Habari za wakati huu ndugu msomaji wa makala za mtandao huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri katika kupambana
kwakwo ili tu kuhakikisha kuwa unajiletea mafanikio makubwa maishaniNi vyema ukashikiria yale unayoyaona ni mema kuyafanya na ukayafanya bila kuchoka ili tu ujiletee mafanikio makubwa maishani. Maisha ni mapambano, mafanikio ni mchakato unaoandaliwa sio kitu kinachokuja tu bila kuelewa kimetoka wapi. Hivyo basi pambana bila kuchoka.
Ikiwa unaendelea kupambana ndugu msomaji ni bora ukatambua jambo hili moja nalo ni kuwa ulishawahi kuwaza juu ya kitu kinachoitwa
kurudia/marudio. Yaani kama ulikuwa unafanya jambo ukajikuta unarirudia na kurirudia unajisikiaje? je huwa unakuwa na hiyo tabia au huwa unachukulia kurudia kufanya jambo au shughuli fulani ni kupoteza muda na kujichelewesha, kama huwa unawaza hivyo basi acha kufanya hivyo mara moja maana unajidanganya na kama huwa unakuwa na tabia ya kurudia kufanya jambo husika basi endelea kufanya hivyo maana upo sahihi sana.
Kwanini nimekuambia kuwa uwe na tabia ya kutaka kurudia
kufanya shughuli fulani au jambo fulani nimekuambia hivyo kwa sababu moja
muhimu nayo ni kuwa kurudia kufanya jambo fulani ndiko huleta mafanikio.
Marudio ni mbolea ya mafanikio kama hauelewi au ulikuwa haujui. Ndio
nakuona umeduwaa ila ukweli ndio huo kuwa marudio ni mbolea ya mafanikio.
Tafsri yake ni nini haswa hapa, hapa tafsiri yake ni kuwa yule mwenye tabia ya
kufanya jambo fulani kisha akaendelea kurirudia na kurirudia atakuwa na kuwa
mwenye mafanikio makubwa sana kuliko yule ambaye huwa hana tabia ya kurudia
kufanya jambo. Kama wewe ni mkulima au ulishawahi kujishughulisha na shughuli
za kilimo utajua tofauti iliyopo kati ya mmea uliowekewa mbolea na ule ambao
haukuwekewa mbolea. Sasa kama unazijua zile tofauti basi hata katika maisha
yetu sisi wanadamu inakuwa hivyo.
Chukulia mfano wa mtu anayejifunza kuendesha baiskeli
huwa anakuwa na wakati mgumu sana katika kutekeleza zoezi hili la kuendesha
baiskeli, lakini pamoja na ugumu huo ikiwemo kuanguka na kuumia lakini huwa
tunaendelea kurudia rudia hili zoezi la kujifunza baiskeli mpaka tunajikuta
sasa tumeshakuwa mafundi na mabingwa wa kuendesha baiskeli na kwetu inakuwa sio
shida tena. Hali sio hivyo tu katika baiskeli bali hata katika vyombo vya moto
kama vile gari, pikipiki, ndege na hata meli. Ujifunzaji huu hutawaliwa na
marudio kwa kiasi kikubwa sana kiasi kwamba uwingi wa marudio ndio uendana
sambamba na ufanikishaji wa jambo husika. Hapa ndio maana tunasema marudio ni
mbolea ya mafanikio.
Wewe unayesoma makala hapa, ulijuaje kusoma, hebu jiulize
kwa dakika moja au mbili, ulijuaje kusoma au ulianzaje anzaje mpaka ukajua
kusoma?. Lazima kuna hatua za ujifunzaji ambazo ulipitia lakini katika hatua
hizo lazima marudio huwa muhimu sana, tulipokuwa watoto wadogo tulikuwa wenye
kutaka kujua kusoma na hapo ndipo tulipoanza kujifunza taratibu kuzitamka
irabu, na konsonati na baadae herufi, katika kujifunza utamkaji huu tulikuwa ni
watu wenye kurudia rudia kujifunza huko matokeo yake leo hii mimi na wewe
kusoma sio shida tena hii ni kutokana na sababu kuwa tulijijengea mazoea ya
kurudia rudia kile tulichojifunza mara kwa mara.
Sasa ajabu ni kuwa
leo hii tumekuwa hatutaki kurudia yale ambayo tumekuwa tukiyafanya na hii ni
baada ya kushindwa na matokeo yake ni kuwa tunajikuta kuwa sasa tuko katika
wakati mgumu kiasi kwamba sio rahisi kwetu sasa kuweza kufanikiwa kwa kuwa
tunapuuzia vitu vidogo kama hivi. Weka marudio kama kanuni yako ya kuelekea
mafanikio hata kama umeshindwa jambo fulani rudia rudia jambo husika na
mafanikio utayaona tu tena kwa kiasi kikubwa. Waingereza husema “practice makes
perfect” wanamafanikio tunasema marudio ni mbolea ya mafanikio. Hivyo basi
uamuzi ni wako kurudia tena kufanya jambo hata kama ulishindwa au kuacha
kurirudia hilo jambo huo ni uamuzi wako maana nilishakuonyesha kipi ni bora na
kipi sio.
Ni mimi rafiki
yako,
Baraka Maganga.
Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0654612410 au kwa barua pepe:- Bmaganga22@gmail.com.
No comments:
Post a Comment