Monday, January 11, 2016

Zifahamu Kauli Kumi (10) Unazozitumia Na Zinakufanya Usifanikiwe.

Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa umeshaianza siku yako vema na unaendelea kupambana ili kuhakikisha kuwa siku yako ya leo mpaka inaisha unakuwa umejisogeza vya kutosha katika kuyatekeleza malengo yako. Nami nakusihi usichoke maana mafanikio yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu hata kama mambo hayajaenda sawa wewe usijali endelea kupambana tu na mafanikio utayaona.
Leo kuna jambo nataka kukushirikisha ndugu msomaji wa mtandao huu, tumekuwa tukiamini kuwa maneno huumba, au wengine husema kauli huumba tukiwa na maana kuwa kadri tujisemeshavyo wenyewe  juu ya maisha yetu ndivyo maisha yetu huwa. Sasa kutokana na hili ndio maana nimekuletea kauli kumi ambazo watu wamekuwa wakizitumia na zimekuwa zikiwafelisha na kuwaweka mbali na mafanikio kauli hizo ni kama ifuatavyo:-,





Sikuzaliwa au kukulia katika familia bora, kuna watu ambao huamini na kuhararisha kutokufanikiwa kwao na kutozaliwa au kuto kukulia katika familia bora. Hizi ni kauli ambazo hazina maana yoyote katika dunia ya leo maaana mafanikio ni wewe na sio familia uliyokulia, na kama wewe unaona hilo ni sahihi ni wangapi kwani ambao wamefanikiwa japo kuwa hawajatoka familia bora?, acha mara moja kauli hizi badala yake anza kufikiria utafanyaje ili ufanikiwe ijapokuwa hujatoka familia bora hilo ndilo jambo la msingi.

2.    Sikuzaliwa upande sahihi, hawa ni waleambao huona kuwa kutokana na wao kuzaliwa bara fulani, au nchi fulani ni mkosi kwao, maana huamini kuwa bara au nchi husika waliyomo haiwaruhusu kufanikiwa. Ni kauli za kijinga na ambazo hutumiwa na watu ambao hawajafanikiwa ndio husema bora kuzaliwa mbwa ulaya kuliko mtu afrika, hizi ni kauli za ajabu sana, kwani ni waafrika wangapi wapo afrika na wamefanikiwa, ni watanzania wangapi wanamafanikio hapa hapa Tanzania, ni wakenya, waganda n.k wangapi wenye mafanikio ndani ya nchi zao?. Acha kauli zisizo za msingi.

3.    Sina elimu ya kutosha, hii ilikuwa na umuhimu enzi zile za zama za kati za mawe lakini sio katika dunia ya sasa ya taarifa. Nani aliyekuambia mafanikio ni kutokana na elimu yako tu?, wangapi wanamafanikio makubwa na hawana hata digrii, masters, wala hizo phd ambazo wewe unaamini lazima uwe nazo ndizo zitakufanya ufanikiwe. Chukulia mfano wa mafanikio ya msanii Diamond na msakata kabumbu  Mbwana Samatta, je wanaelimu kiasi gani?. Jibu baki nalo.


4.    Hayo ni mambo yako sio yangu, kauli kama hizi ndizo huwafanya watu wakose fursa. Utamkuta mtu analetewa wazo la kibiashara ambalo tayari ni fursa kwake lakini utamsikia aa bwana ee hayo ni mambo yako sio yangu. Sasa endelea hivyo hivyo na utaendelea kukosa fursa siku hadi siku.

5.    Sina muda wa kutosha, wewe kila siku muda haukutoshi, wewe ni nani na unafanya nini mpaka muda usikutoshe kila siku?, je unataka upatiwe masaa 70 ndani ya siku moja? Kwanini wewe tu ndio muda haukutoshi? Mbona wengine masaa 24 yanamtosha. Jifunze kutumia muda ulopewa vizuri.


6.    Sina pesa za kutosha, unafikiri pesa inatosha kwa kukaa nayo tu? Au kwa kuiweka tu ndani na kuishangaa au benki?,  acha kufikiri pesa itakuja kukutosha bila kuizungusha, jifunze kuizungusha hiyo pesa ndipo itakutosha.

7.    Sifahamiani na watu sahihi, ni kweli hufamiani na watu sahihi kutokana na matendo yako na ndio maana huwezi kuwapata watu sahihi wa kukusukuma uende mbele. Kama unataka kupata kushirikiana na watu sahihi anza kufanya mambo yanayoendana na hao watu ambao kwako ni sahihi.


8.    Sina mtandao wa watu, hauna mtandao wa watu wa kushirikiana nawe kutokana na wewe mwenyewe ulivyo. Mtandao wa watu wa kushirikiana nao unakuja kutokana na kile ambacho unakifanya na kutokana na ushirikiano wako na watu wengine. Unashirikiana na nani haswa na huyo unayeshirikiana nae je? anamtandao au?.

9.    Mke wangu hanisaidi, ni kweli mke wako hakusaidi lakini wewe kama wewe umechukua juhudi gani kuhakikisha kuwa wewe kama wewe unapigana vilivyo katika kuhakikisha kuwa unasimama wewe kama wewe?,  je mafanikio yako yanamtegemea mke wako tu?, kama asingalikuwepo ungalifanyaje?, acha kutegemea tegemea bila msingi badala yake  jifunze kusimama mwenyewe muda mwingine.


10. Nina watoto wengi wa kulea, kama ulijua kuwa watoto wengi wanakufanya usifanikiwe kwanini umekuwa nao?. Na je ni kweli kwamba bila kuwa na watoto wengi ungefanikiwa au ni visingizio?, je tukiwachukua hao watoto na tukakuacha mtupu utafanikiwa?

Kimsingi kauli hizi kumi kwa maneno mengine tunaweza kuziita kama visingizio ambavyo mtu huwa navyo, na hii ni hatari sana maana visingizio havikufanyi kuwa mwenye mafanikio bali vinazidi kukurudisha nyuma. Hivyo basi uamuzi ni wako kuendelea na visingizio na sababu sababu za kuto kufanikiwa kwako ambzao zitazidi kukufanya usiwe na mafanikio au uziache na kuwa mwenye mafanikio.

Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com



Saturday, January 9, 2016

Sababu Sita (6) Za Kwanini Watu Hawajiwekei Malengo.



Habari za leo ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni matumaini yangu kuwa hu mzima wa afya na unaendeleo kupambana vilivyo katika kuhakikisha kuwa unajiletea mafanikio makubwa maishani mwako. Nami nakusihi ndugu msomaji wa mtandao huu kuwa endelea kupambana, usichoke hata siku mpaka uhakikishe kuwa unajipatia mafanikio makubwa, ambayo umekwisha jiwekea.
Ukiwa unaendelea kujishighulisha na shughuli zako za kila siku basi leo nakuletea kitu kingine ambacho unapaswa ukifahamu vyema. Kama  kichwa cha makala kinavyosema kuwa sababu za kwanini watu huwa hawajiwekei malengp maishani. Tumekuwa tukisisitizana na kuambiana mara nyingi sana juu ya umuhimu wa kuweka malengo, lakini ukweli ni kwamba ni watu wachache sana kati ya wengi ambao wamekuwa na utamaduni wa kujiwekea malengo. Na walio wengi wamekuwa hawajiwekei malengo, sasa kwanini watu hawa huwa hawajiwekei malengo maishani, zifuatazo ni sababu za kwanini watu hawajiwekei malengo:-,




Hawako makini, sababu moja wapo ya kwanini watu hawajiwekei malengo ni kutokana na sababu kuwa hawapo makini maishani. Mtu makini na anayetaka kufanikiwa kwa hali na mali lazima ajiwekee malengo. Lakini kutokana na ukosefu wa umakini miongoni mwetu tumekuwa tukiishi hivyo hivyo bila malengo
.
2.    Hawajayakubali majukumu yao, kama mpaka sasa hujathubutu hata kujiwekea malengo basi tambua kuwa bado hujataka kuyavaa majukumu yako. Yaani watu ambao bado hawajajiwekea malengo ni wale ambao bado wanahisi kuwa yupo mtu fulani maishani ambae ndiye yupo kwa ajili ya kusubiri kufanyiwa kitu fulani jambo ambalo kiukweli ni kujidanganya. Hivyo basi ukosefu wa ile hali ya kuvaa majukumu ndio kimekuwa kikwazo cha watu kujiwekea malengo.

3.    Hawatambui umuhimu wa kujiwekea malengo, watu wamekuwa hawajiwekei malengo kwa sababu hawajui umuhimu wa kujiwekea malengo. Inaonekana kuwa miongoni mwa watu wengi sana hawana uelewa juu ya maswala haya ya kujiwekea malengo ndio maana wamekuwa hawajiwekei malengo maishani mwao. Watu hawaoni umuhimu wowote wa kujiwekea malengo ndio maana wamekuwa hawajiwekei, lakini naomba niseme kuwa hii ni kosa kubwa sana ambalo watu hulifanya, nasema hivyo kwa sababu ni vyema kila mtu akatambua umuhimu wa kuweza malengo na akijua umuhimu atakuwa amejikomboa kwa kiwango kikubwa.

4.    Hawajui ni vipi watapanga/ kuyaandika malengo yao, sababu nyingine ambayo inawafanya watu wasijiwekee malengo ni kutokana na ukweli kwamba hawajui ni vipi wajiwekee malengo. Hii nadhani ndio sababu namba moja ya kwanini watu hawajiwekei malengo maishani, yaani hawaweki malengo kwa sababu hawajui watafanyaje. Kama hujui mpaka leo basi jua kuwa upo katika hatari.
5.    Wanaogopa kukosolewa/ kukataliwa, uoga umekuwa ukichangia sana miongoni mwa watu, na imekuwa sababu inayofanya watu washindwe kujiwekea malengo, watu wamekuwa wakiogopa kujiwekea malengo kwa kuwa wanaogopa kuwa endapo wakimwonesha mtu malengo yake atakosolewa sana hivyo kutokana na woga huu basi unamfanya arudi nyuma na kukaa bila kuweka malengo.

6.    Wanaogopa kushindwa, watu wengi hawaweki malengo kwa kuwa wanaogopa kushindwa yaani anaogopa kuwa itakuwaje nikiweka malengo alafu nisiyatimize hivyo kutokana na kuogopa huko katika kushindwa basi anakaa tu na kutokujiwekea malengo.


Ikiwa unataka kufanikiwa zaidi na zaidi ni muhimu ukatambua kuwa malengo ni kitu muhimu sana tena sana, malengo ni dira katika maisha yako. Ikiwa hujajiwekea malengo basi nishakuwekea sababu sita za kwanini hujafanya hivyo. Kupitia sababu hizo unaweza ukaelewa ufanye nini ili kujiwekea malengo. Mfano umeshajua sababu moja wapo inayokufanya usijiwekee malengo ni kuwa hujayakubali majukumu, sasa nini cha kufanya ni kuyavaa majukumu kisha baada ya hapo utapata uwezo na uelewa wa ni vipi ujiwekee  malengo.


Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com


Friday, January 8, 2016

Mambo(7)Saba Muhimu Ya Kuepuka Ili Uweze Kufanikiwa.


Habari ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa, ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri katika kuhakikisha kuwa unashughulikia ipasavyo yale unayo yahangaikia ili tu kujiletea mafanikio ambayo ndio kila mtu anayoyahangaikia. Nami nikusihi kwa moyo mmoja kuwa endelea kupambana mpaka uyatimize yale unayoyaamini kama mafanikio kwako. Pambana pambana bila kuchoka na mafanikio utayaona tu.
Wakati unaendelea kupigana ili kuyasaka mafanikio yafuatayo ni mambo saba muhimu ambayo nataka uyaepuke kwa hali na mali kama kweli unataka kufanikiwa, ni muhimu ukayasoma mambo haya na kuyaweka akilini mwako ili yakusaidia katika safari yako ya kuelekea mafanikio, mambo hayo ni kama ifuatavyo:-


Epuka woga, ndugu mpendwa msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa ni muhimu ukatambua kuwa woga ni adui wa mafanikio, woga utakukwamisha sana tena sana hivyo basi kama kweli unataka kufanikiwa acha kabisa kujenga woga juu ya yale mambo ambayo unayataka au unataka kuyafanya. Njia moja wapo ya kuepuka woga juu ya kitu fulani ni kwa wewe kufanya kile unachokiogopa zaidi na zaidi. Fanya kile unachokiogopa na woga utaushinda kwa hakika.

2.    Epuka wivu, wivu hauwezi kukupeleka popote, na kwa mtu anaetaka kufanikiwa wivu hatakiwi kuwa nao, kama kweli unataka kufanikiwa achana na habari zile za sijui wivu wa maendeleo sijui nini. Kitu ambacho unatakiwa ukijue ndugu msomaji ni kuwa wivu ni wivu tu achana na habari ya wivu wa maendeleo. Wivu utakuzuia kujifunza kutoka kwa wale waliofanikiwa hivyo basi pingana na habari hizi za wivu na badala yake acha kuwaonea wivu waliofanikiwa na nenda kajifunze kwao.


3.    Epuka chuki, mtu mwenye chuki hatofautiani sana na mtu mwenye chuki. Acha kujenga chuki na watu, usitegemee kufanikiwa ikiwa una chuki moyoni mwako. Chuki juu ya wenzio itakukwamisha maana chuki haina msingi wowote bali ni tabia ambayo ni maalumu na mashuhuri kwa watu ambao hawaelewi ni nini haswa wanakitaka maishani. Hivyo basi kama wewe unataka kufanikiwa basi achana na habari hizi za chuki.

4.    Epuka kisasi, je umekumbwa au unakumbwa na hali ya kisasi yaani unajisikia kulipiza kitu fulani yaani kwamba ukiona mtu fulanii kakufanyia kitu fulani nawe unataka uje ulipize hivyo hivyo. Haimaanishi kuwa mtu akikutendea mambo mabaya basi nawe uweze kumlipizia mabaya hayo hayo. Usipoteze muda wako katika kufikiria juu ya ni vipi ulipize kisasi kwa mwenzio bali tumia muda wako mwingi kuwaza utafanya nini ili uweze kufanikiwa.


5.    Epuka tamaa, achana na habari ya tamaa, tamaa haina msingi wowote kwako kama kweli unataka kufanikiwa. Tamaa ni kitu kibaya sana na ambacho hakiwezi kukufanya usonge mbele, usipende kutamani tamani vitu ovyo badala yake jua jinsi ya kujizuia juu ya matamanio yako. Usiwe mtu wa tamaa ambaye unataka kuwa ma kila kitu badala yake kuwa na vitu vya msingi sio lazima uwe navyo vyote. Hivyo basi achana na habari za tamaa.

6.    Epuka hasira, ikiwa unataka kufanikiwa ni vyema ukatambua kuwa hasira ni kitu kibaya sana. Ni kweli kuwa kila mtu anahasira na viwango vya hasira vinatofautiana kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine. Nachotaka kukushauri ni kuwa jifunze kuzizuia hasira zako. Ikiwa unataka kufanikiwa jifunze kuanzia sasa kuweza kuzizuia hasira zako, hii itakusaidi wewe kuweza kufanya maamuzi yaliyo bora maana mara nyingi sana watu tumekuwa tukifanya maamuzi kutokana na hasira alafu baadae tunakuja kuanza kujuta, hii ni baada ya hasira yetu kuisha. Hivyo basi jifuze kuzizuia hasira zako.


7.    Epuka ushirikina, wapo watu ambao huamini kuwa mafanikio huja kwa kuwa mshirikina, naomba nikuambie kuwa haya ni mawazo ya kijinga na yasiyofaa katika ulimwengu wa sasa. Kama kweli unataka kufanikiwa acha kabisa kutegemea habari za ushirikina.

Hayo ni mambo saba muhimu ambayo inabidi uyaepuke ili uweze kufanikiwa. Epuka mambo haya kwa kuwa hayana msingi wowote na wala hayawezi kukufikisha popote. Hivyo ndugu msomaji pigana uwezavyo kuyaepuka mambo haya.


Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com


Wednesday, January 6, 2016

Mambo Nane (8) Muhimu Ya Kukusaidia Katika Kubadili Tabia Yako Na Kuwa Mwenye Mafanikio

.
Habari ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa, ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri katika kuhakikisha kuwa unashughulikia ipasavyo yale unayo yahangaikia ili tu kujiletea mafanikio ambayo ndio kila mtu anayoyahangaikia. Nami nikusihi kwa moyo mmoja kuwa endelea kupambana mpaka uyatimize yale unayoyaamini kama mafanikio kwako. Pambana pambana bila kuchoka na mafanikio utayaona tu.
Wakati unaendelea kupambana katika kuhakikisha kuwa unafanikiwa ni vyema ukatambua kuwa yafuatayo ni mambo nane ya msingi ambayo yatakusaidia kuweza kubadili tabia yako ambayo pengine umekuwa huipendi na kuwa chanzo cha kuanza ile tabia ambayo unataka kuwa nayo na amabya unaamini kuwa itakuletea mafanikio. Mambo hayo ni yafuatayo:-





 Angalia yale mambo chanya tu, kama unataka kubadili tabia yako na kuifanya tabia yako iweze kukusaidia katika mafanikio, basi anza kuangalia mambo yako unayoyafanya katika upande chanya. Achana na mambo hasi katika maisha yako kwa kuwa mambo hasi hayajengi hata kidogo. Hivyo basi kwa kutambua hilo anza kutazama mambo chanya pekee maishani mwako.

2.    Jenga hali ya kufanya sasa, kama unatatizo la kuhairisha mambo na unataka kubadili tabia hii basi anza mara moja tabia hii ya kufanya sasa. Usiwe mtu wa kujiwekea vipolo vingi kuwa ntafanya baadae ntafanya baadae badala yake kuwa mtu wa kufanya pindi tu jambo hilo linapotakiwa kufanywa. Hii itakusaidia kuepuka ile tabia ya ntafanya baadae au ntafanya kesho matokeo yake unajikuta unarundo la shughuli nyingi sana.


3.    Jenga tabia ya kushukuru, je unajua kuwa neno shukurani ni neon muhimu sana katika kufanikiwa kwako, anza siku yako kwa kushukuru, mshukuru mungu kwa kukuamsha salama salimini, na kwa mengine mengi anayokutendea. Washukuru ndugu, jamaa na marafiki kwa kuwa nawe hata kama sio wakati wa shida au pale tu wanapotokea kukusaidia bali washukuru tu hata kwa kukupatia muda wa kuwa karibu nawe. Jifunze kushukuru na mengi utayaona ndani ya kushukuru.

4.    Jenga misingi ya program za kujifunza mwenyewe, kama ulikuwa na tabia ya kusubiri mpaka kila kitu ufundishwe sasa ni wakati wa kuacha na badala yake jenga tabia ya kuanza kujifunza mwenyewe. Kwa sasa dunia imebadilika, taarifa zipo sehemu nyingi sana hivyo huitaji kusubiri kila kitu badala yake fanya kutafuta taarifa za yale unayoyataka. Unaweza kujifunza juu ya yale unayoyataka kupitia blog kama hii, na nyingine nyingi zenye kufanana nah ii, pia unaweza kujifunza kupitia google, vitabu, majarida na vipeperushi mbalimbali.


5.    Jenga heshima binafsi, kila mtu lazima ajiheshimu kwanza ndipo naye atapaswa kuheshimiwa, kama unakumbwa na kauli mbaya kama zile za mtu mzima ovyo au mtu mzima alafu hujiheshimu, basi ni wakati sasa wa kuamua kujijengea heshima binafsi ili iweze kukusaidia kuweza kuonekana kuwa mtu bora na mwenye kutegemewa na jamii. Anza kujifunza namna ya kuanza kujiheshimu mwenyewe ili nawe uheshimiwe. Heshima itakupa nafasi na kukufungulia mlango wa kushirikiana na watu mbalimbali.

6.    Epuka vishawishi vyote hasi, kama kweli umeamua kubadili tabia hasi basi ni wakati sasa wa kuchukua hatua nyingine muhimu ambayo ni kuepukana na vishawishi vyote vyenye kuleta tabia hasi. Kama unahisi marafiki zako ni chanzo cha tabia zako hasi ni wakati wa kuachana nao sasa na kutafuta marafiki wapya.


7.    Jifunze kuyapenda yale unayotakiwa kuyafanya, kama unatabia ya kuchukia yale unayoyafanya sasa ni wakati na fursa nyingine kwako kubadili tabia hii na badala yake anza kwa kupenda yale unayoyafanya. Hii ndio tabia muhimu ya mtu anayetaka kufanikiwa. Hii ni kwa kuwa mtu anayetaka kufanikiwa lazima akipende kile anachokifanya ndipo atayaona mafanikio, kinyume na hapo hawezi. hivyo basi kwa kulitambua hilo jenga basi hiyo tabia ya kupenda unalolifanya.

8.    Anza siku mpya kwa kitu chanya, hapa unatakiwa unapoamuka kwanza amka na fikira chanya badala ya kusema siku mbaya sema hii ni siku mpya, nzuri ambayo mungu kanipatia ili niweze kufanya yale nayotaka kuyafanya na kuyatimiza. Anza siku yako kwa kauli zenye kutia nguvu na kukujenga kiakili na kifikira.

Mambo hayo nane ni muhimu uyafuatilie kwa makini kama kweli unataka kubadili tabia yako na kuwa mwenye mafanikio makubwa maishani. Yafanyie kazi haya.

Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.
Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com


Monday, January 4, 2016

Mambo (6) Muhimu Ya Kuzingatia Ili Uweze Kufanikiwa.


Habari ndugu msomaji wa mtandao huu wa kona ya maarifa, ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri katika kuhakikisha kuwa unashughulikia ipasavyo yale unayo yahangaikia ili tu kujiletea mafanikio ambayo ndio kila mtu anayoyahangaikia. Nami nikusihi kwa moyo mmoja kuwa endelea kupambana mpaka uyatimize yale unayoyaamini kama mafanikio kwako. Pambana pambana bila kuchoka na mafanikio utayaona tu.
Wakati unaendelea kupambana katika kuhakikisha kuwa unafanikiwa ni vyema ukatambua kuwa yafuatayo ni mambo ya msingi ambayo yatakufanya ufanikiwe zaidi na zaidi. Mambo hayo ni yafuatayo:-


  Wazo, wazo ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu lakini cha ajabu ni kuwa watu hawaelewi na badala yake wamekuwa wakihangaika na vitu vingine na kujikuta wakipoteza muda bure bila mafanikio na hatimaye huanza kuhangaika huku na kule na kutafuta tatizo la kutofanikiwa kwao kumbe tatizo ni kuwa mawazo yao ndio yenye matatizo. Kuna msemo maarufu miongoni mwa watu waliofanikiwa kuwa wazo ni pesa/fedha. Hivyo basi hata katika biashara wazo ndio mtaji muhimu kwa maana hiyo ni kuwa wazo ndilo huleta pesa sio pesa kuleta wazo. Na sio kila wazo huleta pesa bali lile wazo sahihi juu ya pesa ndilo liletalo pesa. Wataalamu wanasema tunakuwa kadri ya fikira zetu. Hivyo kama kweli unataka kufanikiwa jenga mawazo chanya akilini mwako juu ya maisha yako na utafanikiwa tu.

2.    Malengo,hili ni jambo la msingi sana maishani mwako. Zunguka kote duniani tafuta mtu yoyote aliyefanikiwa maishani na ambaye unaamini kuwa anamafanikio unayoyataka muulize siri ya mafanikio yake jambo la msingi atakalokuambia ni kuwa weka malengo. Malengo ni kama dira katika meli, meli haiwezi kwenda bila dira, ndivyo ilivyo kwa binadamu binadamu asiye na malengo juu ya maisha yake hana tofauti na mfugo ambao upo upo tu. Hivyo basi weka malengo kama kweli unataka kufanikiwa maishani.


3.    kujituma, hakika hakuna mtu awezae kufanikiwa pasipo kujituma katika shughuli zile zenye kumletea maendeleo. Kujituma ni jambo la msingi sana maishani jitume katika shughulli zako, zifanye kwa kujitoa kisawasawa, hakikisha unafanya shughuli kiuhakika usifanye tu bora umefanya bali fanya kama mtu anayejielewa kuwa anafanya kitu chenye tija kwake na hapo ndipo utauona umuhimu wa kujituma. Na hatimae mafanikio utayaona.

4.    Uwajibikaji, kama hutaki kuwajibika katika shughuli zako jua kuwa mafanikio kwako yatapita kushoto. Hili naomba nikuambie dhahiri hata kama ikitokea leo umeanzisha kampuni ukaajili wafanyakazi usikae ukabweteka kuwa si kunawafanyakazi watafanya tu, usikae nyumbani kuangalia tamthiliya eti kisa umewaajili watu wanakufanyia kazi. Jiunge nawe kuwa sehemu ya wafanyakazi na utayaona mafanikio kwa kuwa wewe ndiye mwenye wazo la kuanzisha kampuni husika wala sio wafanyakazi hivyo ukiwaachia wafanyakazi pekee hii inamaanisha kuwa umejitoa na wazo lako pia umetoka nalo hivyo basi ni rahisi sana kwako kushindwa kufanikiwa. Uwajibikaji umekuwa tatizo kubwa sana miongonui mwa watanzania wengi ndio maana leo hii utawakuta watu wakiilaumu serikali hata kwa yale ambayo ilibidi wayafanye wao wenyewe.


5.    Kujiamini, maishani lazima ujiamini, amini kuwa unaweza kufanya mambo makubwa na kuwa na mafanikio makubwa sana maishani japo watu wengi wanaweza kuwa wanakukatisha tama kwa kusema kuwa hauwezi lolote. Hakuna aliyezaliwa anajua kila kitu au anajua bali kila mmoja wetu hujifunza kupitia watu fulani, hivyo basi kama waliweza kujifunza basi hata wewe unaweza kujifunza pia. Jambo la msingi ni kujituma, kuweka nia na kuwa na imani kuwa unaweza.

6.    Shirikiana na watu sahihi, sio lazima ushirikiane na kila mwanajamii maana jamii ina watu tofauti tofauti na kila mtu huwa anachagua lile kundi analoliona kuwa lina tija kwake na sio kila mtu. Leo hii inabidi uchague ni nani haswa wa kushirikiana nae na ni kwanini kama unataka kufanikiwa shirikiana na watu wenye mtazamo chanya. Tambua kuwa kila watu hukaa katika makundi yanayofana nao hivyo usije ukajichanganya ukaka katika kundi lisilo kufaa maana utaumia na laweza kuwa kikwazo cha kufanikiwa kwako.

Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Wasiliana nami kwa.
 Simu: 0754612413 au 0652612410.

Barua pepe: Bmaganga22@gmail.com