Saturday, April 9, 2016

Mfahamu Mtu Huyu Vizuri.


Habari za wakati huu ndugu mpenzi msomaji wa makala za mtandao huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vyema katika kuhakikisha kuwa unapambana ilivyo ili kuweza kujiletea mafanikio, nami nasema mapambano yanaendelea kamwe usikate tamaa hata siku moja. Maana mpambanaji huwa hakubali kukata tamaa kirahisi.
Wakati unaendelea kupambana ili kuhakikisha kuwa unajiletea mafanikio ni vyema ukatambua jambo hili,kwa kuwaa ninaaini kuwa wewe hiki kitu unakifanya ndio maana nikakuuliza je? Mtu huyu unamfahamu vizuri? Najua kila mtu anasehemu au ana mtu ambaye huwa anakuwa anamwomba ushauri sasa kutokana na kitendo hiki ndio maana kichwa cha makala hii kinauliza mtu huyu unamfahamu vizuri?

Najua unamshauri wako, tena huyu ni mtu unaemwamini na kumtegemea kwa kiasi kikubwa sana tena sana, kwanini nimekuuuliza basi kuwa mtu huyu unamfahamu vizuri? Hapa nimekuuuliza kwa sababu ndani ya washauri wetu kuna mambo makuu mawili au kuna washhauri wa aina mbili, yaani kuna mtu anaetoa ushauri kwa kutumia uzoefu na kuna mtu anaetoa ushauri kama sehemu ya taaluma yake. Lakini ukiachilia mbali hizi tofauti wote wanafanya kazi moja mabayo ni ushauri. Sasa jambo nalo kuuliza unamfahamu mshauri wako, yaani unaufahamu kama yeye anatoa ushauri kutokana na uzoefu au anafanya kama taaluma?.
Mshauri anaefanya ushauri kwa kutumia uzoefu sio kuwa ni mbaya hapana lakini amekosa kitu kimoja ambacho ni taaluma, pia tatizo moja la mshauri wa namna hii ni kuwa anaendeshwa na matukio yaliyokwisha kutokea nyuma hivyo basi endapo litatokea jambo jipya au changamoto ambayo ni nje na uzoefu wake inakuwa ni ngumu sana kwake yeye kuweza kutatua changamoto husika. Pia mshauri huyu huwa anakuwa akitawaliwa na hisia zake zaidi kuliko za wengine hivyo basi hata kama wewe ukiwa na wazo zuri ila ni kinyume na uzoefu wake pamoja na  hisia zake basi hutoweza kupata ushauri sahihi.

Pia mshauri mwenye taaluma huyu sio kuwa nae ni mbaya ila tatizo linakuja kuwa mshauri wa namna hii ni kuwa anakosa kitu kimoja ambacho ni uzoefu. Lazima utambue kuwa maishani uzoefu una nafasi yake katika utatuzi wa changamoto maana uzoefu huwa unatusaidia kupata hisitoria ya tatizo husika. Hivyo basi uzoefu ni muhimu lakini mshauri mwenye taaluma anaweza kujikuta akiwa katika wakati mgumu pindi linapokuja swala la uzoefu. Lakini uzuri wa mshauri huyu ni kuwa hatawaliwi na hisia bali anafanya kazi yake kutokana na taaluma yake inavyomwongoza.

Hivyo basi nini ufanye sasa, jambo la kufanya hapa ni kuwa hakikisha kuwa unamfahamu vyema mshauri wako kwa kuwa huyu ni mtu ambaye anakuwa na nafasi kubwa sana katika maisha yako, najua ni ngumu kumpata mtu mwenye taaluma na uzoefu hilo lisikupe shida wewe lakini hakikisha kuwa unamfahamu mtu huyu anaekushauri, yaani uwe na uwezo wa kutambua kuwa mshauri huyu je anaongozwa na hisia zake katika kunishauri au anatumia taaluma na je anayonishauri yanaendana. Maana kuna mtu ukimwomba ushauri juu ya jambo fulani ambalo yeye aliwahi kufanya akashindwa tambua kuwa hapo hutoweza kupata ushauri mzuri bali utakuwa ni ushauri wa kukatisha tamaa tena kwa kiwango kikubwa sana, maana siku zote aliyeshindwa hawezi kukupa wewe ushauri wa kukutia moyo kuwa utafanikiwa ili hali yeye alishindwa.  Hivyo basi hakikisha kuwa unamfahamu vyema mshauri wako.
]

Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.

KARIBU KATIKA DARASA HURU.
Je? unataka kujifunza na kuwa bora zaidi?,Je? unataka usihangamie kwa kukosa maarifa?,Je? unataka kujua namna ya kutatua matatizo na changamoto mbalimbali zinazokukabili?,Je? unakumbana na hali ya kukata tama mara kwa mara?,Je? unashindwa kujiwekea malengo n.k.Kama jibu ndio basi karibu katika darasa huru. Namna ya kujiunga na darasa huru tuma kiasi cha pesa cha shilingi 5000/= kwa namba 0754612413 kwa mpesa (jina. Baraka magama) au 0652612410 kwa tigo pesa. (jina: Baraka maganga). Kisha, tuma namba yako ya simu kwenda namba moja kati ya hizo huku ukiwa umeambatanisha na jina lako kamili kama linavyojitokeza katika m-pesa au tigo pesa. Kumbuka kufanya hivyo huku ukiwa na uhakika kuwa pesa yako imepokelewa na hapo utaunganishwa kwenye kundi la whatsapp ambalo litakuwa na jina la DARASA HURU.
N.B, huduma hii itatolewa kwa njia ya whatsapp, hivyo hakikisha simu yako ina uwezo wa whatsapp ndipo ujiunge ili kuepuka usumbufu.
Barikiwa.


No comments:

Post a Comment