Wednesday, February 24, 2016

Yatathimini Matumizi Yako Ya Pesa Kwa Umakini Kabla Hujasema Tatizo Mtaji
Habari za wakati huu ndugu mpendwa msomaji wa makala za mtandao huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri sana katika kutekeleza majukumu yako ya hapa na pale, ni muhimu uendelee kufanya hivyo kwani mapambano yanaendelea kwa kiasi kikubwa sana hivyo jambo la msingi ni kuyaendeleza mapambano hayo kwa kasi ya ajabu ili kuweza kuyatekeleza yale ambayo ni ya msingi na ambayo kwa upande mwingine ndiyo tumekuwa tukiyataka maishani.

Wakati ukiendelea kupambana ndugu mpendwa msomaji wa makala hii hebu kwa dakika moja tu fikiria juu ya matumizi yako. Naposema matumizi najua nakuwa na eleweka kwa kiasi kikubwa tu, matumizi nayo yazungumzia hapa ni matumizi ya pesa. Nilipenda kichwa cha makala ya leo kiwe mtaji sio tatizo lakini nimeamua kukiweka  kama kilivyo kwa kuwa ntakacholenga kukisema kitakuwa na uhusiano tu na mtaji. Tumekuwa ni watu wa kulalamika sana juu ya mitaji, sana tena sana. Lakini leo hii naomba tujadili na tuweze kuelewana kuwa mtaji sio tatizo bali ni vichwa vyetu ndivyo vyenye matatizo. Hapa leo naongea na wafanyakazi uwe mfanyakazi wa serikali au shirika binafsi naongea na wewe hapa leo.

Kwanini nataka niongee na wafanyakazi kwa kiasi kikubwa ni kwa sababu ya vituko vya wafanyakazi, kila mtu leo hii anaamini kuwa wafanyakazi mishahara yao haiwatoshi kwa kuwa wao ni walalamikaji wakubwa kuwa mishahara haiwatoshi. Lakini mimi nataka kusema kuwa mishahara inawatosha. Tutoke huko maana sio lengo la makala. Lengo la makala ni kutaka kuonyesha kuwa mtaji sio tatizo kwa kupitia kuchunguza matumizi yetu ya pesa tunazozipata kama mshahara wa shughuli zetu.

Wakati nikiwa kidato cha sita miaka michache huko nyuma nilijifunza kutoka katika kitabu cha rich dad poor dad cha bw. Kiyosaki tofauti kati ya asset na liabilities.  Kwa mujibu wa kiyosaki anafafanua assets kama kitu ambacho kinachoingiza pesa mfukoni ili hali liabilities ni kitu ambacho kinatoa pesa mfukoni. Hapo hapo rudi katika kichwa cha makala, tathimini matumizi ya pesa zako, wewe pesa zako unazitumia katika nini, je ni asset au liabilities? Jijibu mwenyewe. Kiyosaki aliendelea kusema kama unataka kuwa tajiri nunua assets na kama unataka kuwa masikini nunua liabilities. Hapo hapo turudi kwako huwa unanunua nini?. Rudi nyuma tena jiulize kwanini mpaka leo hauna mtaji wa kuanza biashara au jambo jingine tofauti na kazi yako hiyo. Tatizo mtajii eehe wenzio waliupataje huo mtaji sasa?. Aya nakuambia hivi tatizo sio mtaji tatizo ni akili yako hiyo. Kama unataka kujua kama mshaara wako unaweza kukupatia mtaji chunguza matumizi yako ya pesa. Unatumia pesa nyingi sana kwenye liabilities ndio maana hauna mtaji. Kama unabisha sawa ila huo ndio ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli.

Wafanyakazi wengi wanamtindo wa kununua vikolokolo ndio maana hawapati mitaji, . naposema vikolokolo namaanisha kuwa vitu visivyo na tija wala umuhimu bali katika hali ya kutaka kuuridhisha moyo, mwili au wenzio. wewe huyo kila aina ya simu unataka uwe nayo, baba/mama utaweza kushindana wa wachina kila siku wako na matoleo mapya. Kila uzinduzi wa albamu unataka uende, kila tamasha la muziki wewe humo, kila fashioni mpya ya nguo humo, kila mkopo unataka ukope alafu mkopo huo unataka ukanunue pikipiki ya kuendea kazini. Pikipiki itakudai mafuta alafu utajikuta huna pesa. Kwa matuzimi ya namna hii kweli mshahara haukutoshi na hauwezi kupata mtaji. Lakini ukipunguza mfano ukawa na simu hata teckno p5 inatosha mbona nayo utaingia fb, whatsapp na instrgram, pia makala zangu utasoma sasa yanini bwebwe nyingi za masimu kibao.

Ni muhimu kupendeza kimavazi lakini sio muhimu kuwa na kila aina ya vazi. Ni muhimu kuwa na pikipiki lakini ujue ni assets au liabilites. Ni muhimu kuuzulia matamasha na uzinduzi wa albamu za wasanii uwapendao lakini sio wote. Jiulize kama kwa mwezi unatumia shilingi laki mbili kutoka katika mshahara wako katika liabilities, ukiachana nazo mara mwaka utakuwa hujapata mtaji wewe au unaleta habari gani hapa. Chemsha kichwa sio kulalama tu. Think beyond.

Uwezo wa kupata mtaji kupitia mishahara yetu tunayo sema shida ni akili zetu na vichwa vyetu. Unakopa mkopo unanunua jiko la gesi, sijui sofa, sijui sabufa usiposikiliza mziki utakufa simu yako haina mziki? Kuwa na nidhamu na pesa vinginevyo utaishia kulalamika mpaka siku yesu anarudi.

“If you want to be rich buy assets” ROBERT KIYOSAKI.
“Mtaji sio tatizo tatizo ni vichwa vyetu”.
Je unataka kujipatia kitabu cha Robert kiyosaki ili kujifunza zaidi na zaidi usiwe na shaka.nitumie email kupitia email yangu ya hapo chini na neno, “nataka kitabu cha rich 
dad poor dad” nami ntakutumia.

Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.
Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0654612410 au kwa barua pepe:- Bmaganga22@gmail.com.No comments:

Post a Comment