Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona
ya maarifa ni matumaini yangu kuwa umeshaianza siku yako vema na unaendelea
kupambana ili kuhakikisha kuwa siku yako ya leo mpaka inaisha unakuwa
umejisogeza vya kutosha katika kuyatekeleza malengo yako. Nami nakusihi
usichoke maana mafanikio yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu hata kama mambo
hayajaenda sawa wewe usijali endelea kupambana tu na mafanikio utayaona.
Leo kuna jambo nataka kukushirikisha ndugu msomaji wa
mtandao huu, tumekuwa tukiamini kuwa maneno huumba, au wengine husema kauli
huumba tukiwa na maana kuwa kadri tujisemeshavyo wenyewe juu ya maisha yetu ndivyo maisha yetu huwa. Sasa
kutokana na hili ndio maana nimekuletea kauli kumi ambazo watu wamekuwa
wakizitumia na zimekuwa zikiwafelisha na kuwaweka mbali na mafanikio kauli hizo
ni kama ifuatavyo:-,
Sikuzaliwa au kukulia katika familia
bora,
kuna watu ambao huamini na kuhararisha kutokufanikiwa kwao na kutozaliwa au
kuto kukulia katika familia bora. Hizi ni kauli ambazo hazina maana yoyote
katika dunia ya leo maaana mafanikio ni wewe na sio familia uliyokulia, na kama
wewe unaona hilo ni sahihi ni wangapi kwani ambao wamefanikiwa japo kuwa
hawajatoka familia bora?, acha mara moja kauli hizi badala yake anza kufikiria
utafanyaje ili ufanikiwe ijapokuwa hujatoka familia bora hilo ndilo jambo la
msingi.
2. Sikuzaliwa upande sahihi,
hawa ni waleambao huona kuwa kutokana na wao kuzaliwa bara fulani, au nchi fulani
ni mkosi kwao, maana huamini kuwa bara au nchi husika waliyomo haiwaruhusu
kufanikiwa. Ni kauli za kijinga na ambazo hutumiwa na watu ambao hawajafanikiwa
ndio husema bora kuzaliwa mbwa ulaya kuliko mtu afrika, hizi ni kauli za ajabu
sana, kwani ni waafrika wangapi wapo afrika na wamefanikiwa, ni watanzania
wangapi wanamafanikio hapa hapa Tanzania, ni wakenya, waganda n.k wangapi wenye
mafanikio ndani ya nchi zao?. Acha kauli zisizo za msingi.
3. Sina elimu ya kutosha,
hii ilikuwa na umuhimu enzi zile za zama za kati za mawe lakini sio katika
dunia ya sasa ya taarifa. Nani aliyekuambia mafanikio ni kutokana na elimu yako
tu?, wangapi wanamafanikio makubwa na hawana hata digrii, masters, wala hizo
phd ambazo wewe unaamini lazima uwe nazo ndizo zitakufanya ufanikiwe. Chukulia mfano
wa mafanikio ya msanii Diamond na msakata kabumbu Mbwana Samatta, je wanaelimu kiasi gani?. Jibu
baki nalo.
4. Hayo ni mambo yako sio yangu,
kauli kama hizi ndizo huwafanya watu wakose fursa. Utamkuta mtu analetewa wazo
la kibiashara ambalo tayari ni fursa kwake lakini utamsikia aa bwana ee hayo ni
mambo yako sio yangu. Sasa endelea hivyo hivyo na utaendelea kukosa fursa siku
hadi siku.
5. Sina muda wa kutosha,
wewe kila siku muda haukutoshi, wewe ni nani na unafanya nini mpaka muda
usikutoshe kila siku?, je unataka upatiwe masaa 70 ndani ya siku moja? Kwanini wewe
tu ndio muda haukutoshi? Mbona wengine masaa 24 yanamtosha. Jifunze kutumia
muda ulopewa vizuri.
6. Sina pesa za kutosha,
unafikiri pesa inatosha kwa kukaa nayo tu? Au kwa kuiweka tu ndani na
kuishangaa au benki?, acha kufikiri pesa
itakuja kukutosha bila kuizungusha, jifunze kuizungusha hiyo pesa ndipo
itakutosha.
7. Sifahamiani na watu sahihi, ni
kweli hufamiani na watu sahihi kutokana na matendo yako na ndio maana huwezi kuwapata
watu sahihi wa kukusukuma uende mbele. Kama unataka kupata kushirikiana na watu
sahihi anza kufanya mambo yanayoendana na hao watu ambao kwako ni sahihi.
8. Sina mtandao wa watu,
hauna mtandao wa watu wa kushirikiana nawe kutokana na wewe mwenyewe ulivyo. Mtandao
wa watu wa kushirikiana nao unakuja kutokana na kile ambacho unakifanya na
kutokana na ushirikiano wako na watu wengine. Unashirikiana na nani haswa na
huyo unayeshirikiana nae je? anamtandao au?.
9. Mke wangu hanisaidi, ni
kweli mke wako hakusaidi lakini wewe kama wewe umechukua juhudi gani
kuhakikisha kuwa wewe kama wewe unapigana vilivyo katika kuhakikisha kuwa
unasimama wewe kama wewe?, je mafanikio
yako yanamtegemea mke wako tu?, kama asingalikuwepo ungalifanyaje?, acha
kutegemea tegemea bila msingi badala yake jifunze kusimama mwenyewe muda mwingine.
10. Nina watoto wengi wa kulea,
kama ulijua kuwa watoto wengi wanakufanya usifanikiwe kwanini umekuwa nao?. Na je
ni kweli kwamba bila kuwa na watoto wengi ungefanikiwa au ni visingizio?, je
tukiwachukua hao watoto na tukakuacha mtupu utafanikiwa?
Kimsingi kauli hizi kumi kwa maneno
mengine tunaweza kuziita kama visingizio ambavyo mtu huwa navyo, na hii ni
hatari sana maana visingizio havikufanyi kuwa mwenye mafanikio bali vinazidi
kukurudisha nyuma. Hivyo basi uamuzi ni wako kuendelea na visingizio na sababu
sababu za kuto kufanikiwa kwako ambzao zitazidi kukufanya usiwe na mafanikio au
uziache na kuwa mwenye mafanikio.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua
pepe: Bmaganga22@gmail.com
No comments:
Post a Comment