Habari ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya. Na unaendelea kupambana vikali katika shughuli zako ili tu kuhakikisha kwamba unajiletea mafanikio makubwa. Nami nakuambia vizuri pia nakusihi endelea kupambana mpaka pale utakapo timiza malengo yako. Kama kawaida kila tunapokutana hapa huwa tunakutana kwa lengo moja tu nalo ni kupeana maarifa mapya. Leo jambo nalo taka kukushirikisha ni kuhusiana na upandaji wa mbegu.
Naposema upandaji wa mbegu najua kuna wale ambao mawazo yao yatawatuma kuwa nataka kutoa darasa juu ya upandaji wa mbegu za aina fulani shambani, na kuna wale ambao watabaki na mshanga kuwa namaanisha nini haswa. Usiwe na haraka ndugu msomaji bali endelea kuisoma makala hii kisha utanielewa ni mbegu gani namaanisha. Binadamu tumekuwa wapanda mbegu wakubwa sana tena sana maana hakuna siku ambayo inapita bila sisi kupanda mbegu hizi. Lakini tofauti ya mbegu hii na ile ya zile mbegu tulizozoea kupanda mashambani sio kubwa sana ila utofauti upo tu katika mahali pa kupandia. Yaani zile mbegu za shambani tunazipanda shambani au kuzifukia ardhini. Lakini hii mbegu nayo kuletea ni mbegu inayopandwa katika ubongo wa mwanadamu yaani kichwani au akilini mwa binadamu. Nisikuache nyuma ndugu msomaji wa makala hii utakapo kuwa unasoma makala hii na kukuta neno mbegu jua neno hili linasimama au nimelitumia badala ya neno fikira. Hivyo naposema unapanda mbegu gani namaanisha kuwa unajijengea fikira gani? Nadhani mpaka hapo utakuwa umeanza kunipata sasa. Sasa mbegu tunazopamba zimegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni kama ifuatavyo:-
Mbegu mbovu, /fikira mbovu (hasi), neno mbovu si neno geni kwako ndugu msomaji lakini japokuwa unaielewa maana yake lakini mimi nataka kuielezea au kulielezea neno mbovu zaidi kwako. Tunaposema kuwa kitu Fulani ni kibovu, kwa tafsiri ya haraka haraka ni kuwa tunamaanisha kuwa kitu hicho hakifai kwa matumizi. Na kama hakifai kwa matumizi maana yake ni kuwa haupaswi kukitumia kabisa kwa namna yoyote. Na pindi ukikitumia basi chaweza kukuletea madhara makubwa sana hebu chukulia mfano wa madhara ambayo unaweza kuyapata kutokana na kula chakula kibovu au kilichoharibika, wakati mwingine waweza hata kupoteza maisha. Turudi katika uhalisia sasa, hapa kwa wale ndugu zangu wakulima nadhani mtanielewa zaidi, hivi toka lini mtu akaipanda mbegu mbovu na akategemea mavuno mengi ya kuzii?. Unajua ni kwanini wakulima huchambua mbegu zao kabla ya kuzipanda au unajua ni kwanini wakulima huitaji mbegu bora? Jibu ni rahisi wakulima uchambua mbegu nzuri ili wasipande mbegu ,bovu kwa kuwa wanajua kuwa mbegu mbovu kamwe haiwezi kuzaa matunda na kama ikizaa matunda hayo yatakuwa mabaya.
Sasa chukua mfano huu wa mbegu mbovu ubadilishe jina lake na mifano yake, yaani badala ya mbegu mbovu weka fikira mbovu (hasi). Kwanini ulalamike usiku kucha, mchana kutwa kuwa maisha magumu, maisha hayaendi kila unachofanya hakieleweki na unakalia kumlaumu mungu kuwa kawapendelea wengine nk. Kumbe tatizo ni fikira zako mbovu ndizo zinakuletea matatizo yote hayo. Kama ilivyo katika mbegu kuwa mbegu mbovu haizai basi hata katika fikira ni hivyo hivyo nini cha kufanya sasa cha kufanya ni kufutilia mbali fikira mbovu.
Mbegu bora /fikira njema(chanya), mbegu bora ni ile yenye kuzaa matunda mengi tena kwa wingi sana, hii ni mbegu ambayo haina takataka za aina yoyote yaani ni mbegu ambayo ni safi sana na hivyo mpandaji huipanda pasipo kuwa na wasiwasi wowote ule juu ya uotaji na kipato. Hivi ndivyo ilivyo hata kwa fikira njema au chanya, mtu mwenye fikira chanya hana wasiwasi na maisha yake maana anaamini kuwa karanga iliyopandwa huzaa karanga inayofanana na mbegu husika na wala karanga haiwezi kuzaa mchungwa. Fikira njema haina takataka kama vile woga, ukataji tama, uhairishaji wa mipango ovyo vyo, majungu wala upotezaji wa muda ovyo.
Ni vyema ukajijengea fikira njema au chanya ili usiishi kwa wasiwasi, chagua mbegu bora ili uwe na uhuru na masiha yako. Ikiwa unaishi tu pasipo kuchagua aina ya mbegu inayokufaa basi aina yoyote ile ya matokeo kubaliana nayo lakini nakutaadharisha na uzingatie kuwa hauwezi kuvuna ambacho hukupanda hivyo chunguza matokeo ya mambo yako kisha utajua aina gani ya mbegu umepanda. Nakutakia kila kheri katika safari yako ya kuyaelekea mafanikio.
Ni mimi Rafiki yako,
Baraka maganga.
Bmaganga22@gmail.com
0754612413/0652612410.
Wednesday, November 25, 2015
Ifahamu Aina Ya Mbegu Unayoipanda.
Tuesday, November 24, 2015
Ni Wewe Wa Kufanya Hakuna Mwingine.
Habari za siku ndugu msomaji wa mtandao huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vizuri katika jitihada za kuhakikisha unapambana vikali ili tu kujiletea mafanikio na maendeleo nami nakusihi endelea kuwasha moto huo ulio ukoka ili tu usizime.
Kama kawaida tumekutana hapa lengo ni kutaka kupeana maarifa mapya na leo somo letu/ mada yetu inasema ni wewe wa kufanya na sio mwingine.
Kabla sijaenda mbali nataka ujiulize hili swali je? Unahisi kuna mtu alikuja duniani ili akufanyie jambo Fulani, akupangie mipango, malengo na akuangaikie kila siku ili kutatua matatizo yako. Kama jibu ni hapana, sasa unazani nani yupo ili kufanya kazi zako, kupanga mipango yako, malengo yako n.k. natumaini jibu ni kuwa hakuna mwingine wa kufanya vitu hivyo Bali ni wewe hakuna mwingine bali wewe unaesoma makala hii.
Tambua kuwa kila binadamu anamipango yake, malengo yake, shughuli zake, mawazo yake na fikira zake juu ya maisha yake. Tumekuwa tukiambiana kuwa daaa! Rafiki,ndugu au mwanangu nilikuwa nikikufukiria sana muda mrefu. Hivi unadhani anayekuambia kuwa nilikuwa nakufikiria au anakuwaza aliacha shughuli zako na kuanza kukuwaza tu wewe? Unafikiri wewe unaumuhimu mkubwa sana kwa huyo mtu mpaka aanze kukuwaza wewe sasa kama unategemea au unaamini kuwa kuna mtu anakufikiria umepotea sana tambua hakuna mtu wa kuwazia shughuli zako, wala mikakati yako mingine bali ni wewe mwenyewe yaani usijidanganye kuwa kuna mtu atafikiria juu ya maisha yako hakuna hicho kitu. Atafikiri sawa lakini hawezi kufikiri ama kuwaza kama ambavyo wewe ungefikiri na kuwaza juu ya maisha yako.
Unakaa hutaki kujishughulisha kabisa hutaki kufanya kazi yoyote unategemea watu fulani wakufanyie shughuli hizo hivi unafikiri kuna mtu ni mtumwa wako ambae atakuwa akikufanyia tu shughuli zako huku wewe umekaa tu ukisubiri akufanyie. Unafikiri bado kuna mfumo wa maisha unaoitwa utumwa? Nakuambia hakuna mfumo huo ulikwisha zamani sana pamoja na biashara ya utumwa hivyo leo hii hauwezi kumfanya mtu mtumwa wako kiurahisi. Hivyo tambua kuwa hakuna wa kukufanyia shughuli zako hivyo basi. Inuka ukajishughulishe acha kuona kuwa kuna mtu atakufanyia kazi. Hakuna mwingine wa kukufanyia shughuli bali wewe wenyewe.
Unafikiri kuna mtu maalumu ambaye yupo kwa ajili ya kukupangia malengo yako. Kama unaamini mtu huyo yupo na umempata basi tambua kuwa umepotea na unajidanganya maana hakuna mwingine wa kupanga malengo yako, bali ni we we. Tambua hilo kuanzia leo na ulishike. Malengo bora ni yale ambayo umeyapanga mwenyewe maana utakuwa pindi unapoyasoma yanakuhamasisha na kukumbusha kuwa ni wewe mwenyewe uliye ya panga na kuyaandika hakuna mwingine. Hivyo basi usimruhusu mtu akupangie malengo maana ukifanya hivyo yule anayekupangia malengo ataandika malengo yake na atakuaminisha kuwa hayo malengo ni yako. Hivyo wewe utayafata hayo ukiamini ni yako kumbe umepotea sana tena sana. Hivyo basi tambua kuwa malengo bora ni yale uliyojipangia mwenyewe.
Usipende kujidanganya kuwa fulani ananijali sana huwa anafanya hili na lile kwa ajili yangu, hivyo basi sina haja ya kufanya jambo hilo kwa kuwa kuna mtu yupo anafanya hilo kwa ajili yangu. Nikuulize kitu hivi unauhakika kuwa huyo anayekufanyia hayo mambo mnaendana kiakili, fikira,mtazamo, ubunifu?n.k. kama jibu ni hapana sasa kwanini unamwachia akufanyie. Acha Mara moja na fanya mwenyewe maana mnatofautiana kiufanisi, ubunifu, akili, uwajibikaji nk.
Ni muhimu utambue kuwa hata ukubwe ma matatizo kiasi gani mwenye nafasi ya kutatua matatizo yako ni wewe na sio mwingine. Una nafasi kubwa sana ya kujihusisha na matatizo na changamoto zinazokukabili tofauti na mtu mwingine yoyote. Hivyo basi wa kuwajibika na changamoto zako ni wewe sio mwingine. Daktari pekee hatoshi kukuponya ila uwepo wa daktari na imani yako ndio vitu vya kukuponya wewe hata kwa yale magonjwa yanayoonekana hayawezekani kutibika.
Tambua kuwa haukuja duniani ili ufanyiwe kitu Fulani. Bali ulikuja duniani ili ufanye jambo au mambo Fulani. Hivyo basi kuanzia leo tambua kuwa hakuna mwingine wa kukufanyia bali ni wewe mwenyewe.
Ni Mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.
Bmaganga22@gmail.com.
0754612413/0652612410.
Monday, November 23, 2015
Kitu Hiki Kimoja Kinatushinda Wengi Na Kuturudisha Nyuma.
Sunday, November 22, 2015
Ni Wao Sio Wewe, Ni Wewe Sio Wao
.
Kama wameshindwa ni wao sio wewe. Kushindwa kwa watu kusikufanye nawe ushindwe. Binadamu tumeubwa sawa haya ni maneno ya watu wengi lakini unaposema binadamu tumeubwa sawa ni neno pana kidogo maana huo usawa unaouzungumzia wewe ni katika mawanda yapi. Mfano leo hii ukisema binadamu ni sawa kiakili huoni kama unakosea, maana binadamu tunatofautiana sana tena sana ndio maana kuna warefu, wafupi, weupe, weusi, wenye ulemavu na wasio n.k. wale ambao wanaamini kuwa binadamu ni sawa ndio hutumia watu wengine kama marejeleo yao kwa kiasi kikubwa tena sana ndio maana wao huamini kuwa kama mtu fulani alishindwa basi nao watashindwa kwa kuwa binadamu wote ni sawa. Mara nyingi watu hawa huwa ni wenye mtazamo hasi kwa kuwa wao huamini kuwa binadamu ni sawa na inapotokea mtu fulani anataka kufanya jambo Fulani sawa na mtu au watu Fulani kwa kuwa wao wanamtazamo hasi basi hukimbilia haraka kwenye marejeleo ya watu walioshindwa na sio waliofanikiwa. Hii ni kutokana na mtazamo wao hasi.
Nimekueleza kuwa kauli ya kusema kwamba binadamu wote ni sawa ni kauli pana sana( it is a general term) maana inabidi ueleze huo usawa wako upo katika mawanda yapi? Nafikiri tuseme binadamu ni sawa kwa namna ya uumbaji wao na ukuaji mfano tunaweza kusema binadamu aliubwa na mwenyezi mungu kama vile washikadini wa dini zote tunavyoamini, pia binadamu wote ni sawa kwa kuwa wote huzaliwa na mwanamke hapo pana usawa, binadamu ni sawa katika makuzi yao maana wote huzaliwa na wakiwa hawana uwezo wa kuongea, huanza kutambaa, kutembea hatimaye kuongea. Huwa watoto, wakawa vijana, wakazeeka na hatimaye wakafa. Hivyo ni sawa kwa binadamu wote maana hakuna binadamu ambaye aliwahi kuwa mzee kisha akarudi ujana kisha utoto hapajawahi kutokea kitu kama hicho hapa duniani. Sasa unaposema binadamu wote ni sawa lazima utueleze usawa huo upo katika mawanda yapi?
Binadamu ni sawa katika mawanda ambayo nimekuonyesha hapo juu, lakini nini kimeniasukuma sasa mpaka nikuambie ni wao sio wewe na ni wewe sio wao, hapa namaanisha kuwa kama wameshindwa au walishindwa niwao na sio wewe na kama umeshindwa ni wewe sio wao. Nachotaka kusema hapa ndugu msomaji ni kuwa tambua kuwa binadamu tunatofautiana katika mawanda mbalimbali kama ilivyo katika kufanana, mawanda hayo ndio huleta utofauti miongoni mwetu na ndio maana nimesema ni wao sio wewe na ni wewe sio wao. Nakuletea mawanda hayo ili unielewe zaidi,
1. Utendaji, tunaweza kuwa tunafanya kazi sawa lakini utendaji wetu wa kazi ukawa tofauti kabisa ndio maana waalimu wawili mfano wanaofundisha somo moja wanaweza kutofautiana ambapo itatokea mmoja akaeleweka zaidi kuliko mwingine. Hii ni kutokana na utendaji wao kutofautiana hivyo kutokana na mawanda ya utendaji tunaweza kusema ni wao sio wewe na ni wewe sio wao. Yaani kama wameshindwa/wameweza ni wao, na kama umeshindwa/umeweza au kufanikiwa ni wewe sio wao.
2. Uwajibikaji, binadamu tunatofautia kiuwajibikaji hivyo uwajibikaji wa mtu mmoja na mwingine ni tofauti sana kutokana na utofauti huu wa kiuwajibikaji utakutana na makundi matatu ya watu ambapo la kwanza ni wanawowajibika sana, pili wanawowajibika wastani na tatu na mwisho ni wale wenye uwajibikaji mbovu. Hivyo ndivyo tunavyotofautiana kiuwajibikaji.
3. Fikira, binadamu tunatofautiana kifikira sana tena sana, kuna wengine wana fikira potovu na wengie hawana fikira potofu hivyo kama wanafikira potovu/sahihi ni wao sio wewe na kama unafikira potovu/sahihi ni wewe sio wao.
4. Mtazamo,binadamu tunatofautiana kimtazamo tena kwa kiasi kikubwa sana. Kuna wale wenye mtazamo hasi na wale wenye mtazamo chanya tofauti hizi za kimtazamo huamua tofauti za matendo yetu. Yaani mtu mwenye mtazamo hasi huwa na matendo yenye kuendana na mtazamo wake na yule mwenye mtazamo chanya pia huwa na mtazamo wenye kuendana na mtazamo wake. Hivyo kama wanamtazamo hasi/chanya ni wao sio wewe na kama unamtazamo hasi/chanya ni wewe sio wao.
5. Kiwango cha uvumilivu, hapa pia tunatofautiana sana. Tunaweza kuugawa uvumilivu wa binadamu katika makundi makuu matatu ambapo tutapata uvumilivu mkubwa, wastani na mdogo. Kila aina ya uvumilivu una watu wake hivyo basi kama upo kwenye aina Fulani ni wewe na sio wao na kama yupo kwenye aina Fulani ya uvumilivu ni yeye sio wewe.
6. Umakini, binadamu tunatofautiana katika kiwango cha umakini ambapo wengine ni makini sana na wengine sio makini sana. Ndio maana utawasikia watu wakisema yule jamaa ni mtu makini katika utendaji kazi wake wakati utasikia mwingine akisema yule jamaa hayupo makini kabisa katika utendaji kazi wake.
Sikuandika makala hii ili kukutofautishia tabia za binadamu bali nimeandika makala hii ili kukufungua na kubwa zaidi kukusihi uache kutumia watu kama marejeleo tena watu walioshindwa badala yake jijengee mazoea ya kujiamini na amini kuwa binadamu tunatofautiana sana hivyo basi kama umeshindwa ni wewe na kama wameshindwa ni wao. Pia wewe ulieshindwa usitake kujitumia kama mfano na uwafanye watu waamini kuwa watashindwa kama wewe. Kumbuka ni wao sio wewe na ni wewe sio wao. Zaidi usiruhusu historia ya mtu ikukatishe tamaa maana sio yako ni yake.
Ni Mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.
Bmaganga22@gmail.com.
0754612413/0652612410.
Tuesday, November 17, 2015
Je Waijua Picha Unayojijengea Akilini Mwako?
Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa mtandao ambao upo ili kuhakikisha kuwa unapata mambo mazuri ya kukujenga na kukuhamasisha. Leo nataka kukushirikisha jambo lifuatalo:-
Kwa kawaida binadamu amekuwa ni mtu wa kufikiria mambo mengi juu ya maisha yake. Kutokana na fikira hizo hapo ndipo binadamu huwa anajijengea picha mbalimbali juu ya maisha yake. Picha hizi huendana na fikira za mwanadamu kwa kiasi kikubwa sana. Yaani kama mtu anawaza fikira hasi na kuyaona maisha kwa mtazamo hasi basi picha zote atakazojijengea akilini mwake zitakuwa ni picha hasi ambazo zimejaa kushindwa, visingizio, woga na vipingamizi kadha wa kadha. Wakati kama mtu anawaza fikira chanya atakuwa na mtazamo chanya na hivyo atajijengea picha za ushindi, na mafanikio kwa kila anachokifanya n.k.
Je picha hasi zinatoka wapi?
Picha hasi hutokana na fikira hasi ambazo chanzo chake kikubwa chaweza kuwa kauli za wazazi wetu, ndugu wa jirani au marafiki wa karibu nasi. Mara nyingi watu wanaotuzunguka huwa wana madhara makubwa sana kwetu, madhara haya yaweza kuwa hasi kama nao ni hasi au chanya kama wao wanakauli chanya. Mara nyingi tumekuwa ni watu wa kuamini sana kwa yale ambayo tumekuwa tukiambiwa na watu wa karibu nasi jambo ambalo muda mwingine huweza kutuletea madhara makubwa sana. Katika hali ya kawaida mtoto ambaye amekuwa katika hali ya kusemwa kuwa huna akili, wewe ni mbumbumbu, huwezi lolote pindi anapokuwa amekuwa mtu mzima huwa anachukulia kauli hizi kama ukweli wa maisha yake halisi na hivyo kujijengea picha hasi kichwani mwake ambazo humfanya ajione hawezi lolote na nimbumbumbu haswa.
Ndugu msomaji ni muhimu uelewe vizuri aina ya picha ambazo unajijengea. Kwa kuwa wote tunahitaji mafanikio makubwa maishani basi tusiende kinyume na kanuni za mafanikio kama kanuni hii rahisi ambayo inaseama huwezi kujijengea picha hasi na ukapata matokeo chanya au picha chanya na ukapata matokeo hasi. Yaani ni sawa na mkulima alimaye mtama hutegemea kuvuna mtama na sio ulezi. Kama akipanda mtama akitegemea kupata ulezi basi mkulima huyu atakuwa na matatizo makubwa.
Kimsingi kama unataka kuendelea na kupata mafanikio makubwa jijengee picha chanya ili zikuletee matokeo chanya lakini kumbuka picha chanya inatokana na fikira chanya. Na picha chanya ni ile hali ya kujitabilia au kujionea maisha yako katika hali yakushinda wakati picha hasi ni ile Hali ya kujionea maisha katika kushindwa.
Ni mimi rafiki yako.
Baraka Maganga.
Bmaganga22@gmail.com.
0754612413/0652612410.




