Thursday, January 21, 2016

Furahia Vitu Hivi Wala Usilaumu Sana Juu Yake.

Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea kupambana kwa hali na mali ili tu uweze kufanikisha yale ambayo umekuwa ukiyahangaikia mara kwa mara. Vizuri endelea kupambana naama hakuna kitu cha bure hapa duniani, maana hata miujiza huja kwa wale ambao huwa wanakuwa wakiitafuta miujiza hiyo. Sio waliokaa tu wakisubiri miujiza hivyo nakusihii endelea kupambana ndugu msomaji wa mtandao huu.






Ukiwa bado unaendelea kupambana katika harakati zako basi jifunze kufurahia mateso,matatizo na vipingamizi mbalimbali uvipatavyo kwa sasa. Kwanini nasema jifunze kuyafurahia mateso, matatizo na vipingamizi vya sasa?. Sababu ninazo kupa hapa basi zinaweza kuwa muhimu kwako kuweza kukufanya uyafurahie mateso, matatizo na vipingamizi kadha wa kadha.
1.    Vinakufunza,ni kweli kuwa watu tulishawahi kupita, tunapitia na pengine tunaweza kuja kupitia katika mateso, matatizo na vipingamizi vya aina mbalimbali. Kama ulishawahi kupita katika mateso, vipingamizi au matatizo fulani basi utakubaliana nami kuwa vitu hivi huwa vinafunza. Jiulize swali hili huwa unajisikiaje pindi unapokuwa unapitia katika matatizo?, au pindi unapopitia vipingamizi fulani?, kama huwa unachukulia vitu hivi kwa hasira alafu unaanza kulalamika basi tambua kuwa una mtazamo hasi, na hivyo inabidi ubadili mtazamo huu na ujenge mtazamo wa kuyaangalia mateso, matatizo na vipingamizi vyako kwa hasira kisha acha kulaumu na baadae jiulize umejifunza nini kutokana na mambo hayo?. Huwa unajifunza nini pindi unapopingwa na wenzio je? unajawa na hasira na kuishia kulaumu au huwa unapatwa na hasira na unajifunza kuwa unapaswa kubadilika pengine unapingwa kutokana na kutokuwa bora katika jambo fulani, hivyo jifunze kutokana na kupingwa na ukajiboreshe zaidi na zaidi. Mateso unayoyaona leo yageuze kuwa kama somo. Matatizo pia yawe somo mfano unapokuwa na tatizo la pesa unajisikiaje?, unakubali hali au unajifunza na kulitatua tatizo hilo.

2.    Vinakuimalisha, matatizo, vipingamizi na matatizo, muda mwingine huwa kama viimalisho vyetu. Mfano matatizo yako yapo ili kukufanya uwe bora zaidi na zaidi. Mfano unapopata pingamizi kutoka sehemu mbalimbali kama vile unapopingwa kutokana na kigezo cha ukosefu wa elimu katika sehemu fulani ni muda wa kwenda kujiimalisha sasa ili uwe bora zaidi na usije ukapigwa tena na tena. Mateso muda mwingine usiyachukulie kama yapo kwa ajili ya kukutesa bali yapo kwa ajili ya kukuimalisha zaidi katika Nyanja mbalimbali za maisha.

3.    Vinakuamsha katika usingizi mzito, mateso, vipingamizi na matatizo yapo ili  kukuamsha katika usingizi mzito ambao umelala. Mfano halisi ni kuwa sisi binadamu huwa tunakumbwa na hali ya kujisahau pindi tunapojikuta kuwa tumefanikiwa kwa kiasi fulani na hapo ndipo wakati mwingine vipingamizi huja kwa ajili ya kutuamsha kutoka katika usingizi mzito ambao huwa tunakuwa tumelala pengine ni kutokana na baadhi ya mafanikio ambayo tunakuwa tumelala kwa muda. Binadamu huwa tunakuwa na hali ya kujisahau sana pindi tunapokuwa tumeona kuwa hali kwetu ni nzuri na hapo huwa tunajisahau sasa kwa wakati huu ndio huwa ni muhimu sana tena sana kuweza kuamshwa kutoka katika usingizi huu tulio lala. Matatizo mengi huja kwetu ili kutuamsha kutoka katika usingizi mzito tuliokuwa tumelala na hivyo kuweza kutuamsha. Mfano kama mfanyabiashara ukiwa umezoea kupeleka biadhaa zako mahali Fulani kwa wateja wako, kutokana na kufanya biashara kwa mazoea maana unafanya tu hutaki kuboresha bidhaa zako siku bidhaa yako ikipingwa na wateja wako, utakuwa umeamshwa sana. Pengine unateswa kwa kuwa umelala sasa inatakiwa uamke ili usiendelee kuteseka kama ukiendelea kulala maana yake utaendelea kuteseka.

Hivyo basi furahia mateso, matatizo na vipingamizi kwa maana ndani yake vimebeba mafunzo zaidi na zaidi.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com



Wednesday, January 20, 2016

Lazima Kitu Hiki Kiendelee Kuwepo Duniani, Na Ni Muhimu Kiwepo.

.Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea kupambana kwa hali na mali ili tu uweze kufanikisha yale ambayo umekuwa ukiyahangaikia mara kwa mara. Vizuri endelea kupambana naama hakuna kitu cha bure hapa duniani, maana hata miujiza huja kwa wale ambao huwa wanakuwa wakiitafuta miujiza hiyo. Sio waliokaa tu wakisubiri miujiza hivyo nakusihii endelea kupambana ndugu msomaji wa mtandao huu.



Ikiwa unapambana katika kuhakikisha unasonga mbele na wala sio kurudi nyuma basi ni vyema ukaelewa kuwa kitu hiki kimoja kisikutishe sana maana ni lazima kiendelee kuwepo hapa duniani, yaani usikihofie kitu hiki kwa maana ni cha muhimu sana tena sana. Kitu chenyewe ni tofauti zilizopo baina yetu sisi wanadamu. Ni wazi na ukweli usio pingika kuwa binadamu tunatofautiana sana tena sana na kwa kiasi kikubwa, kama ulikuwa hujui kuwa binadamu tunatofautiana basi anza kuelewa kwanzia sasa kuwa binadamu tunatofautiana na tofauti hizi zipo baina yetu na zinajionesha wazi wazi miongoni mwetu. Ngoja nikuwekeee mifano kadhaa ili uwezo kuelewa ni namna gani binadamu tunatofautiana tena kwa makundi tofauti tofauti.
Mfano katika maisha ya kawaida utofauti wetu unaweza kujionesha kutokana na  shughuli au kazi zetu, ndio maana katika maisha tuna madaktari, tuna manesi, tuna waalimu, tuna wafanyabiashara, tuna madereva, tuna wasio waajiriwa, tuna wawekezaji pamoja na wajasiliamali n.k. bado katika makundi hayo hayo  yanatofauti pia mfano katika kundi la madaktari tuna madaktari bingwa wa macho na wale bingwa kwa magonjwa ya watoto, katika waalimu tuna waalimu wakuu na waalimu wasio na cheo au kitengo chochote, katika kundi la madereva tuna madereva wa mabasi ya mikoani, daladala na madereva wa malori. Huu ni ufafanuzi kidogo ambao unaonesha  jinsi gani binadamu tunatofautiana sana tena sana.
Sasa utofauti huu usikutishe maaana haupo ili ukutishe bali upo ili kukupa changamoto na fursa wewe ili upate kuelewa ni wapi ambapo panakufaa haswa. Utofauti huu upo ili kukufanya wewe ufanye uchaguzi sahihi ni kundi gani linakufaa haswa na ni wapi unapataka. Hivyo basi badala ya kutishika na utofauti huu wewe chukulia utofauti huu kama fursa ya wapi panakufaa. Usitishike wala kuogopa unapoona mtu fulani kawa mfanyabiashara maarufu, fulani kawa daktari bingwa, kawa mchezaji bora, kawa mwamasheria n.k bali chukulia kama fursa ya wewe kuchagua ni wapi haswa panapokufaa na upange ni jinsi gani haswa utaweza kufika pale.
Pia ni muhimu ukatambua kuwa utofauti huu wa kimaisha unaweza kukusaidia wewe kufanya mambo fulani fulani, mfano utofauti unaweza kupelekea yafuatayo kwako:-
1)    Utofauti huu ndio hutukumbusha ya kuwa tunapaswa kuwajibika, kupitia tofauti zilizopo au zinazojitokeza kati yetu ndizo huwa kichocheo cha sisi kupambana ili kuhakikisha kuwa tunasonga mbele au kupata molari ya kujikwamua katika hali ambazo tunazo. Hebu chukulia mfano ni hali gani huwa unakuwa nayo pindi unapokutana na rafiki yako ambaye mnaendana kwa baadhi ya vitu kama vile umri, elimu, historia ya kimalezi na zaidi mlisoma na kucheza pamoja lakini  baada ya kuacha nae kwa muda anarudi akiwa na mafanikio makubwa sana kuliko wewe, tayari mmeshatofautiana japo mlikua na kusoma pamoja, sasa baada ya kuyaona mafanikio ya huyo rafiki yako, ni nini unachopata kwa mara ya kwanza?. Nadhani ni hisia za kuwajibika ili uweze kuwa kama rafiki yako.

2)    Hutufanya tuzichukie hali fulani, kupitia utofauti tulionao basi hutufanya tuzichukie baadhi ya hali zetu. Mfano pindi unapowaona wenzio wakifanikiwa ili hali wewe unabaki kuwa masikini wa kutupwa basi hapa ndipo huwa unapata hasira na kuanza kuuchukia umasikini lakini kiuhakika ni kuwa usingeweza kupata hasira ya kuichukia hali hii ya umasikini. Lakini sababu ya kukufanya uanze kuuchukia umasikini ni baada tu ya kuona tofauti iliyopo kati yako na wengine.


3)    Hutufanya tujifunze zaidi,tofauti zilizopo baina yetu na wengine wakati mwingine huwa kama somo kwetu maana tofauti hizi hutufanya tuanze kujihoji sana ni kwanini wengine wako hivi na sisi tuko hivi. Mfano leo hii unapata wazo gani unapowaona watu waliofanikiwa mbele yako, sina shaka kuwa itakuwa uwa unapata hamu ya kujifunza zaidi kutoka kwa watu hao.

Ni muhimu tofauti ziendelee kuwepo miongoni mwetu ili tuweze kuchagua ni wapi panatufaa, ili tuweze kubadilishana huduma maana  wote tukiwa wafanyabiashara nani atakuwa mnunuzi tena isitoshe wote tukiwa tunauza bidhaa sawa, ingekuwaje kama wote tungekuwa madereva na kila mtu, angelikuwa na gari lake, bila shaka kusingekuwepo abiri kwa sababu hizo na nyingine nyingi ni dhahiri kuwa tofauti ni lazima ziendelee kuwepo miongoni mwetu.


Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com


Tuesday, January 19, 2016

Chagua Timu Sahihi Ya Kushirikiana Nayo.


Habari ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa, ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri katika kuhakikisha kuwa unashughulikia ipasavyo yale unayo yahangaikia ili tu kujiletea mafanikio ambayo ndio kila mtu anayoyahangaikia. Nami nikusihi kwa moyo mmoja kuwa endelea kupambana mpaka uyatimize yale unayoyaamini kama mafanikio kwako. Pambana pambana bila kuchoka na mafanikio utayaona tu.





Katika maisha yetu sisi  wanadamu tumekuwa tukijikuta tunaunda timu ya watu ambao tunakuwa tunashirikiana nao mara kwa mara. Najua kila mtu atakuwa na timu ya kushirikiana nayo yaani una watu wako wa karibu ambao mara kwa mara umekuwa ukishirikiana nao kufanya nao mambo mbalimbali. Hili ni jambo ambalo kila binadamu huwa analifanya kila siku na kila wakati. Sina shida na hilo ila shida iliyopo ni aina ya watu ambao tunashirikiana nao.

 Je tunawafahamu ipasavyo hawa watu ambao tumekuwa tukishirikiana nao mara kwa mara katika mambo yetu yawe ya muhimu na yale yasiyo ya muhimu. Kama unataka kufanikiwa maishani hakikisha kuwa unashirikiana na watu ambao ni sahihi na munaendana nao, sisemi  kuwa lazima muwe mnaendana kielimu, kiumri, urefu na rangi za mwili lakini jambo la msingi ni kule kuendana kimtazamo na mawazo.

Mafanikio yanahusisha sana fikira yaaani fikira zako ndizo hukuletea mafanikio au kuto kukuletea mafanikio. Mwenendo wa fikira zako ndio ambao huamua wewe uwe wapi. Ndio maana kama unataka kuwa mwenye mafanikio basi hakikisha kuwa unazichunguza kwa kiwango kikubwa sana fikira zako. Na kama unataka kutoka kule uliko kwenda mbele zaidi yaani kwenye mafanikio  basi hakikisha kuwa una badili fikira zako kama ulikuwa na fikira mbovu kuhusu maisha, mafanikio, utajiri na umiliki mali basi anza kuzibadili na ukishazibadili nenda mbali zaidi kwa kutafuta timu sahihi ya kushirikiana nayo.

 Ni muhimu ukatambua kuwa ndugu msomaji mafanikio huendana sana na watu ambao unashirikiana nao. Wazungu wana msemo usemao kuwa “birds of feather floks tugeza” kwa tafsiri sisi tunaweza sema ndege wenye mabawa hutembea pamoja. Msemo huu unamaana sana na kama kweli unataka kufanikiwa basi hakikisha kuwa msemo huu unakukaa kichwani na haukutoki kamwe, yaani ufanye msemo huu kama kichochea chako cha kuelekea mafanikio.

Msemo huu unauhalisia mkubwa sana maishani hebu yachunguze makundi mbalimbali ya watu hata hapo mtaani kwako na kwingineko, waangalie watu ambao huwa wanashirikiana je wanaendana au huwa hawaendani?, waangalie walevi au watu wanaokunywa pombe huwa wanakuwa wanafahamiana na huwa hata wana namna yao ya kuwasiliana na wewe ambaye sio mlevi unaweza ukapata shida kuwaelewa hii ni kutokana na lugha yao, waangalie vijana wa kijiweni, waangalie walokole, waangalie watu wanaopenda michezo n.k.

Leo hii ni ngumiu kumkuta mlokole aliekomaa kijiweni akishirikiana na vijana hao wa kijiweni, au ni vigumu sana kumkuta mlevi amekaa na mtu ambayehatumii pombe wala kilevi cha aina yoyote ile. Sasa unajua kwanini watu hawa huwa wanachagua watu wanao endana nao, ni kwasababu wanajua kupitia watu hao watapata mawazo na fikira zenye kuendana nao. Yaani watakuwa wakibadilishana mawazo yao juu ya yale ambayo wanayafanya.

Sasa kwa kupitia mifano ya watu hawa ambao nimekuwekea hapo juu basi nawe unaetaka kufanikiwa hakikisha unajipatia timu sahihi ya kushirikiana nayo, timu hii itakuwa chachu ya mafanikio yako, maana utapata mawazo mbalimbali, utapata changamoto mbalimnbali ambazo zitakufanya uwe bora zaidi na zaidi na uweze kusonga mbele.
Kama kweli unataka kufanikiwa hakikisha unakuwa na fikira chanya na fikira chanya ndio utazipata kutokana na watu ambao unashirikiana nao. Watu wapo tu shida ni kuwa wewe ukoje kama unamtazamo chanya basi utafanya mambo chanya na utapata watu wenye fikira chanya hivyo ni wewe tu na sio kuwa huwezi kupata watu, watu wapo tu.

Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com



Friday, January 15, 2016

Huwezi Kufanikiwa Kama Utashindwa Kuepuka Jambo Hili.

Habari za wakati huu ndugu mpendwa msomaji wa makala za mtandao huu wa kona ya maarifa, ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vizuri katika kuhakikisha kuwa unayatekeleza yale ambayo umepanga kuyatekeleza. Vizuri endelea kupigana mpaka yale unayoyataka yamekamilika.





Wakati unaendelea kupambana, ili kuhakikisha kuwa unayatekeleza yale unayoyataka basi nakusihii epuka kitu hiki kimoja kama kweli unataka kufanikiwa katika maisha yako.jambo lenyewe ni kukosa ubunifu. Nimeamua kukuandikia hili ndugu msomaji ili uweze kuelewa madhara ya jambo hili. Na hili nimeamua kuliandika kutokana na ongezeko la tabia hii miongoni mwa watu wengi, na watanzania tukiwa ndio tunao ongoza kwa tabia hii ambayo kwangu naiona kama tabia isiyofaa kabisa kuigwa wala kufuatwa na jamii.


Tabia yenyewe ni ya kukosa ubunifu miongoni mwetu. Ukitazama shughuli nyingi sana za watanzania ni shughuli ambazo zimwekosa ubunifu, kabisa angalia sanaa zetu, biashara n.k, ni shughuli chache sana zenye kubeba ubunifu ndani yake. Watu siku hizi hawaangaiki kubuni kitu chochote badala yake wamekuwa ni watu wa kuhamisha mambo kama yalivyo kutoka walikoyatoa na kuyaleta kwetu,(coping and pasting), na kwa kuwa watu pia ubunifu umewapiga chenga basi nao huwa wanakubali kuamini mambo hayo hata kama wanajua hayaendani na sisi. Kutokana na ukosefu wa ubunifu ndio maana leo hii kumekuwa na tabia kubwa sana ya mambo ya kuigana igana tu na matokeo yake hakuna jipya linalo fanyika bali ni yale yale.


Ikiwa unataka kufanikiwa katika dunia ya leo basi hakikisha kuwa unakuwa mbunifu. Dunia ya leo imejaa ushindani wa hali ya juu, hii ikimaanisha kuwa kwa kila unalolifanya unaweza usiwe peke yako badala yake mtakuwa wengi. Sasa kama ikitokea mmekuwa wengi basi jambo la msingi la wewe kufanya ni kutafuta namna ya pekee ya kuweza kulifanya jambo lile ambalo litakutofautisha wewe na wengine. Kama ukishindwa kufanya hivyo basi tambua kuwa hautopata mafanikio makubwa katika yale unayoyafanya.


Chukulia mfano wa wachezaji Ronaldo na Messi, unajua ni kwa nini wanakuwa wachezaji bora wao tu kuliko wengine?, je wao ndio wachezaji pekee duniani kwamba hakuna wenzao. Ukiwaangalia wao kama wao hawana tofauti na wachezaji wengine maana wao wana miguu miwili kama wenzao wapo watu duniani ambao wanacheza namba kama zao lakini nini kinachofanya wao wafanikiwae kuliko wenzao, hakuna kingine bali ni ubunifu ambao wanao. Ubunifu wao ndio unawatofautisha wao na wenzao na kuwafanya waonekane bora kuliko wao. Wote wanafunga magoli, wanapiga chenga na bwebwe zingine zote unazozijua katika mpira lakini nini kinawatofautisha na wengine? Ni ubunifu walio nao ndio maana unakuta wanamagoli mengi kuliko wenzao. Wamebuni mbinu tofauti za kucheza mpira ambazo wenzao hawana muda wa kuzibuni ndio maana wanakuwa bora.


Tukirudi katika biashara za hapa kwetu Tanzania, ni biashara bora kwa kiasi chake lakini ni biashara ambazo zimejaa maswala ya kuigana tu hakuna jipya. Leo hii kumezuka maswala ya biashara za mtandao sasa kila mtu anataka afanye, achilia mbali maswala hayo, kutokana na maendeleo ya watu kutumia mitandao ya kijamiii watu wamekuwa na uwezo wa kutangaza biashara zao katika mitandao hiyo, lakini angalia namna ya utangazaji wao, kila mtu anapiga picha ya bidhaa na kuipost kisha ataandika tu kwa anae hitaji mawasiliano haya hapa, anatoa namba yake pale. Kama  sio hivyo utasikia, jipatie laba kali, tisheti n.k tunakuletea ulipo. Sasa biashara hizi sio kuwa nazipinga au kuwacheka wanaozifanya lakini nalo hoji ni kuwa ni lazima wote tuandike matangazo sawa hakuna anaeweza kubuni namna nyingine ambayo itamtofautisha na mwingine.


Angalia leo kuna makundi kibao katika mitandao mbalimbali makundi haya huanza kwa namna nzuri sana lakini kutokana na kuwa wote tumeathiriwa na namna moja ya kufikiri na hivyo tukakosa ubunifu, utakuta mtu kaanzisha kundi kaliita jina la kibiashara kabisa lakini ukiingia kwenye kundi hilo unakutana na stori za mapenzi, kwa kuwa ameona kuwa stori hizo ndizo zinazopendwa na kufuatiliwa na kuwapatia watu wengi sana umaarufu mkubwa. Angalia leo hii ni makundi mangapi yanazungumzia mapenzi, hakika yatakuwa mengi sana na yote yanaandika kitu kile kile hii inaonyesha kuwa hatuna ubunifu wa kutuwezesha watu  kuweza kufanya kitu cha tofauti.


Kimsingi ni vyema ukatambua kuwa katika dunia ya sasa, yenye kujaa ushindani wa hali ya juu huitaji kufanya kitu cha tofauti sana ila unatakiwa ufanye kitu kwa utofauti na hiyo ndio tabia ya watu walio fanikiwa. Sio kuwa wanafanya vitu tofauti bali wanafanya vitu kwa utofauti, na utofauti huo ndio ujulikanao kama ubunifu.  Na ndio huwafanya waonekane watu wa tofauti sana duniani.


Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com.


Wednesday, January 13, 2016

Ifahamu Njia Ya Kutumia Ili Kupanga Shughuli Zako Katika Vipaumbele.

Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendelea vizuri katika kuyatekeleza majukumu yako ya kila siku. Nami nasema vizuri endelea kupambana mpaka uyatekeleze yale uliyokwisha kujiwekea.
Wakati unaendelea kupambana ili kuhakikisha kuwa unafanikiwa, wapo watu ambao wanahisi kuwa wanashughuli nyingi sana na hawajui ni ipi shughuli waanze nayo. Ikiwa unaona au kuhisi kuwa unashughuli nyingi sana na haujui ni ipi sahihi kuanza nayo basi hapa nakuletea njia sahihi ya kutumia ili uweze kujua ni shughuli ipi ya kuanza nayo, njia yenyewe inaitwa ABCDE. Hii ndiyo njia yetu ya kuweza kukusaidia kupanga shughuli zako. Ntaifafanua njia hii kama ifuatavyo:-,





Shughuli A- shughuli ya kuwa katika kundi hili inapaswa kuwa shughuli ya muhimu sana, hapa kinapaswa kuwa kitu cha muhimu sana ambacho ni lazima ukifanye au kifanyike. Shughuli ambayo inapaswa kuwa na jina la A ni lazima utambue kuwa ni shughulia ambayo isipofanyika basi ina madhara makubwa sana. Mfano wewe ni mfanyabiashara na unaitegemea biashara husika katika kuendesha maisha yako basi hiyo shughuli ndio inapaswa kuwa hapo, maana kwanza ni muhimu, lazima ufanye ili uishi na mwisho ukiacha kufanya basi madhara yapo.
Shughuli B- hii ni shughuli ambayo inatakiwa uifanye, shughuli ambayo inatakiwa iwepo hapa ni ile ambayo pia isipofanyika ina madhara lakini sio muhimu sana kama ilivyo katika shughuli A. mfano kama umeamua kuanzisha program ya kufanya mazoezi kila siku asubuhi kabla ya kuelekea katika shughuli zako ni muhimu ukafanya hivyo ingawa kuto kufanya kuna madhara ya kuwa afya yako itadhoofika lakini sio muhimu sana maana wapo ambao hawafanyi zoezi na afya zao ni nzuri tu.
Shughuli C- katika kundi hili linapaswa kuwa na shughuli ambayo ni vizuri ifanyike lakini haina madhara yoyote. Mfano kuamua kwenda kuwatembelea ndugu mahali fulani kama vile dada, kaka, shangazi, bibi au babu, ukitazama vizuri swala la kwenda kuwatembelea ndugu mara kwa mara ni vizuri lakini hakuna madhara yoyote makubwa. Au shughuli nyingine ni kama vile kwa mfanyakazi ambae anataka kwenda kunywa chai au kula chakula pahali fulani na wafanyakazi wenzake, ni vizuri kufanya hivyo lakini kuto fanya hivyo hakuna madhara makubwa. Au kwa yule aliyeoa ni vizuri kupiga simu kuulizia leo mkeo kapika nini lakini hakuna madhara yoyote usipo fanya hivyo. Hivyo basi shughuli zote zenye kufanana na hizo zinapaswa kuwa hapa katika kundi hili.
Shughuli D- hapa pana husisha shughuli yoyote ile ambayo unaweza kumwachia mtu aifanye.  Ni muhimu utambue kuwa yakupasa uyaache yale ambayo yanaweza kufanywa na mtu fulani ili ayafanye yeye badala yako. Hii itasaidia nini haswa?, hii itakusaidia wewe kuokoa muda ambao ungeupoteza kufanya jambo ambalo linaweza kufanywa na mtu mwingine. Mfano mama mwenye binti zake wakubwa nyumbani anapaswa kuwaachia shughuli kama vile za usafi wa nyumba na yeye akawahi katika shughuli zake kama vile biashara zake.
Shughuli E- hapa ni shughuli ambazo unaweza kuamua kutokuzifanya kabisa. Hizi ni shughuli ambazo unaweza kuamua kuzifanya au kutokuzifanya na hazina madhara yoyote. Mfano shughuli ya kujibu kila jumbe au  kila unachokiona katika makundi ya whatsapp.
Mara nyingi sana watu huwa tunakabiliwa na changamoto pale ambapo tunapaswa kufanya jambo fulani, hii ni kutokana na kuwa na shughuli nyingi sana ambazo tunaamini kuwa zote ni za muhimu, utakuta mtu anataka kwenda kwenye biashara, mara kufanya zoezi, mara kwenda kumtembelea shangazi n.k. huyu ni mtu mmoja ambae anataka kuyafanya yote haya na hajui aanze na lipi. Kama unakubwa na shida hizo basi dawa ndiyo hiyo nimekupatia.  

Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com