Kuna njia muhimu za
kuikuza biashara yako katika namna ambayo itakupendeza na kukuridhisha,
biashara ambayo itawafurahisha wateja wako, na kuweza kukupatia kipato
unachokitaka. Zifuatazo ni funguo tatu zitakazokusaidia
kupata mafanikio ya kweli katika biashara na kuweza kuifanya biashara yako kuwa
na ukuaji endelevu.
1. Kuwa kiongozi wa biashara yako.
Ili kuweza kujenga
biashara yenye mafanikio na yenye ukuaji endelevu unahitaji kuwa kiongozi wa
biashara yako, badala kuwa mfanya kazi tu katika biashara hiyo, jione kama
kiongozi wa biashara yako. Anza kwa kuwa wazi kuhusu kwa nini umeamua kuanzisha
au ulianzisha biashara yako, na vipi kuhusu maono yako, unataka nini kutoka
kwenye biashara yako na kwa ajiri ya maisha yako. Waza na ufikiri kama kiongozi
wa biashara, na ubakie mwenye nguvu na
mwenye hamasa kubwa ili uweze kuiongoza biashara yako katika mwelekeo ulio sahihi.
2. Weka umakini kwa wateja wako.
Wajue wateja wako,
Jitumbukize katika matatizo yao, changamoto zao, masuala yao na malengo yao ili uweze kujenga,
kutoa bidhaa na huduma zenye kiwango kikubwa na zenye ubora kwa wateja wako.
Kutoa huduma na bidhaa ambazo zitaweza kupata matokeo makubwa na kuleta majibu
chanya kutoka kwao. Na kama mteja wako ataweza kufurahia huduma na bidhaa zako
unazotoa, kwa kiasi kikubwa sana atakusaidia katika kukuongezea wateja, na kipato kwenye biashara
yako kitaongezeka ikiwa atawaambia wengine kuhusiana na huduma zako nzuri pamoja
na bidhaa unazotoa.
3. Weka umakini katika biashara yako.
Unachopaswa
kuzingatia hapa ni kufahamu mambo muhimu katika biashara yako ( masoko, mauzo n.k.) ili kuweza kuifanya biashara yako ifanye kile
inachosema, kwa kufanya hivi utakuwa unaiweka biashara yako katika njia ya
kuelekea kwenye mafanikio na ukuaji. Unahitaji kuwa na ufanisi katika maeneo
muhimu ya biashara yako, kuwa na ufanisi katika masoko, uuzaji na utunzaji wa
fedha za biashara na hata kwenye mambo ya sheria. inakupasa kujua wajibu wako
kama mmiliki wa biashara, unapaswa kujua rasilimali muhimu zinazoitajiwa na
biashara yako, ili uweze kuiendesha biashara yako vizuri na kuweza kukupatia
faida.
Hizo ni funguo tatu
za kujenga biashara yenye mafanikio na ukuaji endelevu, nakutakia kila la kheri
katika kuanzisha, kuendeleza na kuboresha biashara yako. Endelea kutembelea
mtandao huu kila siku kwa mambo mazuri ya kujifunza na kujihamasisha na pia
harika na wenzako ili nao waweze kupata mambo haya mazuri.
Ni mimi rafiki yako.
Geofrey mwakatika.
0767382324/0675555987.
No comments:
Post a Comment