Habari za leo ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya
maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendeleo kupambana
vilivyo katika kuhakikisha kuwa unajiletea mafanikio makubwa maishani mwako.
Nami nakusihi ndugu msomaji wa mtandao huu kuwa endelea kupambana, usichoke
hata siku mpaka uhakikishe kuwa unajipatia mafanikio makubwa, ambayo umekwisha
jiwekea.
Ukiwa unaendelea kujishighulisha na shughuli zako za kila
siku basi leo nakuletea kitu kingine ambacho unapaswa ukifahamu vyema. Kama kichwa cha makala kinavyosema kuwa sababu za
kwanini watu huwa hawajiwekei malengp maishani. Tumekuwa tukisisitizana na
kuambiana mara nyingi sana juu ya umuhimu wa kuweka malengo, lakini ukweli ni
kwamba ni watu wachache sana kati ya wengi ambao wamekuwa na utamaduni wa
kujiwekea malengo. Na walio wengi wamekuwa hawajiwekei malengo, sasa kwanini
watu hawa huwa hawajiwekei malengo maishani, zifuatazo ni sababu za kwanini
watu hawajiwekei malengo:-,
Hawako makini,
sababu moja wapo ya kwanini watu hawajiwekei malengo ni kutokana na sababu kuwa
hawapo makini maishani. Mtu makini na anayetaka kufanikiwa kwa hali na mali
lazima ajiwekee malengo. Lakini kutokana na ukosefu wa umakini miongoni mwetu
tumekuwa tukiishi hivyo hivyo bila malengo
.
2. Hawajayakubali majukumu yao,
kama mpaka sasa hujathubutu hata kujiwekea malengo basi tambua kuwa bado
hujataka kuyavaa majukumu yako. Yaani watu ambao bado hawajajiwekea malengo ni
wale ambao bado wanahisi kuwa yupo mtu fulani maishani ambae ndiye yupo kwa
ajili ya kusubiri kufanyiwa kitu fulani jambo ambalo kiukweli ni kujidanganya.
Hivyo basi ukosefu wa ile hali ya kuvaa majukumu ndio kimekuwa kikwazo cha watu
kujiwekea malengo.
3. Hawatambui umuhimu wa kujiwekea malengo,
watu wamekuwa hawajiwekei malengo kwa sababu hawajui umuhimu wa kujiwekea
malengo. Inaonekana kuwa miongoni mwa watu wengi sana hawana uelewa juu ya
maswala haya ya kujiwekea malengo ndio maana wamekuwa hawajiwekei malengo
maishani mwao. Watu hawaoni umuhimu wowote wa kujiwekea malengo ndio maana
wamekuwa hawajiwekei, lakini naomba niseme kuwa hii ni kosa kubwa sana ambalo
watu hulifanya, nasema hivyo kwa sababu ni vyema kila mtu akatambua umuhimu wa
kuweza malengo na akijua umuhimu atakuwa amejikomboa kwa kiwango kikubwa.
4. Hawajui ni vipi watapanga/ kuyaandika
malengo yao, sababu nyingine ambayo inawafanya watu
wasijiwekee malengo ni kutokana na ukweli kwamba hawajui ni vipi wajiwekee
malengo. Hii nadhani ndio sababu namba moja ya kwanini watu hawajiwekei malengo
maishani, yaani hawaweki malengo kwa sababu hawajui watafanyaje. Kama hujui
mpaka leo basi jua kuwa upo katika hatari.
5. Wanaogopa kukosolewa/ kukataliwa,
uoga umekuwa ukichangia sana miongoni mwa watu, na imekuwa sababu inayofanya
watu washindwe kujiwekea malengo, watu wamekuwa wakiogopa kujiwekea malengo kwa
kuwa wanaogopa kuwa endapo wakimwonesha mtu malengo yake atakosolewa sana hivyo
kutokana na woga huu basi unamfanya arudi nyuma na kukaa bila kuweka malengo.
6. Wanaogopa kushindwa,
watu wengi hawaweki malengo kwa kuwa wanaogopa kushindwa yaani anaogopa kuwa
itakuwaje nikiweka malengo alafu nisiyatimize hivyo kutokana na kuogopa huko
katika kushindwa basi anakaa tu na kutokujiwekea malengo.
Ikiwa unataka kufanikiwa zaidi na zaidi
ni muhimu ukatambua kuwa malengo ni kitu muhimu sana tena sana, malengo ni dira
katika maisha yako. Ikiwa hujajiwekea malengo basi nishakuwekea sababu sita za
kwanini hujafanya hivyo. Kupitia sababu hizo unaweza ukaelewa ufanye nini ili
kujiwekea malengo. Mfano umeshajua sababu moja wapo inayokufanya usijiwekee
malengo ni kuwa hujayakubali majukumu, sasa nini cha kufanya ni kuyavaa
majukumu kisha baada ya hapo utapata uwezo na uelewa wa ni vipi ujiwekee malengo.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua
pepe: Bmaganga22@gmail.com
No comments:
Post a Comment