Maisha yamejaa changamoto za namna mbalimbali, wakati
unapambana ili kujihakikishia kuwa unapata mafanikio au matokeo mazuri juu ya
mambo fulani swala la changamoto huwa linakuwa ni jambo ambalo halihepukiki
wakati mwingine. Ni muhimu tupitie katika changamoto kwani changamoto hizi huwa
zinatujenga na kutufanya tuwe imara zaidi na zaidi maishani,
Ni muhimu kusimama imara pindi tunapokuwa tunakabiliwa na
changamoto hizo. Hii ni kutokana na sababu kuwa uwezo wa kupambana na
changamoto hizi huwa upo mikononi mwetu. Ni muhimu kutambua kuwa kwa kila
changamoto inayokukabili ni muhimu uanze kujihoji kwanza na kujiuliza wewe
mwenyewe ufanye nini juu ya changamoto husika. Kwa kufanya hivyo utajikuta
unapata majibu ambayo yanakuwa msaada mkubwa sana kwako. Pamoja na hayo
zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo zaweza kukusaidia wewe katika utatuzi wa
changamoto inayokukabili:-
Kuwa mkweli, hapa
nazungumzia ukweli baina ya pande mbili. Ukweli wa nafsi yako na ukweli kwa
wengine. Unapokabiliwa na changamoto na unapotaka kuitatua changamoto husika
basi hakikisha kuwa hu mkweli wa nafsi yako na kwa wengine. Ukweli wa nafsi
yako ni muhimu pale ambapo utakuwa unajihoji mwenyewe ili kutaka kujua nini
haswa chanzo cha changamoto ile, na ufanye nini wewe kama wewe ili kuitatua
changamoto hiyo. Ukweli wa nafsi yako mwenyewe ni muhimu kwa kuwa huu
utakuondolea ile hali ya kutaka kuwasingizia watu wengine kuwa wao ndio chanzo
cha changamoto husika wakati sio kweli, pengine wewe mwenyewe ndio chanzo cha
changamoto husika.
Ukweli kwa watu wengine huu utakuwa na
msada pale ambapo unataka kumshirikisha mtu fulani ili aweze kukupa msaada wa
mawazo juu ya nini ufanye kuhusiana na changamoto hiyo. Ni muhimu kuwa mkweli
pale unapotaka kupata msada wa mawazo kutoka kwa wengine, hii itawasaidia wao
kuelewa changamoto inayokukabili kinagaubaga na hatimaye wakaweza kutoa mchango
wao kwa usahihi kwa kuwa umeiweka wazi changamoto na wameielewa kuliko
ungeficha ficha mambo.
2. Omba ushauri kwa mtu sahihi,
hapa nachomaanisha ni kuwa unapokabiliwa na changamoto ni muhimu ukaelewa kuwa
sio kila mtu anaweza kukupa ushauri wa ni nini haswa unapaswa kufanya ili
kuweza kukabiliana na changamoto husika. Ndio maana ninakuambia omba ushauri
kwa mtu sahihi. Mfano unakabiliwa na
changamoto katika kilimo cha nyanya ni muhimu ukaomba ushauri kwa mkulima au
mtaalamu wa kilimo hicho cha nyanya na sio unachangamoto katika kilimo cha
nyanya wewe unaenda kuomba ushauri kwa mkulima yoyote yule au mtaalamu yoyote
yule wa maswala ya kilimo. Ni muhimu utambuwe kuwa kuna kitu kinaitwa ubinafsi
katika maisha, yaani kutokana na upana wa jambo fulani kila mtu leo hii
anafanya ubinafsi katika taaluma fulani
ndio maana leo hii unaweza kukuta kuna daktari wa macho pekee mengine hajui hii
ni kutokana na ubinafsi alioamua kuufanya katika taaluma husika, hivyo ni
muhimu ukaelewa mtu unaemfata kutaka ushauri yuko katika jambo hilo kiusahihi.
Nimekupatia njia mbili rahisi sana za
kuzifuata pindi unapokabiliwa na changamoto, nina imani kuwa njia hizi hazina
ugumu wowote katika kuzitekeleza ndio maana nikasema ni rahisi. pia nina imani
kuwa ukizifuata njia hizi utapata matokeo mazuri na utaweza kuitatua aina
yoyote ile ya changamoto inayokukabili. Kumbuka changamoto ni kitu ambacho
mwanadamu hawezi kukiepuka ila anao uwezo wa kukabiliana nazo.
Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.
:-barua
pepe -Bmaganga22@gmail.com.
KARIBU KATIKA DARASA HURU.
Je?
unataka kujifunza na kuwa bora zaidi?,Je? unataka usihangamie kwa kukosa
maarifa?,Je? unataka kujua namna ya kutatua matatizo na changamoto mbalimbali
zinazokukabili?,Je? unakumbana na hali ya kukata tama mara kwa mara?,Je?
unashindwa kujiwekea malengo n.k.Kama jibu ndio basi karibu katika darasa huru. Namna ya kujiunga na
darasa huru tuma kiasi cha pesa cha shilingi 5000/= kwa namba 0754612413
kwa mpesa (jina. Baraka magama) au 0652612410 kwa tigo pesa. (jina: Baraka
maganga). Kisha, tuma namba yako ya simu kwenda namba moja kati ya hizo
huku ukiwa umeambatanisha na jina lako kamili kama linavyojitokeza katika
m-pesa au tigo pesa. Kumbuka kufanya hivyo huku ukiwa na uhakika kuwa pesa yako
imepokelewa na hapo utaunganishwa kwenye kundi la whatsapp ambalo litakuwa na
jina la DARASA HURU.
N.B, huduma hii itatolewa kwa njia ya whatsapp, hivyo
hakikisha simu yako ina uwezo wa whatsapp ndipo ujiunge ili kuepuka usumbufu.
Barikiwa.
Karibu sana.
No comments:
Post a Comment