamaanisha kuwa hauwezi kuyapata mafanikio kamwe na kwako wewe ulie na mafanikio alafu ni jibu hapa litakalo tokea ni kuwa utapata anguko kubwa sana.

Nimesema usiishie kuwa shabiki tu wa hili neno la kutumbua majipu, maana wakati mwingine kuwa shabiki tu kunakufanya ushindwe kufikiri nje ya boksi. Leo hii kila mtu anafurahi akisikia kiongozi fulani katumbuliwa jipu lakini turudi kwako wewe baba wa familia ambaye ukiamka tu ni wewe na mambo yako tu hujui familia itakula nini, watoto wameenda shule au la, hujui hata kama familia ni wazima au la ila swala ni kuwa wewe ukiamka tu unakurupuka na kwenda kijiweni kucheza bao na kupiga stori nyingi kweli wakati hutaki kuwajibika kwa lolote lile linalohusu familia, nataka nikuulize kwa maana niliyoitoa kuhusu jipu, je hapo wewe sio jipu?.
Wewe mfanyakazi kwanini hutaki kufanya kazi ipasavyo unafanya kazi ilimradi umefanya nataka nikuulize hiyo kazi uliombewa au uliomba mwenyewe, hivi kuna aja gani na kufanya kazi ambayo huipendi, nakusikia unasema aa bhana kazi tunafanya hivyo hivyo tu. Ukiwa unasema hivyo kuwa unafanya kazi hivyo hivyo tu ndio maana unajikuta ukitumbuliwa jipu maana kitendo cha kusema kazi unafanya hivyo hivyo hii inamaanisha kuwa huwajibiki ipasavyo, sasa nataka nikuulize uliajiliwa ili ukafanye kazi au ili ukafanye kazi hivyo hivyo?

Nakuona mkulima unafurahi maana hakuna wa kukutumbua jibu, ni vizuri lakini nataka nikuambie ukiona kila siku kipata chako cha mazao ni kile kile miaka nenda miaka rudi jua na wewe mkulima ni jipu, tena jipu kubwa tu sema hakuna wa kukutumbua tu ndio maana unafurahi furahi tu. Nataka nikusisitize sana ndugu mkulima kuwa jibidiishe katika kilimo, tafuta mbinu mpya za kilimo, tafuta taarifa mpya za kilimo ili usiwe mkulima jipu hata kama hakuna wa kujitumbua.


Katika mafanikio tunasema jipu zuri ni lile la kujitumbua mwenyewe, yaani njia bora ya kuwajibika ni kujiwajibisha mwenyewe usisuubiri kujakuwajibishwa kama watumishi wa serikali.
Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.

KARIBU KATIKA DARASA HURU.
Je? unataka kujifunza na kuwa bora zaidi?,Je? unataka usihangamie kwa kukosa maarifa?,Je? unataka kujua namna ya kutatua matatizo na changamoto mbalimbali zinazokukabili?,Je? unakumbana na hali ya kukata tama mara kwa mara?,Je? unashindwa kujiwekea malengo n.k.Kama jibu ndio basi karibu katika darasa huru. Namna ya kujiunga na darasa huru tuma kiasi cha pesa cha shilingi 5000/= kwa namba 0754612413 kwa mpesa (jina. Baraka magama) au 0652612410 kwa tigo pesa. (jina: Baraka maganga). Kisha, tuma namba yako ya simu kwenda namba moja kati ya hizo huku ukiwa umeambatanisha na jina lako kamili kama linavyojitokeza katika m-pesa au tigo pesa. Kumbuka kufanya hivyo huku ukiwa na uhakika kuwa pesa yako imepokelewa na hapo utaunganishwa kwenye kundi la whatsapp ambalo litakuwa na jina la DARASA HURU.
N.B, huduma hii itatolewa kwa njia ya whatsapp, hivyo hakikisha simu yako ina uwezo wa whatsapp ndipo ujiunge ili kuepuka usumbufu.
Barikiwa.No comments:

Post a Comment