Kihistoria tumejenga
utamaduni Fulani ambao binafsi naomba niuite utamaduni mbovu sana, utamaduni
huo ni ule wa kukubali kila tunaloambiwa na watu ambao wapo juu yetu kiuwezo,
kiumri hata kielimu. Utamaduni huu binafsi nauona kuwa muda mwingine huwa kikwazo
kikubwa sana katika maisha yetu na hata kuua ndoto na malengo yetu. Leo ndungu
msomaji nataka nikushauri haswa kwa wewe ambaye unataka mafanikio kuwa jifunze
kusema hapana kwa watu wafuatao:-
1. Wazazi, tumeaminishwa kuwa kuwakubalia wazazi
kwa kila jambo ambalo wanatuambia na hicho ndio kipimo cha heshima na adabu ya
mtoto kwa wazazi wake. Tumeaminishwa kuwa mtoto anayekubali kila analoambiwa na
wazazi wake huyo ndio mtoto mtiifu. Lakini leo nakushauri jifunze kusema hapana
kwa wazazi wako, hii haitakufanya uonekane mtoto asiye na heshima wala adabu na
unaposema hapana sema hapana ukiwa na lengo la kutaka kutetea ndoto na malengo
yako. Chukulia leo wazazi wanataka usome masomo ya sayansi ili uje kuwa daktari
lakini wewe ukiangalia huyawezi hayo masomo, kwa kuogopa kusema hapana
unakubali ili hali ulitaka kusoma masomo ya biashara matokeo yake unakuja
kufeli na udakitari haupati. Wazazi wale wale wanaanza kukulaumu kwa kushindwa
kuwaambia ukweli mwanzo na matokeo yake umefeli. Angalia ulivyojialibia leo hii
lakini yote haya yametokana na wewe kushindwa kutamka neno hapana.
2. Rafiki, tumekuwa ni watu wa kukubaliana na
marafiki zetu hata kwa mambo tusiyoyataka. Pengine tumekuwa tukifanya hivyo ili
tu tuonekane marafiki wema na watii na wenyekujari ama tumekuwa tukifanya hivyo
kwa lengo la kuogopa kuvunja urafiki wetu. Lakini kushindwa kusema hapana kwa
marafiki zetu kumetuponza wengi sana leo
hii wengine wapo jera kwa kesi za kuiba, wengine ni vibaka, wengine wavuta madawa
ya kulevya na wengine wamepoteza maisha yote haya ni kwasababu tulishindwa
kusema hapana kwa marafiki zetu. Mwambie rafiki yako hapana pindi unapohisi
anakushawishi ufanye mambo ambayo huyataki.
3. Ndugu,jiulize ni Mara ngapi unekuwa
ukifanya mambo usiyoyapenda wala kuyataka kisa alikuambia kaka, dada, babu,
bibi, mjomba, shangazi n.k. bila shaka jibu ni Mara nyingi. Jiulize tena
kwanini nilifanya hayo mambo nisiyoyapenda ili hali nilijua siyapendi? Jibu ni
kwasababu ulishindwa kusema hapana kwa kuwa uliogopa watakuona sio mtiifu tena
mwenye kukosa adabu. Jiulize tena kama unataka kuendelea na tabia hiyo ya
kushindwa kusema hapana. Natumaini jibu ni hautaki tena kuendelea maana umegundua
kufanya hivyo kunakuweka mbali na malengo yako.
4. Viongozi wako wa dini, hawa ni watu ambao
wamekuwa na mchango mkubwa sana katika maisha yetu. Lakini tunachokosea ni kuwa
tumewaamini sana hawa watu kiasi kwamba tumewafanya kuwa wao hawakoseagi hivyo badala
ya kuwaheshimu tunawaogopa sana tukiamini woga wetu kwao ndio heshima kwao.
Ndio maana hata ikitokea wanatuambia kitu ambacho hatukiitaji sisi hujikuta
tumekikubali tu ili tuonekane watiifu kwao. Jifunze kusema hapana kwa watu hawa
pia futa woga kabisa sema hapana kama kiongozi wako wa dini atakuambia vitu
usivyovipenda.
Kusema
hapana kwa mtu aliye juu yako kiumri, uwezo, elimu, kiongozi wa dini au waalimu
wako sio utovu wa nidhamu na tafadhari unaposema hapana hakikisha unatamka neno
hili ukiwa na uhakika kuwa unasimamia ndoto na malengo yako usiseme hapana kisa
umesoma hapa. Kabla hujasema hapana tafakari kwa kina sana ndipo useme hapana.
E
ndelea kutembelea mtandao huu kwa mambo mengi mazuri ya kujifunza na kujijenga. TWENDE SOTE.
No comments:
Post a Comment