Friday, February 12, 2016

Watu Sahihi, Taarifa Sahihi Tunaenda Mbele.


Kumekuwa na tatizo moja kwa sasa ambalo limekuwa likitusumbua kwa kiasi kikubwa sana na tatizo hili limekuwa likitugharimu wengi sana na kujikuta
tumepoteza muda mrefu sana katika kufikia hatua fulani ambayo tulikuwa tukitaka kuifikia. Tunaishi katika dunia ya taarifa (information age), yaani katika dunia ya saizi ni kuwa taarifa fulani ambayo wewe unaijua ambayo mwingine haijui inaweka tofauti kati yako na mtu mwingine.

Sasa leo hii nimekuja kukupa kitu kimoja kuwa unajua kuwa huwezi kupata taarifa sahihi ikiwa hautopata mtu sahihi wa kukupatia taarifa hizo. Umekuwa ukihangaika sana katika kupata taarifa fulani ambayo itakusaidia lakini cha ajabu ni kuwa haupati na wengine hujikuta wanatapeliwa katika kutafuta taarifa hizi. Usipo jua kutafuta taarifa katika dunia ya sasa utakuwa upo nyuma sana na unaweza kujikuta haufanikiwi kabisa maishani 
mwako.ukimtafuta mtu asiye sahihi utapata taarifa ambazo zimejaa kubashiri kwingi na ni wazi kuwa taarifa hizi haziwezi kukufanya ukasonga mbele zaidi ni kuwa utabaki pale pale au kurudi nyuma. Sasa nataka hapa nipinge ile tabia ya kujifanya tunatumia uzoefu kwa mambo ya kitaalamu na hapa nataka kusema kuwa kazi ya kitaalamu ifanywe na mtaalamu sio mzoefu, ulishawahi kuwaza kutafuta au kupata ushauri wa kitaalamu, hili ndilo nalotaka kuzungumzia kuwa jitahidi kutafuta wataalamu kwa kila linalokukabili.

Umehangaika na sasa umeona kuwa katika kilimo kuna fursa sasa ni wakati sahihi wa kuwatafuta wataalamu wa kilimo ili uweze kupata taarifa sahihi juu ya kilimo husika. Kilimo ni neno la jumla sana huwezi kusema mimi najishughulisha na kilimo bali inabidi ufafanue kuwa kilimo cha zao gani husika mfano umeamua kulima nyanya, mahindi, maharagwe, pilipili hoho au vitunguu ni muhimu ukawatafuta wataalamu wa zao husika ili uweze kupata ushauri wa kitaalamu na sio kila ukimkuta mkulima analima vitunguu unaanza kupapalika nawe ni vizuri kumuuliza sawa huyo mkulima wa vitunguu lakini nenda hatua zaidi na upate ushauri wa kitaalamu ambao utakupeleka mbele.
Unamatatizo ya kifamilia ua ndoa, ni muhimu ukaenda kuwaona watu waliosoma maswala ya kimahusiano au wanasaikolojia ambao watakusaidia katika mahusiano sio kwenda kuyaanika matatizo yako ya kifamilia kijiweni ambayo huko wanaweza kukupatia ushauri ambao ni wa kubomoa na wala sio ule wenye kukujenga na kukufanya uweze kusonga mbele kimaisha.

Una matatizo ya kiafya ni muhimu sasa uweze kutafuta mtaalamu wa matatizo ya kiafya ili uweze kutatua matatizo yako na sio kwenda kwa kila mtu na kuweza kuhangaika hangaikua huku na huku uku ukiomba ushauri wa mambo ya kiafya ambayo wengine wanaweza kuwa na taarifa fupi tu au maelezo machache tu juu ya mambo ya kiafya. Nenda kwa madaktari ukaombe ushauri na sio kuishi kwa mazoea maana hizi sio zama zake.

Ni muhimu ukatambua kuanzia leo kuwa kitakachokufanya uweze kufanikiwa sio kingine balli ni pamoja na taarifa sahihi ambazo utakuwa ukizipata kutoka kwa watu sahihi mfano ukipata taarifa sahihi kuhusu fursa fulani tayari utakuwa umepiga hatua moja zaidi kuelekea mafanikio. Kumbuka pia hatupo katika zama za kati za mawe ambapo watu walihishi kwa mazoea sio wakati wake leo hii kinachohitajika ni taarifa na sio taarifa bora taarifa, bali ni taarifa sahihi ambazo nazo hazipatikana kwa kila mtu bali wa sahihi.

Naomba nikusisitizie kuwa sio kuwa wataalamu pekee ndio wa kuwafuata na kuwaomba taarifa sahihi lakini ni bora ukaelewa kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo wataalamu wananafasi kubwa sana lakini pia kwa mfano katika maswala ya kilimo unaweza kwenda kwa mkulima mwenye mafanikio ambaye huyu sio mkulima pekee bali ni mtaalamu pia na ukapata taarifa sahihi kwa mtu sahihi. Tafuta taarifa tafuta taarifa kwa mtu sahihi kwa mtu sahihi.

Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.
Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0654612410 au kwa barua pepe:- Bmaganga22@gmail.com.


No comments:

Post a Comment