Saturday, February 13, 2016

Mambo Sita (6) Ambayo Sio Msaada Katika Kutatua Changamoto Zetu Lakini Tunayafanya.


Maisha ni mapambano, ni mapambano dhidi ya changamoto ambazo huibuka kila leo na hatuna budi kuweza kukabiliana na changamoto husika
maana sisi ndio wanajeshi ambao tumejitolea kupambana na adui changamoto ili tuweze kutetea nchi yetu na kushindwa kupambana na adui changamoto kunamaanisha kuwa nchi yetu itavamiwa na tutakuwa mateka wa jumla wa adui yetu mkubwa. Hapa neno nchi yetu limetumika kuwakilisha maisha yetu na mateka wa jumla limetumika kama kuwa masikini. Naamu kushindwa kupambana na changamoto ni kujitakia umasikini.






Tumekuwa tukikumbwa na changamoto mabalimbali na uwezo wa kupambana na changamoto unabaki kwetu, kila mtu amekuwa na namna yake ya kuweza kupambana na changamoto ambayo ama kwa nafsi yake huiona kuwa inafaa, lakini hapa nakuletea njia sita ambazo sio msaada katika kupambana na changamoto hata kama unazitumiaga na unaona zinafaa lakini changamoto hubaki pale pale. Endelea kusoma

1.    Lawama, hii kwangu ni njia namba moja ambayo tumekuwa tukiitumia wengi wetu, na wengi wetu huamini kuwa hii ndio njia sahihi ya kupambana na changamoto zinapotukabili. Lakini leo nakuambia hii ni njia moja mbaya tena ni namba moja katika ubaya kama kweli unapambana changamoto. Haifai haifai nakusihi acha acha acha mara moja. Hebu chukulia wewe ulikuwa mwanafunzi uliye maliza kidato cha nne na baada ya matokeo kuja unajikuta umefeli vibaya, lakini kuna uwezekano wa wewe kurudia tena mtihani na ukasonga mbele lakini wewe hulioni hilo badala yake unakaa na kuanza kuwalaumu waalimu kuwa hawakufundisha vizuri. Nakuuliza hivi kumlaumu mwalimu kuwa hakukufundisha vizuri kunakusaidia nini? Je kunabadilisha matokeo?. Umefukuzwa kazi unaanza kumlaumu bosi wakati makosa ni yako, je kumlaumu bosi kunakurudisha kazini wewe?

2.    Visingizio, namba mbili kwa mujibu wangu katika njia za kukabiliana na changamoto. Utakuta mtu ni masikini ananza kusingizia ooh mimi niko hivi kwasababu sikusoma, oo wazazi wangu waliishi kijijini, ooh kwetu hatunaga bahati ya kufanikiwa. Mbona unapoteza muda wao ovyo  kuongelea mambo ambayo hayana uhusianao na umasikini wako. Na je kusingizia huko sasa kumekufanya kuwa tajiri sasa?. Acha visingizio wewe ndiye chanzo wa kila kitu nenda katafute ufumbuzi sio kusingizia.


3.    Kulia, nakuona unalia eti kisa unachangamoto fulani. Nani alikuambia kulia kunatatua changamoto. Kama unaamini ukilia unatatua changamoto vizuri sana ila nakuambia unajidanganya. Hebu chukulia mfano unanjaa, njaa imekuuma sana. Njia yako ya kukabiliana na changamoto si kulia anza kulia sasa kama njaa itaisha. Njaa inatibiwa kwa kutafuta msosi sio kulia.

4.    Kufikiri kujinyonga, haya ndio mawazo mfu kabisa, umesalitiwa na mpenzi wako eti unataka kujinyoga, hivi umeiona hiyo ndiyo njia rahisi sana. Hivi ukijinyonga ndio unakuwa umetatua changamoto au. Aya kama unasema ni sahihi sasa nakuuliza kama kila mtu angekuwa anakabiliwa na changamoto fulani na anaamua kujinyonga basi dunia hii ingekuwepo miti tu maana hakuna mtu ambaye hapitiwi na changamoto fulani za kimaisha. Acha kufikiri kujinyonga sasa.


5.    Kuhairisha jambo husika,ukiona unafanya jambo fulani ukakumbana na ugumu unakimbilia kuacha au kuhairisha jambo husika, je umeona hiyo ndio njia sahihi sio. Kwahiyo ukihairisha maana yake utafanya baadae au ukiacha kabisa unakuwa umemamaanisha kuwa utakuwa umetatua changamoto hiyo?. Huko ni kukimbia majukumu tabia ambayo ni mbovu sana.

6.    Kwenda kuombewa ikiwa huna imani kuwa itakusaidia, umepigika unajikuta sasa ngoja niende kwa watumishi nikajaribu kama wanaweza kunisaidia kutatua changamoto hii lakini sina imani kama wataweza maana, sasa kama huna imani na kitu kwanini ukifanye sasa, mi naona bora ungeacha kufanya jambo husika. Maana unapoteza muda wako bure na hautofanikiwa.

Hizo ni njia sita ambazo hautakiwi kuzifuata ewe mwanamafanikio pindi unapokuwa umekabiliwa na changamoto, lakini kinyume chake ndio jibu mfano badala ya kulaumu wewe usifanye hivyo badala yake tafuta njia nyingine.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.
Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0654612410 au kwa barua pepe:- Bmaganga22@gmail.com.


No comments:

Post a Comment