Habari za wakati huu
ndugu msomaji wa mtandao huu. Ni matumaini yangu unaendelea vizuri katika
harakati zako za kupambana katika kuyatimiza yale uliyokwisha kujiwekea kama
malengo yako. Tumekutana tena katika kutaka kuelimishana na kujengana yote haya
ni katika kuhakikisha kuwa safari yetu ya kuyaelekea mafanikio inakuwa bora
zaidi na zaidi.
Leo ndugu msomajia nataka kukushirikisha jambo
moja ambalo binafsi naliona ni kama imani potofu ambayo inaendelea kupandikizwa
miongoni mwetu. Imani hii in ile yenye kutufanya tuamini kuwa mafanikio yako
mjini tu na hivyo basi kijijini hakuna mafanikio.
Tumekuwa ni watu wenye kuamini kuwa watu
wanaoishi mjini ndio wenye mafanikio tofauti na wale wanaoishi vijijini,
sidhani kama jambo hili lina ukweli wowote japo kuwa kiukweli ni kwamba
ukilinganisha mafanikio ya mjini na mafanikio ya kijijini ni dhahiri mjini.
kunaonekana kuna mafanikio lakini hapa tunazungumzia mafanikio ya mtu mmoja
mmoja. Ukiangalia leo hii utagundua kuna Lindi kubwa sana la watu (haswa
vijana).ambao wanahama kijijini kuelekea mjini wakiamini kuwa mjini ndiko kwenye
mafanikio tofauti na kijijini. Lakini wengi wao wakifika mjini hukuta mambo
yamekuwa magumu sana kiasi kwamba hutamani kurudi tena kijijini.
Kimsingi mafanikio yana husisha fursa jambo la
msingi ni kutafuta fursa na kutumia fursa hizo, leo hii utamkuta mtu akikimbia
kijijini huku akitelekeza mashamba mengi sana na kuamua kwenda mjini kutafuta kazi,
mtu huyu ameamua kwenda mjini kwa kuwa ameaminishwa kuwa mjini ndiko kwenye
mafanikio lakini mafanikio sio wingi wa watu, magorofa, magari n.k. mafanikio ni
pale ambapo umeweza kuyatekeleza malengo yako binafsi na uwezo wa kutekeleza
malengo hauna uhusiano na niwapi haswa ulipo. Yaaani hakuna sheria ya kwamba
ukitekeleza mafanikio yako ili hali uko mjini ndipo watakuita mwenye mafanikio
na kama ukitekeleza malengo yako ili hali ukiwa kijijini hautaitwa mwenye mafanikio.
Jifunze kuchunguza fursa mahali ulipo na
uzitumie usiwe mtu wa kukurupuka na kukimbilia sehemu zingine huku ukiamini
sehemu hizo ndizo zenye mafanikio kuliko zingine pasipo kufanya tathimini yoyote
ya msingi.
Ni Mimi rafiki yako
Baraka Maganga.
Bmaganga22@gmail.com.
0754612413/0652612410.
No comments:
Post a Comment