Tuesday, February 23, 2016

Utavuna Ulichopanda Na Huto Vuna Usichopanda.
Habari za wakati huu ndugu mpenzi msomaji wa makala za mtandao huu, mtandao ambao umelenga kukupatia maarifa ambayo ukiyatumia huta kaa ujute kwanini uliamua kujiunga na mtandao huu ili uwe unasoma makala zake. Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri sana katika mapambano nami nasema mapambano yanaendelea na yataendelea.

Ukipanda mahindi utavuna mahindi.
Ukipanda mtama utavuna mtama
Ukipanda matikiti utavuna matikiti.
Usipopanda maharage hutovuna vuna maharage.
Usipopanda mti hutovuna  mti.
Usipopanda alizeti hutovuna alizeti.

Nimeweka kauli hizo hapo juu lengo sio kukuchosha au kukutaka uzisome tu na kuishia kuzishangaa hapana lengo la kuziweka kauli hizo hapo juu ni kutaka uweze kunielewa toka mwako ambacho nakimaanisha maana hapa nataka tuelewane kiurahisi zaidi pengine kuliko siku zote ndugu msomaji wa makala hii. Kama kichwa kisemavyo kuwa utavuna ulichopanda na hutovuna usichokipanda. Hivi nikikuuliza ndugu msomaji wa makala hii kuwa uonapo kauli hii unajifikiria nini juu ya maisha yako. Yaani unaonaje juu ya matokeo uyapatayo kutokana na shughuli zako?. Na uionapo kauli hii unahusianisha vipi na ulalamishi au ulalamikaji wa watanzania wa leo. Binafsi naamini kuwa kama watanzania tungekuwa wenye kuielewa kauli hii vizuri basi leo hii kusingalikuwa na mtanzania anayekaa na kuanza kuilaumu serikali, wazazi, ndugu au walezi wake kuwa wao ndio chanzo cha yeye kuto kufanikiwa. Kwanini nasema hivyo mimi nasema hivyo kutokana na kauli ilivyo.

Kauli inasema utavuna ulichopanda. Kwahiyo ukipanda ulalamishi utavuna ulalamishi kwahiyo ni kuwa ukimlaumu mtu nae atakulaumu au nawewe utalaumiwa na wengine. Kauli inasema utavuna ulichopanda na hautovuna usichopanda hakuna sehemu ambayo imesema utavuna ulichopandiwa na hautovuna ulichopandiwa hapa naweza kusema kauli hii haitambui jambo linaloitwa utegemezi hivyo basi kama vijana wangekuwa wanaielewa vyema kauli hii wangeacha maswala ya kuwategemea wazazi wao kwa kila kitu badala yake wangeanza kupanda mbegu Fulani ambazo zingeweza kuwazalia matunda Fulani ambayo kwa siku za baadae zingewaletea matokeo mazuri.

Kauli hii pia inatukumbusha juu ya uwajibikaji nikiisoma kauli hii nakumbuka juu ya uwajibikaji kuwa kila mtu anapaswa kuwajibika kwa mafanikio yake na sio kumtegemea mtu akuletee mafanikio. Huwa tunakwepa majukumu yetu kwa kiasi kikubwa sana, sasa kauli hii inatukumbusha juu ya uwajibikaji juu ya maisha yetu. Utavuna ulichopanda maana yake unahusikia moja kwa moja juu ya matokeo uyapatayo maishani. Kama wewe ni masikini mpaka sasa tambua kuwa umepanda mbegu za umasikini na ndio maana uko masikini mpaka leo. Hakuna mtu anayehusika na umasikini wako bali ni wewe mwenyewe ndiye unayehusika nao maana ni mbegu ambazo umepanda wewe mwenyewe bila kumhusisha mtu mwingine hivyo basi unawajibika kwa umasikini wako na sio vinginevyo.

Kauli hii inanikumbusha juu ya ubora wa mbegu zetu yaani kama unataka kupata matokeo bora  ni wakati sasa wa kupanda mbegu bora, maana si utavuna ulichopanda maana yake ni kuwa mbegu bora huzaa mbegu bora  na mbaya huzaa mbaya nyenziye. Hivyo basi panda mbegu bora maana ndiyo ikufahayo.

Maishani tumekuwa tukikumbwa na mambo mengi sana na tumekuwa watu wa kuwasakizia wengine kuwa ndio wahusika wa mambo hayo yanayotutokea hata kama ni kwa kuwasingizia lakini huwa tunataka kuuaminisha umma kuwa hali zetu mbaya ni matokeo ya watu au vitu fulani kumbe tunakuwa tunajidanganya sasa jambo la msingi hapa ni kuwa kwa kuwa umegundua kuwa utavuna ulichopanda hata ikitokea watu wanakushawishi uanze kulalamika juu ya jambo fulani we achana nao maana ukweli wa mambo ushaujua.
Uvivu huzaa uvivu.
Lawama huzaa lawama.
Visingizio huzaa vizingizio.
Tamaa huzaa tamaa.n.k

Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.
Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0654612410 au kwa barua pepe:- Bmaganga22@gmail.com.


No comments:

Post a Comment