Kila mtu anataka kufanikiwa, hakika hakuna
mtu asiyependa kufanikiwa. Lakini mafanikio hayaji hivi hivi mafanikio
yanapitia mambo mengi sana yenye kufurahisha na yanayovunja moyo. Lakini yote hayo hayatoshwi kukufanya
usifanikiwe jambo jingine ambalo nalo litakufanya usifanikiwe katika safari
yako ya kuyaelekea mafanikio ni ile tabia ya
kuwaendekeza marafiki.
Kila
mtu ana marafiki hilo halipingiki na sikatazi watu kuwa na marafiki lakini
jambo ambalo nataka kukutaadharisha Leo hii ni kuwa tabia ya kuwaendekeza
marafiki itakufanya usifanikiwe kabisa. Namaanisha nini kusema kuwaendekeza
marafiki?. Kuwaendekeza marafiki ni pale ambapo unajikuta ukishindwa kufanya
mambo yako na shughuli zako ulizojiwekea kisa marafiki wamekuja na kukushawishi
ufanye jambo jingine ambalo ni kinyume na ratiba yako binafsi.
Jiulize ndugu msomaji ni mara ngapi rafiki
yako amekuwa akija na kukuomba mwende sehemu mkatembee, mkaangalie Mpira kwenye
vibanda vya mpira, mwende kwenye kumbi za sinema au hata kwenda kubalizi
ufukweni. Na ukamkubalia ili hali ulikuwa na shughuli zako ambazo ulipanga
kuzitekeleza. Chukulia mfano umejiwekea malengo ya kupunguza uzito hivyo
ukaweka ratiba ya kufanya mazoezi ili kutimiza lengo lako la kupunguza uzito,
unapoanza tu kufanya zoezi anakuja rafiki yako na kukuomba mkaangalie mpira,
nawe kwa kuwa umemwendekeza rafiki yako unaamua kuhairisha mazoezi na
kuambatana nae kwenye kibanda cha mpira ili mkaangalie mpira. Sasa jiulize kwa
kufanya hivyo utayatekeleza malengo yako kweli?.
Jifunze kumkatalia rafiki yako kwa baadhi ya
mambo Fulani Fulani ili tu uweze kutekeleza ratiba zako ulizojipangia. Hiyo
haitapunguza urafiki wenu kama kweli mnapendana na nimarafiki haswa kwani
nachoamini Mimi rafiki yako lazima awe mwelewa na mwenye kuzijua na kuziheshimu
ratiba zako, pia asiyeweza kuzivunja ratiba zako ovyoovyo. Nawe inatakiwa uwe
na uwezo wa kuitetea ratiba yako ambayo itakufanya utekeleze malengo yako.
Usipende kumfurahisha rafiki yako wakati wewe unajiumiza Mara kwa Mara. Kuwa na
rafiki haimaanishi umnyenyekee maana kufanya hivyo unaweza kujikuta umekuwa
mtumwa na sio rafiki.
Marafiki
ni watu muhimu sana tena sana lakini ni watu wa kuwa nao makini kwa kuwa rafiki
anaweza kuwa mtu wa kwanza kukuulia ndoto zako bila wewe kujua kuwa ni rafiki
yako ndiye chanzo cha wewe kushindwa kutekeleza malengo yako jambo la msingi na
kubwa la kufanya chunguza sana ratiba anazokuletea rafiki yako.
Ni mimi rafiki yako
Baraka maganga
Bmaganga22@gmail.com
0754612413/0652612410.
No comments:
Post a Comment